Dakika 25 za hoja ya Mbunge Ole Sendeka, Mawaziri waingia 18 za Spika Tulia

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 2 чер 2024
  • Spika w Bunge, Dk Tulia Ackson ameielekeza Serikali ikafanyie kazi madai ya mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka kwamba Serikali imepanga kuchukua vijiji 80 vya wafugaji wa Simajiro na vijiji vingine kadhaa vya wafugaji wa maeneo mingine kwa ajili ya hifadhi ya wanyamapori.
    Hayo yametoke bungeni leo Jumatatu ya Juni 3, 2024 wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo Spika alitoa maelekezo hayo baada ya maelekezo yake ya kwanza ya kumtuma Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia Elimu, Zainabu Katimba kumtafuta Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Simanjiro, Gracian Makota ili aeleze kama aliandika barua hiyo.
    “Nimepokea barua hapa kutoka kwa mheshimiwa Ole Sendeka hii barua imeandikwa na mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Simanjiro, Gracian Makota (amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro toka Agosti 2021).
    “Mheshimiwa Naibu Waziri wa Tamisemi huyu bado ni mkurugenzi wa Simanjiro (sauti zikasikika ndiyo). Mheshimiwa Naibu Waziri hebu nenda hapo nje mpigie simu kuhusu hii barua.
    Barua imeandikwa kwa ofisa mtednaji Kijiji cha olcholoni tarehe 16 tathmini ya maeneo yenye wanyamapori katika mapori ya Simanjiro na Berela na Simanjiro Kitiangare. Mkurugenzi akaseme aliandika hiyo barua au hapana.”
    Tazama zaidi.

КОМЕНТАРІ • 47

  • @BIGBOSS-hl3bu
    @BIGBOSS-hl3bu 28 днів тому +3

    Naiomba sana Serikali yetu ifike wakati wabunge wakifika umri flani wastaafu Kwa MASLAHI ya taifa letu

  • @PauloAlfayo-qi1gn
    @PauloAlfayo-qi1gn 29 днів тому +3

    Kwa hio tuseme waziri hawanui kazi zao kweli speaker uko sawa,endelea kuwaelimisha tu

  • @shomari_Msumi
    @shomari_Msumi Місяць тому +4

    Ole Sendeka👏👏

  • @YakoboMolell-t7w
    @YakoboMolell-t7w День тому

    Nakupenda Tanzania 🇹🇿 yangu ,uzalendo na uadilifu.

  • @Olerumas
    @Olerumas 17 днів тому

    Spiker be blessed ww ni kiongozi nimependa sanaaa hoja zako

  • @lomunyaklesikar
    @lomunyaklesikar 27 днів тому

    Kweli Baba mungu akupe ulimi Safi ile uteteye Sisi Wana simanyiro

  • @josephmilandononi1096
    @josephmilandononi1096 29 днів тому

    Safi Sana Mh Speaker Dr Tulia kweli wewe ni Rais wa Dunia.

  • @MossesiMosessilaizerlaizer
    @MossesiMosessilaizerlaizer 28 днів тому

    Thank you mh ole sendeka ilove you mh

  • @benny4345
    @benny4345 Місяць тому +2

    Kwa mara ya kwanza, nimependa Tulia alivyoshughulika na jambo hili. Wanarukaruka tu hawataki kukubali wala kukataa.

  • @SARAHKATAGIRA
    @SARAHKATAGIRA 26 днів тому +1

    Ni Bora ktk huo mkoa wampeleke makonda ndoo atamaliza utata

  • @mkondomkondo4721
    @mkondomkondo4721 8 днів тому

    Angalia wapiga debe wengine,umezeeka hujui unachokiongea,eti samia hafananishwi,hiloooooo...

  • @OlaIseya
    @OlaIseya 29 днів тому

    Tendeni haki

  • @Rokonga
    @Rokonga 11 днів тому

  • @williammbuzimai5744
    @williammbuzimai5744 26 днів тому

    Kumbe ole sendeka nawe unapoint eeeeeh

  • @dassustephen731
    @dassustephen731 23 дні тому

    Kama mawaziri wenyewe ndo hawa ukweli hatuna viongozi Tutaendelea kuwa omba omba milele.

  • @user-ij2lp1om6i
    @user-ij2lp1om6i 28 днів тому +1

    Jenista ni mtu wa hovyo cjawai kuona

  • @user-zk9ox3di4b
    @user-zk9ox3di4b 29 днів тому

    asante sana kaka yetu olesendeka pole sana kwa shambulio la kutaka kuuawa je serekali inasemaje je nauliza. Wanyama wanapotuvamia mbona sisi wamasai atuwakamati lakini sisi ngombe zetu zinakamatwa na kuuzwa na je nauliza wabunge mkowapi mmelala usingizi tunataka katiba mpya nilazima watanganyika nilazima tujikomboe kwa asante sana wenu Simba sauti ya wanyonge tupewe haki

    • @aloycemruma6552
      @aloycemruma6552 29 днів тому

      Hao Watu ni wajanja wajanja chenga ni nyimgi baadae litakwepo

    • @MiriamAbdallah
      @MiriamAbdallah 27 днів тому

      ​@@aloycemruma6552Hilo lilishapitishwa wanasubiri wakishapigiwa kura waliweke wazi na madharau kibao

  • @StanleySewando-nb4xm
    @StanleySewando-nb4xm 27 днів тому

    Bado Tanzania tuko mbali sana hiyo taarifa Ina mwenye kiti aliyesimia timu na walilipwa posho Sasa bunge lilitakiwa kuagiza kamati iitwe iseme ilitumwa na nani

  • @KasangaKalanga-vo6od
    @KasangaKalanga-vo6od 29 днів тому

    Lipo bwana kaskazini ni mbaya Sana kwa mgogoro ya ardhi yote imekua pori tengefu

  • @HassanMkotya
    @HassanMkotya 28 днів тому

    Kuna mawaziri dhamana waliyonayo si haiba yao.

  • @RichardMgweno
    @RichardMgweno 28 днів тому

    Tukuite chawa

  • @kindysuleiman5935
    @kindysuleiman5935 26 днів тому

    Kime uka waparurana wenyewe. Kwa wenyewe

  • @emmanuelmasele9585
    @emmanuelmasele9585 29 днів тому +3

    Mh.Spika utapata kazi sana kwa maamzi uliyoanza kuyachukua ya kusimamia hoja za Wabunge .Mawaziri wako matapeli sana na ni waongo sana

  • @mokiaolenaputu7648
    @mokiaolenaputu7648 24 дні тому

    Huyu mama Jenister ndiyo waziri wa hovyo kuliko wote kwenye hili baraza

  • @yokoi3970
    @yokoi3970 29 днів тому

    Huku makonda ana piga spana huku wengine wanafanya yao dah noma sana 😂😂😂😂😂

  • @user-kv2cx8kx4j
    @user-kv2cx8kx4j 29 днів тому

    Baba waseme tu ukweli wanaficha siri kwanza mpaka wachaguliwe kwanza ndiyo watasema ukweli

  • @audifacejosephat7071
    @audifacejosephat7071 29 днів тому

    Hawa mawaziri janjajanja nawasiwasi na elimu zao

  • @mohammedkhimji7505
    @mohammedkhimji7505 29 днів тому

    semeni tu mnasubiri uchaguzi ipite 🤣🤣🤣 acheni kutuzungusha zungusha na vitambi vyenu

  • @DanielLambalelo
    @DanielLambalelo 28 днів тому

    Serikali tatueni shda kwa wananch

  • @joelilukumay9137
    @joelilukumay9137 29 днів тому +2

    Mh spika Tulia Ackson, nimekukubali kwa jinsi unavyoonyesha ushirikiano na mh Cristopher Ole sendeka ili kuwatetea wananchi wanyonge. Yawezekana kuna ujanja ujanja. Mh waziri atamke kua jambo hilo hamna ili kuondoa wasiwasi kwa wananchi. Mungu akubariki sana mh Tulia Ackson spika wa bunge. Hio ndio uongozi inayotakiwa.

  • @hollymore4904
    @hollymore4904 29 днів тому

    Shameful

  • @healingsschool4630
    @healingsschool4630 29 днів тому

    Waarabu ni watu waajabu saana Wana mapesa isiyo na kazi . Soma historia kuna kipindi walinunua visiwa pamoja na kilomita kumi za Tanganyika toka baharini. Nakumbuka kabla ya 2010 kuna mmoja aliuziwa toka Kigamboni mpaka kimbiji akaweka mabango hakuna kilichoendele. Juzi nilishangaa hawa dpworld tuliambiwa wamechukua bandari zote kumbe wamekodishiwa gati 7 tu! na wao hawapo wameweka wahindi tu cio!

  • @daudimchileg307
    @daudimchileg307 26 днів тому

    Kwanini mpo hivo nyie watanzania? Mlisena maguful ni Rais wa mfano kwa uongoz wake mzur, mlimsifia hadi saaana, leo samia ni bola kuliko marais wote waliopta. sasa nyie ni machawa zaid ya baba levo na mwijaku.

  • @johnlaizer5925
    @johnlaizer5925 25 днів тому

    Mungu wetu tulindie mtetezi wetu

  • @user-kv2cx8kx4j
    @user-kv2cx8kx4j 29 днів тому

    Ole sendeka aliwahi kusema hawaniwatapeli tu watu kuwanyang'anya watu maenewo yao hata raisi hausiki mimi naona hilo jambo lifutwe tu halipo kabisa niwajanjanja wanataka kutapeli watu maenewo yao

    • @MiriamAbdallah
      @MiriamAbdallah 27 днів тому

      Asikudanganye mtu hii imetoka juu hakuna linalopitishwa bila raisi kusaini wanasubiri wakishapigiwa kura kwanza ndio waliweke wazi

  • @user-ij2lp1om6i
    @user-ij2lp1om6i 28 днів тому +1

    Ccm ni wahuni kama wahuni wengine

  • @1961nungwi
    @1961nungwi 29 днів тому

    Serikali imeikana, maana yake ni taarifa feki!

  • @salmanmagwe2612
    @salmanmagwe2612 29 днів тому

    Hizi pesa zinazopotea kuwalipa kijiji ni bora wajenge fance ya umeme kuzunguka hifadhi zetu na mtakuwa mmemaliza migogoro isiyokuwa na sababu,kwani hata hawa wabunge wengi wao wana yao nyuma yake.

  • @nkwazigatsha
    @nkwazigatsha Місяць тому +1

    Du kumbe umalaya wa kisiasa unarejea taratibu! Unamlinganisha rais wa kudra na waliopita? Wamasai wenzio wanafukuzwa wewe unasifia ujinga mtupu? Nilikuwa nakuheshimu sana Ole Sendeka sasa sikuheshimu tena.

  • @aloycemruma6552
    @aloycemruma6552 29 днів тому

    Umeona kama uchawi hali hii instesa taifa kwani historia ya ofisi hawakabidhiani Mtu anaingia ofisini kwa mihemko