Kamwe usitumie pesa ya biashara kiholela(hovyo),tumia njia hii ili biashara yako isife-Mchumi

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 27 сер 2024
  • Umewahi kuona kuna watu wameanzisha biashara zao lakini baada ya muda mfupi biashara zile zinakufa.
    Mojawapo ya sababu zinazofanya biashara nyingi kufa ni pamoja na matumizi mabaya ya pesa za biashara kwenda kwenye matumizi binafsi.
    Unaweza kujiuliza kwamba tafanyaje sasa ili niweze kumudu mahitaji yangu binafsi ya msingi na wakati mimi ndie mwenye biashara?
    Jibu ni kuwa unatakiwa uwe na utaratibu mzuri wa kujilipa mshahara kwenye biashara yako ili kuweka sawa mahesabu.
    Ukijilipa mshahara utakua na nidhamu na matumizi ya pesa zinazotoka kwenye biashara yako na hutachota pesa kiholela na pesa zako zitaondoka kiutaratibu.
    Njia hii ni nzuri na imesaidia wafanyabiashara wengi ambao wanaendelea kudumu na biashara zao,tofauti na ukifanya mazoea ya kawaida ya kuchota pesa za biashara bila utaratibu
    👉Gusa hapo chini ili kuona huduma na ofa zetu hapa Mchumi Consulting 👇
    linktr.ee/mchu...
    #biashara #masoko #mtandaoni #mtaji

КОМЕНТАРІ • 2

  • @mchumi_digital
    @mchumi_digital  5 місяців тому

    Fahamu OFA na huduma zetu hapa
    👇👇
    linktr.ee/mchumi_consulting

  • @user-sf8sr1sg5y
    @user-sf8sr1sg5y 5 місяців тому

    Asanteh boss