Це відео не доступне.
Перепрошуємо.

KAMA UNATAKA KUFUGA NYATI MAJI 'MILANGO IKO WAZI NJOO UCHUKUWE MBEGU SERIKALINI'

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 25 гру 2019
  • Shamba la Mifugo la Mabuki lililopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza lilianzishwa mnamo mwaka 1966 baada ya Uhuru wa Tanganyika kwa ajili ya kuzalisha F1, hii ilikuja baada ya kugundua kuwa wafugaji wachache waliopewa ng’ombe wa kisasa kutoka Ulaya, wengi wao walishindwa kuwamudu wakafa ndipo wataalamu wa Mifugo waliokuwepo enzi hizo wakaona ni vyema kuzalisha ng’ombe wa maziwa wanaoweza kuhimili mazingira ya nyanda za nchi zenye joto ikiwemo Tanzania.
    Shuhudia ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina akizuru Shamba hilo la Mabuki kama sehemu ya mwendelezo wa Agenda ya Kitaifa ya Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji viumbe kwenye maji 2020 - 2025 ambapo pia amepata fursa ya kuwaona Nyati Maji wanaofugwa kituoni hapo, mbegu iliyoingizwa nchini enzi za utawala wa Rais wa Kwanza nchini Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere.
    Kwa wale wanaotaka kufuga Nyati hao, kitambo sana Serikali ilishafungua milango.
    TAFITI ZA AWALI.
    Kwa tafiti za URT za Mwaka 2015, Tanzania inashika nafasi ya pili kwa wingi wa mifugo barani Afrika ikiwa na ng'ombe milioni 25, mbuzi milioni 16.7, kondoo milioni 8, nguruwe milioni 2.4, na kuku milioni 36.
    Kati ya ng'ombe milioni 25 ng'ombe wa asili ni 98%. Hivyo, ni 2% tu ya ng'ombe wote Tanzania wanaofugwa kwa mfumo wa ufugaji wa kisasa.
    Tafiti hizo zinaonesha kuwa ufugaji wa asili unachangia 7.4% ya pato la Taifa na ongezeko la ukuaji la 2.2% kila mwaka. Ufugaji wa asili umethibitika kiuchumi kuwa na ufanisi mkubwa katika matumizi ya ardhi na uhifadhi wa mazingira.
    Ufugaji wa asili unategemewa na idadi kubwa ya Watanzania kwa kuendesha maisha yao; iwe kwa chakula, mavazi, na maendeleo kwa mapana yake.
    Mchango wake katika uchumi rasmi na usio rasmi (informal and formal economies) ni dhahiri hasa kupitia kodi na tozo mbalimbali katika masoko ya mifugo, usafirishaji wa mifugo, ukaguzi wa mifugo, na upatikanaji wa malighafi kwa matumizi ya viwanda mbalimbali.

КОМЕНТАРІ • 19

  • @frankjackson2784
    @frankjackson2784 3 місяці тому

    Nimeipenda

  • @matukiosafaris6508
    @matukiosafaris6508 3 роки тому +2

    Maelezo mazuri lakini kila ukipiga simu ili ununue ngombe unaambiwa hakuna

  • @SimonShoo-mw8nk
    @SimonShoo-mw8nk 27 днів тому

    Swali unango'mbe wangap
    Jibu tunaweza kuzalisha kadhaa sasa takwimu za ranch hamuna au???

  • @Nyanimzee
    @Nyanimzee 14 днів тому

    Minataka ndapateje

  • @amanibwire4423
    @amanibwire4423 3 роки тому +1

    Pamoja na yote kama mfungaji nayeanza unapenda niwakumbushe kuwa ng'ombe wa kienyeji wana maziwa mazur na nyama nzr

  • @elisantemrita9894
    @elisantemrita9894 3 роки тому +1

    Embu acheni siasa kwenye ufugaji Ongezeni akili katka ufugaji

  • @damasmaleo4845
    @damasmaleo4845 2 роки тому

    Mbuzi mauza bei gani

  • @chuzilapweza6517
    @chuzilapweza6517 3 місяці тому

    kwanini sasa wanajitangaza kipindi cha nane nane na matasha peke yake?

  • @habibuluyangi2702
    @habibuluyangi2702 Рік тому

    Mabuki iko mkoa gani na hao nyati maji bei gani

  • @davidmsalilwa9687
    @davidmsalilwa9687 2 роки тому

    Wanapatikana wapi

  • @omarimnyeshani1810
    @omarimnyeshani1810 4 роки тому +2

    Duuh!! Nyati tunao wengi tu mbugani halafu wataalamu mnaomba mbegu kutoka nje ya nchi? Hivi mnafeli wapi?

    • @avyalimanaathanassambuta6577
      @avyalimanaathanassambuta6577 4 роки тому +1

      Nyati wanao tafutwa ni Domesticated

    • @TM.Sullusi
      @TM.Sullusi 3 роки тому +1

      Usikariri mkuu, sio hao nyati wa mbugani kwetu. Ni aina tofauti kabisa ya nyati 😀😀😀😀😀

    • @matukiosafaris6508
      @matukiosafaris6508 3 роки тому +2

      Kungekuwa na nyati wa mbugani hapo hao watu wote wangekuwa marehemu na wengine hospitali

    • @ndukulusudikucho_
      @ndukulusudikucho_ 2 роки тому

      @@matukiosafaris6508 hahahahahaa

    • @mebumohammed6844
      @mebumohammed6844 3 місяці тому

      @@avyalimanaathanassambuta6577naweza pata number naitaji madume tu

  • @husseinhussein9971
    @husseinhussein9971 4 роки тому

    Hao nyati ndio wale wa India?