Salama Na Fid Q Ep 7 | NGOSHA WA MBASA Part 2

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 14 бер 2020
  • #YAHStoneTown #SalamaNa #PodCast
    Listen our Podcast on
    ‪Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcasts Link apple.co/2Ou1bru‬
    ‪UA-cam Link bit.ly/UA-camSalamaNa
    NGOSHA WA MBASA
    Nakumbuka kipindi ambacho Fidi alikua anaamini kabisa kama kuweka ‘uso wa mbuzi’ ndo kulikua kunakufanya uwe ‘hard core’, sina uhakika lini aliachana na dhana hiyo ila kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi tabasamu na bashasha vimekua havibanduki kwenye uso wake, jambo ambalo mimi kama rafiki nalifurahia sana. Nakumbuka baadhi ya marafiki zangu wa kike ambao ni wapenzi haswa wa mziki wake walikua wakiniambia eh, sema rafiki yako mgumu jamani, Kha! Mi hucheka tu na baadae wakishazoeana basi sidhani kama kuna hata mmoja anaweza kusema kitu kibaya kuhusu yeye. Nilikua nacheka kwasababu mimi naamini namfahamu rafiki yangu huyu, yeye hupenda sana matani, na kucheka na marafiki wa karibu wanaweza wakathibitisha hilo maana katika watu ambao unaweza ukawatania weeee mpaka asubuhi, na utani mpaka wa vitu vyengine ambavyo wewe wa karibu unaweza kusema ey, hiyo sasa imepitiliza, yeye waala... Atacheka tu!
    Mwenye kipaji chake cha kujifunza mwenyewe, nasema hivyo kwasababu nadhani kufahamiana kwetu na kuelewana kwetu pia kunatokana na kuwa na vitu vinavyofanana ndani yetu. Kajifunza jinsi ya kupenda kusoma vitabu mwenyewe, kujifunza jinsi ya kuandika na kurap mwenyewe, kajiendeleza mwenyewe (bila ya shaka kuna watu walomsaidia kwa tafu za hapa na pale ila walitokea baada ya kuona jitihada zake). Alihakikisha anasafiri kwenda nje ya nchi na Africa kwa jitihada zake mwenyewe na mpaka leo, kukiitwa watu ambao wamesaidia kwa kiasi kikubwa kufikisha Hip Hop ya nyumbani hapa ilipo basi jina lake litakua ni miungoni ya yale yatakayopata heshima ya juu kabisa. Pia anachekesha sana. Uelewa wake wa baadhi ya vitu unaweza ukakuacha mdomo wazi wakati mwengine. Kwenye uwepo wake? Vicheko lazima vitawale.
    Hii siku nilitia nae story haikua kama kazi, bali kama mtu na rafikiye tu wakitia story juu ya njia za maisha ambazo tumepitia mpaka sasa. Fidi amekuzwa na Mama yake ambae alikua ni mfanyakazi wa serikalini (ameshastaafu), alikulia mkoani kama wengi wetu, alifika Dar akakaa kwa ndugu kama wengi wetu, alianzia sehemu na kutoka hapo mdogomdogo akajijenga kufikia hapa alipo. Humu tumeongelea hayo, watoto, muziki, ndoa, maisha ya wasanii na maendeleo kwa ujumla. Yangu matumaini uta enjoy na kuelewa baadhi ya vitu zaidi na zaidi.
    Here’s to Ngosha wa Mbasa.
    Love,
    Salama.
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown
  • Розваги

КОМЕНТАРІ • 142

  • @latriciah01augustino67
    @latriciah01augustino67 4 роки тому +50

    Mafanikio ni nini? Jitengenezee tafsiri yako kisha ishi nayo🙌🏽🙌🏽🙌🏽 Ahsante fid

  • @christopherjames3684
    @christopherjames3684 4 роки тому +14

    Hii ni zaidi ya shule asente salama kwa kutuletea mtu kama hyu anaetujenga kwa maongezi herimu nzuri sana hii...

  • @abdulaziz703
    @abdulaziz703 4 роки тому +10

    Ngosha, we jamaa nakukubali always. Umenifanya niipe kazi akili yangu kuchanganua maana ya maneno kwenye mistari ya nyimbo zako. Binafsi sijutii kufahamu pamoja na kusikiliza chochote kinachotoka kinywani mwako coz naamini utakuwa hujakitoa kwa bahati mbaya.

  • @ffredy70
    @ffredy70 4 роки тому +30

    Best interview ever
    Tofauti kabisa na mkasi
    Yani kama ndo mara ya kwanza fid kuhojiwa na Salama

    • @afrorango1432
      @afrorango1432 4 роки тому

      Fid ashawahi kuhojiwa wewe na salama ingia mkasi

    • @ffredy70
      @ffredy70 4 роки тому +2

      Broo jiongeze ...soma upya hiyo comment....#usikurupuke

  • @abbysauko3725
    @abbysauko3725 4 роки тому +5

    Yan muuliza maswal ametulia kwenye kuuliza na anaejibu maswal ametulia kwenye kujibu..
    Best interview

  • @paulolwila4253
    @paulolwila4253 4 роки тому +5

    Nampenda Bure salama namna alivyopoz sio wanahabr wengine huwez jua nan ana muitaview muingine coz wote unakuta waongeaz mpka c poah but hapa salama karelax fid Q anaflow vzr sana. Love you all .

  • @kapagaanimalcare5523
    @kapagaanimalcare5523 4 роки тому +12

    Naenjoy na kujifunza kwenye kila interview ninayo kusikiliz na uwa siachi interview yoyote inipite ambayo umeojiwa. WE NI DARASA LINALOTEMBEA, MZIKI WAKO NI SHULE TOSHA

    • @shaibumahanda5190
      @shaibumahanda5190 4 роки тому

      Jamaa nilikuwa simfuatilii ila ep ya kwanza na hii haijaisha nataman kutafuta intview nyingine zaidi umeongea point pia hilo n darasa kabsa

  • @abdallahmakombo3866
    @abdallahmakombo3866 4 роки тому +2

    Hiki kichwa hiki ,kweli maisha NI elimu na SI ya darasani NI vitabu tu,Kisha uhalisia !!,

  • @joycekinyange6179
    @joycekinyange6179 Рік тому +2

    Yaani Fid Q is so deep, appreciate you sharing your story and experiences especially around single parenthood and blended family life. You are doing a great job and an exemplary role model for others in similar circumstances. Asante bro, continue living your truth 🙏🏽

  • @kingungeii6520
    @kingungeii6520 4 роки тому +11

    Fid Q ni chanzo cha busara yangu

  • @deustrackson6035
    @deustrackson6035 3 роки тому +1

    Unaeza mckiliza fid badae ukahisi ulisoma ktabu Cha professor flan.......MAY GOD BLESS U MUCH BRO

  • @peninaancon1256
    @peninaancon1256 4 роки тому +2

    Exactly, Mafanikio ni kujitengenezea tafsiri yako na kuiishi kila siku..
    Ila Salama umenichekesha, ukaamua kumalizia na ya Fid eti..

  • @bonniegtmagabe2009
    @bonniegtmagabe2009 4 роки тому +13

    kama kuna kitu mmegundua kweny hii interview...sio intervention ya mwaka huu niya mwaka jana....kwhyo ilkuw imefanywa tayar...🔥🔥🔥

    • @gthirty
      @gthirty 4 роки тому +2

      Ni pale aliposema mwaka huu godzilla amepotea, Kumbe ilikuwa ni mwaka jana yan 2019

    • @riphatmuhene9615
      @riphatmuhene9615 4 роки тому +1

      Ndio kifo cha zilla

    • @nyemondagalla608
      @nyemondagalla608 4 роки тому +1

      Sawa kabisa,
      Lkn pia kuna madini ambayo si ya Mwaka huu ni ya miaka 100 ijayo.

    • @adamayubu157
      @adamayubu157 4 роки тому

      Makini sana

  • @simonsanga2129
    @simonsanga2129 4 роки тому +15

    Salama big up,can you bring his friend Nikki wa Pili

  • @erickmbiso9939
    @erickmbiso9939 4 роки тому +15

    Interview iko vzr san jinsi unauliza maswali na anavyojibu iko poa sana nadhan ndio salama na best mpaka sasa lakini jaribu kumpa airtime Niki mbishi amwage madini yake

  • @philimonsoka2325
    @philimonsoka2325 4 роки тому +9

    The best hip hop artist ever in tanzania

  • @adamidrisa9232
    @adamidrisa9232 4 роки тому +4

    sema salama ni kizuri kinyama big up sn kwahuyo muhuni anae ishi na huyu manzi

  • @ahmedaziz7853
    @ahmedaziz7853 4 роки тому +8

    Nimetaman sana hii interview isiishe madini ya ghali sana yapo humu

  • @christopherjames3684
    @christopherjames3684 4 роки тому +5

    Mrete na joseph kusaga

  • @josephatmapesa5171
    @josephatmapesa5171 4 роки тому +5

    Fid Q ni mwalimu.

  • @elninothetragedy3121
    @elninothetragedy3121 4 роки тому +4

    Fid nakuelewa sana... nakumbuka KAN Festival nlivamia jukwaa ulivyopanda tu... duh nakukubali sana bro

  • @johnpantaleo6962
    @johnpantaleo6962 4 роки тому +5

    Dah nimepata faida kubwa sana kuingalia hii interview kwani nimejifunza kitu kikubwa sana kutoka kwa fid q

  • @eliasmlundwa3880
    @eliasmlundwa3880 3 роки тому +1

    safi!

  • @Therealjoh
    @Therealjoh 4 роки тому +6

    Muda Kama ni Mdogo sana kuna madini mengi sana yamebaki kwenye hicho kichwa

  • @annamichael1433
    @annamichael1433 4 роки тому +6

    lov this women no reason

  • @kijokombao5345
    @kijokombao5345 4 роки тому +5

    Nimependa show ilivyoisha 👏👏

  • @allimwakalebella3789
    @allimwakalebella3789 4 роки тому +5

    Salama na #Djfetty itakua poa sana

  • @ayubduma4856
    @ayubduma4856 4 роки тому +3

    Madini tosh namkubali ngosha

  • @jamalomar7829
    @jamalomar7829 4 роки тому +5

    mmmetisha sana wakongwe

  • @nongishishihaule5847
    @nongishishihaule5847 4 роки тому +3

    Sio mnaojiwa na wasafi basi kelele nyingi sana

  • @irenegervas8477
    @irenegervas8477 4 роки тому +1

    Salam kipind Chako kizur ila Jitahdn Saut Maik Unaziweka Mbalii Sanaa hautisikii Vzr

  • @ezekiampinga8106
    @ezekiampinga8106 4 роки тому +3

    Daah natama niwe naangalia anavyo hojiwa fid q everyday

  • @joycejohn7754
    @joycejohn7754 4 роки тому +2

    Napenda interview za hv sio zile za no comment

  • @yusuphanyimike9945
    @yusuphanyimike9945 4 роки тому +2

    Changa moto IPO kwenye saut hatuwasikii vzr lifanyieni kaz tu enjoy kpind

  • @ashasiaga3197
    @ashasiaga3197 4 роки тому

    Nimempenda sana mama faridi ni mama bora. Huwezi kuweka chuki kwa mtoto kwa matatizo yenu ambayo yy hayamuhusu baba atabaki kua baba na mama atabaki kua mama haiwez kubadirika

  • @saddymwamba7072
    @saddymwamba7072 4 роки тому +5

    Thanks fid Q God bless you

  • @stephanojofrey6757
    @stephanojofrey6757 4 роки тому +3

    Salama tuletee mnyamwezi P funk majani militisha sana kwenye Mkasi.

  • @dannuru6385
    @dannuru6385 4 роки тому +3

    igot u broo

  • @kaskaziniansgang1288
    @kaskaziniansgang1288 4 роки тому +2

    Kinachoniumizaga ni watangazaji waloshindwaga kuuliza maswali kuhusu maisha ya fid na rado hadi kufikia kuwa na beef

    • @khalidsalum1740
      @khalidsalum1740 4 роки тому

      Rado alikuwa mshikaji wake ijapo sio kivile Ila alitaka kutoka kwa kupitia fid q

  • @scripturetz1056
    @scripturetz1056 4 роки тому +2

    #madsoft

  • @robertandrea9257
    @robertandrea9257 4 роки тому +3

    vibe up salama kipindi leo kizur ila vibe up maan

  • @patricktravis6575
    @patricktravis6575 4 роки тому +2

    Nomaa sanaa hii show ya ngosha

  • @bernad_1
    @bernad_1 4 роки тому +8

    one of the lately best interview, big up both of y'áll

  • @johnleonard6894
    @johnleonard6894 4 роки тому +3

    Mkal wa rap tz

  • @binbaya923
    @binbaya923 4 роки тому +1

    Eb mm namkubali sana huyu mzee. Lkn sijui kwanini waafrika walio wengi wakishakua maarufu wanatafuta wanawake au kama ni wanawake wanatafuta wanaume weupe. Japo huyu mzee ameeleza sababu zake. Ila wenzetu weupe inakua ktk 10 basi mmoja ndio atakua kimapenzi na mtu mweusi tena labda awe star🤷🏿‍♂️

  • @alexshallom3094
    @alexshallom3094 4 роки тому +3

    Farid kibandan (ELIMU PURE YA KUWA MZAZI BORA)

  • @mkombozimstaff4830
    @mkombozimstaff4830 4 роки тому +2

    Salama umeolewa coz l Love U

  • @fatmasayid8895
    @fatmasayid8895 4 роки тому +3

    Best interview salama big up Faridi kubanda

  • @omarikisungu7630
    @omarikisungu7630 4 роки тому +3

    Good

  • @guccij3549
    @guccij3549 4 роки тому +3

    Makin

  • @amanimushi1466
    @amanimushi1466 4 роки тому +2

    Fid katisha sana 😂😂😂👌👌👌👌👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍

  • @ezekiambise2595
    @ezekiambise2595 4 роки тому +2

    Master mind

  • @shwahibumassawe2555
    @shwahibumassawe2555 3 роки тому +1

    Perfect Conclusion

  • @twalibabubakar2016
    @twalibabubakar2016 4 роки тому +2

    moja safi sana

  • @manothorhymes6137
    @manothorhymes6137 4 роки тому

    Heshima kwako Dada Salama Jabir & Fid Q Ngoshaaa mwanzo mwixho nimeipenda Sana hii interview kinomanoma big up kinomanoma tangu Vina Mwanzo Kati na Mwisho mpaka KitaaOlojia heshima kama zoteeee

  • @zildatwahid6526
    @zildatwahid6526 4 роки тому +2

    I love salama jabir💕

  • @gthirty
    @gthirty 4 роки тому +1

    Salama na Mwana FA... Naisubir hii

  • @nelsonmwombeki5243
    @nelsonmwombeki5243 3 роки тому +1

    Heee kanywa zoteee??

  • @mollellominis2267
    @mollellominis2267 4 роки тому +1

    nice

  • @nicksonjohn5676
    @nicksonjohn5676 4 роки тому +2

    Fid q mwn hisabati

  • @robsonwisdom2647
    @robsonwisdom2647 4 роки тому +2

    Fid q anajib vizur sana

  • @idditoufiq649
    @idditoufiq649 4 роки тому +2

    Entertaining plus Educating
    Its The best 🔥🔥🔥

  • @johnphilipoaugustino6100
    @johnphilipoaugustino6100 4 роки тому +2

    Sasa tuletee na mwana fa yaaani daah mtatisha sana

  • @nozgeniuz1812
    @nozgeniuz1812 4 роки тому +3

    Yahstone nmependa

  • @judamsaki5609
    @judamsaki5609 3 роки тому

    Namwelewa sana sana FIDQ

  • @mababiyoo8099
    @mababiyoo8099 4 роки тому +1

    One love

  • @fanuelmtewele5660
    @fanuelmtewele5660 Рік тому

    Madam unajua sana Mungu akujalie tu

  • @chumayaoinvestment1647
    @chumayaoinvestment1647 4 роки тому +3

    Hip hop has spoken

  • @samwelmussa5794
    @samwelmussa5794 4 роки тому +2

    Duh nashkuru sana fid q mafanikio sio magorofa na magari

  • @mwanaramadhan6670
    @mwanaramadhan6670 4 роки тому

    Bless up Sana salama

  • @othumanomary4032
    @othumanomary4032 4 роки тому +2

    Majani aise niwe aingie

  • @awadhmohamed7668
    @awadhmohamed7668 4 роки тому

    Mashaallah utulivu na interview nzurii Sana salama jabir wwe mkongwe na hii kazi big up

  • @yassinkassim5241
    @yassinkassim5241 4 роки тому +1

    Two geniuses 👌🏿👌🏿

  • @wilsongona8066
    @wilsongona8066 2 роки тому

    You guys are amazing

  • @johnphilipoaugustino6100
    @johnphilipoaugustino6100 4 роки тому +6

    Mbn hii interview fupi asee

  • @wibrotouchz5370
    @wibrotouchz5370 4 роки тому +3

    😂😂😂kujifunza na kuburudika Mungu azid kuwasimamia

  • @abduly.snootie
    @abduly.snootie 2 роки тому +2

    WoooW Hii ni Moja Kati ya "INTERVIEW" Kaliii Kabisa Kuwai Kuiona 🧠💯. #SalamaNaFidQ
    ​📌 Maswali Magumu na Mzuri & Majibu Mepesi na Mazuri + MADINI, nime'ENJOY Sana Kuiangalia Hii "CONVO"👑✨ #SalamaNa MOJA KATI YA KIPINDI KIKUBWA KABISA KUWAI KUTOKEA TZ 📌 🎥🎞️🎬📽️🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

    • @abduly.snootie
      @abduly.snootie 2 роки тому +1

      📽️🎬🎞️🎥🔥🔥🔥🔥🔥

  • @kinigarm8239
    @kinigarm8239 4 роки тому +3

    Kama nakuona Sine Club miaka ya 2004 vile. Uligayanda ga nguzu nkoi.

  • @vedastusmatagi4860
    @vedastusmatagi4860 4 роки тому +1

    dah kipindi kizuri

  • @doricephineas4262
    @doricephineas4262 4 роки тому +2

    Fareed nakuelewa sana.

  • @saumuhassan6365
    @saumuhassan6365 4 роки тому

    Shukran my dear brother, kila la khery ndugu zetu 🙏

  • @mtumweusitv7944
    @mtumweusitv7944 4 роки тому

    Super interview

  • @abuumwichumu5520
    @abuumwichumu5520 4 роки тому +1

    Wadau, labda mimi nafikir tofauti , ivi hichi kipindi ni chakutoa siri zako au? Nauliza tu maana mtu anajieleza yote nazani hiii si pow

  • @khadijahbanana5602
    @khadijahbanana5602 3 роки тому

    True like me napenda sana creole na french zouk halafu sielewi

  • @saumusalimuhassan2499
    @saumusalimuhassan2499 2 роки тому

    *FARID UMETISHA* Good job Salama respect 😘

  • @innocentmushi1550
    @innocentmushi1550 4 роки тому +2

    ongeza bando inaendelea😂😂

  • @mchomvuhassani8521
    @mchomvuhassani8521 4 роки тому

    Nimemuelewa sana huyu jamaa

  • @mtumweusitv7944
    @mtumweusitv7944 4 роки тому

    😂😂😂😂😂😂 Leo mmekutana wana appetite

  • @maalimmwenge5002
    @maalimmwenge5002 3 роки тому +1

    13:24

  • @ilovejesus9303
    @ilovejesus9303 4 роки тому +4

    😍😍😍😍😘😘😘 Salama sikuwezi, huwa nakupenda sana. Your interview are awesome

  • @Wachuoni
    @Wachuoni 4 роки тому

    Sauti iko chini sana, ... NO comments

  • @lujobilz7482
    @lujobilz7482 4 роки тому +3

    Sorry madame Salama nakutafuta nikupe madini usikilize unipe madini niyafanyie kazi excuse madame

  • @galusmbele5410
    @galusmbele5410 3 роки тому

    "Kama kilichokutambulisha kwenye jamii ni kiki, endelea kutengeneza kiki nying...." mwisho wa kunukuu

  • @juliusfungo2754
    @juliusfungo2754 4 роки тому +3

    Bando lipo lakutosha haina haja ya kuongeza

  • @convilsabato7596
    @convilsabato7596 2 роки тому

    " Bill Naz or Zizi?Zizi anytime " a good one

  • @barakanyamhagata3499
    @barakanyamhagata3499 4 роки тому +2

    Salama tupe utaratibu tuna msika vp kaka mkubwa!!

  • @magulumakenzi5342
    @magulumakenzi5342 4 роки тому +1

    Musukuma utampindisha hivi na vile ila hawezi kusahau chakula
    Just tease on you ngosha

  • @philimonsoka2325
    @philimonsoka2325 4 роки тому +7

    Salama Fanya kumdondosha mwana falsafa apo yahstone twn

  • @mandizzle8807
    @mandizzle8807 4 роки тому +2

    mbn hazifungk

  • @mtongamohd5665
    @mtongamohd5665 4 роки тому +1

    Kubanda