Salama Na LAMATA SE6 EP 04 FULL SHOW |WATASWIRA PART 1| SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 19 жов 2024
  • #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
    WA TASWIRA
    Kupitia maongezi yangu haya na Bi Leah Richard Mwendamseke huyu ambaye tunamfahamu kama Lamata ndo niliamini kwamba si kila umsikiae akiongea kwa sauti ya juu wakati yuko kazini kwake basi anaweza kuja kwenye meza ya Salama Na pia akaongea kama ambavyo anaongea anapokua kwenye comfort zone yake. Nayasema haya kwasababu wakati tunaandaa kipindi hiki ndo niligundua Lamata ni muoga au ni mtu asopenda kuwa mbele ya kamera kiasi gani!
    Binafsi sina mazoea naye ya hivyo zaidi ya kuifahamu kazi yake ambayo inaongea yenyewe. Tunafahamiana kupitia rafiki wa rafiki ila hatujawahi kukaa chini tukatia story na kufahamiana kama ambayo tulifanya kwenye maongezi haya. Namshkuru kwa kutafuta wasaa katika ratiba yake inayombana haswa lakini alihakikisha anatafuta wasaa ili aje akae nasi na tuongee kuhusu yeye na fikira zake kwenye mambo mengi.
    Mzaliwa wa Mbeya na ambaye kipaji chake cha uandishi kilianza kuonekana alfajiri kabisa, Lamata anasema Mama yake mzazi ndo shabiki nambari moja wa kazi yake. Kwenye dunia hii na maisha ambayo wengi wetu tumepitia ni nadra sana kumkuta mzazi anaamini kwenye kipaji cha mwanae na kumpa moyo wa kutaka akiendeleze. Mama yake alikua anamsifia uandishi wake na kutaka amalizie zile aliziandika ili yeye ndo awe wa kwanza kuzisoma. Au wakiwa wamekaa wanaangalia tamthilia au sinema atahakikisha anamkiliza mwanawe juu ya maoni yake na hata wakati mwengine kumuuliza kama ingekua yeye angemaliza hiyo sinema au tamthilia kwa angle ipi.
    Story kadhaa alinipa juu ya safari yake hiyo, shuleni nako alikua burudani pia kwa baadhi ya waalimu na wanafunzi wenzake. Kitu ambacho kilikua kinafanya mambo yake yaende ki ulaini kabisa.
    Kwa sasa tamthilia zake anazoandika ndo moja ya vivutio vikubwa kwenye DSTV kwa upande wa channel za ukanda wetu huu, ila tukumbuke pia alianzia kwenye filamu kabla ya kujikita rasmi kwenye tamthilia. Safari yake haikua tu rahisi. Alinihadithia jinsi alivyosaka upenyo na kuhangaika huku na kule ilimradi tu apate mtu wa kumuingiza ndani ITV na aweze KUSIKILIZWA na yoyote anayehusika. Tukumbuke pia ilibidi awe muingizaji wakati flani na hiyo pia ilikua ni moja ya njia za yeye kutaka kupata upenyo, kuwa mbele ya camera si vitu pendwa vya Lamata KABISA ila ilibidi afanye hivyo ili mambo yake yakae sawa.
    Haya maongezi yetu yalijaa ukweli na uwazi juu ya karibu kila kitu kinachohusu maisha yake. Marafiki pia tuliwazungumzia. Ukaribu wake na baadhi ya waigizaji anaofanya nao kazi, jinsi anavyotoa nafasi kwa wenye vipaji na vile vile tuliongelea suala la ajira na ushawishi kwenye kiwanda cha filamu na burudani hapa nyumbani. Yangu matumaini utapata mawili matatu hapa ya kuwezesha boti yako iende unapotaka.
    Kwa hilo, nakutakia kheri.
    Love,
    Salama.
    Support us through anchor.fm/yahs...
    SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
    Listen our Podcast on
    Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
    GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
    Audiomack Link bit.ly/YahSton...
    ‪UA-cam Link bit.ly/UA-camS...
    Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown
    Channel Administered by Slide Digital
    Instagram: slidedigitaltz

КОМЕНТАРІ • 34

  • @asnatirichard313
    @asnatirichard313 Рік тому +2

    I am proud of you my mom young sister keep it up ,almight bless my super woman lamata

  • @OnlyRuky
    @OnlyRuky 2 роки тому +5

    Its true wasanii wengii wageni kutoka jua kali hawakuwa wanajulikana. Keep it up lamata

  • @rahmamlela
    @rahmamlela 2 роки тому +4

    Mind blowing!! Congrats🙏🏾 tunejifunza saana hapa!!

  • @neemaalbert2731
    @neemaalbert2731 2 роки тому +1

    Hongera lamata,unaonajee huyo directa aletaka kukubaka umshtaki,umtajee

  • @sakinamohamedy4646
    @sakinamohamedy4646 2 роки тому +3

    Salama this z best interview

  • @giantdaniel1932
    @giantdaniel1932 2 роки тому +1

    Shikamoo dada angu me napenda sana kuigiza

  • @emmanurichares6589
    @emmanurichares6589 2 роки тому +2

    anaongea vzuri Yuko amazing sana

  • @remeniurasa4866
    @remeniurasa4866 2 роки тому +2

    😂😂 exchange mandaz kwa story . Nmependa sana.

  • @bettykauye7691
    @bettykauye7691 Рік тому

    I love lamata hoping to meet her one day

  • @chunanachu2529
    @chunanachu2529 2 роки тому +2

    Makupenda sana salama

  • @Jejee125
    @Jejee125 4 місяці тому

    Natamani kuigiza na mm nifanye kazi na lamata

  • @saumusalimuhassan2499
    @saumusalimuhassan2499 2 роки тому +1

    Mashallah, good talking

  • @amytullah2175
    @amytullah2175 Рік тому

    Very interesting kwakweli 😅

  • @princessdiana5350
    @princessdiana5350 2 роки тому +1

    Nampenda sana huyu dada

  • @mzizirashid709
    @mzizirashid709 2 роки тому +1

    Nataman Kukutana Na Lamata Sana

  • @rosegideon336
    @rosegideon336 2 роки тому

    Mungu azidi kukupa Vitu zaidi Una kitu kikubwa mnoooo....

  • @julianamaganga4803
    @julianamaganga4803 2 роки тому

    Huyu dada namkubali sana

  • @sassboy9360
    @sassboy9360 2 роки тому

    Hiyo short black na tshirt ni uniform au ??? Though always you’re good in your job

  • @maryschroeder521
    @maryschroeder521 2 роки тому

    Good stuff salama

  • @esterdoriye4780
    @esterdoriye4780 2 роки тому +4

    Lamata unavyoongea fasta story c unajaza makaratasi

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 2 роки тому +1

    🤦‍♀️🤦‍♀️🤦‍♀️NAKUPEND sana 🙌

  • @ezekielmussa2440
    @ezekielmussa2440 2 роки тому

    Nakukubal xn salama

  • @ipyanamwakapola2176
    @ipyanamwakapola2176 2 роки тому +4

    Lamata i need to work with you

    • @luckyshija6649
      @luckyshija6649 2 роки тому +1

      The same as me dear, but famous people don't want unknown pple like as, maybe we work alone first

  • @aminathaabubakarmasoud565
    @aminathaabubakarmasoud565 2 роки тому

    Toa maandazi upewe story''''''''so nice 🤣🤣

  • @tigerchristmas5491
    @tigerchristmas5491 2 роки тому

    Jmn n anaongea kama kajala

  • @aishajafari7525
    @aishajafari7525 2 роки тому

    Dah huyu ndio aliandika kigodoro

  • @ngoshachaula172
    @ngoshachaula172 2 роки тому +1

    Anaongea haraka haraka adi atuelew

    • @roxannerickkky8513
      @roxannerickkky8513 2 роки тому

      Kwel yaan she’s too high.

    • @bisharamohd9951
      @bisharamohd9951 2 роки тому +1

      Carrier yake imempelekea awe jaribu kuappreciate analofany mwenzako neno gani kasem hapo hujafahamu hem linote tukutafsirie

    • @othumanlorenzo260
      @othumanlorenzo260 2 роки тому

      @@bisharamohd9951 mjinga huyu watu Hawa appreciate karama za wengine

  • @maireshsaid1628
    @maireshsaid1628 2 роки тому

    nilikuwa naisubiri kwa hamu