Mamia ya waombolezaji wafurika kumzika aliyekuwa dereva wa RAS Kilimanjaro

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 23 чер 2024
  • Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ameongoza mamia ya waombolezaji kwenye mazishi ya aliyekuwa dereva wa Katibu Tawala wa Mkoa huo, Alphonce Edson(54) aliyefariki kwa ajali ya gari Juni 18, mwaka huu.
    Edson na Katibu Tawala huyo(RAS),Tixon Nzunda ambaye amezikwa Juni 22, Mkoani Songwe walifariki kwa ajali ya gari saa 8:30 mchana , Juni 18, mwaka huu, eneo la Njia panda ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati wakienda kumpokea Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ambaye alikuwa akielekea Mkoani Arusha kikazi.
    Dereva huyo, anazikwa nyumbani kwake Kahe na baada ya maziko hayo, familia iliyopo Moshi, wataupeleka msiba nyumbani kwao Rungwe, Mkoani Mbeya.
    Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema kuondokewa na Katibu tawala na dereva wake ni pigo kubwa kwa Mkoa huo na kwamba pengo lao halitaweza kufutika kwa urahisi.
    Babu amesema Alphonce alikuwa kijana mtulivu mchapakazi na hakuwa mtu wa manung'uniko wakati wa utendaji kazi wake.
    Akitoa salamu za pole, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Zephania Sumaye ameitia moyo familia ya dereva huyo kumshukuru Mungu kwa kila jambo kwa kuwa kila kinachotokea hapa duniani ni kusudi la Mungu.
    Naye, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa madereva Tanzania, Venus Wanyangi amesema taarifa za kifo cha dereva mwenzao haikuwa rahisi kuzipokea kwa kuwa muda mchache walikuwa naye katika majukumu yao ya kazi na kwamba ni pigo kwa tasnia yao.

КОМЕНТАРІ • 2