ZAIDI YA WATU 11 MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI SINGIDA - DC GONDWE

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 8 жов 2024
  • Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego amesema Mamlaka za Serikali zitawakamata wote waliohusika na vifo vya Watu watatu ambao miili yao imefukuliwa nyumbani kwa Mganga wa kienyeji aitwaye Namba Kasubi Mkoani Singida.
    Akiongea na Wananchi kupitia simu ya DC wa Singida, Godwin Gondwe ambaye alikuwa eneo la tukio, Dendego amesema "Naungana na nyinyi kuwapa pole kwa kadhia mliyoipata na nawashukuru kwa ushirikiano na naomba tuendelee kufichua Wahalifu lakini natoa pole kwa Familia, yoyote aliyeshiriki katikard mambo ya hovyo hayo lazima mkono wa dola umchukue"
    Kwa upande wake DC Gondwe amesema "Baada ya kufanya uchunguzi ndio tukagundua kaburi la kwanza, waliogundua hilo ni Vyombo vyetu vya usalama, Serikali kama ilivyoanza itamaliza suala hili"

КОМЕНТАРІ • 1