Miili mingine miwili yafukuliwa kwa mganga Singida, ulinzi waimarishwa

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 8 жов 2024
  • Mara baada ya kuzuka kwa taharuki ya miili mingine miwili kufukuliwa katika nyumba ya mganga wa kienyeji mkoani Singida, Jeshi la Polisi mkoani humo limeimarisha ulinzi katika eneo hilo huku miili hiyo ikifikia mitatu mpaka sasa.
    Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Amon Kakwale wakati akizungumza na wananchi leo Jumapili, Agosti 25, 2024 akisema eneo hilo litakuwa chini ya Jeshi la Polisi mpaka taratibu zote zitakapokamilika.
    Amesema miili hiyo mingine iliyofukuliwa imeshindwa kutambulika, hivyo kitakachofanyika ni kupima vinasaba vya miili hiyo na wote waliopotelewa na ndugu zao ili waweze kutambua miili hiyo ni jinsia gani na imetokana na familia gani.
    “Tukishachukua sampuli za miili hii na ndugu ambao walipotelewa tutafanya uchunguzi wa vinasaba vinavyoweza kututambulisha jinsia ya mwili mmoja na mwingine kwa sasa sio rahisi kutambua. Kuanzia sasa na kuendelea eneo hili litakuwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi,” amesema Kamishna Kakwale.
    Aidha Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Singida, Elia Digha amesema katika maeneo yao wameingia waganga wa kienyeji maarufu kama lambalamba ambao hujitafutia fedha kwa njia zisizo halali.

КОМЕНТАРІ • 3

  • @HidayaJamali-v1g
    @HidayaJamali-v1g Місяць тому

    Sbhanallah 😢😢

  • @GasperSenso
    @GasperSenso Місяць тому

    Uyo anatakiwa anyongwe

  • @petermisungwi3229
    @petermisungwi3229 Місяць тому

    Huyo ahukumiwe kulingana na matendo yake pasipo kumhusianisha na kabila. Watanzania tuendelee kuwafichua, tusiwafiche wahalifu hawa wasiofaa kabisa kwenye jamii yetu!