A-Z Kardinali Rugamba alivyovikwa Pallia Takatifu/Akiri imani na kula kiapo mbele ya Balozi wa Papa.

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 2 лип 2024
  • IFAHAMU PALLIUM TAKATIFU
    ▪ Pallium ni neno la Kiswahili lililotoholewa kwa Lugha ya Kingereza Pallium au kwa Kilatini Palla, likimaanisha vazi linalovaliwa juu ya (Chasuble - vazi la Kiliturujia) na Papa, Maaskofu Wakuu na baadhi ya Maaskofu katika Kanisa Katoliki la kiroma.
    Mwanzoni lilitumiwa na Papa wa Roma tu, lakini baadaye alianza kuwatunuku Maaskofu Wakuu kuonyesha Mamlaka waliyonayo juu ya Maaskofu kwa kushirikishwa na Upapa wa Roma.
    Pallium hutokana na sufu (manyoya ya kondoo) yaliyokatwa kutoka kwa kondoo wakati wa sherehe ya Mt. Anyesi ambayo huadhimishwa Januari 21 kila mwaka. Jina Anyesi (au Agnes) limetokana na neno la Kilatin “Agnus” lenye maana ya “Mwanakondoo”. Kwa nini hutengenezwa kutokana na sufu ya kondoo? Kwenye Agano Jipya Kristo anatambulishwa kama “Mwanakondoo wa Mungu” (rejea Yn. 1:29, 36). Kama ambavyo kondoo wanatoa sufu kwa ajili ya kutengeneza Pallium.
    ▪ Pallium huenda ilianza kuvaliwa na Wagiriki wa zamani waliovaa nguo ambazo Warumi waliziita Pallium kama nguo iliyovaliwa nje yenye umbo la kimstatili kuzunguka mwili wa mtu ikiwa imetupwa mabegani kama mtandio wa kuzuia baridi.
    Ila kadiri ya miaka ilivyoenda Pallium ikawa nyembamba ikifanana na skafu/mtandio mrefu. Baadaye Karne ya Saba (7) Pallium ilibadilika na kuwa na umbo la herufi Y (Ikionekana hivyo mbele na nyuma) ikiwa na misalaba meusi sita, nne kuzunguka shingo, moja mbele na moja nyuma.
    ▪ Matumizi ya Pallium kikanisa yalianza enzi za tamaduni za zamani za Wafalme na baadhi ya maafisa waliovaa skafu maalumu kama vitambulisho vya ofisi bug.
    Pallium ilivaliwa na Maaskofu kwenye karne ya 4 na 5 na karne ya 6 Papa akawa anawatunukia (conferring) wao kama alama ya heshima au sifa. Kuanzia karne ya 9 ikawa kwamba Askofu Mkuu asingeweza kuonyesha mamlaka ndani ya Jimbo Kuu bila kutunukiwa Pallium na Papa. Aina hii ya vazi huvaliwa shingoni wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu katika Jimbo Kuu na majimbo ya Kanda yake, ila Papa huvaa duniani kote kuonyesha hadhi yake kama Mchungaji Mkuu wa kundi lote la Kristo kadiri ya imani ya Kanisa Katoliki.
    .
  • Розваги

КОМЕНТАРІ • 7