KUMNGOJEA BWANA - PASTOR SUNBELLA KYANDO

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 8 вер 2024
  • Haukuzaliwa kwenye familia uliyomo kwa bahati mbaya, Mungu aliamua iwe hivyo ili aje akutumie kuvunja laana za kwenu si tu kwa ajili yako, ila kwa ajili ya familia na kizazi chako,
    Isaka alitaka kuondoka Kanaan kwenda Misri kwa sababu ya njaa, asijue Mungu aliruhusu azaliwe mahali pale kwa ajili ya kuja kumtumia kipindi kile cha njaa.
    Kuna wakati adui anacheza na mazingira kukandamiza mbegu na uwezo ulioko ndani yako. Lakini kama Mungu alifanya kwa Isaka katika mazingira magumu kama yale hata sisi tutafikishwa kwenye hizo hatima zetu kwa msaada wake.
    Hata kama unaona unapitia njaa, kama ndani yako unaona kuvumilia basi usitafute "shortcut" vumilia na kuna jambo Mungu ataliachilia kwenye maisha yako.
    Adui akikupiga au akikuwinda anakua anawinda ulichobeba, na anajua akikukosa ukafanikiwa, anakukosa wewe na vivilivyo viunoni mwako(ulivyobeba). Watu wengi wanajua mbegu ambayo Mungu ameweka ndani yao, lakini watu wengi pia hawawezi kuona hiyo mbegu iki-manifest na wakijiangalia wanajijua wao ni nani.
    Kama kuna vitu baba zetu hawakuviweka sawa, basi Sisi tupo kwa ajili hiyo!
    Mungu ametupa upako, lakini kwa upande mwingine wapo watu wanapaswa kuwa na hela ili kazi ya Mungu iweze kwenda.
    Vita unayopitia sio yako ni kwa sababu ya kitu umebeba na adui analijua hilo kuliko wewe ulivyo|unavyojijua. Anapambana na destiny yako, hana shida na wewe ana shida na vilivyoko ndani yako. Anajitahidi kuvifunika, kukuhamisha focus lakini sio wewe ni kwasababu ya kile ulichokibeba.
    Usijidharau, kuna watu kuokoka kwao wanasubiri "manifestation" ya fedha zako, ukiwa na pesa kuna mikutano itafanyika na watu wataokoka!
    Kilichoko ndani yako usikichukulie kirahisi, kama ni mfanya biashara kaa magoti pa Bwana, kwenye hilo eneo kipo kilele ambapo ndipo Mungu atakuketisha.
    Kuna sehemu Mungu anataka tukae kama kanisa, poverty is not our portion.
    #PastorSunbella#KumngojeaBwana

КОМЕНТАРІ • 32