Salama Na ZITTO SE6 EP05 FULL SHOW |MWANDIGA'S VERY OWN PART 1| SendTip MPESA LIPA NO 5578460
Вставка
- Опубліковано 6 лют 2025
- #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
MWANDIGA’S VERY OWN.
Rafiki yangu na Kaka yangu , mpinzani wangu na mwalimu wangu Ndugu Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe ni mtoto na rafiki wa karibu sana wa Marehemu Hajjat Shida Salum Mohammed. Asili yake ni Kigoma kutoka kwenye Kijiji cha Mwandiga, huko ndiko aliko zaliwa na kupata elimu yake ya msingi na sekondari kabla ya kwenda Kibohehe, Galanos na Tosamanganga. Zitto hakusoma kwenye shule zinazomilikiwa na watu binafsi au taasisi maalum kama ambavyo watoto wake Wiza, Josina na Alaa wanavyopata elimu zao kwa sasa, na pengine hii ndo imemsaidia kumjenga kabisa na kuanzisha mapambano yake ya kutaka Tanzania yenye mabadiliko na bora kwaajili ya watoto wake na wetu na kwa vizazi vijavyo pia.
Mtaani huitwa ‘mtoto wa Mama’ (ingawa sote ni watoto wa Mama), hii hutokana na ukaribu ambao mtoto wa kiume anakua nao na Mama yake, haikua tofauti kwa rafiki yangu Z. Ingawa mwenyewe Ameniambia ukaribu wao ulikua ni kama wa mtu na mdogo wake zaidi kuliko wa mtu na Mama yake. Bi Shida (Mwenyezi Mungu Amrehemu) ndiye alikua mwalimu wake, amejifunza mengi kutoka kwake yanayohusu Uongozi na Siasa. Mpaka Mama yake anafariki alikua ndo Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Viungo cha hapa Tanzania.
Kama nikiendelea kukuelezea historia yake ambayo tumeizungumzia kwa kiasi kirefu kwenye maongezi yetu haya basi nitakua kama nakukosesha utamu wa kusikia kutoka kwenye mdomo wake mwenyewe, na mimi na wewe tunajua kama utamu zaidi wa simulizi hii itaniga zzaidi kama utaiskia kutoka kwa mhusika Mkuu.
Ilikua ki mtihani kidogo kuweza kupata nafasi hii maana Z ni mtu wa mambo mengi ingawa sasa siye tena Mbunge wa Kigoma, ila pengine sasa ndo anapata nafasi ya kufanya mambo yake mengi ya binafsi na ki Chama kwahiyo kutulia sehemu moja inakua ngumu kidogo. Ila tuliweza kugonganisha tarehe zetu na kupata nafasi ya sit down hii nzuri kabisa kwaajili yako na yangu.
Humu tuliongea kuhusu asili yake, Mama yake, kazi yake, elimu, uongozi, uzazi, mapenzi yake kwenye kujisomea na kujifunza, michezo, muziki na burudani, inspiration zake za ki maisha na uongozi na mambo mengine mengi.Na kwa kiasi kikubwa nili enjoy na kuyapenda sana.
Nikutakia utizamaji na usikilizaji mwema wa maongezi haya.
Until next time…
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahs...
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm
ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru
GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
Audiomack Link bit.ly/YahSton...
UA-cam Link bit.ly/UA-camS...
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz