Salama Na LAMATA SE6 EP 04 FULL SHOW | WATASWIRA PART 2| SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 6 лют 2022
  • #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
    WA TASWIRA
    Kupitia maongezi yangu haya na Bi Leah Richard Mwendamseke huyu ambaye tunamfahamu kama Lamata ndo niliamini kwamba si kila umsikiae akiongea kwa sauti ya juu wakati yuko kazini kwake basi anaweza kuja kwenye meza ya Salama Na pia akaongea kama ambavyo anaongea anapokua kwenye comfort zone yake. Nayasema haya kwasababu wakati tunaandaa kipindi hiki ndo niligundua Lamata ni muoga au ni mtu asopenda kuwa mbele ya kamera kiasi gani!
    Binafsi sina mazoea naye ya hivyo zaidi ya kuifahamu kazi yake ambayo inaongea yenyewe. Tunafahamiana kupitia rafiki wa rafiki ila hatujawahi kukaa chini tukatia story na kufahamiana kama ambayo tulifanya kwenye maongezi haya. Namshkuru kwa kutafuta wasaa katika ratiba yake inayombana haswa lakini alihakikisha anatafuta wasaa ili aje akae nasi na tuongee kuhusu yeye na fikira zake kwenye mambo mengi.
    Mzaliwa wa Mbeya na ambaye kipaji chake cha uandishi kilianza kuonekana alfajiri kabisa, Lamata anasema Mama yake mzazi ndo shabiki nambari moja wa kazi yake. Kwenye dunia hii na maisha ambayo wengi wetu tumepitia ni nadra sana kumkuta mzazi anaamini kwenye kipaji cha mwanae na kumpa moyo wa kutaka akiendeleze. Mama yake alikua anamsifia uandishi wake na kutaka amalizie zile aliziandika ili yeye ndo awe wa kwanza kuzisoma. Au wakiwa wamekaa wanaangalia tamthilia au sinema atahakikisha anamkiliza mwanawe juu ya maoni yake na hata wakati mwengine kumuuliza kama ingekua yeye angemaliza hiyo sinema au tamthilia kwa angle ipi.
    Story kadhaa alinipa juu ya safari yake hiyo, shuleni nako alikua burudani pia kwa baadhi ya waalimu na wanafunzi wenzake. Kitu ambacho kilikua kinafanya mambo yake yaende ki ulaini kabisa.
    Kwa sasa tamthilia zake anazoandika ndo moja ya vivutio vikubwa kwenye DSTV kwa upande wa channel za ukanda wetu huu, ila tukumbuke pia alianzia kwenye filamu kabla ya kujikita rasmi kwenye tamthilia. Safari yake haikua tu rahisi. Alinihadithia jinsi alivyosaka upenyo na kuhangaika huku na kule ilimradi tu apate mtu wa kumuingiza ndani ITV na aweze KUSIKILIZWA na yoyote anayehusika. Tukumbuke pia ilibidi awe muingizaji wakati flani na hiyo pia ilikua ni moja ya njia za yeye kutaka kupata upenyo, kuwa mbele ya camera si vitu pendwa vya Lamata KABISA ila ilibidi afanye hivyo ili mambo yake yakae sawa.
    Haya maongezi yetu yalijaa ukweli na uwazi juu ya karibu kila kitu kinachohusu maisha yake. Marafiki pia tuliwazungumzia. Ukaribu wake na baadhi ya waigizaji anaofanya nao kazi, jinsi anavyotoa nafasi kwa wenye vipaji na vile vile tuliongelea suala la ajira na ushawishi kwenye kiwanda cha filamu na burudani hapa nyumbani. Yangu matumaini utapata mawili matatu hapa ya kuwezesha boti yako iende unapotaka.
    Kwa hilo, nakutakia kheri.
    Love,
    Salama.
    Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
    SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
    Listen our Podcast on
    Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
    GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
    Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
    ‪UA-cam Link bit.ly/UA-camSalamaNa
    Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown
    Channel Administered by Slide Digital
    Instagram: slidedigitaltz
  • Розваги

КОМЕНТАРІ • 28

  • @LilacAlm
    @LilacAlm 2 роки тому +6

    Big up Lamata,keep up the good work👍,Da Salama na wewe mungu akubarik kwa kazi yako nzuri🙏,not only that you sit down and talk to different artist but you are giving them a platform and exposure.
    Keep doing what you're doing👊

  • @prettypretty9745
    @prettypretty9745 2 роки тому +1

    Hongera zako lamata umenifanya kwa Mara nyengineee niangalieee bongo movie, wallahy kila siku nikitoka mfano wa maisha halisi ya bongo naiona kigodoroooo na sikujua Kama wewe ndio ulioiandika wewe ni hodari mamaaaaaaa

  • @petermaro9852
    @petermaro9852 2 роки тому +4

    Tuwekee Salama na T.I.D full episode bn.

  • @vummymeela1091
    @vummymeela1091 2 роки тому +3

    Doing well, Lamanta✔️💪 naipenda Sana Jua kali

  • @Yvonnerukundo9250
    @Yvonnerukundo9250 Рік тому

    Lamata I love you so much unani inspire kinyama yani, wewe ni super woman

  • @farajampogolo9840
    @farajampogolo9840 Рік тому

    Nawakubali sana nyie madada,ni watu ninaowapenda sanaaa,big up Salama,big up Lamata.

  • @hadijajumanne5493
    @hadijajumanne5493 2 роки тому +3

    Tunakupataje lamata jamani

  • @ziyandamhlana8776
    @ziyandamhlana8776 2 роки тому

    Ñic interview big up

  • @binamubinamu1151
    @binamubinamu1151 2 роки тому

    Ahsante sana

  • @mamunote3507
    @mamunote3507 2 роки тому +1

    Thanks

  • @user-xc3xt4jq6i
    @user-xc3xt4jq6i 5 місяців тому

    Good

  • @adamsilumbe8356
    @adamsilumbe8356 2 роки тому +2

    Ningependa umuulize kuhusu yule mnigeria aliweza vipi kumualika

  • @mussambaga5832
    @mussambaga5832 2 роки тому

    Aunty weka ya togolani🙏

  • @reinatave3022
    @reinatave3022 Рік тому

    Hata mim nikiona Jina kwenye movie limeandikwa leah mwendamseke na nunua kwakwer huyu dada anajua aisee...!!!

  • @sassboy9360
    @sassboy9360 2 роки тому +1

    Swali la mahusiano limemtoa kwenye mood na salama kaliona kaona amtoe uko ...

  • @jumakhang4383
    @jumakhang4383 2 роки тому

    🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿👏👏

  • @asmahussein2779
    @asmahussein2779 2 роки тому +1

    ILove u booth..

  • @ejoym9165
    @ejoym9165 Рік тому

    Kunyimwa uwanja wa ndege ni aibu

  • @zenarashid930
    @zenarashid930 2 роки тому

    Tuletee Dr. Kumbuka.

  • @zaynabmwanjovu8277
    @zaynabmwanjovu8277 2 роки тому +2

    Na unaweza dada kwa bongo hakuna kama wew huo ndo ukwel...sema unaongea harakaharaka sana......

  • @stevenmakalla
    @stevenmakalla Рік тому

    VFX location si zinatengenezwa... wainvest kwenye CGI VFX.. Green & Blue screen

    • @chamballaally8767
      @chamballaally8767 28 днів тому

      Nilikuwa naitafuta hii comment…sidhani km wapo Bongo wataalamu wa hiyo fani ngoja niisomee nije kufungua kampuni yangu