KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA MORNING GLORY: THE SCHOOL OF HEALING: 16/ 07/ 2024

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 21 сер 2024
  • KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA MORNING GLORY: THE SCHOOL OF HEALING: 16/ 07/ 2024
    SEMINA YA NENO LA MUNGU:
    MADA:
    "HOFU YA MABADILIKO"
    (FEAR OF CHANGE)
    SOMO LA LEO:
    "BARAKA YA KUTOKA"
    & NIDHAMU YA MFUMO WA KIMAONO.
    (VISION CONNECTIONS & NETWORKING DISCIPLINE)
    Mwanzo 30 : 22 43
    Mathayo 4 : 4
    NENO KUU:
    "UTABARIKIWA UINGIAPO, UTABARIKIWA NA UTOKAPO"
    KUMBUKUMBU LA
    TORATI 28 : 6
    &
    Yohana 12 : 24
    24 Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.
    MAANDIKO YA LEO:
    Mwanzo 30 : 22 43
    22 Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo.
    23 Akapata mimba, akazaa mwana, akasema, Mungu ameondoa aibu yangu.
    24 Akamwita jina lake Yusufu, akisema, Bwana aniongeze mwana mwingine.
    25 Ikawa Raheli alipomzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, Nipe ruhusa niende kwetu, na kwenye nchi yangu.
    26 Nipe wake zangu na watoto wangu, niliokutumikia, niende zangu, maana umejua utumishi wangu niliokutumikia.
    27 Labani akamwambia, Iwapo nimeona fadhili machoni pako, kaa, maana nimetambua ya kwamba Bwana amenibariki kwa ajili yako.
    28 Akasema, Sema mshahara wako utakao, nami nitatoa.
    29 Akamwambia, Umejua jinsi nilivyokutumikia, na jinsi wanyama wako walivyokuwa kwangu.
    30 Maana mali yako ilikuwa haba kabla sijaja, nayo imezidi kuwa nyingi, Bwana akakubariki kila nilikokwenda. Basi sasa, nitaangalia lini mambo ya nyumba yangu mwenyewe?
    31 Akamwuliza, Nikupe nini? Yakobo akasema, Usinipe kitu; ukinifanyia neno hili, nitalisha wanyama wako tena na kuwalinda.
    32 Nitapita katika wanyama wako wote leo, na kutoa huko kila mnyama aliye na madoadoa na marakaraka, na kila mnyama mweusi katika hao kondoo, na aliye na marakaraka na madoadoa katika mbuzi; nao watakuwa mshahara wangu.
    33 Na haki yangu itanishuhudia katika siku zijazo, utakapokuja kwa habari ya mshahara wangu ulioko kwako. Kila asiye madoadoa au marakaraka katika mbuzi, au asiye mweusi katika kondoo, akionekana kwangu, itahesabiwa kuwa ameibiwa.
    34 Labani akasema, Tazama, na iwe hivi kama usemavyo.
    35 Basi akatoa siku ile mbuzi waume walio na milia na madoadoa, na mbuzi wake walio na madoadoa na marakaraka, kila aliye na doa jeupe, na kondoo wote waliokuwa weusi, akawatia mikononi mwa wanawe.
    36 Akajitenga na Yakobo mwendo wa siku tatu; naye Yakobo akachunga wanyama wa Labani waliosalia.
    37 Yakobo akatwaa fito za mlubna mbichi, na mlozi, na mwaramoni, akazibambua maganda, mistari myeupe ionekane ndani ya hizo fito.
    38 Akazisimamisha fito hizo alizozibambua katika mabirika ya kunyweshea maji, pale walipokuja wanyama wanywe; wakachukua mimba walipokuja kunywa.
    39 Wanyama wakapata mimba mbele ya hizo fito, wakazaa wanyama walio na milia, na madoadoa, na marakaraka.
    40 Na Yakobo akawatenga wana-kondoo, akazielekeza nyuso za makundi zielekee wale waliokuwa na milia, na kila aliyekuwa mweusi katika wanyama wa Labani. Akaweka kando wanyama wake mwenyewe, wala hakuwachanganya pamoja na wanyama wa Labani.
    41 Ikawa kila walipopata mimba wanyama wenye nguvu, Yakobo akaziweka zile fito mbele ya macho ya hao wanyama katika mabirika ili kwamba wachukue mimba kati ya zile fito,
    42 lakini wanyama walipodhoofika hakuziweka zile fito. Basi wale dhaifu walikuwa wa Labani, na wenye nguvu walikuwa wa Yakobo.
    43 Kwa hiyo mtu huyo akazidi mno, akawa na wanyama wengi, na vijakazi, na watumwa, na ngamia, na punda.
    Mathayo 4 : 4
    4 Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
    Mhubiri: Rev. Dr. Eliona Kimaro
    Kwa maombi na ushauri :
    Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
    Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
    Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
    Simu: +255 713 553 443
    UA-cam: Kijitonyama Lutheran church
    Barua Pepe: Kijitonyamalutheran@gmail.com

КОМЕНТАРІ • 29

  • @lizpallangyo8057
    @lizpallangyo8057 Місяць тому +1

    Amen baba mchungaji barikiwa mno mno mno umenifanye nipate nguvu mpya hakika wakinyamaza mawe yatainuka kupiga kelele

  • @frankwinani4458
    @frankwinani4458 22 дні тому

    Hakika nabarikiwa sana na Mahubiri yako pasta, Mungu alie mkuu akatufikishe nyumbani salama,Madini yaliokwenye kichwa chako ikawaongoe hata walio mbali zaidi AMEN

  • @Alicemdee
    @Alicemdee Місяць тому

    Ameen ameen babaa MUNGU akubariki 🙏

  • @lizpallangyo8057
    @lizpallangyo8057 Місяць тому

    Ameeen watanitangazia heshima kwa Jina la Yesu

  • @lizpallangyo8057
    @lizpallangyo8057 Місяць тому

    Ameeen hakika mawe yatasema na kupiga kelele juu yangu

  • @marianchamba3898
    @marianchamba3898 Місяць тому

    Amen

  • @Gladys-oh2wj
    @Gladys-oh2wj Місяць тому

    Amen 🙏🙏🙏

  • @ritapiusnicolaus7068
    @ritapiusnicolaus7068 Місяць тому

    Amen 🙏

  • @AliceHatibu
    @AliceHatibu Місяць тому

    Amen 🙏 🙏 🙏

  • @dicksonkunambi8615
    @dicksonkunambi8615 Місяць тому

    Amen Amen Baba Mchungaji, leo umenigusa na maombi haya.
    Hakika siku chache zilizopita, nilichagua kubaki kimfumo, heshima yangu na kuangalia pesa.
    Mungu huyu ni Mkubwa - nimemaliza masomo yangu na kupata Masters yangu.
    Lihimidiwe jina lake Mungu kama siku zile za Moldekai

  • @esterjohn1332
    @esterjohn1332 Місяць тому

    Amen in Jesus name.

  • @wolterkimaro1221
    @wolterkimaro1221 Місяць тому

    Aminaaa!!

  • @user-gx4mt7my3d
    @user-gx4mt7my3d Місяць тому

    Mawe na yapige kelele amina

  • @giftmasharo4018
    @giftmasharo4018 Місяць тому

    👏🏻👏🏻👏🏻👏🏻

  • @janem5805
    @janem5805 Місяць тому

    Amen! I received and declare miracles in Jesus Christ

  • @berthamaega-nt7dr
    @berthamaega-nt7dr Місяць тому

    Ameeen eehh Mungu nisaidie macho yangu ya Rohoni yaone ili nielewe mbinu za adui

  • @giftmasharo4018
    @giftmasharo4018 Місяць тому

    Ameen Ameen Ameen IN Jesus Name, I CONNECT TO COLLECT IN JESUS NAME AMEN

  • @goodluckfungo3511
    @goodluckfungo3511 Місяць тому

    Ameen asante kwa huduma na Mungu akubariki...

  • @reginajohnmaghisa322
    @reginajohnmaghisa322 Місяць тому

    Amen, Barikiwa sana Mtumishi wa Mungu 🙏

  • @user-ki7bs7kn6l
    @user-ki7bs7kn6l Місяць тому

    AMEN AMEN MCHUNGAJI WASEMEA ROHONI MWANGU

  • @monikamadahamasanja2868
    @monikamadahamasanja2868 Місяць тому

    Ameen Mtumishi Wa Mungu ubarikiwe Sana

  • @giftmasharo4018
    @giftmasharo4018 Місяць тому

    Amen!! Mungu nipe akili njema na utulivu wa ndani Gifty niweze kubaki kwenye mfumo

  • @magetemu
    @magetemu Місяць тому

    Mawe yatasema.

  • @user-gt9ns5ej5t
    @user-gt9ns5ej5t Місяць тому +1

    Mawe yatapiga kelele

  • @hemedmsella6496
    @hemedmsella6496 Місяць тому

    Eimen

  • @user-gx4mt7my3d
    @user-gx4mt7my3d Місяць тому

    Tuliyo zurumiwa na kusigiziwa kesi za uhujumu uchumu na kufirisiwa mali na fedha mawe yapige kelele

  • @NasraSaidi-dq7fh
    @NasraSaidi-dq7fh Місяць тому

    Amen 🙏

  • @zepinashatibu5149
    @zepinashatibu5149 Місяць тому +1

    Amen