Salama Na Profesa ep 55 | MAPINDUZI HALISI Part 1

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 26 лют 2021
  • #SalamaNa #SendTip Through MPESA #0762797291
    Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
    SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
    Listen our Podcast on
    Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
    GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
    Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
    ‪UA-cam Link bit.ly/UA-camSalamaNa
    Joseph Haule ni mmoja ya binadamu ambao nawapenda sana kwenye dunia hii na huwezi kuamini hata yeye anajiskia hivyo juu yangu, nikiwa naye vibe na story zetu huwa zinabamba sana. Kuanzia story za maisha, muziki, historia na hata kuwacheka watu wakati mwengine, ndo zetu.
    Nakumbuka baada ya kumsaka asubuhi moja hivi na yeye kutodaka simu (ambayo baadae aliniambia alimpigia Sallam simu akidhani yeye ndo aliyempigia badala ya Salama), hayo maelezo niliyapata baada ya yeye kukutana na tweet ya kulalamika kwangu juu ya yeye kutorudisha simu yangu.
    Tumetoka mbali kiasi chetu, mkubwa kwangu kwa miaka 7 na heshima yangu kwake si ya kupima kwa kisoda. Unaweza ukawa unajiuliza sasa mbona hatukuoni naye na mambo kama hayo (hiyo mambo kama hayo nimeongea kama yeye) well... Urafiki wetu si ule wa kugandana kama kifungo na shati, au kichwa na nywele au kucha na kidole ndugu yangu, urafiki wetu ni ule wa kuendeleza pale tulipoishia na kuangalia na kwa mbali juu ya kitu mwenzio anafanya huku tukitakiana Kheri.
    Nakumbuka vizuri mara yangu ya kwanza kukutana na Profesa, enzi za Times FM kule mjini, kipindi hiko mimi ndo nimepata ajira yangu ya kwanza na yeye ndo alikua Msanii wa mooto sana, hard blasters wako na moto wa tipa, na nani ndo kiongozi wa nyika? Nigga Jay. Urafiki wetu ulianzia hapo, na mpaka leo tunamshkuru Mungu.
    Ukuaji wake hasa ndo nia na madhumuni ya mimi na wenzangu kuona Prof atatufaa sana kumalizia episode yetu ya 55 na ngwe ya kwanza ya kazi yetu hii. Zaidi kama tujuavyo, hakuna msanii hata mmoja ambaye hajawahi kuvutiwa na hustle zake za kuanzia juzi mpaka leo hapa tulipo. Na hiyo inajumuisha kipaji na UANDISHI ulosimamia kucha. Jay tunakuzimia indeed!
    So wapi haya yoooote yalianzia? Mpaka sasa Mbunge nje ya Bunge? Well... Hata mbuyu ulianza kama mchicha, humu Prof anazungumza na sisi juu ya masuala ya familia na safari alizopitia, mikoa aliyowahi kuishi, mahusiano kati ya Marehemu Baba yake na Mama yake, wadogo zake, Kaka na Dada zake, elimu yake, experience yake mjengoni, nini maana ya baadhi ya vitu na mambo aliyowahi kuyapitia. Pia tuliongelea kupatikana kwa binti yake pekee Lisa, jinsi alivyokutana na mke wake, kipaji chake, kwanini Mikumi na kwa mbaaali uchaguzi mkuu uliopita.
    Profesa ni mwana flani ivi ambaye toka zamani ramani ya mambo yake yako mfuko wa nyuma, kupotea au kupoteza malengo si jambo rahisi kwake, labda kuchelewa tu kwa hayo aloyapanga. Na hivi sasa kwa miaka mitano hii ambayo yuko nje ya bunge, pengine ndo wakati wetu wa kufaidi kipaji chake na kuokota mawili matatu kwa wale wote tunao muangalia na kupenda nyenendo zake.
    Tafadhali enjoy.
    Love,
    Salama.
    Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown
    Channel Administered by Slide Digital
    Instagram: slidedigitaltz
  • Розваги

КОМЕНТАРІ • 164

  • @samwelkavwanga4491
    @samwelkavwanga4491 3 роки тому +16

    Prof. Ajengewe mnara Ni msanii ambye kautoa mbali sana huu mziki. Kipaji chake nikubwa mno👏👏

  • @ronniebertin3563
    @ronniebertin3563 11 місяців тому +1

    Profesa j nakusiliza machozi yanatoka good memory

  • @rodrickmataba8999
    @rodrickmataba8999 3 роки тому +16

    Hapa natamani kumsikiliza Nature, tujue ilikuaje enzi zile za Tmk wanaume mpaka Tmk wanaume halisi mpaka ile ishu ya kufukuzwa studio kisa amevaa ndala... #sendtip #salamanaNature

  • @charlesmichael5921
    @charlesmichael5921 3 роки тому +9

    Leo mapema tu...likes kwa wote walioielewa hii interview

  • @fubanjenjele521
    @fubanjenjele521 3 роки тому +5

    Daaaaaaa!!! Jay anaongea facts, yupo real, Hana maringo, Jay ananiinspire sn

  • @andreamwamewa749
    @andreamwamewa749 3 роки тому +14

    Mbunge nje ya bunge the heavy weight MC I preciate brother💪.

  • @fiziparadise7808
    @fiziparadise7808 3 роки тому +14

    Prof Jay - the most credible, wise and consistent bongo musician of all times.
    Fid-Q - the most intelligent bongo musician (and possibly with the highest IQ) and the best rapper of all times.
    P-Funk Majani & Mater-J - the best bongo producers of all times.
    TMK wanaume & East Cost - the best bongo groups of all times.
    Respect from Congo 🇨🇩 tunapendaka music yenu sana huku East of Congo.

  • @d79d26
    @d79d26 3 роки тому +12

    I'm first view salama tuletee na mtu mzima P funk majani please 👍

  • @danielhaule155
    @danielhaule155 3 роки тому +8

    Mwana muziki Wa hiphop ninaekukubali tangu nianze kukusikia Mpaka Leo,u deserve that name professor🔥🔥🔥

    • @leonidasifrance8903
      @leonidasifrance8903 3 роки тому +1

      Professor jay naweza msaidia ndani ya cku 24 aweze kipungua uzito wake na aweze kumantain hiyo 0789650225

  • @switbertchenya6362
    @switbertchenya6362 3 роки тому +4

    Salama bonge la mwana habari. Good IQ.

  • @kingbidder
    @kingbidder 2 роки тому +1

    Salama we chupi sanaaa.. Ume nufuraisha sana.. Eti piza ina pikwaje.. J na yeye dah inapigwa PAH.. i love you both.. St8 from UK🇬🇧

  • @nz6181
    @nz6181 3 роки тому +5

    Nakufagilia Profesor J. "Your legend of Bongo Flava"
    Salama 👌👌
    @🇬🇧🇬🇧🇬🇧🇬🇧

  • @beshuuambarali4960
    @beshuuambarali4960 3 роки тому +4

    Mbna Raha sana..prfs j..hauzeeki toka nakua hadi leo upo vzri.maisha maref kwko

  • @konceptualagency4837
    @konceptualagency4837 3 роки тому +2

    Magufuli hana ubinadamu na huruma alikua nao Kikwete Allah ambariki yule mzee

  • @mohahmed6423
    @mohahmed6423 3 роки тому +4

    First Tanzanian artists i known about, This is the Heavyweight MC boys! This guy is a Legendary 💪💪💪

  • @lotinyumba1573
    @lotinyumba1573 3 роки тому +4

    Mgodi unaotembea, my favorite rapa in tanzania

  • @rasjoe9948
    @rasjoe9948 3 роки тому +3

    Profesa ni legend much love from kenya 🇰🇪🇰🇪🇰🇪

  • @zulfikakalumba1977
    @zulfikakalumba1977 3 роки тому +2

    Tunawakubali sana wanetu wa mtaa ila mlitusahau mlipofika mjengo hadi mkadiriki kusema mmepata wana wengine wakina Chenge... Ilibidi mtuoneshe bado mpo na sisi wanenu wakina Nature wakina Afande wakina Mkoloni, zaidi mliwabwaga wanenu.
    Wala tusiwasifu sana mlizingua kwa upande flani halafu Pro upo vizuri kwenye speech zako hapo ila unaiweka mbele sana hali yakujisifu...

  • @binbaya923
    @binbaya923 3 роки тому +2

    Hongera Dada Salama kumleta huyu Mzee. Respect Bro

  • @innocentmushi1550
    @innocentmushi1550 3 роки тому +5

    Salama ni mnoma. Jinsi alivyolichomeka hilo suala la pizza🙌

  • @erickmweta8215
    @erickmweta8215 3 роки тому +3

    MP nje ya P
    The real MC El Prof

  • @trumpetoflife7312
    @trumpetoflife7312 3 роки тому +2

    Nimekubali sana hii!
    Salama bigup km zote...
    Prof akili kubwa ( sound mind)

  • @rubenmkilima4681
    @rubenmkilima4681 3 роки тому +4

    Dream always come true 🔥🔥🔥🔥 nilikuwa natamani sanaaa hii kitu... Salama na profesa Jay... Congratulations sister salama

  • @ramzy5280
    @ramzy5280 3 роки тому +4

    Tuletee Baba Levo tena siku nyingi hatucheki 😂😂

  • @gnmbi
    @gnmbi 3 роки тому +2

    Huwa na enjoy Sana interview za professor Jay

  • @fadhiliswidhun9779
    @fadhiliswidhun9779 3 роки тому +1

    Hk salama n bonge la kpnd lnatufunzaa meng kwel kwel asante.

  • @kowech2626
    @kowech2626 2 роки тому +1

    Nimecheka sana. He is a legend.

  • @r.kassimtoutautre3432
    @r.kassimtoutautre3432 3 роки тому +1

    Kitu bomba 🇧🇮Who lives 🇹🇷

  • @samwelyarkado552
    @samwelyarkado552 3 роки тому

    Sart sana PJ hauna majivno! Bomba za Maziwwa, nchinzimaaaaaa, safiiii!!

  • @musaeliad4744
    @musaeliad4744 3 роки тому +2

    Salama ur too genius real appriciate

  • @corebaraka7823
    @corebaraka7823 2 роки тому

    respect profesa jay may the lord bless you keep you safe and give you peace

  • @gerrarddanken5168
    @gerrarddanken5168 3 роки тому +1

    Good Pon't kuhusu Lunya na con boy waige hvo anaongea mzee J mnyama

  • @mashakashobo979
    @mashakashobo979 3 роки тому +2

    Prof nakukubali Sana bro,,nakumbuka miaka ile unatangaza majiko ya ges umevalishwa nguo za kike 😁😁😁😁😁

    • @mugadimon3563
      @mugadimon3563 3 роки тому

      😁😁😁😁😁 nakumbuka hilo tangazo ni la siku nyingi sana

  • @zefaniachowe4420
    @zefaniachowe4420 3 роки тому +15

    Prof. Jay is a good story teller. Big up bro.

  • @rickomba
    @rickomba 3 роки тому +2

    Salama is a superb interviewer.

  • @musahmichael3480
    @musahmichael3480 3 роки тому +2

    aliye vunja kitanda kama mm like comments

  • @starsaver763
    @starsaver763 3 роки тому +2

    Salama nakupenda bure

  • @safiyatheonlything7848
    @safiyatheonlything7848 3 роки тому

    Nice interview nakubali sana professor j

  • @mihambofilm
    @mihambofilm Рік тому +1

    Prof Jize is My role model Ever🔥

  • @mariammbande7697
    @mariammbande7697 3 роки тому +6

    Salama una kazi kubwa sana kumsikiliza mtu dakika zote na una get na maswali on it 😁😁 mi ningekuwa nasinzia yaani😎

  • @mohamedothman9769
    @mohamedothman9769 3 роки тому +2

    Salama naomba umlete Pfunk na Chidi Benzi, itakuwa hot

  • @vidovidal1
    @vidovidal1 3 роки тому +1

    Alie skia lutengano high schoool mbeya tukuyu twende sawaa

  • @hunterevents9132
    @hunterevents9132 3 роки тому

    Salama namkubali sana kwenye kazi zake. As a reminder, Salama naomba sana ktk list yako ya ratiba, umuweke Afande Sele msanii mwenye busara sana pia kama hao wakina Prof n.k...

  • @abdulazizimohamed3093
    @abdulazizimohamed3093 3 роки тому +1

    Mbunge nje ya bunge umeeleweka sana

  • @tulinagwembangula8976
    @tulinagwembangula8976 3 роки тому +1

    Salama
    Mbona kimya sana. Sipata Ep nyingine

  • @kelvinokelo7992
    @kelvinokelo7992 3 роки тому +1

    Wamitulinga💥💥

  • @jastonelazaro5944
    @jastonelazaro5944 3 роки тому +1

    Nmekukubali sana professor kwa kusema ukweli kuhusu uchaguz wa 2020

  • @hopeobeth9806
    @hopeobeth9806 3 роки тому +2

    Sema kitanda baba shikamoo

  • @daudimatelot9339
    @daudimatelot9339 3 роки тому +2

    Professor " Bado sina chochote unataka nisote unafaidika nn ukiniona sipo popote kiumbe mwenye akili butu na roho za kutu "

  • @sadickallykingengena4034
    @sadickallykingengena4034 3 роки тому +1

    Big love broo

  • @nellysosteness9898
    @nellysosteness9898 7 місяців тому

    Nzuri sana

  • @mariamkaaya939
    @mariamkaaya939 3 роки тому +2

    Majinaa ya vyakula. 🤣🤣🤣

  • @erickmachua8829
    @erickmachua8829 3 роки тому +1

    Legendary

  • @Fgldesigns
    @Fgldesigns 3 роки тому +2

    Naombeni sapoti yenu karibuni kusubscrine kwenye channel yangu kutazama video za ubunifu wa majengo mbalimbali.

  • @yusufumulumba5242
    @yusufumulumba5242 3 роки тому +1

    Pendeza muzungu 💕

  • @swahiliwithZita
    @swahiliwithZita 3 роки тому

    jamani "nikusaidiaje" days! I love the song mpaka leo

  • @owlbig
    @owlbig 3 роки тому +1

    I like this guy 🇧🇮❤️

  • @salumjumah5648
    @salumjumah5648 2 роки тому

    Interview kubwa sana hii 2021 prof jizeeeee

  • @mutwalesylvie7443
    @mutwalesylvie7443 3 роки тому

    Nice sana

  • @_ayuma
    @_ayuma 3 роки тому +4

    A LIVING LEGEND!!!!

  • @nginirasaire5876
    @nginirasaire5876 2 роки тому +1

    Salama will never live out a question you wanted an answer too... I guarantee

  • @richardcastromzena5136
    @richardcastromzena5136 3 роки тому +1

    Nimejifunza kuna watu hukutana kabla ya wao kuwa this big

  • @bensakibu8394
    @bensakibu8394 Рік тому

    Keep it up salama.

  • @abdulazizimohamed3093
    @abdulazizimohamed3093 3 роки тому +2

    Salama acha kumchanganya mheshimiwa na kupika piza wapi na wapi

  • @HansBwoi
    @HansBwoi 3 роки тому +3

    Mlete Jay Moe

  • @leblue4768
    @leblue4768 3 роки тому

    Tafadhali Salam tunatamani utuletee chid benz

  • @saumusalimuhassan2499
    @saumusalimuhassan2499 2 роки тому

    Allah akupe shifaa brother, una comedy ndani yako Pf jz

  • @mwanzashinyanga8060
    @mwanzashinyanga8060 3 роки тому +1

    wewe ni genius

  • @andrewkubo4050
    @andrewkubo4050 3 роки тому +3

    Nimeipenda sana hii episode. Mbunge ana mambo mengi mazuri. Big up Salama kwa kazi nzuri. Alafu katika ile changia changia ningependa kukuona unakaa na Nikki Mbishi au One the Incredible.

    • @collethadavid9126
      @collethadavid9126 2 роки тому

      Hata mie nishamwambia aache utofauti One The Incredible na Nikki mbishi waje apa

  • @RONALDOTRUCKDRIVER
    @RONALDOTRUCKDRIVER 3 роки тому +2

    Brother 4 life jay

  • @husseinmaingo7116
    @husseinmaingo7116 3 роки тому +8

    Salama tunaomba tulete King Kong " Chid Benz"

  • @mohamedimwijuma1882
    @mohamedimwijuma1882 3 роки тому +2

    RIP DJ Omy ulinipa sapoti sana wakati naimba kaka

  • @khadijahali4837
    @khadijahali4837 3 роки тому +1

    Leo nmewahi na mm

  • @ijumaawikienda5435
    @ijumaawikienda5435 3 роки тому

    j buana very confident

  • @shabanbuchu2130
    @shabanbuchu2130 3 роки тому +4

    Na hio kilo lazima kitanda kivunjike

  • @PeterJohnRukiko
    @PeterJohnRukiko 3 роки тому +1

    G.O.A.T 👑🐐✊🏾✊🏾✊🏾💪🏽💪🏽💪🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🔥🔥🔥💯💯💯

  • @benhamza5649
    @benhamza5649 3 роки тому

    @Salama I’m not sure if you usually read comments however, will go ahead and drop it. Prof sounds like a real man/human who speaks from his heart regarding something his passionate about. He got lost into it. I like it, although this might not be the right place to speak that deep about MIKUMI ( apologies if misspelled) but it certainly the right time. If I’m not mistaken, @Salama , the face and expression recognition /psychological book you have been glancing on are being very helpful in terms of saving time on this emission. I love how you took him off course and derailed him from going even deeper into his feelings. If all things @Salama , you decided to come up with PIZZA cooking methods?🤣🤣🤣🤣. But anyway, he noticed and it worked. So it’s a win-win .

    • @gilbertkasikila5294
      @gilbertkasikila5294 7 місяців тому

      😂😂😂 niliona pia baada ya kuona prof anaongea kwa hisia na anaenda deep sana kwenye hiyo topic

  • @justinmmbando5386
    @justinmmbando5386 3 роки тому

    Ukiwa na kipaji utafurahia maisha yako milele na milele

    • @ilundafarm2798
      @ilundafarm2798 3 роки тому

      Hahaha jamaaa kaongea mambo ya siasa sana mpk salama kamuamisha mada

  • @samsonmaiko6089
    @samsonmaiko6089 2 роки тому

    Salama wejama itachukua muda Sana kupata mtu Kama wewe, unaisha na utamuwakoo.

  • @hamedabashir9
    @hamedabashir9 3 роки тому

    Ngoja nisikilize kwanza

  • @bish_daddiyao
    @bish_daddiyao 3 роки тому +2

    Just Love This Show:-

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 3 роки тому

    Prof. Jay 💥

  • @herrymadini4656
    @herrymadini4656 3 роки тому

    Professor jay babaaa..

  • @nicksoncharles8240
    @nicksoncharles8240 3 роки тому +1

    Tuleteee na unju@nikk mbish

  • @nyimbozakihehe3967
    @nyimbozakihehe3967 3 роки тому +2

    Eti Mpitimbi 😀😀😀😀😀

  • @napster2558
    @napster2558 3 роки тому

    Sooo BiG ❤

  • @adamrafiki5219
    @adamrafiki5219 3 роки тому +1

    Marufuku kukata tamaaa tulio skia hyo!* Like

  • @rukiachamani1101
    @rukiachamani1101 3 роки тому +2

    I love this interview.

  • @mrfashion1687
    @mrfashion1687 3 роки тому +4

    Next salama na Adam Mchomvu

  • @beckachonka5906
    @beckachonka5906 3 роки тому

    safi

  • @emmakiwaya4607
    @emmakiwaya4607 3 роки тому +1

    hapo mwenye scratch za mdomo nmeskiliza zaidi ya mara 5

  • @shabanimwambi4949
    @shabanimwambi4949 3 роки тому

    Salama show zako Zina na maswali ambayo Kila mtu hujikuta umemuulizia yaani Raha tupu

  • @prochesnorbert8720
    @prochesnorbert8720 3 роки тому +1

    Jamani Salama, Leo Jessica umemuweka wapi????

  • @mdathirumagayane688
    @mdathirumagayane688 3 роки тому +2

    Nakukubali sana mwamba,ndio mzee

  • @mwljohnray1725
    @mwljohnray1725 3 роки тому

    Salama niletee JB -Jacobo Steven

  • @jumamalilo749
    @jumamalilo749 3 роки тому +3

    Prof J

  • @hamedabashir9
    @hamedabashir9 3 роки тому +1

    1995wengine hatyujazaliwa😂🤣🤣🤣😅😅😅😅

  • @safiyatheonlything7848
    @safiyatheonlything7848 3 роки тому +1

    leo Jessica ayupo

  • @mmn7480
    @mmn7480 2 роки тому +1

    😂😂😂mkavunja kitanda

  • @exaudychatta6150
    @exaudychatta6150 3 роки тому +1

    2namuomba na chuma kingkong