Zembwela Afunguka Ukweli Wote Mpaka Kuacha Kazi East Africa | SALAMA NA ZEMBWELA PART 1

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 28 вер 2024
  • #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
    MSAFIRI HUFIKIRI
    Moja ya jambo ambalo nimejifunza kuhusu maisha na kufanikiwa ni KUTOKATA TAMAA wakati unatafuta ila kubwa kuliko ni wajibu wetu kutojiona tuko JUU zaidi ya wengine na kuamini kwamba pale ulipo hakuna siku ambayo utakuja KUTETEREKA. Katika makosa ambayo unaweza kuyafanya ni kuamini hilo jambo KUBWA.
    Hillary Daudi ni Kaka yangu na Rafiki yangu, mimi nilianza kwa kumuona yeye kwenye TV kabla sijakutana naye rasmi kwenye mwanzo kwa miaka ya 2013 kupitia Rafiki yangu mwengine aneyeitwa Mussa Hussein, Mussa na Zembwela ni washkaji ambao wali click tu mara ya kwanza walivyoonana na Mussa alipomsikia tu Zembwela aliona atamfaa sana kama atakua partner wake kwenye kile kipindi alichokua akifanya cha kuanzia saa tatu asubuhi pale EA Radio.
    Zembwela alikua mmoja wa waanzilishi wa kipindi cha vichekesho pale ITV akiwa na Rafiki yake Marehemu Max, na jambo ambalo mimi nilikua silijui ni kwamba Zembwela yeye ndiye aliyekua muandishi wa yale maigizo mafupi mafupi waliyokua wanafanya, na hilo swali nilimuuliza baada ya kusikia tetesi mtaani kwamba toka Max atangulie mbele ya haki yeye Zembwela amepoteza kabisa ile ladha na kwamba sasa si yule wa zamani. Ki kawaida tu kwanza hawezi kuwa kama yule wa zamani na zaidi ni kweli ladha pengine lazima ipotee maana sasa hivi yuko peke yake, ila je kipaji? Binafsi nadhani Zembwela ana kipaji na utashi wa hali ya juu ambao unamfanya aendelee kuwepo pale alipo na sasa akiwa anasimama kama Ndimu kwenye Radio ya Wasafi FM pale asubuhi anapokua anachambua magazeti.
    Mwanzo nilikuambia Zembwela alianzia EA Radio baada ya kuvutwa na Mussa pale, na alikaa kwa kipindi hata baada ya Mussa kuondoka yeye aliendelea kuzungusha gurudumu la Super Mix ila baadae mambo yakabadilika na ikambidi aende kutafuta ustaarabu mwengine na sehemu nyengine. Maisha yako wakati mwengine yanaweza kukupeleka sehemu ambayo wala ulikua huitarajii.
    Sasa pia amerudi kwenye TV na kaniibia siri pia kwamba hivi karibuni anatarajia kuanza series ambayo wao kama Wasafi TV wamekua wakiipika kwa kipindi sasa. Naamini hii itakua habari njema kwa wengi ambao wamekua wakiisubiria kwa hamu.
    Na pia kasema itaanza hivi karibuni.
    Mimi na Zembwela pia tumeongelea maisha yake binafsi, kuondoa kwa Max, kazi za kileo na mustakabali wa Siasa na wana Siasa na mengine tele. Moja kubwa ambalo naweza kukuahidi ni enjoyment na kucheka, hakika haya UTAYAPATA.
    Tafadhali enjoy,
    Love,
    Salama.
    Support us through anchor.fm/yahs...
    SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
    Listen our Podcast on
    Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
    GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
    Audiomack Link bit.ly/YahSton...
    ‪UA-cam Link bit.ly/UA-camS...
    Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown
    Channel Administered by Slide Digital
    Instagram: slidedigitaltz

КОМЕНТАРІ • 232

  • @CoachHafidh
    @CoachHafidh 2 роки тому +15

    Afya ya Akili, afya ya kinywa na Afya ya Mwili...So Powerful. ✊🏾💯

  • @echolude
    @echolude 2 роки тому +23

    finally someone who treats Swahili with proper respect and depth

  • @mnenedrogba1218
    @mnenedrogba1218 2 роки тому +17

    Now I get the reason or reasons as to why Diamond keep mentioning Zembwela babu, this man is very wise and he is on point in almost everything question sent.respect big bro 🤝🙏💯

  • @jonahbirgen6946
    @jonahbirgen6946 2 роки тому +7

    I use to enjoy his show at East Africa radio sometimes back from Kenya cheers

  • @dastonamichaels1854
    @dastonamichaels1854 2 роки тому +10

    From 🇰🇪Huyu bro nilianza kumcheki zamani na maxi kwa comedy flani alikuwa mpangaji mkorofi 😅🤣

  • @alexkalonga5323
    @alexkalonga5323 2 роки тому +12

    Zembwella na Gabo wakikaa meza moja wanaweza fanya kitu fulani kikapendwa na watanzania wote

  • @mozasaid3869
    @mozasaid3869 2 роки тому +4

    Penda sana Zembwela❤❤❤👊👊👊

  • @shd12m55
    @shd12m55 2 роки тому +10

    Juice ya awamu ya kwanza kwa zembwela 🔥🔥

  • @sevelinamartin7752
    @sevelinamartin7752 2 роки тому +4

    Namuelewa Zembwela nakupenda salama,so nimeinjoi sn

  • @uzungupoint
    @uzungupoint 2 роки тому +9

    UMENIUA KWA JPM TU 🔥🔥🙌

    • @majidypapeny1527
      @majidypapeny1527 2 роки тому +1

      Na bonge la fumbo ambalo m2 wakawaida hawezi kulijua kwa haraka R.I.P magufur

    • @uzungupoint
      @uzungupoint 2 роки тому

      @@majidypapeny1527 Kabisa kaka

    • @josephlorri431
      @josephlorri431 2 роки тому

      Majambazi na wezi wa mali zetu ndo tunawashangilia..

  • @dayocha1855
    @dayocha1855 2 роки тому +6

    Hii interview ya leo bomba sana ila zembwela katisha sana bila kumsahau salama kwa maswali yake mazuri

  • @ditrickhinju9684
    @ditrickhinju9684 2 роки тому +3

    Good interview ujawai kukosea kwahilo interview killer u sister nice

  • @lovenessselemani4949
    @lovenessselemani4949 2 роки тому +10

    Bonge moja ya interview

    • @rashidomar1558
      @rashidomar1558 2 роки тому

      Lessons zinapatikana kwa kufanya interview za maana kama hizi

  • @marcoemanuel6892
    @marcoemanuel6892 2 роки тому +3

    Kari sanaaa hii interview

  • @mjkinyonga38
    @mjkinyonga38 2 роки тому +4

    Mahojiano bora zaidi 2022

  • @christophertemba6915
    @christophertemba6915 2 роки тому +11

    huyu mwamba zembwela ni fundi sana wa maneno mpka salama anabaki kucheka tu.

  • @ilhamsalum6815
    @ilhamsalum6815 2 роки тому +12

    😂😂😂ninavompenda salama nataman ata apate copy yake💞 mtoto ,akiondoka awepo atakae chukua muonekan na tabia zake NAKUPENDAA😣😩🥰

  • @jameskimei5438
    @jameskimei5438 2 роки тому +2

    Nice one l love it

  • @iddyrashidi8961
    @iddyrashidi8961 2 роки тому +2

    hongereni sana kwa hichi kipindi kinatuelimisha sana 🙏

  • @BongoCryptos
    @BongoCryptos 2 роки тому +2

    JPM! SAFI SANA ZEMBWELA

  • @theresiatarimo3616
    @theresiatarimo3616 2 роки тому +2

    Hapo kwa maguful nimemuelewa...hongera zmbwela...

    • @cineplus-tv255
      @cineplus-tv255 2 роки тому

      ua-cam.com/video/3GyDw7shVsA/v-deo.html

  • @edenngiluke8493
    @edenngiluke8493 2 роки тому +3

    Interview Kali Sana.. One Of The Best

  • @davidnchoji
    @davidnchoji 2 роки тому +11

    Poor Me😥, namfahamu Zembwela lakini sikuwahi kutenga muda wa kumfuatilia zaidi, na kumbe nimekuwa nikikosa maneno ya busara kutoka kwa mtu mwenyewe busara na akili pana sana. Keep it up Da Salama kwa kutuletea mtu wa aina ya Zembwela...😍❤️

  • @mbakomileakim1783
    @mbakomileakim1783 2 роки тому +3

    Iyo background music ni ngoma ya nan anaejua please

  • @yohanayohana199
    @yohanayohana199 2 роки тому +5

    Zebwera wewe ni mkweli sana nakumbuka uliwahi kuomba mkombozi wa Tanzania ulipiga magoti ktk redio

  • @rachelkristellagodlove2404
    @rachelkristellagodlove2404 Рік тому

    Best episode kwa mwaka huo zembwela ana madini mengi sana

  • @salomecomedyofficial
    @salomecomedyofficial 2 роки тому +4

    Zembwela tunaomba kwa heshima umrudishe kwenye game Mr 20%, ni mwandishi na mwimbaji mwenye mziki wa kuelimisha

  • @stevenasunga3917
    @stevenasunga3917 2 роки тому +1

    Umeongea point sana

  • @ballisticsound4796
    @ballisticsound4796 2 роки тому +14

    Bila kupindisha Maneno IPP Media imetoa mchango mkubwa sana kwenye tasnia ya Habari ahapa TZ... pamoja na kutoa vichwa mahiri kabisa

  • @TemuTV
    @TemuTV 2 роки тому +2

    💯💯💯🙌🙌

  • @akkidume8312
    @akkidume8312 2 роки тому +4

    Hahahahahaha nimeipenda

  • @ashurajengela3926
    @ashurajengela3926 2 роки тому +1

    Zembwela Babu Mswahili 🔥

  • @omariathuman9998
    @omariathuman9998 2 роки тому +3

    i just comparing mkasi na hii show guest zembwela aisee zembwela ananifanya nisome nje ya syllabus ....salama nakuona kama ellen wa ellen show america

  • @sevarinijrchitandachitanda138
    @sevarinijrchitandachitanda138 2 роки тому +13

    Bonge la interview🔥🔥

  • @fanuelkatoto8913
    @fanuelkatoto8913 2 роки тому +2

    Kongole sana kwa kipindi kizuri.. Heshima kubwa kwa babu Zembwela

  • @angellomarcel5677
    @angellomarcel5677 2 роки тому +4

    Duh Zembwela ni mtu na nusu aseee

  • @eliakimeliakim7082
    @eliakimeliakim7082 Рік тому

    Interview nzur sana .

  • @hamzakamaze5532
    @hamzakamaze5532 12 днів тому

    Chuma cha puaaaaa❤

  • @habimanayasin4223
    @habimanayasin4223 2 роки тому +2

    Mungu wetu sote mkubwa .

  • @khamissasita4559
    @khamissasita4559 2 роки тому +11

    Joseph John Pombe Magufuri daaaah!!. R.I.P daddy 👨....

  • @anthophile786
    @anthophile786 2 роки тому +3

    Only a piece of interview ❤️

  • @UlimeA
    @UlimeA 2 роки тому +2

    Hilo fumbo la jpm ni zito sana

  • @didomanyota5344
    @didomanyota5344 2 роки тому

    Kuna legendary mmoja umemsahau hapo Mwamba wa kaskazini

  • @jacobmsigwa383
    @jacobmsigwa383 2 роки тому +2

    "Gari bovu huvutwa gari zima" ha ha ha

  • @josephngowoambroce418
    @josephngowoambroce418 2 роки тому

    Kwenye juice noma saaaana bro

  • @emanuelleopod3949
    @emanuelleopod3949 2 роки тому +1

    Hapo kwa Twent aisee tupo wote

  • @dominickvitus4665
    @dominickvitus4665 2 роки тому +4

    Manguli wa hizi show

  • @tausijarufu
    @tausijarufu 2 роки тому +2

    👏👏

  • @mbwanamtessa8607
    @mbwanamtessa8607 2 роки тому +3

    Yani wejamaa ni mshenzi sana... daaaah....😂😂

  • @agustinohizza1395
    @agustinohizza1395 2 роки тому +3

    Hiyo juice ulivyo ipiga tarupeta!!!

  • @rayanndizeyes3161
    @rayanndizeyes3161 2 роки тому +1

    Jouniowe babu

  • @johnmalembeka3546
    @johnmalembeka3546 2 роки тому +2

    Next mleteee dudubaya konki master putin

  • @florenceblack4492
    @florenceblack4492 2 роки тому +2

    Nimekupanda bure zembwela

  • @josephngowoambroce418
    @josephngowoambroce418 2 роки тому +1

    Barrier

  • @hussseinmasangya7130
    @hussseinmasangya7130 2 роки тому +2

    Akili kubwaaaa

  • @mustaphalushoto3262
    @mustaphalushoto3262 2 роки тому +2

    Juice 🥤 kanywa au imepotea kwenye glasi

  • @chumachareli6530
    @chumachareli6530 2 роки тому +2

    Kuna interview nyingine waliifanya kwenye mkasi.Niko nayo naiskiza kwa miaka

  • @malkavoice2570
    @malkavoice2570 2 роки тому +3

    Sisi tunatska Salama na Zuchu why unatubania?

  • @nelsonibrahim6844
    @nelsonibrahim6844 2 роки тому +2

    💯❤❤❤

  • @isihakasaid5644
    @isihakasaid5644 2 роки тому +2

    Nimeinjoi kusikia uyo jamaa kwakweli

  • @Teachercandle
    @Teachercandle Рік тому

    Fumbo alilolitumia lina tafsiri nyng mno...

  • @tumainidaniel5789
    @tumainidaniel5789 2 роки тому +3

    Hivi zembwela na tin white Wana undungu

  • @n7428
    @n7428 2 роки тому +2

    Zembwela ni mkweli 🤣🤣🤣

  • @adammlonganile7921
    @adammlonganile7921 2 роки тому +1

    Humkumbuki Maxi, kweli?

  • @araskiezgoldskies
    @araskiezgoldskies 2 роки тому +1

    Kabali yao zembwela

  • @rithluqka4103
    @rithluqka4103 2 роки тому +2

    Huyu jamaa Nilikuwa namsubiri kwa hamu

    • @cineplus-tv255
      @cineplus-tv255 2 роки тому

      ua-cam.com/video/3GyDw7shVsA/v-deo.html

  • @yusuphmbugi8594
    @yusuphmbugi8594 2 роки тому +1

    hichi kweli chuma

  • @saidadam2165
    @saidadam2165 2 роки тому +2

    Babu 😀😀😀😀😀

  • @robertohtesh3193
    @robertohtesh3193 2 роки тому

    Kama naiona Mkasi 2012....."vijana wengi hatujielewi"

  • @rayanndizeyes3161
    @rayanndizeyes3161 2 роки тому +1

    Ila muze😂😂😂

  • @dullaubinadamu8465
    @dullaubinadamu8465 2 роки тому +1

    CMG

  • @egnokapinga16
    @egnokapinga16 2 роки тому

    Jamaa akili kubwa sana uyu😅✊

  • @salomewandya7257
    @salomewandya7257 2 роки тому +1

    Salama leo umenoga

  • @Chadibwa9519
    @Chadibwa9519 11 місяців тому

    @salama naona jamaa anamadini makali sana vipi kitabu kinaweza tengeneza hapa???

  • @asmarajabu5786
    @asmarajabu5786 2 роки тому +3

    😀😀😀

  • @King_Of_Everything
    @King_Of_Everything 2 роки тому +1

    🇹🇿🇹🇿🇹🇿✌👍.

  • @valencyminde5246
    @valencyminde5246 2 роки тому +1

    Nakupenda salama🥰🥰🥰

  • @faridhamad3678
    @faridhamad3678 2 роки тому +1

    Et ki tv au kama nilivyozoea😂😂😂

  • @moricemorice75
    @moricemorice75 2 роки тому

    Salama naomba mwana id niowe

  • @allywaziri9838
    @allywaziri9838 Рік тому

    Gari bovu huvutwa na zima😂kuna gari zima linanivuta

  • @mwanaidimuhindi6671
    @mwanaidimuhindi6671 2 роки тому +1

    Mwanaidi nimeambiwa nilete juice nyengine 😅

    • @cineplus-tv255
      @cineplus-tv255 2 роки тому

      ua-cam.com/video/3GyDw7shVsA/v-deo.html

  • @rashidmashaka1065
    @rashidmashaka1065 2 роки тому +1

    Uyu jmaa 😆😆

  • @universitylink
    @universitylink 2 роки тому +1

    Gari bovu huvutwa na zima

  • @kharounngavason8012
    @kharounngavason8012 2 роки тому

    SALAMA wwe ssa kabla hujadanja je

  • @johnchitete
    @johnchitete Рік тому

    Duh Nimechoka ghafla 😂

  • @kimfernandes1678
    @kimfernandes1678 2 роки тому +1

    zembuuuuuu babuuu

  • @mirroyjunior8348
    @mirroyjunior8348 Рік тому

    Leo mekutana na watu ninaowafatili san

  • @godfreybenny5120
    @godfreybenny5120 Рік тому

    Mutu mkweli mwingine

  • @MohamedHassan-xi5zz
    @MohamedHassan-xi5zz 2 роки тому +1

    😂😂😂

  • @sefoadelino6684
    @sefoadelino6684 Рік тому

    😂😂😂😂😂😂😂😂

  • @christopherkanyalakc8941
    @christopherkanyalakc8941 2 роки тому +1

    Fanya mpango uzae Acha ukijuju " mwambie B.leve akutafasirie or mwijaku ata Mr.Pimbi He knows what I mean

  • @salhakristina9434
    @salhakristina9434 2 роки тому +1

    🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🙏

    • @cineplus-tv255
      @cineplus-tv255 2 роки тому

      ua-cam.com/video/3GyDw7shVsA/v-deo.html

  • @johnchitete
    @johnchitete Рік тому

    Salama tunaomba utuletee Madebe Lidai 😂

  • @mzhsk1386
    @mzhsk1386 2 роки тому +1

    Zembwela kumbe muslm mashallah

    • @gordiansoko9113
      @gordiansoko9113 2 роки тому

      Ndugu yangu mbona umechelewa uko karne ya ngapi bado unafikiria mambo ya dini katika interview hii. Dini hapa ina umuhimu gani au ina nafasi gani pole sana badilika.

    • @mzhsk1386
      @mzhsk1386 2 роки тому

      @@gordiansoko9113 ooo dini haina thamani kwako

  • @drmussa1220
    @drmussa1220 2 роки тому +1

    ua-cam.com/video/QN5ACFcSBIE/v-deo.html
    DAWA YA MAJIPU, HUSAFISHA MFUMO WOTE WA DAM*#

  • @rogathesarwatt
    @rogathesarwatt 2 роки тому +13

    ZEMBWELA NA SALAMA MNAITENDEA HAKI LUGHA ADHIMU YA KISWAHILI KUNA LADHA YAKIPEKEE SANA

  • @drmussa1220
    @drmussa1220 2 роки тому

    ua-cam.com/video/QN5ACFcSBIE/v-deo.html
    DAWA YA MAJIPU, HUSAFISHA MFUMO WOTE WA DAM*#

    • @isaacluwondo4506
      @isaacluwondo4506 2 роки тому

      jamani mwambieni salama amlete MCHUNGAJI HANANJA

  • @msusasandali5833
    @msusasandali5833 2 роки тому +30

    Ni moja ya interview niliyokuwa naisubiri kwa hamu kubwa Sana.... ☺️

  • @mkaapwekekariakoo6417
    @mkaapwekekariakoo6417 2 роки тому +16

    Mali iliyotafutwa na mtu, na wale wasioitafuta kuja kuihitaji hata kama hawahusiki nayo... KInywa, afya ya akili na mwili. Dah.... karibu kila neno la Zembwera ni msumali wa mabadiliko kwa hata kwa wanaozipata simulizi kwa walisikiliza wenyewe. Asante Salama na....Natamani kipindi kisiishe maana hawa hakika marafiki kufa kupona, maaana si kwa cheko na furaha hizo

  • @tangaoldtv1067
    @tangaoldtv1067 2 роки тому +7

    SALAMA KATKA MAHOJIANO YA WATU TOFAUTI NANI ALIKUWA MAJIBU YAKE YALIKUWA YA KUCHEKESH SAN NA ULICHEK KIASI KUJIKAZA?