DDC Mlimani Park - Barua Toka Kwa Mama

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 29 сер 2024
  • Mlimani Park Orchestra at their best with Barua Toka Kwa Mama Part One

КОМЕНТАРІ • 429

  • @pandoemmanuel2051
    @pandoemmanuel2051 2 місяці тому +4

    1983 na 84 nilikuwa nikisikia wimbo huu nilikuwa nalia sana sana. NI wakati nasoma primary, wakati huo naishi kwa bibi yangu na wazazi wangu walikuwa wametengana. Nikapoka barua kutoka wa mama. Mungu ampumzishe baba yangu. Bado nasikiliza 2024

  • @abdallamatemba7484
    @abdallamatemba7484 Рік тому +9

    Hapo Kuna pacha mbili, Abel, Mulenga na Gama (gitaaa),Cosmas, Hamis Juma na Gurumo(waimbaji)aliyefunga kazi na midomo ya Bata ni King Enock, hayo yote yamo kwenye maisha tuliyonayo Leo na vijana wa Sasa mgogoro wa wazazi anaamua kulalia upande mmoja, Cosmas katoa funzo Sana kwenye wimbo huo, ndio nyimbo za kwanza kabisa baada ya bendi kuanzishwa, (1)Barua-Cosmas(2)Celina-Mulenga(3)Kassimu-Gurumo, Nchi ilisimama kwa muda baada ya nyimbo hizi kutoka redioni kwa Mara ya kwanza, hongereni Sana Mlimani hasa hasa Abel Barthazal

  • @stanleyadamson9522
    @stanleyadamson9522 6 років тому +10

    Kwa kweli hii nyimbo inanikumbusha mbali sana kuna siku nimetoka Shule hela sikuwa nayo nimeshinda na njaa toka asubuhi mpaka natoka Shule mchana .nikapita nyumba moja hivi nikaona mama na mwanae wamekaa wanakula nikaenda nikaomba wanisaidie chakula wakanikaribisha nikakaa na kuanza kula.mda huo kulikuwa na Redio ya mkulima ukawa unaimba HUU wimbo. Daah kila nikiusikia nakumbuka hiyo siku aisee

  • @omaryjuma3714
    @omaryjuma3714 Рік тому +8

    Kisa Cha kweli kabisa Mwenyezi mungu awapumzishe wazazi wangu mbele za haki Mama yangu amenilea kwa shida sna Sina baba simjui hata kwa sura kwa roho inaniuma R.I.P wazazi wote waliotanguria mbele za haki

    • @jumannemwakalinga2586
      @jumannemwakalinga2586 6 місяців тому

      Pole sana Ndugu yangu, endelea kuwapmbea Wazazi maana wote tutaenda huko.

    • @fatumahamadi1379
      @fatumahamadi1379 Місяць тому

      Pole My Dear ALLAH aupoze moyo wako n zid kuwaombea Dua

  • @mursalseleman2174
    @mursalseleman2174 4 роки тому +7

    Hakika hii nyimbo inasisimua mpka machozi yanatoka yenyew bila kujua duh ama kweli ya kale dhahabu gonga like 2020

  • @hintazom1456
    @hintazom1456 4 роки тому +16

    Niligombana na mke wangu mtoto wangu wa kwanza alilia sana huku akisema,"dad plz don't ditch my mom i beg ye",ikabidi nimsikilize na mpaka leo tupo pamoja.

  • @aidannzowa5502
    @aidannzowa5502 5 років тому +6

    Miaka ya 78 baba akiwa masomoni Mzumbe, ss watoto na mama tunaenda shambani njaa inauma kishenzi lkn baba akirudi likizo ilikuwa faraja sana kwa kila mtoto, pia santuri mpya za muziki tunacheza tunakesha! It was real goldsh family! Hongera sana mama yangu! R.I.P. my dady

  • @georgeodoo9924
    @georgeodoo9924 3 роки тому +7

    Inanikumbusha wakati nilipokua nikisoma Chuo ki Kikuu Dar es Salaam 1978/80. Mimi msudani na pia muamerikani. Ninapenda wa Tanzania na nchi yenu sana.

  • @othumanyahya9168
    @othumanyahya9168 5 років тому +5

    Wimbo huu sitoweza kuusahau katika maisha yangu, kwani mwaka 1986 nikiwa chuo cha elimu ya ualimu ilinibidi nifanye uamuzi mgumu ili kuwapatanisha wazazi wangu ambao walitengana. Daah! Chidumule Cosmas nitaendelea kukumbuka kwa kuwa mkweli katika maisha halisi.

  • @jacksonchiwalanga4817
    @jacksonchiwalanga4817 3 роки тому +22

    My parents separated 27 years now,, my mom struggle alone all those years and she only have me,, the only son,,, My love to her is unmeasurable this song make me cry 😭

    • @omondiabdi1971
      @omondiabdi1971 2 роки тому +1

      Just a part of life bro.

    • @josiahmuthemba115
      @josiahmuthemba115 2 роки тому +1

      Ploe sana hayo ni mapito

    • @husseinhumbi6373
      @husseinhumbi6373 2 роки тому +1

      Muda mwingine tunaweza kuwalaumu wazazi wa kiume lakini hatujui mama na baba walitengana kwa nn huwenda kuna Jambo gumu kuvumilika

    • @petersaria7125
      @petersaria7125 2 роки тому +1

      @@husseinhumbi6373 kweli kiikubwa kuwapenda wote

    • @johnginni9926
      @johnginni9926 2 роки тому +1

      Pole sana nadhani mengi Leo unashuhudia ndg yangu wangekuwa pamoja pengine wangukuwa hawapo kwani ugonvi huleta maafa

  • @khadijakassimu3710
    @khadijakassimu3710 4 роки тому +9

    I miss my baba😍😍😘😘R.I.P my lovely father.Ndo vilikuwa vitu vyake hivi hadi nasi wanawe vimetuingia kwenye damu,Sasa mwezi wa 7 huu sinae duniani,.Nikisikiliza hivi kama namuona vile 😭😭😭dah sina la kusema yani

  • @fredrickkassilly8479
    @fredrickkassilly8479 Місяць тому +1

    I Heard This Song When I Was In High School At Alliance High School In Kenya. We Used To Sing It Without Paying Much Attention To It. Now I Do. A Master Piece For All Ages!! Congratulations DDC Mlimani Park.

  • @mosesnjeru1455
    @mosesnjeru1455 Рік тому +14

    2022 listening to this song and I feel like crying....may the lord continue to keep my parents with good health and long life nawapenda sana...this song makes me visit my aged parents more often....

  • @sylvesterokumu2695
    @sylvesterokumu2695 6 років тому +13

    I watched mzee Chidumule narrating how he came with this song.This is a true story that was happening in his family.His father and mother were separated and thus the song.He is an inteligent old man.Kongole kwa utunzi huo.

  • @linusleon7018
    @linusleon7018 7 років тому +59

    N iutunzi wa cosmas chidumule.akiimba pamoja na hamisi juma maalim kinyasi.na muhidini gurumo.solo Abel Baltazar.ibass joseph mulenga.ridhim Abdala gama.tumba Haruna Lwali.drums Habib Abassj eff.saxfone juma town.Joseph Bernard.King michaelEnock Teacher.Trumpet Ibrahim mwinchande Bonifas Kachale.mafundi mitambo.chuma na kitwana....Sikinde ilitisha.....

    • @wilsonlukuwi8941
      @wilsonlukuwi8941 6 років тому +6

      Linus Leon namna ulivyo wataja musicians hao unaninikumbusha namna Julius nyaisanga (RTD)na Fred obachi machoka (VOK) walivyokua wakiwataja kwa mbwembwe!

    • @henrychaula1174
      @henrychaula1174 6 років тому +2

      Umepatia hasa huyo ni Cosmas Thobias Chidumule akiwana Hassan Rehan Bitchuka na Gurumo enzi zao za Sikinde ngoma ya ukae 1979 nikiwa darasa LA Vi, walitisha mno mno.

    • @michaellukandi6800
      @michaellukandi6800 6 років тому +7

      A true story refering to Chidumules' parents.They had familiy issue of which later they divorced.This song is as a consequence of this situation.Chidumules mother wrote to his son LETTERS (referred to this song)b regarding the hardships she was experiencing in her marriage.Fantastic,touching, song

    • @dominicmaluki5242
      @dominicmaluki5242 6 років тому +1

      Pia marehemu MDJ Eddie Fondo,the best radio dj in the late 70s and 80s,complete with their dates and places of birth.Those were them days.I wonder whether any of our so called musician today will ever reach such levels.

    • @mathewmunthali3684
      @mathewmunthali3684 6 років тому +1

      Burudani kwelikweli

  • @fatumahamadi1379
    @fatumahamadi1379 Місяць тому

    Huu wimbo unanikumbusha Mbali sana NI Wimbo Wenye Mafunzo Ndani Yake ALLAH Awarehemu Wzz Wangu n Wote Waliotangulia Mbele y Haki

  • @josephinejoseph7358
    @josephinejoseph7358 8 років тому +11

    loooh...!! jamani kipande hiki namaliza kdt cha 6 Mzumbe High School Morogoro. ...lkn nikaendelea kuupenda mpaka nikiwa " kuruta Mafinga National Service 1979.

  • @sammylwendo1496
    @sammylwendo1496 22 дні тому

    Kama mama yangu angekua hai, I swear baada ya kusikiliza wimbo huu, kesho ningepanda basi niende popote alipo nikamsalimie na kumuambia nampenda kwa kiwango gani!Rest in power my mom Christina Mballa Mwakatah!

  • @abiudoluoch7668
    @abiudoluoch7668 5 років тому +31

    Ninaposikia nyimbo kama hizi natamani kutembelea ndugu zetu kule Tanzania, the home of many great musicians kama Mbaraka Mwinshehe, Remmy Ongala, DDC Milimani Park, Ramadhan Rajab na wengine wengi. Tz you're a blessed nation

  • @leahngugi5918
    @leahngugi5918 8 років тому +10

    Ujumbe wa wimbo huu unaonyesha vile watoto wanavyoteseka wazazi wao wakiachana.

  • @jumaomary5657
    @jumaomary5657 5 років тому +2

    Nimekumbuka 1976 baba yangu alipofariki RIP my daddy pia nakumbuka 1993 alipofariki mama yangu RIP my mummy!!

  • @jimmymayunga9070
    @jimmymayunga9070 8 років тому +12

    kwakweli tungo za mashiri ya mziki huu imetulia, inagusa huwa ninapo usikiliza wimbo huu huwa namkumbuka sana mamaangu, kwakweli mziki wa zamani bado ungali unaishi.....

  • @AthumanyakawaidamwanaJuma
    @AthumanyakawaidamwanaJuma 8 років тому +29

    Unanifanya kesho niende home nikamuone mama kijijini.

  • @AllyMsita
    @AllyMsita 2 місяці тому

    Ni wimbo wa miaka mingi sana rakin unaishi mwaka2006 juzi tu apa niradhimika kusikiliza wimbo wa mwyaka ya 80 nikiwa bukoba mama akiwa wilaya ya manyoni Kijiji Cha makale, hakika watunzi mulikuwepo hatuko nanyi nyimbo zenu zinaishi duniani tunapita nyie mbele sisi nyuma yenu

  • @kakuruchiganga507
    @kakuruchiganga507 6 років тому +5

    Barua zangu wakati niko shule nimezitunza hadi leo haswa zile zilizokuwa unakunja karatasi hiyohiyo upande mwingine ni bahasha, huu wimbo huwa unanitoa machozi kwani mama na baba walitengana nikiwa na miaka 3, na mama akapambana hadi nikamaliza chuo.Mwezi mmoja toka nimalize chuo kbla hata kazi sijapata mama yangu akatangulia mbele za haki, Mwenyezi Mungu aiweke roho ya mama yangu pahala pema peponi, Amina.

  • @damaskimaro9111
    @damaskimaro9111 6 років тому +60

    Kisa cha kweli wazazi wa chidumule walitengana wakati huo wakiw Tanga,chidumule alilazimika kurudi songea pamoja na mama yake,then alijiunga na Butiama jazz ,Urafiki jazz,Dar international then akaenda kuanzisha Mlimani park na ndio akatunga wimbo huo

    • @mwinyimgeni8850
      @mwinyimgeni8850 5 років тому +1

      Damas Kimaro Hapana mlimani hajaanzisha yeye

    • @jovinjoseph4887
      @jovinjoseph4887 5 років тому +2

      Chidumule bado yupo ila siku hizi ameokoka

    • @chasoh
      @chasoh 5 років тому +1

      Huyu hapa Chidumule na ushuhuda wake, ua-cam.com/video/nZnavV13DpI/v-deo.html

    • @johnndambuki21
      @johnndambuki21 4 роки тому +1

      Thanks for the story behind the song.

    • @henrychaula1174
      @henrychaula1174 4 роки тому +3

      Hakuanzisha aliwakuta kina Hassan Rehan Bichuka, Gurumo na wengineo pale

  • @mujahidalinaseem6213
    @mujahidalinaseem6213 4 роки тому +2

    2020.. niliishi na kulelewa na mama wa kambo na alikuwa muungwana sana kwangu lkn bado nilikuwa nikisikiliza kibao hiki nilimkumbuka mama mzazi ambaye kimsingi alishaachika na baba..!!

  • @pslymrobert4627
    @pslymrobert4627 8 років тому +9

    Daah huu wimbo unaniliza ila sina jinsi... God protect my family mom and dad though they are not together.

  • @fridachally6150
    @fridachally6150 4 роки тому

    aehe mama ee jaribuni kuyasuluhisha mambo hayo kutengana kwenu kunanipa wasisi ,sina kaka ,sina dada kwa hiyo naomba muishi kama vile mwanzo.

  • @ibrahimmrisho3646
    @ibrahimmrisho3646 2 місяці тому

    Nyimbo hizi Zina mafundisho makubwa na ujumbe sahihi kabisa nakumbuka mbali sana

  • @sangomamourice3539
    @sangomamourice3539 22 дні тому

    Sifa za fasihi ni kuishi asante ddc kwa zawadi hii asante waimbaji

  • @saidihabibu8779
    @saidihabibu8779 5 років тому +1

    Hizi nyimbo za kale kwa kweli hazina mfano ni nzuri sana na zinafikisha ujumbe kwa jamii,mimi binafsi kwa ujumla ni shabiki kindakindaki wa nyimbo hizi nawapongezeni sana kutupatia uhondo huu asanteni sana

  • @emmanuelpaul5704
    @emmanuelpaul5704 6 років тому +1

    kweli mimi ni kijana wa 90 lkn napenda sana hz nyimbo ujumbe wake unapelekea hsia zangu kwenda mbali sana

  • @joyceamogolla5473
    @joyceamogolla5473 8 років тому +8

    Heard this song recently on Rogaroga radio citizen when Obachi Machoka was hosting Chidimule the composer of the song. Very inspiring music! The songs had a message and lesson to be learnt. Gone are those days.

    • @stephenmwithiga164
      @stephenmwithiga164 8 років тому +3

      Thank Machokaa for hosting Chidimule. song that bring back the days of VOK, natuma salamu nikiwa kakamega show.Ujumbe dawa ya ndeni ni kulipa.Goods days No HIV,No CORD NO JAP.

    • @edwardgerald8602
      @edwardgerald8602 7 років тому +2

      I have never known Chidumule to have worked together with Muhidin Gurumo!

    • @ipyanamwakanosya2744
      @ipyanamwakanosya2744 6 років тому

      Joyce Amogolla where is Rogaroga radio?

    • @saidachekaaali1307
      @saidachekaaali1307 6 років тому +2

      Ipyana Mwakanosya
      Rogaroga ni kipindi kwenye Radio Citizen ya Kenya.Na Fred Obachi Machokaa ndie anaekiendesha hicho kipindi.Husikika siku ya Jumamosi na Jumapili,kianzia saa Nne asubuhi hadi saa Saba mchana.Na sasa pia kiko kwenye runinga ya Citizen.Hata mie nlipata fursa ya kusikia hayo mahojiano kati yake Fred naye Chidumule,pia nkawahi kurekodi sehemu tu ya hayo mahojiano.Natumai nmekujibu vyema ndugu.

    • @fredmachoka8599
      @fredmachoka8599 Рік тому

      Thanks for listening to RogaRoga on Radio Citizen FM-Kenya. Hope you enjoyed listening. It was indeed a privilege and pleasure to host the legend of Rhumba.

  • @gracechalagwa1122
    @gracechalagwa1122 5 років тому +2

    Mungu atusaidie , inaonesha Mtoto aliumia sana!

  • @josephkazungukombe8688
    @josephkazungukombe8688 3 роки тому +1

    Nasikia kanyimbo kanapenya mpaka ndani,old is gold

  • @rashidymsenga714
    @rashidymsenga714 6 років тому +1

    Nani kama mama, kila nisikiapo wimbo huu huwa najiuliza nimlipe mama yangu kitu gani ukweli nikwamba sina chakumlipa mama yangu nampenda sana mama.

  • @leahngugi5918
    @leahngugi5918 8 років тому +16

    And the message is as relevant today as it was those days the song was compossed.

    • @irenebilauni7534
      @irenebilauni7534 6 років тому +2

      Leah Ngugi kama ujuavyo msani ni kioo cha jamii, wana foreseability, waliona mbali,jumbe zao zitadumu milele

    • @danieljuma1921
      @danieljuma1921 6 років тому

      Leah Ngugi And even more relevant today than ever before....with deterioration in family values....

    • @leahngugi5918
      @leahngugi5918 2 роки тому

      @@danieljuma1921
      Very true.
      We need to hear such today than ever before

  • @hamidually1138
    @hamidually1138 8 років тому +8

    Ddc mlimani park
    wanajua, hasa hiyo sauti ya marehemu Hamisi juma huwa naipenda Sana.

  • @jamesmnjeru824
    @jamesmnjeru824 4 роки тому +6

    still love this song decades later...

  • @mohamedikilinga2889
    @mohamedikilinga2889 6 років тому +2

    Nilikuepo kwenye tamasha la kutimiza miaka 40 ya mlimani park pale viwanja vya bandari wiki iliyopita lkn badala ya kufurahi nilitoka pale nikiwa na huzuni kubwa baada ya kumuona mpiga rythim ya wimbo huu ABDALAH GAMA akiwa hoi bin taaban,ni mlevi kupindukia hawez tena kufanya chochote,,,kwakweli iliniuma sana nikimuangalia

    • @najmasaleh9231
      @najmasaleh9231 5 років тому

      Mohamedi Kilinga Ni kweri Gama kachoka sana yuko na kibendi kinaitwa Exel bend wanapiga zing zong

    • @mujahidalinaseem6213
      @mujahidalinaseem6213 4 роки тому

      Wakati strees zinachangia kuwatoa nje ya mstari wamefanya makubwa lakini of the and NOTHING EVERTHING

  • @Salisalum
    @Salisalum 2 місяці тому

    Aee mama eeh jaribuni kuyasuruhisha mambo hayo
    Kutengana kwenu kunanipa wasiwasi manenu
    Sina kaka sina dada kwa hiyo naomba muishi kama vile mwanzo
    Ningali mdogo ninahitaji msaada wenu wazazi wangu
    Aee mama eeh jaribuni kuyasuruhisha mambo hayo
    Kutengana kwenu kunanipa wasiwasi manenu
    Sina kaka sina dada kwa hiyo naomba muishi kama vile mwanzo
    Ningali mdogo ninahitaji msaada wenu wazazi wangu
    Aee mama eeh jaribuni kuyasuruhisha mambo hayo
    Sina kaka sina dada
    Kwa hiyo naomba
    Muishi kama vile mwanzo

  • @maheligati2936
    @maheligati2936 5 років тому +1

    hizo ndo nyimbo sio hizi za kizazi kipya nakupenda nakupenda Mara unanipa mambo ya uani kesho wa meachana

    • @ambakisyemwakatumbula4238
      @ambakisyemwakatumbula4238 5 років тому

      Daaaaaah yani natamani ningekuwa na helaa nyingi awa wazee wotee walikuwa wanaimba izi nyimbo niwaweke kwenye maisha mazuri ngoja nipigane kwa nguvu zote daaaah

  • @rizikimsule6592
    @rizikimsule6592 5 років тому +5

    Tears falling down on my chicks

  • @philipmbunda3610
    @philipmbunda3610 8 років тому +1

    Mama salamu zako nimezipata, ninashukuru kwa kunikumbuka. Taabu na mateso unayoyapata yananiumiza roho......Mambo haya yapo sana katika jamii yetu, hongera sana Mlimani Park.

  • @jacksonshiling8956
    @jacksonshiling8956 5 років тому +1

    Hii nyimbo imeimbwa kwa hisia sana hadi chozi linalenga lenga

  • @dominicmaluki5242
    @dominicmaluki5242 10 місяців тому

    The moment I listen to this sad song I always go visiting my mother the following day bearing in mind that she lives alone with home assistants and my father died many years ago and we her children left to start our own homes far apart

  • @simonjosephnyangusi569
    @simonjosephnyangusi569 8 років тому +6

    Wazungu wengine wanasema miziki ya waafrika vurugu kelele tu,,ngoma ngoma na kuruka...lakini hapo JEE meseji ya maana mziki umetulia classic namiss hiome mama yangu

    • @irenebilauni7534
      @irenebilauni7534 6 років тому

      simon joseph nyangusi wazungu wanataka waonekane kiichopo afrika ni upumbavu, ila sisi tunayaju mambo yetu yalivyo azuri kama haya ya wazee wetu,hivyo tuwaenzi.

  • @hildermkamburi1301
    @hildermkamburi1301 Рік тому

    Jamani old is Gold nyimbo imepangika inaimbika vizuri, sio nyimbo za kisasa zimechanikachanika

  • @epson5446
    @epson5446 4 роки тому +1

    Wimbo huu unanikumbusha mbali sana. enzi hizo nasoma Malangali Secondary School mwaka 1985

  • @uhondotv7335
    @uhondotv7335 2 роки тому +1

    Ujumbe wa aina yake, heko na kongole zangu zimfikie Mzee Cosmas Chidimule popote alipo, kazi kuntu kwa vizazi vya kale na vizazi vijavyo🇰🇪💥

  • @judithoguna8265
    @judithoguna8265 5 років тому +1

    DDC Asante Sana Tena kwa hiki kipande jameni naenda nyumbani Tuesday asubui kumwona mama

  • @73Bundala
    @73Bundala 9 років тому +11

    No comment! Machozi tu,

  • @ramadhanisebogwe9011
    @ramadhanisebogwe9011 8 років тому +33

    Huwezi choka kusikiliza hizi nyimbo kamwe, zamani ndio kulikuwa na wanamuziki sasa hv kuna wasanii tu

    • @omand1761
      @omand1761 8 років тому +1

      na hata mtu akiisifu sikinde kwa nyimbo hizi anamaanisha sikinde ya enzi hizooo sio ya sasa.Asikilize safu ya wanasikinde ktk tufurahi na wanasikinde.Asifkirie hii ya sasa.Ilikuwa nadra kuiskia sauti ya muhidin ngurumo bila rehani bitchuka.

    • @omand1761
      @omand1761 8 років тому +4

      hazichoshi,mimi binafsi nikizungumzia zilipendwa mziki wa dansi,moja kwa moja namaanisha sikinde

    • @stephenmwithiga164
      @stephenmwithiga164 8 років тому +4

      Bwana Ramadhani siku hizi kila mtu ni msanii.

    • @gasperleonard9411
      @gasperleonard9411 6 років тому +1

      Chidumule kweli ulikuwa na kipaji cha sauti kutoka kwa mungu

    • @nicholaslikombe4900
      @nicholaslikombe4900 4 роки тому +1

      Sasa hivi wapo wasanii wa kuganga njaa basi.......☺😁😉😉

  • @bingwason
    @bingwason 11 років тому +16

    Vocalists: Muhidin Mwalimu 'Gurumo', Hamisi Juma, Cosmas Chidumule
    Solo: Abel Balthazar
    Rhythm: Abdallah Gama
    Bass: Joseph Mulenga
    Keyboard: George Kessy Omondi
    Alto Sax: Michael Enock
    Drums: Habib Abbas 'Jeff'

    • @richardgaya3965
      @richardgaya3965 3 роки тому

      Most appreciative of the information...it acts as a perpetual record of heritage!!!

    • @charlesbayona9090
      @charlesbayona9090 2 роки тому +1

      Tshmanga Kalala Assosa one of vocalists in this song.

    • @kondonassoro26
      @kondonassoro26 Рік тому

      Mzee Gurumo kipindi hicho Hahaha R I P hakika ya kale ni dhahabu

    • @wilsonmalias3122
      @wilsonmalias3122 9 місяців тому

      Assosa aliondoka kabla ya recording ila ndiye mtunzi wa wimbo gama

  • @Mwl_Sanga
    @Mwl_Sanga 12 років тому +2

    4 th 1st tym I heard dis song ma heart became happy 4 a moment an then tears followed I dont know why dis happened.
    God bless th artists who sang dis song

  • @neattechnologiestz8636
    @neattechnologiestz8636 3 місяці тому

    Ninakumbuka mbali sana. Utoto una raha ila nikikumbuka ndugu waliotangulia mbele ya haki machozi yananitoka kwa masikitiko

  • @rwezahurarevocatus1886
    @rwezahurarevocatus1886 4 роки тому +2

    I salute all musicians who organized this massage espeially Mr chidumule .

  • @gordonnyagudi8166
    @gordonnyagudi8166 Рік тому +3

    Great and nostalgic music around 1978. Great vocals and instrument organization

  • @christopherokado5054
    @christopherokado5054 10 місяців тому

    Have separated with my wife for 24 yes. This song makes remember my children's feelings. So sad.

    • @royalmbwana
      @royalmbwana 8 місяців тому

      My apologies sir, do you make an effort to connect with the kids

  • @davidwanjohi1733
    @davidwanjohi1733 4 роки тому +3

    I salute all musicians from Tanzania!nice song i like it

  • @mohameddaawahkenyatv5529
    @mohameddaawahkenyatv5529 2 роки тому

    Dah hii Nyimbo inanikumbusha zamani sana nilipokuwa darasa la nne kule Kijijini kwetu tulipokuwa naenda shamba kulinda zao la mpunga na Mahindi yasiliwe na tumbiri

  • @careyrume
    @careyrume Рік тому +1

    I miss my mama and my father 😭😭😭

  • @danieljuma1921
    @danieljuma1921 6 років тому +5

    The true feeling of parents separation...

  • @petertosh1057
    @petertosh1057 4 роки тому +1

    Mungu mkubwa.
    In Krefeld,Germany.

  • @whanson2001
    @whanson2001 6 років тому +1

    How can you dislike something like this... Kuna watu wanahitaji kupiwa akili

  • @mordally
    @mordally 11 років тому +2

    ndugu yangu Abdallah nimekuwa naitafuta ile nyimbo ya DDC inyoanza na kusema ''niliusiwa na babu na babu, ukimya busara ndio heshima, maisha bora popote duniani, sio chuki choyo au fitina, '' tafadhali sikumbuki inaitwaje ila utenzi wake unaanza hivyo, tafadhali

  • @user-ov4vo9ly3z
    @user-ov4vo9ly3z 7 місяців тому

    Hisia ni kubwa sana moyoni kutokana na huu wimbo baada ya Allah wazazi ni muhimu katika maisha big up mlimani pack

    • @user-ki1zz9hg6o
      @user-ki1zz9hg6o 5 місяців тому

      Yan acha tuuu nikiusikiliza huu wimbo machoz yananibubujika mno

  • @simbaphonez
    @simbaphonez 7 годин тому

    “MAISHA YA ZAMANI🪘
    Ukienda Kwa Mjomba Unakaa Muda Mrefu Huwezi Kusikia Hata Kelele za Kuchokwa..😭
    Mnakaa Kwenye Mbalamwezi Mnapiga Story..🎑
    Siku Hizi Muda Wote Watu Wanafuatilia Watu Amabao Hata Hawajawai Kuwaona Kuliko Ndugu😥
    HAYA MAISHA YA PESA HAYANA FURAHA KABISA😭

  • @shabanishija3489
    @shabanishija3489 7 років тому +4

    R I P mungu akulaze mahali pema pepon AMINA

  • @edquest5764
    @edquest5764 5 років тому +1

    Haya sasa, zama kweli,
    Hino inanikumbusha Magongo Mombasa 1982 tumehamia Soweto customes
    Mjombangu ametuelekeza radio daresalama
    Dhaaa!!!!! Time fly's Kelli.

  • @najmasaleh9231
    @najmasaleh9231 8 років тому +9

    There is a football made in Spain but there is aRhumba made inTanzania like that one hii sio mchezo mzee Ngurumo ananung'unika mno

    • @yahyasoud7721
      @yahyasoud7721 6 років тому +1

      najma saleh yes yes he was one of the best rip gurumo

    • @chillogeorge1383
      @chillogeorge1383 6 років тому

      Huu ni utunzi wake Cosmas Thobias Chidumule. Na wimbo huu ni kisa cha kweli cha kutengana kwa wazazi wake.

  • @fatumamahanakah8725
    @fatumamahanakah8725 8 років тому

    imenikumbusha mbali sana hasa pale wazazi wangu walipotengana. kweli huu wimbo una mchango mkubwa sana kwa wazazi na wanandoa kwa ujumla......

  • @latasimon5708
    @latasimon5708 6 років тому +1

    Zitaendelea kuvutamba milele tofaut na nyimbo za sku hz ikitoka sku mbili mmeshaichoka

  • @batholomeodonatus3274
    @batholomeodonatus3274 2 роки тому +1

    Daaah ,good music forever
    Very touching song

  • @mwantummakoa4253
    @mwantummakoa4253 5 років тому

    Mamangu nakuombea maisha marefu hapa dunian mungu akuondoshee dhiki na mateso yadunia

  • @danielnjuguna1635
    @danielnjuguna1635 8 років тому +2

    am without words....awesome!

  • @mohamedshineni2122
    @mohamedshineni2122 2 роки тому +1

    Huu wimbo unanikumbusha mbali hadi unanitoa machozi

  • @alexandermkwavi9471
    @alexandermkwavi9471 7 років тому +1

    hii ngoma inaumiza kiakili kwa wale inaotuhusu,akumbukwe daima

  • @henrychaula1174
    @henrychaula1174 4 роки тому +1

    Beat ya hii nyimbo inafanana sana na ile ya Celina

  • @nicksavio3697
    @nicksavio3697 Рік тому

    Ah eeeh mama eeh. Jaribuni kuyasuluhisha mambo hayo...

  • @norbertkyara96
    @norbertkyara96 6 років тому

    Binasfi huwa nazikubali mno hz nyimbo nakumbuka miaka ya 90- nikiwa kijana nlikua Namibia baba dude prufuu yake nakanayo chumbani kipindi hicho rdo Tanzania wanapiga nyimbo hz....

  • @robertmutai3762
    @robertmutai3762 Рік тому

    let me shed torrents of tears......... nakumbuka mbali saaaana..................

  • @richardgaya3965
    @richardgaya3965 3 роки тому +2

    An Iconic number.... shows a band which was not only creative but that which also had its fingers on the pulse of technological changes in both instruments and sound.....The lyrics are something to die for...so is the delivery..... these were always strong points in popular Tanzanian dance music and the trend has continued to date with the younger generation!!!! KUDOS MINGI!!!

    • @gordonnyagudi8166
      @gordonnyagudi8166 Рік тому

      Great observation Richard. Where are you bwana?

    • @catsimcybercafe6024
      @catsimcybercafe6024 Рік тому

      True, their lyrics, music composition is out of this world. Their songs are full of maturity.

  • @ngulathfundikira4205
    @ngulathfundikira4205 4 роки тому

    Zinanikosha sana nyimbo za zamana,jaman vijana wa zaman walifaidi sana

  • @bernhardscharleskogolla8476
    @bernhardscharleskogolla8476 3 роки тому +2

    A real painful experience some go through! May the mighty Lord be their comfort🙏🙏🙏🙏🙏

  • @mariaemmanuel6479
    @mariaemmanuel6479 4 роки тому

    Umenikumbusha mbali sana nikiusikilza unanipa uchungu kipindi Baba na mama wametengana nami Mdogo naumia tu

  • @raskenneth1981
    @raskenneth1981 9 років тому

    Nyimbo hii imenikumbusha enzi za makuzi yangu wakati huo RTD tupo shule ya msingi nk nimekumbuka mengi sana na watu kibao wengine wapo hai wengi Marehemu RIP.

  • @philipachikindubi5128
    @philipachikindubi5128 10 місяців тому

    Nostalgia, how i miss those days i was growing up.when music was music.

  • @mokogotiobwari7697
    @mokogotiobwari7697 6 років тому

    Kama wazazi wangeheshimu watoto wenye Mungu amewabariki nao hakungetokea na taraka......matesoooo...

  • @kennethkilonzo1293
    @kennethkilonzo1293 2 роки тому +1

    Childhood memories in Makande Mombasa

  • @mohamedshineni2122
    @mohamedshineni2122 7 років тому +4

    ukisema cha kale ni dhahabu nadhani hakuna wa kubisha usemi huu NYIMBO ZILIKUWA NA MAFUNDISHO NA HUKUCHOKA KUZISIKILIZA

  • @sibongilemasina8779
    @sibongilemasina8779 4 роки тому

    Weee acha tu, big up DDC nina kumbuka mbali sana wakati niko kijana mdogo sana wakati huo No stress my mum doing everything for me

  • @onesmusouma7109
    @onesmusouma7109 Рік тому +2

    Real music, sweet memories.

  • @ashritaabdallah6474
    @ashritaabdallah6474 4 роки тому

    Rtd huku salam za jambo uku majira uku kipindi cha ugua pole uku mama na mwana duh Sara dumba malima ndelema Ahmed kipozi EDA sanga

  • @nakoemponda6453
    @nakoemponda6453 4 роки тому

    DUUHH NIKO MUSOMA SARAGANA NYAMBONO P/SCHOOL STD 4 1978.RAAHA.

  • @raeloka7642
    @raeloka7642 2 роки тому

    I used to listen to this song,Was in highschool and my father had just married another wife,We Went through Alot,I still listen to it,Am old now and staying with my Mum,
    My dad is still marrying

  • @aishamkomwa6125
    @aishamkomwa6125 5 років тому

    Hii nyimbo imeniliza nimewakumbuka kakazangu nadadaangu pia babaangu kipindi hicho tunasikiliza.kwenye.redio yetu.mkulima.huu.wimbo.kwasasa wote. wamefariki.dah.inauma sana

  • @deogratiuswakwesa5894
    @deogratiuswakwesa5894 5 років тому +1

    Wimbo unaeza kukuliza Kama ni kweli wazazi wako kuna ugumu wanapitia

  • @florakabola4253
    @florakabola4253 7 років тому

    Inanikumbusha mbali sana. shukrani za dhati zimwendee mamangu mzazi Sophia nampenda sana.