JERRY SLAA AMALIZA MGOGORO WA DDC NA WAKAZI WA BUNJU, MBOPO DSM

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 20 січ 2024
  • Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amemaliza mgogoro wa ardhi wa muda mrefu kati ya wakazi wa mtaa wa Mbopo kata ya Bunju jijini Dar es salaam wanaodaiwa kuwa ni wavamizi na Shirika la Uchumi la Jiji la Dar es Salaam (DDC).
    Aidha, amewataka wakazi wa maeneo hayo kuacha kutumia watu ambao sio viongozi wa kisheria ambao wanadanyanya wananchi na kusababisha uvamizi.
    Katika kusisitiza hilo ameelekeza kukamatwa kwa mtu anayejulika kwa jina la Diwani ambaye amekuwa akisababisha migogoro ya ardhi katika meneo ya mtaa wa Mbopo kata ya Bunju jijini Dar es salaam.
    Waziri Silaa ametoa maelekezo hayo kwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule wakati alipofanya ziara katika eneo lililokuwa na mgogoro wa ardhi wa muda mrefu kati ya wakazi wa maeneo hayo wanaodaiwa kuwa ni wavamizi na Shirika la Uchumi la Jiji la Dar es Salaam (DDC).

КОМЕНТАРІ •