RAIS DKT.JOHN MAGUFULI AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE NYUMBANI KWAKE MSASANI

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 10 вер 2024
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kuhakikisha fikra na mipango mizuri aliyoiweka inatekelezwa kwa manufaa ya Watanzania wote.
    Mhe. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo tarehe 14 Oktoba, 2018 wakati akizungumza na Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam alikokwenda kumtembelea muda mfupi baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay.
    Mhe. Rais Magufuli amebainisha kuwa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere alifanya kazi kubwa ya kujenga misingi imara ya nchi kuwa na amani, umoja na mshikamano na pia kujenga misingi ya uchumi wa kujitegemea kupitia Azimio la Arusha.
    Ametoa wito kwa Watanzania wote hasa vijana kuungana na Serikali katika kuyaenzi yaliyofanywa na Baba wa Taifa, na pia kuliombea Taifa.
    Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuendelea kumuenzi Baba wa Taifa na amemhakikishia kuwa yeye na wanamaombi wenzake pamoja na Watanzania wote wanamuombea heri yeye, viongozi wote na Taifa kwa ujumla.
    Aidha, akiwa nyumbani hapo Mhe. Rais Magufuli aliyeongoza na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli amekutana na mtoto wa Baba wa Taifa Bw. Makongoro Nyerere na Wajukuu wa Baba wa Taifa.
    Mapema leo asubuhi Mhe. Rais Magufuli ameungana na Waumini wa Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay Jijini Dar es Salaam kusali Misa Takatifu ambapo Waumini hao wamemuombea Baba wa Taifa, aliyefariki dunia tarehe 14 Oktoba, 1999.

КОМЕНТАРІ • 291

  • @fredytarimo9107
    @fredytarimo9107 5 років тому +262

    Safi sana mjomba.we ndo rais watanzania tumeanza kukuelewa.nchi iko shwari kama unamkubali magu gonga hapa.

  • @70SIXER7
    @70SIXER7 5 років тому +53

    Mungu Amlinde Kaka Yetu Magufuli Pamoja na Very Humble!...First Lady Mama Janet!

  • @rezegerezege691
    @rezegerezege691 3 роки тому +25

    😭😭😭😭😭 R.I.P BABA YANGU NAWE TUTAANZA KUKUOMBEA 17/3/2021 TUTAKUENZI HAKIKA.

  • @Eniola0ne
    @Eniola0ne 4 роки тому +24

    When I saw Madaraka Nyerere at Julius Nyerere International in Dar Es Salaam, I was shock with his simplicity, Not like other African President Sons bragging and strolling in land cruiser. He was just Walking like every Tanzania. I walk past before, I realize that, This Nyerere Son. I wanted take Picture with him, but he already went far. He was very wonderful guy, with his humility

  • @japhetdaud3889
    @japhetdaud3889 5 років тому +43

    JPM unafaa Mungu na akusaadie pia kwa kazi unayoifanya 👍👏👏💪

    • @prospermauki7304
      @prospermauki7304 4 роки тому

      Huyu magufuli ni mfano wakuigwa na kama ukutangulia baba wa taifa basi angekua yeye. Tunakupenda raisi wetu

  • @mumyhendry2919
    @mumyhendry2919 3 роки тому +38

    Baba leo wewe ndio tunakuzungumzia hvyo kweli😭😭😭
    Namuomba Mungu akupe pumziko la Milele Baba🙏🙏🙏

    • @nyotawauniquem7462
      @nyotawauniquem7462 3 роки тому +4

      Mpaka machozi yamentoka 😢😢😢

    • @mumyhendry2919
      @mumyhendry2919 3 роки тому +3

      @@nyotawauniquem7462 pole sana mpndwa,ndio maisha haya kesho hatujui tutaamkia wap

    • @karanichris2007
      @karanichris2007 2 роки тому +1

      Imagine 😭😭😭

  • @abuunomaz2323
    @abuunomaz2323 5 років тому +31

    Rais wangu uko vzr....Mungu ibariki Tanzania Mungu m'bariki Magufuli

    • @peacelove1572
      @peacelove1572 4 роки тому +1

      Amen

    • @aime2937
      @aime2937 3 роки тому

      mungu pokeya mtotoyako rais njoni pombemangufuri tunamuririya Africa yote

  • @nyanchokachacha6975
    @nyanchokachacha6975 5 років тому +33

    Hongera sana RAIS wetu, Mama yetu Janeth, na Bibi yetu Mama NYERERE Mungu awabariki sana na Maisha Marefu.

  • @Eniola0ne
    @Eniola0ne 5 років тому +40

    Tanzanian are Special People, they are kind, humble People
    I am very happy to be associated with this great humble People

  • @mumbisdesigns
    @mumbisdesigns 3 роки тому +45

    I'm watching all of Dr. Magufuli's videos while he was alive and loving him and his pure, kind heart even more. I wish I could have met him. Such loss and pain! Poleni sana ndugu zetu waTanzania, mie mwenzenu hapa USA 😢😢😢😭😭😭🙏.

  • @happinessjoseph3146
    @happinessjoseph3146 5 років тому +26

    Magufuli Mungu akupe maisha marefu baba napenda busara zako

  • @nyanchokachacha6975
    @nyanchokachacha6975 5 років тому +21

    Big up my president I am very happy to see you struggling to bring up Tanzania with industrial Economy.

  • @hasnathamza8438
    @hasnathamza8438 3 роки тому +16

    Hatimae umemfata baba wa taifa pia kakumzike kwa amn bb yetu maguful tutendelea kukuombea kipenz cha watanzania wotee😭😭😭

  • @mansarayify
    @mansarayify 3 роки тому +9

    This man was really humble, I I'm loving him more in his grave than ever even than when he was alive as more evidences of his panafrican spirits are coming out. RIP my hero.

  • @mansarayify
    @mansarayify 3 роки тому +13

    I'm not from Tanzania nor do I speak swahili but i love the humbleness and the peaceful nature of the Tanzanians.

  • @saidbarawa9096
    @saidbarawa9096 5 років тому +18

    Jpm umejaza nafasi ya baba wa Taifa Nyerere vizuri sana kushinda waliokutangulia,heko jpm, heko tena kwa uongozi wako bora,Mimi ni mkenya Lakini naenzi utawala wa Nyerere na utawala wako,mungu akubariki

    • @albertulikaye5951
      @albertulikaye5951 4 роки тому

      Mtu akimsema vibaya Raise wetu mpendwa Dr. Magufuli akili yake haiko vizuri, anatakiwa kuombewa. Raise anayemtanguliza Mungu katika Kila Jambo!

    • @asantekwahuuwimbozubeda873
      @asantekwahuuwimbozubeda873 4 роки тому +1

      Asante baba magufuli kwa wema wako tunaouwona wa kumkumbuka mama maria mke wa baba wa taifa letu la tanzania ubarikiwe sana rais wetu mungu akupe maisha marefu yenye kheri na anae kutakia mabaya mungu amuwaibishe

  • @DottRoBroc
    @DottRoBroc 3 роки тому +7

    I am an italian man. I studied Magufuli, a politician I discovered and appreciated for his complaint against the effectiveness of tampons. He was a great and courageous president, an honest man who had reduced his salary (from $ 15,000 to $ 4,000) defended the interests of the people. I also appreciated his position on covid and against dangerous vaccines. In my opinion they killed him even though he officially died of heart problems. Magufuli will forever remain a political example of integrity for all. I agree about Magulification of Africa!

  • @kabaranamaganga6646
    @kabaranamaganga6646 5 років тому +5

    Ubarikiwe Mh Rais kwa kumkumbuka Madame Maria Nyerere

  • @JoyceAudax
    @JoyceAudax 5 місяців тому

    Asante Sana baba yetu unafa kuigwa kwa kazi yako nzuri unayoifanya mungu akulinde na kukuongoza kwa kila ulifanyalo katika maixha yako yote.Amina tutaixhi Kama alivyotuelekeza 🙏

  • @samuelmusungu1056
    @samuelmusungu1056 2 роки тому +2

    Very humble President,
    I wish I was a Tanzanian...... very calm n with pure heart.
    RIP Rais

  • @mbabaziscovia4832
    @mbabaziscovia4832 4 роки тому +11

    Tanzania's ur so lucky n blessed to be led by a leader who's full of love, humanity n with a mind of peace. Come test museveni, hmmm Uganda is in hell. N thx to Nyerere the work he did on liberating Tz

    • @sylversserubiri3765
      @sylversserubiri3765 4 роки тому +1

      Thanks for your compliment. We need people like us who stand by the truth . God bless you 🙏.

  • @uwamaliyadidacienne6052
    @uwamaliyadidacienne6052 4 роки тому +1

    Nashukulu sana kwa Rais wa Tanzania na unyenyekevu wake Mungu amubaliki,mimi siyo mtanzania lakini napenda Watanzania na Rais wao sana!Mbalikiwe!

  • @kudranyome319
    @kudranyome319 5 років тому +3

    Asante sana mheshimiwa kwa busara zako mungu akuongezee miaka mingi

  • @undulemwakibabala8119
    @undulemwakibabala8119 3 роки тому +2

    Asante Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya Rais Magufuri kwa kuzaliwa Tanzania yawezekana angezaliwa Nchi nyingine lakini ulipenda atokee Tanzania, Nina Imani huko uliko umeshafika kwa Mkombozi wetu YESU KRISTO amekupeleka kwa Muumba wetu 🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼

  • @esaumahundi5076
    @esaumahundi5076 4 роки тому +1

    Mungu akubariki mtumishi wa mungu rais wetu kwa busara zko bwana akuzidishie uheri ukawe na hekima Kama mfalme seleman niwachache wanaofanya hayo tunashukuru baba unaenzi yote aliyotaka mwl tunakushukuru unatengeneza amani ya vizazi vijavyo hutatafuti vya Koko Bari vya Uma sante

  • @sankungyork6665
    @sankungyork6665 Рік тому +1

    I never see a such leader like him in my life a very humble man to earth and he respect everyone

  • @kaobamaabel5561
    @kaobamaabel5561 5 років тому +16

    Jpm,asanteeeeee

  • @edsonlaurencemwagamasasi9074
    @edsonlaurencemwagamasasi9074 5 років тому +3

    Asante Sana kwa Kazi nzuri juu ya kumbukizi ya hayati baba wa Taifa

  • @doramarcel1013
    @doramarcel1013 5 років тому +11

    Huwa unabusara sana J.P.M umefanya jambo jema kbs

  • @apolinashirima7424
    @apolinashirima7424 4 роки тому +6

    Mungu ni mwema kila wakati.

  • @binurusm8886
    @binurusm8886 5 років тому +45

    UnapoComent humu usiongee tu kwa chuki zako, Ni Lini Raisi Magufuli alikataa mfumo wa Vyama vingi, tuwe waungwana Na Uzalendo tuwe nao, huyu Baba anaweza Na Mungu atamlinda tu, acheni chuki binafsi.

    • @priscarchiragi5826
      @priscarchiragi5826 5 років тому

      Binuru Sm hakuna anae mchukia ndugu yangu na pia ujuwe kuwa hata huyu anamapungufu yake na mema yake ila nilazima tuyaseme aache kuuwa wanyinge aache kuteka watu aache kukandamiza wanyonge mi ananikera tu hapo kubukeni hata shetani nae anajifanya mwema ila sio mwema ukicheza nae atakupeleka pa baya

    • @dinawankaba8205
      @dinawankaba8205 4 роки тому

      Binuru Sm mungu akubarika JP

  • @wisdomuta1039
    @wisdomuta1039 5 років тому +6

    Mungu akubariki jpm

  • @abelsabibi6192
    @abelsabibi6192 5 років тому +13

    May God bless our nation,our president together with all Tamzanian's

  • @wilondjanyengawilliam4893
    @wilondjanyengawilliam4893 2 роки тому +2

    je préfère avoir cette gentillesse , cette humilité 🙏🙏🙏

  • @lashansoky1437
    @lashansoky1437 2 роки тому +3

    The humble and kind people don't last long 😭😭😭,, Tanzanians are so simple in the eyes of the Lord .
    Ewe Mungu nipe hii roho katika nchi taifa la Kenya.

  • @saudaligomba600
    @saudaligomba600 5 років тому +10

    Rais uyu uyu anatutosha tumuombeen kwa mungu uyu rais wa watu wote

    • @elizabetymushi2500
      @elizabetymushi2500 4 роки тому

      Mungu peke yake amlinde rais wetu nasi tuzidi kumwombea

  • @pikipikiusedtanzaniacoltd4596
    @pikipikiusedtanzaniacoltd4596 5 років тому +10

    Rais superstar jpm. Mpenda watu na rais unaependwa na wanyonge koteeee inch ata km ukichukiwa basi wachache ila ww km nyerere

  • @masanjawiza1734
    @masanjawiza1734 5 років тому +1

    kwa kweli kazi unayoifanya mheshimiwa tunaiona wananchi wako hongera sana na mungu akuongoze vyema katika utendaji wako Wa kazi

    • @shebysheby607
      @shebysheby607 5 років тому

      Kilambuz atakula kwaurefu wakamba yake ukiwa umetenda mema bs na mungu atakulipa mema kama ulitenda maovu ata tukuombee vp

  • @princesarykhan4761
    @princesarykhan4761 4 роки тому +1

    Mungu akuongoze na akubariki katika kulijenga Taifa letu Ameen

  • @doricatenga4096
    @doricatenga4096 5 років тому +14

    Mama wa kwanza wa Tanzania mama Maria.Magufuli wewe ni mstaarabu mnooooo.big up.

    • @fezahagumi924
      @fezahagumi924 4 роки тому

      Sinazaidi yakusema mungu akulinde mimi ni Mukongo mani goma

  • @gladyssembojas5308
    @gladyssembojas5308 5 років тому +12

    Yeah first Lady original

  • @keithochieng8805
    @keithochieng8805 3 роки тому +7

    Rest well Daddy 💕💕

  • @saumusulaiman4742
    @saumusulaiman4742 9 місяців тому +1

    So sad 😢 dady magufuli wetu na ww tutakuenzi milele ameen😢🤲🤲tutakukumbuka sana dady mungu akupumzishe kwa amani😭😭😭😭😭😭

  • @mahamoudabas8555
    @mahamoudabas8555 5 років тому +1

    Pole mama Maria, badala ya baba wa Taifa Nyerere, waliofatia walikua ni rushwa tupu na tamaa kuiibia nchi na watanzania, lakin kwa bahati nzuri tumempata JPM rais wa ukweli mpiga kazi hata baba wa Taifa huko alipo ana mbariki. Jamani mama Nyerere aangaliwe sana atunzwe huyo mama. RIP baba wa Taifa.

  • @timotheondimbo8322
    @timotheondimbo8322 5 років тому +38

    hata kwenda kumtembelea Mama Maria bado mtu ana dislike, tujitafakari

  • @saumuhassan6365
    @saumuhassan6365 3 роки тому +3

    Rest In peace Rais John Pombe Maguful 17/3/2021, DAIMA nawe TUTAKUKUMBUKA, hakika wewe Magufuli ndio Baba wa TAIFA. 😭😭😭🙏

  • @Okwash1
    @Okwash1 4 роки тому +2

    Tanzanians are very respectful...I can't imagine Moi's or Kenyatta's grandchildren kneeling down for any future head of state.

    • @thebossman4875
      @thebossman4875 4 роки тому

      And this is why I love Tanzania more than any other African country, the respect the people have for each other and their president is extraordinary

  • @gracejohn886
    @gracejohn886 4 роки тому +2

    Asante Rais wetu kwa kwenda kumtembelea Bibi yetu amejisikia vizuri

  • @anifaally1179
    @anifaally1179 5 років тому +2

    Mungu azidi kukupa afya njema nakupenda sana rais wetu

  • @georgemhalla3515
    @georgemhalla3515 4 роки тому +5

    I have nothing to comment ,but Machozi ya furaha yananitoka!

  • @veronicadaniel1122
    @veronicadaniel1122 4 роки тому +3

    Nimependa Nimelia Kwa furaha kumuona bibi maria ana furaha mwenyezi mungu tulindie bibietu WA Taifa 🙏🙏🙏🙏

  • @mugishaherve6854
    @mugishaherve6854 5 років тому +4

    Good president for Tanzania

  • @cassiusniyimpagaritse5347
    @cassiusniyimpagaritse5347 4 роки тому +4

    Raisi Jpm nakosa cakusema ,so mungu akubariki sana

  • @saimonmanyerezi7169
    @saimonmanyerezi7169 4 роки тому

    Napenda the way ulivyomnyenyekev kwa wananchi wa Tanzania na pia mjeuri kwa watu wanaoenda ndivyo sivyo ,big up sana mh.

  • @neemapatrick8293
    @neemapatrick8293 4 роки тому +2

    Huyu ndie raisi anajuwa kuongea kwa unyeyekevu sana na anaofu ya mungu sana mungu akufikishe bali baba

  • @marrysaimon4330
    @marrysaimon4330 3 роки тому +1

    R.I.P Rais wetu twakuombea Mungu akupe pumzika la milele

  • @muchunofrank1326
    @muchunofrank1326 5 років тому +7

    Vizuri sana mheshimiwa

  • @MariamMandi-io5sq
    @MariamMandi-io5sq 5 місяців тому

    Mungu akubariki baba yetu Magufuli popote ulipo.

  • @korongoibrahim3524
    @korongoibrahim3524 4 роки тому

    Dk jpm verr good baba yangu Nirahis wa mfano umeletwa na mungu Asante tunakuombea babayetu

  • @nyanchokachacha6975
    @nyanchokachacha6975 5 років тому +7

    Ni RAIS WANGU ambae nikifuatilia vizuri anaefata Nyayo za Baba wataifa kwan katika kupitia nyaraka mbalimbali nagundua kumbe hadi Stgiler mwalimu aliwaza kuijenga.

  • @user-mn7ic6wt6j
    @user-mn7ic6wt6j 9 місяців тому

    Ubarikiwe sanaaaaaa na magufuli ubarikiwe kwa kuwakumbuka wajane hawa

  • @mudingogo6573
    @mudingogo6573 5 років тому +5

    mm hua napenda unyenyekevu wako tu mungu akurinde jemedari wangu

  • @user-ik6jo6zy2v
    @user-ik6jo6zy2v 6 місяців тому

    Roho inaniuma sana nikikumbuka❤❤❤

  • @danieljohn2741
    @danieljohn2741 4 роки тому

    Ubarikiwe na Mungu akuinue

  • @samnsadhameyer458
    @samnsadhameyer458 4 роки тому +2

    This is Awesome!
    Wow!!

  • @christophercheruiyot5755
    @christophercheruiyot5755 5 років тому +5

    I like this president oo

  • @user-wl8ux7dg7w
    @user-wl8ux7dg7w 10 місяців тому

    Nothing and nothing forever but we shall remember him no where tu see him but too painful for his absence

  • @amranimkakanzi5977
    @amranimkakanzi5977 5 років тому +2

    Ubarikiwe

  • @priscabuzoya3087
    @priscabuzoya3087 8 місяців тому

    Ulale salama mzee, tutaku enzi pia ,milele

  • @edwinc9421
    @edwinc9421 5 років тому +5

    Ubarikiwe , umetuwakilisha wananchi wote

  • @bobm4381
    @bobm4381 5 років тому +4

    Umefanya vizuri Rais

  • @oddahoward4902
    @oddahoward4902 4 роки тому +1

    The best African President.
    May God continue to bless him.

  • @hamiafasta
    @hamiafasta 5 років тому +2

    you are my President and always you bless me on what you are doing,,keep it up

  • @eliuskalangaeliuskalanga104
    @eliuskalangaeliuskalanga104 10 місяців тому

    Duuuu i love you magufuli jembe wa watanzani nilikuwa na mengi sana ya kusema lakini nitayazuia kwa sababu sina mwingine wa kumwambia lakini nitakuombea kwa mungu baba akulalishe mahali salama ❤❤❤ nakupenda sana sana sana sana tena sio kidogo mungu alinde na familia yako yote kwa ujumla milele na milele amen ❤❤❤

  • @mfubwakilua5380
    @mfubwakilua5380 5 років тому +2

    Mungu awabariki woote

  • @godfreymuyenjwa6053
    @godfreymuyenjwa6053 5 років тому +2

    Asante sana.

  • @swalehabdallah502
    @swalehabdallah502 4 роки тому +3

    Kwa kweli hakuna rais kama ww magufuli kwa Africa nzima kwa uongozi bora na mwenye hekima hongera na mola akuhifadhi kwa Shari katika uongozi wako, mm nikutoka Kenya

  • @RepdcObama
    @RepdcObama 9 місяців тому

    Upumuzike kwa Amani baba MAGUFULI

  • @rudakemwafelicien7776
    @rudakemwafelicien7776 5 років тому +4

    Nawashukuru sana wa Tanzania nyinyi muko mufano wawa frica wote

  • @geofreyruta1723
    @geofreyruta1723 2 роки тому

    Inauma sana hata siamini kama hayupo kweli Dunia tunapita

  • @edmondkataya5723
    @edmondkataya5723 Рік тому

    Kila Leo nataka kuona picha za Magufuli, ni rais kwelikweli. Mungu amulaze mahala pema peponi.

  • @angemaguru780
    @angemaguru780 4 роки тому +2

    Asante magufuri ndiye wewe nyerere wapiri Dinia muzima na Afurika .

  • @musamagot6013
    @musamagot6013 4 роки тому +1

    Jpm safii sana ktk marais wote Ww tu nakukubali akitoka nyerere ni ww

  • @sheysarahnjeno5207
    @sheysarahnjeno5207 Рік тому

    Endlea kupumzika BABA WA TAIFA..Pia Endlea kupumzika Hayati JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI,,,

  • @nyangimarwa3448
    @nyangimarwa3448 3 роки тому +1

    Dah 😭😭😭 Kweli kabisa Rais wetu umetuacha 😭😭

  • @isayakimbe9610
    @isayakimbe9610 4 роки тому +4

    Mama amefanana na nyerere

  • @khalfanmustafa6615
    @khalfanmustafa6615 Рік тому

    Mugufuli mungu akulaze mahala pema umetuacha tuna pigwa vibaya

  • @lucasalphonce7820
    @lucasalphonce7820 Рік тому

    Rais Magufuli akumbukwe milele,pia yatupasa kumuombea rais wetu kipenzi mama Samia Mungu amulinde sana.ame.

  • @sheysarahnjeno5207
    @sheysarahnjeno5207 Рік тому

    Endlea. Kupumzika Hayati MAGUFULI 17/3/2021

  • @jacklinmasawe2697
    @jacklinmasawe2697 2 роки тому +1

    Baba yetu umatuacha tutakukumbuka daima milele

  • @ijamboryimana5687
    @ijamboryimana5687 4 роки тому

    From Rda , love you so much magufuri God bless you

  • @deokessy6288
    @deokessy6288 3 роки тому +2

    Daaaa!!! Duniani mapito

  • @shabinahashiri8365
    @shabinahashiri8365 3 роки тому +1

    Kila jambo anastahiki mungu

  • @younglisah5582
    @younglisah5582 3 роки тому

    Leo nimewakumbuka jmn 2021 jumanne ya tarehe 17

  • @lucialeonard6734
    @lucialeonard6734 3 роки тому

    Jambo zuri sana mh raisi umefanya mungu azidi kukupa heri raisi wetu

  • @ignaspius
    @ignaspius 2 роки тому +1

    😭😭😭😭 masikin😭😭😭😭

  • @captenndunga9385
    @captenndunga9385 5 років тому +4

    Hiyo ni nyumba au hizo ni nyumba mana ziko zaidi ya 1

  • @mwinyisiwa-vl3gs
    @mwinyisiwa-vl3gs Рік тому

    Tutakukumbuka Sana baba mungu akulinde uko ulipo

  • @sifangwira90
    @sifangwira90 4 роки тому

    Mungu Asante kwa huyu rais wetu mpendwa,kwa kweli magufuli ni raisi wa watu,mungu amlimde.

  • @jumaibrahim7605
    @jumaibrahim7605 5 років тому +6

    Mweshimiwa Mimi naitwa juma Ibrahim nipo mwanza naomba msaada wa geleji Mimi ni fundi Makenika we ndio mpenda watu na sisi ni watoto wako toka nimeanza kuona malaisi tz Basi akitoka baba wa taifa unakuja wewe hakuna mwingine