Salama Na MASOUD KIPANYA SE6 EP60 | HERI KUFA MACHO… PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460
Вставка
- Опубліковано 27 бер 2023
- #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Habibi Masoud Kipanya ni Ally Masoud Nyomwa ambaye ni LEGEND. Kwa mujibu wake alizaliwa huku kakunja ngumi na dhana yake ni kwamba alizaliwa ili awe bondia! Kwa anacho kifanya na ambacho amekua akikifanya tena kwa ufasaha kwa miaka nenda miaka rudi bila ya shaka ni UBONDIA. Hakuna ambaye atabisha juu ya hilo. Amekua akipigania mambo tele na kuyasemea mengi pamoja na kuchekesha na kuelimisha kupitia kalamu yake. Kwa mujibu wake yeye ni mbobevu katika taaluma ya kupuuza na kuchukulia mambo poa kwa kipindi sasa. Lakini pia anaamini yeye ni MTATA. Tukienda mbele na kurudi nyuma, hapo kwenye UTATA hakuna ambaye anaweza kumbishia, hasa kwa wale ambao kalamu yake imewanyoosha kwa kiasi kikubwa.
Mimi na yeye tulikutana kwa mara ya kwanza takriban miaka kumi na tisa iliyopita, wakati huo mimi mbichi hasa na yeye akiwa kashajielewa na chemchem yake ya kipato tayari ilikua inatoa neema. Mimi nilikua ndo kwanza naanza kazi ya kujishikiza pale Times FM kipindi hiko bado ilikua kule Kamata. Masoud alikua analichorea gazeti la Majira ambalo lilikua liko kwenye mwamvuli mmoja na Radio ambayo nami nilikua nimejishikiza baada tu ya kumaliza skuli. Urafiki wetu ulikuja naturally tu maana sote tunapenda kucheka. Kupitia Zuhura Yunus na Binti mwengine wa kuitwa Rahma ndo mimi naye tulifahamiana. Wakati huo yeye alikua na gari kwahiyo lifti za hapa na pale zilikua hazikauki. Pia tulikua tunaitumia gari yake kama sehemu ya ku chill na kuskiliza muziki kwenye parking za Times FM.
Huwezi kukaa kwenye tasnia moja kwa muda mrefu kama wewe si hodari na mwenye kujielewa. Moja ya vitu ambavyo naviusudu kutoka kwake ni uelewa wake wa mambo tele wa tele, IQ yake ni ya juu sana na jinsi ambavyo ana reason ndo huwa anamaliza kabisa, kama binadamu wakati mwengine ni bora kukubaliana kuto kukubaliana na kwakwe yeye wakati mwengine jinsi anavyo wachora baadhi ya matukio na watu huwa haviishii kuzuri lakini hiyo haikuwahi kuwa sababu ya yeye kuacha kufanya ambacho anakifanya na ambacho amekua akikifanya kwa muda sasa. Uelewa wake kwenye mambo ambayo yanaendelea, uwezo wake wa kuona mbali na kuweka sanaa yake hiyo kwenye karatasi kisha kutuachia sisi tung’amue maana yake kwa kweli ni kipaji cha kipekee ya sana. Mmoja anatakiwa akae tu mbali na ku admire akifanyacho na hiko ndo ambacho mimi nimeamua kufanya.
Nilikua nataka anielezee maana halisi ya baadhi ya michoro yake ambayo iliacha gumzo kwa muda mrefu lakini kwa sababu ambazo niliziheshimu alisema asingependa iwe hivyo, uhuru wa kuwaacha watu watafsiri wao ndo raha ya kazi yake ingawa yeye anajua hasa kwanini alichora na maana yake hasa ni nini! Kwa heshima ya sanaa ilibidi nikubali matokeo. Toka umeanza kumjua na kufuatilia kazi yake, mara ngapi ushawahi kuskia Masoud yuko matatani? Yaani kakamatwa au hajulikani alipo? Kwangu mara kadhaa lakini haikuwahi kuwa kizuizi cha yeye kuacha kufanya afanyacho, kuogopa je? Nadhani kama binadamu kuwa na uoga ni jambo la kawaida, ila unafanyaje baada ya hapo ndo tofauti yetu.
Episode hii inajumuisha karibu yote ambayo niliwahi kutaka kumuuliza, mengine nilipata majibu nlotaka na mengine yalitolewa mbavuni, kwa ki vyovyote vile nili enjoy sana mimi na wenzangu na kutoka kwetu tunatumai nawe uta enjoy kama ambayo nasi tuli enjoy na kujifunza kutoka kwa MWAMBA huyu.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm
ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
UA-cam Link bit.ly/UA-camSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz - Розваги
Masoud aliwahi kunifundisha kuchora cartoon ilikua ni semina ya wikimbili kwa watoto wa shule ya msingi wenye vipaji vya uchoraji yalikua ni maswala ya usalama barabarani shule ya msingi Naura Arusha Central namshukuru sana nilipata basics nzuri juu ya comic na sasa nafanya Graphics web development na 3d graphics making big up to him.
I wonder why hizi doctorate za heshima hapewi Dr Kipanya
Sa ajanunua atapewa vipi na umesikia watu wananunua😂😂😂
Yani yuko very genius
Nadhan busara ilitumika wakaona apewe Babu Tale kwanza
Tatizo mbahili mno huyu jamaa 😅
Masoud ni Kijana wa Sasa anayeishi mifumo ya Zamani, Birthday, Anniversary SIO ISHUUU... Safi sana 👊🏽👊🏽👊🏽
From a Kenyan based in the states: Masoud has that rare quality of exuding wisdom without much affectation, a wisdom that is edifying & actually locally derived. Apwe Heshima Yake! The same can be states of Salama: a wise woman indeed without being off putting & hyperbolic.
Sichoki kumuangalia Kipanya toka mkasi hadi Yah Stonetown bonge moja la kolabo Masoud na Salama
Salama unajua ya jufanya mahojiano mazito yawe kama 'kupiga stori'
Big up sana
We ❤ you masoud kwaajili ya Allah Asante Salama kwa kumleta kipenzi chetu ❤🙏🇹🇿🇨🇭
Kipanya Kama kipanya
Huyu jamaa anahitaji heshima yake 👍
Nakukubali sana Masoud, sijawahi kukereka kwenye interview yako yoyote ile, bro Nakupenda sana 😘 *Masoud Kipanya*
Salama uu mwanamke jasiri na mwerevu sana
Big up
Wewe ni mtu poa sana masudi
Ushauri mzuri sana
Pride of Africa Masoud kipanya
Mzee wa vipanya 🎉
Nimependa sana brother Masoud,nimepata kitu❤️🔥
nimeipenda hii, #siyo issue
Masoud Kipanya ni akili kubwa sana wallah
Incredible interview.
Ahaaaa😀😀😀😀😀 salama bhana
Kiukweli nimejifunza ktu...elimu nzuri sana
Duh Allah amsameh huyo mtu unafurahiya maradhi ya mwenzio kweli
🔥🔥🔥
Masoud is a very smart man aisee.
Salama sasa tuletee Podcast.
Superb interview, never thought KP atakuwa down to earth like this.
Asante Kaka Mosoud kuna jambo nimejifunza kupitia maelezo ya Malcom. Barikiwa sana kwa hili.
Kp 🗽
Mwamba Kabsa, Mtu Makin Jamaa Ambaye Sijawah kuchoka Kumsikiliza Na Kujifunza Kutoka Kwake KP
Umeandikaje hujaeleweka
@@emmamatemu8225 typing error
Nimecheka sana kwakweli
Logic sister salama 👊🏻
Genius
Yaan story ya malcom hua lazima nlie pole sana masud😢😢😢
✌️✌️
nimesubir sana hii yani
Kumbe wengine hawapeleki michango SHUBAMIT..😀😀
I was waiting for this interview so badly.
❤❤❤❤Nimejiona
salama nimependa sana,maswali yako,na jinsi masoud kipanya anavyo jibu,maswali yako,natamani sana kujua jinsi ya kununua hisa
Nafikir ni vyema utafute taarifa za makampuni mbalimbali. Kuna muda wanatangaza hiza
Leo ndo umeamua kuiachia si ndio😅😅😅 haya bwana master mind salama
Hio ya makochi jamani hata mie nilishachanaa😅😅😅😅 daah!! Nilichezea zakufa mtu😅😅😅
Nilikuwa Naisubiliaa Kwa Muda Hii Interview 🏃🏃
Masoud arudishe ile #MaishaPlus
Haya bhana kwa hiyo mmeamua kurudi nyuma miaka,2022 😁
Masudi anamuonekano wa umwakyembe flani ivi
Hilo cheko la Salama
Sister Salama Leo umecheka sana Jamani :), Huu sio 2022 ni 2023.
ni ya muda kweli.. usidhani ni wamekosea. ivi vipindi vingi vya salama ni vya muda.
2022 😀
Jamani tujifunze kupitia interview za ece jay not always tunataka kuona makosa t,ila we need to be strong bhna as broo kp did to handle Malcolm's issues
Akili mingi mno mwamba hasa
Nlijua dr harison 😅
et huu mwaka gani salama
Tuna hitaji elimu kwenye hisa
Kumbe ya kitambo salama 22 tena
13:30 😂
16:10 😂
19:52
22:40 kaka imara sana
Jaman kuna benk flan ilitaka kuanzishwa nikanunua hisa. Huu mwaka wa kumi sijapewa gawio. Inauma jmn
huyu #Mzee Hanaga shidah.
Masoud ni mwamba hasa ila nashangaa kwanini kwenye teuzi zinazofanywa wanamsahau, Ana kitu huyu 😂😂😂😂
Salama ivi nikifikia level gani ya kimaisha naweza fanyiwa Interview na wewe
Hakuna mzee asiyejua siku za kuzaliwa watoto wake huyo mzee mjanja sana namkubali sana big up masoud. Huyu jamaa ni mind reader 😂😂😂😂😂
Kubali ukakae watoto 8 utakumbuka siku zao za kuzaliwa kuna sis unakumbuka siku ya kuzaliwa imepita
Kipanya
Watu wawili wenye IQ kubwa wamekutana.
kumbe ni ya mwaka 2022? Dah
Apo kweny family dah nmechKaaa saNaa Brooo kipaNya! Birthday na hio namba yao Dah! But ....
Making sana,jamaa alinifany nipend kuchor
Mwamba wamda marefu like kwake👊
Salma ume una ma swali 😮
😂😂😂😂 Masoudy kama Masoudy
Shubaamiti😝hapo ndo kashatukana
Tunatak interview yak salama
Yan apatikane mtu wa kumuhoji vizuri kama yeye anavyowahoji wengine
Miaka imeridi nyuma mwaka 2022😂😂😂😂
Wanarekodi kisha wanapandisha muda wowote. Hii ni ya zamani
OPENING YA KIBABE KABISA
Sana
17:00 hizi interview nyingine zilifanyika mwaka jana nini.
Yawezekana naona pia mtangazaji kasema 2022
🤔😂salama hii ni 2022😓🤔realy😳👀😳hii ni 2023 tafadhali✋🏿
Kipindi kilisha recodiwa mzee kama ww ni mfatiliaji kwa tv ungesha jua,humu kwa youtube huwa wanaweka baada ya kuonekana kwa tv kwhyo walio kosa show kwa tv basi utakutana nayo huku
Interview yooteee umeona hilo kosa tu
Interview was badly .salama anakuuliza swali .but swali halijibu anatoa maelezo mengi sana nje ya swali.
Utakuwa unachuki zako tu
I know you was want to act like genius. But wasn't what happens like you was wish .try to listen question carefully before answering questions
Tatizo kujifanya "much know" kiingereza gani hicho sasa wewe chizi? Hujui chochote kipindi kama hiki hakikufai kasikilize singeli ndio saizi yako.
""anivesari""???🤣🤣🤣🤣🤣@masoudkipanya🙌🙌🙌🙌