MAZITO YAIBUKA MGANGA ALIYEFUKIA MTU SINGIDA, WANANCHI WAFUNGUKA MAZITO, WATU 3 WAPOTEA KIJIJIN .

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 9 жов 2024
  • 23.8.2024
    Jeshi la polisi mkoani singida linawashikilia watu 3 akiwemo mganga wa kienyeji ambaye hajaweza kufahamika jina lake baada ya kutuhumiwa kumuua kijana samwaja na kumnyofoa baadhi ya viungo na kuufukia mwili wa kijana huyo katika makazi yake .
    Tukio hilo limetokea katika kijiji cha makuro kata ya makuro tarafa ya mtinko halmashauri ya singida vijijin mkoan singida baada ya ndugu wa kijana raphael samwaja na wananchi wa kata hiyo kumtafuta kijana huyo aliyepotea toka tarehe 8. 8.2024 wakati akitizama mechi ya ngao ya hisani yanga na simba ambapo baadhi ya wananchi walianza kumtilia shaka mganga huyo wa kienyeji aliyehamia katika kijiji hicho hivi karibuni huku akiwa na matukio ya kuchinja mbuzi na ng’ombe za watu katika kijiji hicho licha ya wananchi hao kuripoti matukio hayo kwa viongozi .
    Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya singida godwin gondwe amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akielezea hatua ambazo zimechukuliwa na serikali .
    Licha ya kupatikana kwa mwili huo wa kijana samwaja ukiwa umenyofolewa baadhi ya viungo bado wananchi wa kata hiyo wanaeleza kuwa kuna watu 3 ambao wamepotea katika mazingira ya kutatanisha katika kata hiyo ambao bado hawajapatikana .

КОМЕНТАРІ • 1