Dizasta Vina - Chupa moja ya ziada

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 13 жов 2024
  • Official UA-cam video of Dizasta Vina performing Chupa moja ya ziada Off the album 'A Father Figure'
    Produced and mastered by Ringle Beatz
    Stream/Download Chupa moja ya ziada
    Mdundo - mdundo.com/son...
    Audiomack - audiomack.com/...
    Spotify - open.spotify.c...
    Boomplay - www.boomplay.c...
    Connect with Dizasta Vina on social medias
    Instagram - / dizastavina
    Twitter - / dizastavina
    Facebook - / dizastavina07
    Business: Pan.authentik@yahoo.com
    Website - bio.link/dizas...,
    Lyrics
    Kalala chini ubongo na fuvu vimetengana
    Hatoi sauti hana hata nguvu ya kulalama
    Macho yetu yanagongana ya kwangu yanaona haya
    Natamani kufumba maana naona uchungu kumtazama
    Ni butwaa siwezi eleza hali yake
    Mifupa imezagaa kadhaa haipo mahali pake
    Waungwana wamejaa wanauliza ka' mi' timamu
    Damu nyingi nataka niamini ni filamu
    Hata nikifumba macho naona jambo hili hili
    Nafsi yangu inahofu na inatukana kwa siri siri
    Ameumia siwezi kumtazama mara mbili mbili
    Mguu mmoja umetengana na kiwiliwili
    Kweli nimeamini utu wa mtu ni uhai wake
    Mja amelala watu wamewahi karai lake
    Wengi wanatabiri tanzia bila kuficha
    Wema wanalia na mabazazi wanapiga picha
    Amechanika nyama kuonyesha nyama si tunu
    Anapata maumivu kabla hajaikumbata huru
    Anaonyesha kuwa mwili ni kasha lisilodumu
    Na kujua siku ya uhai kutoka ilivyo sumu
    Mtoto wake analia ameisoma ajenda
    Kuwa baba uhai umetoka na roho yake ishakwenda
    Anahitaji uthibitisho na picha inajieleza
    Ananiona mimi nami sina ninachokiweza
    Natamani niamke nigundue picha nicheke
    Au labda naota ndoto ya kutisha nikeshe
    Huku wapita njia wakipiga kelele
    Kuona mtoto anakuwa yatima milele
    Chorus
    Chupa moja ya ziada
    Chupa moja ya ziada
    Nilipigiwa simu ikisema njoo baa
    Maana mtungi wa nyumbani haunogi
    Nikalewa kisha nikataka kuondoka
    Mpumbavu mwingine akasema one for the .....
    Chupa nikazipanga panga
    Mfuko ulipokauka wakanijaza
    Nikanywa nikijitapa kama mjanja
    Wana wakipiga kelele kuniita
    (mwamba mwamba)
    Sikio la mlevi likashika habari
    Sifa walizonipa zikanishika hatari
    Sikuwaza kuwajibika kuwa nani nitamuumiza
    Nilikuwa mbinafsi kiasi nilishindwa kujali
    Labda ningebakia kwenye kijiwe nongwa cha Biafra
    Ninywe kahawa nikisikiliza soga za siasa
    Ningekunywa kidogo labda nisingerudia
    nimeua mpita njia sababu ya chupa moja tu ya ziada
    Nimefanya kosa na muda unakwenda hasa
    Hasa nitaongea kipi? kipi nitaeleza sasa?
    Sababu chupa moja tu ya ziada
    Mke anamkosa mume aliyempenda
    Mtoto anampoteza baba
    Maji yameshamwagika nani wa kunifundisha lugha?
    Niseme kwa nani ama nani wa kuunganisha nyufa?
    Nani wa kuujuza umma kuwa nami najuta nafsi?
    Nani asimamishe siku kisha akaurudisha muda?
    Malipo gani yakurudisha pumzi kwenye mwili
    Uamke tena? uhai hata kwa hela tu haukopwi
    Adhabu gani itamfaa mpuuzi kama mimi
    Asiyejua maana ya pumzi?
    Maana hata jela tu hainitoshi
    Hata nikiamua kufunga na kuuungama
    Siwezi kuzuia uuma wa watu wakiungana
    Kuamua kumwaga damu kwa mja nilie na laana
    Nife nilipe deni kwa hii dhuluma niliyoifanya
    Muda umesimama moyo unaingia baridi
    Nimemgonga na gari picha inanijia saa hizi
    Mja anakata roho picha inayoingia zaidi
    Ni kuona vibaka wanaiibia maiti
    Chorus
    Chupa moja ya ziada
    Ziada ziada ziada ziada ziada
    Chupa moja ya ziada
    genius.com/Diz...

КОМЕНТАРІ • 518

  • @dizastavinafanaccount
    @dizastavinafanaccount 2 місяці тому +106

    The fact kwamba hii hadithi imesimuliwa kutoka nyuma kwenda mbele is intriguing. GENIUS at work.

    • @abdulshakoursalumsaid7125
      @abdulshakoursalumsaid7125 2 місяці тому +7

      Flashback wanaita 🔥.

    • @mwasavevo
      @mwasavevo 2 місяці тому +10

      Nilikuwa nakufuatilia Toka kipindi Cha sister kadata mpaka Leo huwa najiuliza kuhusu utunzi wako

    • @sangavilley2792
      @sangavilley2792 2 місяці тому +1

      Teacher not sister ​@@mwasavevo

    • @kibwamoko8767
      @kibwamoko8767 2 місяці тому +7

      ​@@sangavilley2792 Yuko sahihi ni Sister Kadata. Vipi umeanza kumfuatilia Dizasta Juzi nini? Sisi tulioanza kufuatilia Mziki wake tangu 2014 tunafahamu ngoma nyingi sana za dizasta ikiwemo sister kadata na album yake ya kipindi kile cha nyuma ya kuitwa Jesusta.
      Na hiyo Ngoma haiitwi Sister Kadata bali inaitwa Sister. Kitu kama hicho.

    • @elishaobadia8829
      @elishaobadia8829 2 місяці тому

      ​@@sangavilley2792fala wewe humjui vina

  • @Suleiman99
    @Suleiman99 2 місяці тому +9

    Nafurahi sana kuona msanii wangu anaingia kwenye trending ingawa yeye sio mtu wa trending ila kazi zake zinampeleka huko

  • @charleskitoki4648
    @charleskitoki4648 2 місяці тому +5

    Hii hadithi imeanzia katikati ikaenda mwisho itarudi mwanzo. Akili kubwa dizasta vina

  • @godfreycleophas1371
    @godfreycleophas1371 2 місяці тому +6

    Kuna wasanii wa hip hop alaf kuna dizasta vina hivi ni vitu viwili tofautii

  • @MKALISHOUSEOFGAME9189
    @MKALISHOUSEOFGAME9189 2 місяці тому +5

    Hip hop itakua mikono salama kama tukiiikabidhishaa kwa dizasta vina

  • @gidylawrence5604
    @gidylawrence5604 2 місяці тому +8

    Wanaojua mziki pekee ndo wanamuelewa huyu mwamba

  • @NewadyNzuyu
    @NewadyNzuyu 2 місяці тому +6

    Uhai hat kwa hela tyu haukopwii 🎉🎉🎉 Nimemgong na gali pich ndo inanijia saizi

  • @HAMISICHOTI
    @HAMISICHOTI 2 місяці тому +5

    Jamn 2semen ukwel hv yupo kiumbe mweny kuijuw fasihi ambaye hampend na hamueli master DzstvN 4 my xide I appreciate ya kuw No one amby anamchkia DzstvN

  • @LandrickXl
    @LandrickXl 2 місяці тому +6

    RINGLE BEATS POPOTE ULIPO TUNAKUSHUKURU SANA MAANA WE NDO KIUMBE PEKEE ULIYEMUELEWA DIZASTA KIPINDI DUNIA IKIJIULIZA 🎉🎉🎉🎉🎉❤

  • @mchinatz6009
    @mchinatz6009 6 днів тому +2

    Kumbe hii nyimbo umeanzia mwisho alafu inaenda mwanzo nimechukua muda sana kuelewa kali sana hii ngoma😂😂😂😂😂

  • @Peterngalula-xo1el
    @Peterngalula-xo1el 2 місяці тому +5

    Kuna mda nawaza Dizasta ndio angekuwa Darasa🤜🤛
    Like comment hii tuipeleke top 5 Trending hii ngoma🔥

    • @SaluMaige-sc8bm
      @SaluMaige-sc8bm 2 місяці тому +1

      Darasa alikuwaga mkali mwanzo lakn akabadilika akaanza utopolo

  • @mchattachattanoga7795
    @mchattachattanoga7795 2 місяці тому +6

    Kama umesikiliza zaidi ya mara moja like hapa

  • @abdulshakoursalumsaid7125
    @abdulshakoursalumsaid7125 2 місяці тому +3

    Katka nyimbo niliyotaman iachiwe ya kwanza hii, bado karbu duniani na last Confession sas na karbu duniani, kwa tulionunua album tujuane..

  • @Black_zero112
    @Black_zero112 2 місяці тому +3

    Oi oi oi oi kama una amini maskio yako yako safe ukumsikiliza dizasta like hapa

  • @navinnia3286
    @navinnia3286 2 місяці тому +13

    Wakenya🇰🇪pitieni hapa tumpe like zake huyu mwamba

    • @kombakomba3854
      @kombakomba3854 2 місяці тому

      Ngoma Kali sana ,mafunzo mazuri respect kwa D vina

    • @SammyMabawasi
      @SammyMabawasi Місяць тому

      Kenya Mombasa ,huku mwamba anajua ...nko na album zake ya jesusta, verteller na wonder boy

  • @AllanSimon-z8t
    @AllanSimon-z8t 2 місяці тому +3

    D vina nakubar unacho kifanya na sio mm pekeangu tuko kama 💯

  • @ibrahimmtema2212
    @ibrahimmtema2212 2 місяці тому +3

    Tuliomsikia Nature hapo mwisho...
    Tuna-Like hapa 😂😂😂😂
    Meen This is Masterpiece

  • @hassanihanzel
    @hassanihanzel 2 місяці тому +5

    Kisengere nyuma

  • @magawila
    @magawila 2 місяці тому +4

    Nilipigiwa simu njoo bar maana mtungi wa nyumban haunogii
    Nikalewa nikataka kuondoka mpumbavu mmoja akasema oya one for the road
    😅😅😅😅😅😅
    Daaagh

  • @raphaelmwangosi9295
    @raphaelmwangosi9295 2 місяці тому +19

    @ringlebeatz hatukadai kwa hii beat mwanang D vina legendary kak daah cjui nseme nn ww ndioo kioo na sanaaa ya wale madog wanayoililia kule mainstream forever legend🙌💯🍾

    • @DIMONKAT
      @DIMONKAT 2 місяці тому +1

      Siri ya Mchezo

    • @JeronimoSimon65
      @JeronimoSimon65 2 місяці тому

      ​​@@DIMONKAT by fid q prod by Ben Mwamba

    • @camsher5972
      @camsher5972 2 місяці тому +1

      Hii beat ni sample ya beat ya siri ya mchezo ya FID Q ft nature

  • @yobrake5856
    @yobrake5856 2 місяці тому +2

    Jana tu ndo nilikua nimrkuja kuangalia kama jamaa ametoa ngoma mpya, kumbe my instincts weren't far from reality,,
    Love from KENYA🔥🔥🇰🇪🤝🏽

  • @derickthabit
    @derickthabit 2 місяці тому +5

    kuna mda uwa nahisi wewe jamaa ni yule roho 7 amna wanao furahia mziki kama wale tunafutilia nyimbo zako 🔥🔥🔥🔥

  • @JuliusMakaya
    @JuliusMakaya Місяць тому +4

    Kama Fid Q Tu Alieleza Wazi Kuwa Hakuna Mwandishi Wa Muziki Wa Hip-hop Kumzidi Dizasta Vina, Jeeee Mimi Nani Nipinge..!!! Big Up Sana Bro Unajua Mpaka Unajua Tena❤❤

  • @AllyHashim-u7x
    @AllyHashim-u7x 2 місяці тому +5

    Dizasta n combination ya rappers wote bongo

  • @MohamedIssa-p2p
    @MohamedIssa-p2p 2 місяці тому +4

    Wa kwanzaaa ❤

  • @YoungKahama
    @YoungKahama 2 місяці тому +5

    HIP HOP is back mpaka uwe na D2 ndo watakuelewa wapuuzi

  • @mtengwadj9390
    @mtengwadj9390 2 місяці тому +3

    Akili mingi Dizasta Vina Sagittarius 🏹

  • @mosesdavid-vm5hk
    @mosesdavid-vm5hk 2 місяці тому +5

    RINGLEBEAT😎🎧🎹📌

    • @navinnia3286
      @navinnia3286 2 місяці тому

      Nlikuwa nasema "wiggo" sikuzote

  • @anoldmmari-mi7qg
    @anoldmmari-mi7qg 2 місяці тому +3

    Bar builder🎉

  • @dausonsamwel7959
    @dausonsamwel7959 2 місяці тому +2

    Kweliiii hii 🔥🔥🔥🔥 kizazi jeuli

  • @timotheovitalis4147
    @timotheovitalis4147 2 місяці тому +3

    Da aseh unakarama sana yan sjapata kuona ngoma zako daa ee tunakukubali👊

  • @ibrahimnjohole1684
    @ibrahimnjohole1684 2 місяці тому +4

    Moja ya wimbo wangu pendwa kutoka kwenye album.....UNAJUA SANA MWANANGU HESHIMA YAKO ZIJE KWAKO.

  • @TellaaxisTz
    @TellaaxisTz 10 днів тому +2

    Katika ngoma dizasta kaimba, ni hii. Kama umerudi zaid ya mara moja tujuane

  • @amoskizigha4781
    @amoskizigha4781 2 місяці тому +5

    Hongera sana wew msikilizaji mwenzangu uliepata bahati ya kumfahamu Dizasta Vina..maana wasio mfaham huyu jamaa wanapitwa na mambo ya msingi sana 😰😰😰

  • @senior1one129
    @senior1one129 2 місяці тому +2

    Dah..!! 🔥🔥

  • @MohamedAyubu-c2z
    @MohamedAyubu-c2z 2 місяці тому +4

    Bro huwa nakusikiliza Sana pia natamani kukutana na wewe kwa sababu Mimi shabiki yako natamani nikupestory ambazo tumepitia kwenye maisha ya nyuma kidogo

  • @EmmanuelGurtu
    @EmmanuelGurtu 2 місяці тому +4

    Hii ni kali Ila siku ukidondosha FANANI lazima ishike number one UA-cam

  • @michaelpaschal5679
    @michaelpaschal5679 2 місяці тому +4

    Vina anaishi kwnye demission ambayO ni miungU tU ina settle .. miaku buku respect dizasta vina

  • @JoelGodfrey-i4i
    @JoelGodfrey-i4i 2 місяці тому +4

    haujawahi kutuangusha MASHABIKI WAKO

  • @kelvinpaul2808
    @kelvinpaul2808 2 місяці тому +4

    Duuuuhhh hizi verses ni high level em tulizeni sikio kwa umakini muone ni namna gani alivyoflow kwa mtindo wa kipekee

  • @mikephototz6624
    @mikephototz6624 2 місяці тому +3

    nyimbo imeanza mwisho ikaja mwanzo...kama umejaelewa sikiliza mara mbili....

  • @MAGIDACHIMIJA
    @MAGIDACHIMIJA 2 місяці тому +5

    DIZASTA TUHESHIMIANE BASI KAKA NAOMBA UTOE CONFESION PART 2. NAKUPA MIEZI6. KILA SIKU NASUBILI PART2 WEWE UKO BIZE TU KUTENGENEZA MANGOMA MAKALI.
    TOA CONFESION OF A MAD MAN PART 2 AMA SIO TUANDAMANE.
    ..... nikatoa visu na nyundo......

    • @leonardmhagama5828
      @leonardmhagama5828 2 місяці тому +2

      Iliisha kibabe sana.....hata ile ya mzee wa kunyonga ganja kwenye plama kaniacha ewan tu😂😂

    • @MAGIDACHIMIJA
      @MAGIDACHIMIJA 2 місяці тому

      @@leonardmhagama5828 huyu jamaa anatukata utamu sana.. yani mimi nasubilia viporo vyetu adi atoe😂 stori nzuri inaisha kikatili afu anachelewesha mwendelezo ku**ke

    • @enerikoselemani8579
      @enerikoselemani8579 2 місяці тому

      ​@@leonardmhagama5828duniani kuzimu kwanni ukeshe kushika protocol wakati ulaji muhimu.

  • @hansharuna
    @hansharuna 2 місяці тому +2

    Tega ndonga uelewe hii imetoka mbele kend nyuma
    Hatar xana vinaaaa

  • @YunusYahya-gr6ks
    @YunusYahya-gr6ks 2 місяці тому +5

    Nkimsikiliza dizasta namuona fid Q kama SAJNA au Ali kibaa jamaa anakaza kinomaa UYO rapcha mnaemfananisha na dizasta ni kumkosea heshima huyuu jamaaa

    • @KlikHapaTV
      @KlikHapaTV 2 місяці тому

      Kuwa na Heshima wewe

    • @KlikHapaTV
      @KlikHapaTV 2 місяці тому

      Hakuna Anachofanya ambacho Fid Q hajafanya

  • @EllyOfficial-ij5yd
    @EllyOfficial-ij5yd 2 місяці тому +2

    Big brain una dunia yako🔥🔥🔥

  • @BarakaZakayo-w1p
    @BarakaZakayo-w1p 2 місяці тому +2

    Mwambaaa nakukubaliii haunagaaa kaziii mbovuu hata sikuu mojaa❤❤❤

  • @Heisbry_
    @Heisbry_ 2 місяці тому +2

    Genius ❤

  • @ibrahimmrutu
    @ibrahimmrutu 2 місяці тому +4

    Hii ngoma n ubaya ubwela

  • @SamwelMakori-i2h
    @SamwelMakori-i2h 2 місяці тому +2

    Kazi safi🫡

  • @AllyHashim-u7x
    @AllyHashim-u7x 2 місяці тому +3

    Dizasta sio wa kwny hii planet salute [rap machine]

  • @ferdnandshija2334
    @ferdnandshija2334 2 місяці тому +4

    Muda umesimama moyo umeingia baridi
    Nimemgonga na gari picha inanijia asaivi
    Mja anakata roho picha inayo ingia zaidi nikuona vibaka wanaiibia maiti.

  • @imanimarandu
    @imanimarandu 2 місяці тому +4

    Hii Material ni TOP SHELF

  • @morganmwaikusa8194
    @morganmwaikusa8194 2 місяці тому +2

    Kuna jamaa anasema kula bia😅😅😅 ila vina ww fala unajua mpk unazingua sana😅😅😅

  • @martjune2734
    @martjune2734 2 місяці тому +2

    Wimbo umeanza mbele umerudi nyuma, waliolewa hili wachache sana

  • @MazulaKwacha
    @MazulaKwacha 2 місяці тому +4

    VINA MWANZO MWISHO

  • @mapheneino
    @mapheneino 2 місяці тому +3

    Mwenye kibichwa kidogo hawezi elewa kitu

  • @staffwamjimpya7210
    @staffwamjimpya7210 2 місяці тому +3

    Sijawahi kukupinga bado

  • @nickman4435
    @nickman4435 2 місяці тому +2

    🔥🔥🔥🔥

  • @soudyruge-fi9xv
    @soudyruge-fi9xv 2 місяці тому +6

    Huyu mwamba hakustaili kuzaliwa Tz maana tunamuelewa wachache huyu ndo the Great Thinker

    • @abdulshakoursalumsaid7125
      @abdulshakoursalumsaid7125 2 місяці тому

      Dah fanani ni moto sana mwanang jamaa kachora sana mule..

    • @gastarmuhangala4506
      @gastarmuhangala4506 2 місяці тому

      Kuna ngoma anasema alikotoka bingwa lakini jamii imeshiba sanaa ujinga ndio maana yeye sio famous

  • @ashuramuhammed3257
    @ashuramuhammed3257 2 місяці тому +5

    Kama hukupita skuli huwezi elewa kilichoimbwa

  • @zamkiller911
    @zamkiller911 2 місяці тому +2

    Noma Sana We Nigga Ni Hatari Sana 💥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

  • @youngzubelyzubely2288
    @youngzubelyzubely2288 2 місяці тому +4

    Hii beat ukiipiga kqenye SPIANO BUFA halafu demu akiwa kitandan anasubilia show,, oyaaa sio powa . Beat inatone za kimambele😅😅

  • @edwinmatuhouseboy6237
    @edwinmatuhouseboy6237 2 місяці тому +3

    Daaa kubababake Bonge moja la Mbupu!!!💥💣🔥🔥🔥🔥🔥🙌🙌🙌

  • @41Company-g5d
    @41Company-g5d 2 місяці тому +4

    Masterpiece

  • @GiggleTz-Himself
    @GiggleTz-Himself 2 місяці тому +4

    That's why he's the goat... The G.O.A.T

  • @sadikimasawa4048
    @sadikimasawa4048 2 місяці тому +2

    G.O.A.T!

  • @taojuma3277
    @taojuma3277 2 місяці тому +1

    Nasikiliza huku Machozi yakinitoka...D Legendary

  • @osiahstimah
    @osiahstimah 2 місяці тому +3

    Fid q pacha nakukubali

  • @alphanlukombe3774
    @alphanlukombe3774 2 місяці тому +2

    Kichwa kinatema madini

  • @SelisiMsuya-ll8rr
    @SelisiMsuya-ll8rr 2 місяці тому +3

    Unyama wa kwenda

  • @GerryAllen98
    @GerryAllen98 2 місяці тому +3

    Beat la kiregendary hili watoto wa 2000 hawawez elewa

  • @kalziidazamba2862
    @kalziidazamba2862 2 місяці тому +2

    Mimi binafsi nakubaliana na uyu VINA.. hakika hii ngoma imefika sehemu salama hapa mozambique 🇲🇿🇲🇿

  • @kaJEMBEvip
    @kaJEMBEvip 2 місяці тому +2

    Mtungi wa nyumban aunogi....njoo bar weee

  • @IsackVedasta
    @IsackVedasta 2 місяці тому +2

    NIPO TOP TWO NA SIO SECOND 🔥

  • @ahmedmasoud3296
    @ahmedmasoud3296 20 днів тому +1

    Ufundi ulotumika ni kama wa Nas katika Ngoma ya rewind ⏪, perfect story telling.
    The best for a reason 🐐

  • @wakitaaofficialaccount4930
    @wakitaaofficialaccount4930 2 місяці тому +2

    Mkali wa hip hop asili hayebaki

  • @Fundikichwa
    @Fundikichwa 2 місяці тому +2

    Ooyaa hii kichwa Ya dizasta ni mashine ingne kbs hapa Tz, uyu jamaa anaweza andikia hta Holywood Movie

  • @theatlastz67
    @theatlastz67 2 місяці тому +1

    TAKUTA NGAZA RASMI @DIZASTA NDIE MSANII NAMBA MOJA WA RAP AFRICA MASHARIKI

  • @officialdinaize
    @officialdinaize 2 місяці тому +3

    My brother 🔥

  • @AlphaxardMakongoro-dc3df
    @AlphaxardMakongoro-dc3df 2 місяці тому +3

    Huyu jamaa ni nyoko aisee❤😊

  • @Raphaeldaudi-q7m
    @Raphaeldaudi-q7m 2 місяці тому +3

    Thanks son.

  • @gimobakari6609
    @gimobakari6609 2 місяці тому +2

    Umetisha mwambaa

  • @Suleiman99
    @Suleiman99 2 місяці тому +3

    No one like d vina
    I repeat this again

  • @mesha_photographer
    @mesha_photographer 2 місяці тому +2

    Noma sana 💯. Gonga like apa kama umeikubali hii ngoma

  • @anoldmmari-mi7qg
    @anoldmmari-mi7qg 2 місяці тому +2

    Chupaaaaaaaa🙌

  • @frankmunisi1883
    @frankmunisi1883 2 місяці тому +2

    Kusanya wana hiphop wa Bongo wote uwafundishe Content... we nimkali zaidi ya xana...

  • @douglaszaidi
    @douglaszaidi 2 місяці тому +4

    GOATED

  • @morganmwaikusa8194
    @morganmwaikusa8194 2 місяці тому +1

    Genius vinna. Fahar kubwa ni kuwa umezaliwa ktk wakt wangu. Sijui ungezaliwa baada ya mm kufa ningejilaumu kwa kias gan

  • @legawayz6093
    @legawayz6093 2 місяці тому +2

    Hip hop mziki wenye tungo imara
    big up D vina👏👏👏
    chupa moja 🔥🔥🔥🔥🔥

  • @YoungKahama
    @YoungKahama 2 місяці тому +2

    Nakubali sanaa vichupa vyako brother sio hao mambwinga wengine wapo wakali lakn Sion wa kukupata

  • @Ndokezi-1
    @Ndokezi-1 7 днів тому +1

    OYAAAH WANNGU NAPATAJE ALBUM YA DZSTVN YA A FATHER FIGURE

  • @RamadanPaul
    @RamadanPaul 2 місяці тому +3

    Dizasta wa moto❤❤❤

  • @trapnondo873
    @trapnondo873 2 місяці тому +2

    Kwa kile kizazi kijachoo....nilikua hapa 2024/7/19🎉🎉🎉🎉

  • @SuleimaniHamadi-o3u
    @SuleimaniHamadi-o3u 2 місяці тому +3

    Vina bad guy appreciate hommie

  • @mrphylophylo7842
    @mrphylophylo7842 2 місяці тому +3

    Hapa hata B mbili huelewi

  • @saurijafary3581
    @saurijafary3581 2 місяці тому +2

    Siku moja natamani nikutane na Dizasta nipige nae story 🫡

  • @nelsontemba-zc4zt
    @nelsontemba-zc4zt 2 місяці тому +2

    Ni dizasta kwa kweli mazingira yanaweza kukunyima utajiri mkubwa sana

  • @asilumnandaje9803
    @asilumnandaje9803 2 місяці тому +1

    Ngoma Kali saa hii D. Vina

  • @godfreygabriel4141
    @godfreygabriel4141 2 місяці тому +2

    Uyu hata nisipo sikilizaaa nanjua tuu ni mwambaaa

  • @ProfessaRashidy
    @ProfessaRashidy 2 місяці тому +1

    Black Maradona...🔥🔥🔥