AMBWENE MWASONGWE: BINTI WA IMANI

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 9 лют 2025
  • Nimeona nikubariki kwa wimbo huu ambao ni ushuhuda wa kweli wa Binti mwenye Imani ambaye nilisimuliwa story yake ya kusisimua sana...
    alikuwa na Nia ya kusoma Ila uwezo haukuwepo na alikuwa amezaliwa hamjui baba yake, alipata kazi Dar, kazi za ndani (housemaid) na akaamua kujiendeleza kwa kumuomba boss wake aende shule...
    na boss wake alikuwa mwema akamruhusu, lakini ombi la pili lilikuwa gumu zaidi, huyu msichana aliomba akamchukue mama yake kijijini aje afanye kazi za ndani badala yake ili yeye akasoma, ili ule mshahara mdogo mama akichukua awe anamtumia shule imsaidie.
    Imani ya namna hii Mungu hawezi iacha ianguke bure.
    Kuelekea ibada ya shukrani pamoja na live recording niliyoiandaa mwezi wa December tar 08 Mlimani City... nitakuwa nikikuletea baadhi ya shuhuda na nyimbo kama hizi ili Imani yako pia iinuke.
    Kama utataka kutusupport kifedha kufanikisha maandalizi ya ibada hii tafadhari wasiliana nami kwa number 0767619931 na 0713619931 Utaongea nami Ambwene Mwasongwe moja kwa moja.

КОМЕНТАРІ • 593