AMBWENE MWASONGWE - NITAAMBATANA (official music video)

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 12 вер 2024
  • STORY BEHIND #NITAAMBATANA
    Yakiwa yamebaki masaa machache wimbo #Nitaambatana uwe hewani. Leo Ijumaa saa 19:00 yaani saa moja usiku. NAOMBA NIKUSHIRIKISHE SABABU YA WIMBO HUU ILIYO NYUMA YAKE.
    Tarehe 15 April 2018 Nilipata neema ya kufunga ndoa na Jaqualine Mushi kwa kipindi hicho sasa Jaqualine Mwasongwe,.
    Tulikutana kwa mara ya kwanza mwaka 2013 tar 4 November siku ya birthday yake, akiwa Mbeya mwaka wa Kwanza chuo cha Mzumbe akisoma Baf (Bacherol of Accounting and Finance) Mimi wakati huo nilikuwa nasoma Diploma Chuo cha uhasibu Mbeya Tia Pia nikifanya DA (Diploma in Accountacy).
    Tulianza vizuri mahusiano yetu na baada ya wiki moja tu presha, misukosuko majaribu yaliibuka toka kila pande, lakini tulisimama kwa msaada wa Mungu hatimaye baada ya miaka mitano yaani Mwaka 2018 Ndipo tukafanikiwa kufunga ndoa, Jaqualine akiwa ameshamaliza Degree yale 2016 nami nikifuatia mwaka mmoja baadaye yaani 2017.
    Tarehe 15 April 2023 Jumamosi tutakuwa tunatimiza Miaka mitano ya ndoa, Unaweza ona tuna miaka 10 tangu tumekuwa kwa mahusiano miaka 5 ya uchumba na 5 ya ndoa.
    Hili kwetu sio jambo dogo hata kidogo, ni jambo kubwa na zito sana ambalo hatujaliacha lipite tu kimyakimya bila kukumbuka na kufanya kitu ambacho kitakuwa baraka, kumbukumbu, na SHUKRANI ZETU KWA MUNGU.
    Tukihesabu tuliyosikia, tuliyopitia, tuliyotenda, tuliyotendewa, tuliyosemwa na kusema tunabaki tunashangaa is imekuwaje tumefika hapa? Jibu ni moja tu BWANA AMETUSAIDIA.
    Sisi hatuna kitu cha kujivuna wala kujivunia tunayaona maisha yetu, furaha, amani upendo, vitu, watu, ndugu, uhai, afya nk Tumepewa tu kwa neema Kwa nini tusimshukuru Mungu kwa haya?
    TUMEANDAA WIMBO #NITAAMBATANA kama zawadi yetu kwa wanaondoa wote, na wale watakaowa na kuolewa mwaka huu, watakaochumbia na kuchumbiwa na watakaobariki ndoa zao... Huu ni wimbo wenu sisi tumewawakilisha tu.
    TUNATAMANI SANA WIMBO HUU UPIGWE KWENYE HARUSI YAKO NA UKAWE BARAKA NA MANENO YA WIMBO HUU YAKAWE MAOMBI YENU NA KIAPO CHENU KWA MUNGU.
    Mkifanya hivyo tutakuwa sehemu ya furaha yenu na tutakuwa sehemu ya familia yenu pia.
    Mungu awabariki sana na ninaamini utaenda kuupokea wimbo huu kwa furaha na amani tele.
    Tunawapenda sana.
    Watch All Music Videos by Ambwene Mwasongwe: • Ambwene Mwasongwe All ...
    Follow Ambwene Mwasongwe
    Instagram: / ambwenemwasongwe_
    Subscribe to Ambwene Mwasongwe: / @ambweneobadiamwasongwe
    Digital Branding & Marketing By:
    Black Ozen Entertainment Limited: / blackozenentertainment...
    #AmbweneMwasongwe #Nitaambatana

КОМЕНТАРІ • 1,2 тис.

  • @ambindwilehosea6837
    @ambindwilehosea6837 Рік тому +178

    Mungu awege na wewe mtumishi Naam anae support Huduma ya mwasongwe like zije hapa

  • @invocavitmbise5296
    @invocavitmbise5296 Рік тому +457

    Kuna siku namimi nitaimba huu wimbo nikiwa nimevaa Pete 2(ya uchumba na ya ndoa) nikiwa na mme wangu halisi...Ameni

    • @neemajulius8017
      @neemajulius8017 Рік тому +25

      Tuko pamoja mpendwa Mungu atusaidie nami ndoto yangu kama yako kuvaa pete mbili💃🙏

    • @invocavitmbise5296
      @invocavitmbise5296 Рік тому +10

      @@neemajulius8017 Ameeni.... Amen...Tutarudi hapa kushuhudia siku moja

    • @misshappie8234
      @misshappie8234 Рік тому +9

      Amen na ikawe hvyo kwako

    • @pendokissatu937
      @pendokissatu937 Рік тому +11

      Pokea Sawa sawa Na uhitaji wako

    • @invocavitmbise5296
      @invocavitmbise5296 Рік тому +7

      @@pendokissatu937 ameni Pendo ubarikiwe

  • @elenlazaro3192
    @elenlazaro3192 Рік тому +57

    Ntaimbaa huu wimbo na mume wangu mwakani in Jesus name....a better marriage is the portion of my life 🙏🤲....am blessed with this song...any one manifesting marriage or anyone blessed drope your likes here formore blessings ❤️❤️

    • @SMEDIA298
      @SMEDIA298 Рік тому

      Kiu yako ikaendelee hata katika maisha Ya Ndoa isishie hapo tu

    • @janety1933
      @janety1933 Рік тому +1

      Mungu akupe haja ya Moyo wako, akujalie sawasawa na neno lake

    • @annamgaya5299
      @annamgaya5299 Рік тому

      Yesu awafikishe na kuwafanikisha

    • @williammbuli4583
      @williammbuli4583 Рік тому

      MUNGU amutendee mtumishi Kwa majira yake sahihi. Pokea katika JINA LA YESU KRISTO. AMENI!!!

  • @boazdanken
    @boazdanken Рік тому +34

    Powerful Kaka Wewe ni Mwalimu Mungu amekuweka Ili uzidi kutufundisha

  • @JanethKapange-wq7iq
    @JanethKapange-wq7iq Рік тому +13

    Naamin kupitia wimbo huu mwaka hautoish nitavalishwa Pete na kufunga ndoa.amen MUNGU awabariki mtumishi

  • @upendodickson897
    @upendodickson897 Рік тому +12

    Huu wimbo niliuona kuanzia day 1: nimetafakari sana maneno ya wimbo huu, kaka yangu Mungu akutunze na kukuimarisha. Najua sio kwamba ndoa yako haina changamoto ila umechagua kumfuata Kristo no matter what. Najua haya maneno yanaweza kujaribiwa ili yaonekane uimara wake; ombi angu kwenu ni kwamba hata wakati wa maneno ya wimbo huu kujaribiwa na kupimwa Damu ya Kristo ikawafunike na mkatoke salama.

  • @praytest6087
    @praytest6087 Рік тому +73

    What a beautiful song, 3 weeks to my wedding and i have got the song to sing with my other betterhalf 😊! God bless all married couples and those about to get married like ours 🙂

    • @dadajoy8684
      @dadajoy8684 Рік тому

      Congrats 🎉

    • @theresiagideon2178
      @theresiagideon2178 Рік тому

      All the best on your wedding, congratulations

    • @maryyegella595
      @maryyegella595 Рік тому +1

      😍same here three weeks to go for my wedding🥰

    • @theresiagideon2178
      @theresiagideon2178 Рік тому

      @@maryyegella595 Our Lord God be with you and your husband to be Mary

    • @maryyegella595
      @maryyegella595 Рік тому

      @@theresiagideon2178 thankyou so much dear🥰🙏🙏

  • @tusekilemwaisabila4603
    @tusekilemwaisabila4603 Рік тому +38

    Hongereni sana.
    Wimbo huu utakuwa baraka kwa ndoa nyingi. Mungu awabariki na awapeni haja ya mioyo yenu. Nawapenda sana.

  • @carolinejohn9201
    @carolinejohn9201 Рік тому +11

    One day yes nitaingia ukumbini nikicheza wimbo huu in Jesus name 🙏🏾

  • @chikumbwilo9565
    @chikumbwilo9565 Рік тому +5

    Chukuliana na lugha yangu,
    Chukuliana na historia yangu,
    Chukuliana na madhaifu yangu,
    Tubebe Yale madhaifu yetu.
    🤲🤲🤲🤲🤲🤲

  • @gideonleonceelias5423
    @gideonleonceelias5423 Рік тому +7

    Nasikiliza hii song nikiwa nina wiki chache tu nime kutana na msichana niliye mtafuta kwa miaka na mikaka. Msichana niliye dhani yumo ndani ya wasichana kumi na tano walio nikataa huko nyuma. Hatimae nakuja kukutana nae nikiwa nimechoka na kukata tamaa. Baada ya kumpata ndio nimegundua kwanini wale wote Yesu aliruhusu waondoke ili niambatane na huyu. Nimegundua amewazidi wote, nimegundua nilikuwa nang'ang'ania moto ambao ungenichoma maisha, sasa niko mahali ambapo mawazo na moyo wangu vyote vina nithibitishia kuwa ni mikono salama.
    Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.
    1 Yohana 2:19
    Asante kwa nyimbo Nzuri, nami nita ambatana nae mpaka dakika ya mwisho nampenda ana nipenda, najivunia naye anajivunia mimi. 💕🌹

  • @benjaminmangu4833
    @benjaminmangu4833 Рік тому +29

    Mbarikiwe sana Mr. & Mrs Ambwene Mwasongwe.
    Hamjui ni ndoa ngapi mnaenda kuziokoa kupitia wimbo huu.
    Hamjui ni watoto wangapi mnaenda kuwaokoa waweze kuishi pamoja na Baba na Mama zao bila kutelekezwa.
    Mbarikiwe tena na tena 🙏🙏🙏🙏

  • @veronicalufingo3513
    @veronicalufingo3513 Рік тому +10

    Nikibahatika kufunga harusi ntatumia hii nyimbo kumtafuta mchumba angu siku ya sendof ❤😢

  • @ndavadumayai4250
    @ndavadumayai4250 10 місяців тому +5

    Wifi yetu mzuri jamani, Mungu awape maisha marefu yenye furaha

  • @saraphinajohn9112
    @saraphinajohn9112 Рік тому +9

    Kuna siku na Mimi nitampata ambae nitasema huyu ndie nyama katika nyama zangu, mungu nipe hitaji la moyo 🙏 wangu

  • @rahelwilson4824
    @rahelwilson4824 Рік тому +6

    Wimbo umetoka cku ya anniversary ya miaka miwili ya ndoa yetu, trh 16, mm na mme wngu tumebarikiwa sana na tumejifunza kitu kutoka kwenu,barikiwa sana na Mungu akumbuke hitaji la mioyo yenu🤗

  • @elishazanzibar979
    @elishazanzibar979 Рік тому +9

    One day i will get the only one for me and i will move with her to the next step 😢🎉let me keep things holly for her

  • @juddiegodlove4563
    @juddiegodlove4563 Рік тому +10

    Mh sie tulio Single tujuane Kwa like 😭

  • @nancyg8664
    @nancyg8664 Рік тому +6

    Mtumishi unamama mzuri😅,
    Nabarikiwa sana na huduma yako

    • @felixlewa
      @felixlewa Рік тому +1

      Kumbe kaona vile 😅😅😅

  • @heriethgoodson8874
    @heriethgoodson8874 Рік тому +6

    Ipo siku ambayo naamini haipo mbali nitaambatana na wangu aliyeumbwa kwaajili yangu eeeh Mungu nakusihi nikumbuke katika ili🙏🙏

  • @kissesmariesydney1523
    @kissesmariesydney1523 Рік тому +11

    Na mie nimekuja💛😘😘sikiliza wa kwanzaaa❤❤❤bless nyimbo zako znatubariki sanaaaa..... Mungu azidi kukutunza mtumishi wa Mungu na famlia yakoo. Likes jmn nirud sikiliza tenaa🎉

  • @stephaniejeremiah9566
    @stephaniejeremiah9566 10 місяців тому +6

    ❤❤❤ww ni nyama ktk nyama zangu❤❤❤ kula chuma hikooooo🎉🎉🎉🎉

  • @wilfredlazarus8130
    @wilfredlazarus8130 10 місяців тому +4

    Brother, umenifanya ni urudie wimbo huu mara kwa mara, HONGERENI SANA na MUNGU AWABARIKI sana... Kazi nzuri...mmeutendea haki wimbo, umetulia ile haswaa...Big up

  • @SaraphinaKasinje-yx4ne
    @SaraphinaKasinje-yx4ne Рік тому +4

    Najikuta nina smile peke yangu kama nimeimbiwa mimi 😂😂, barikiwa Kwa wimbo mzuri

  • @evilahmponzi2768
    @evilahmponzi2768 Рік тому +4

    Mweee ka mke kazuri saana ila hongera Sana br Ambwene naamini ntaingia na hii wimbo Nov kwenye ndoa yangu🥰🥰🥰

  • @lilyluholela8924
    @lilyluholela8924 Рік тому +11

    Libarikiwe tumbo lililombeba Ambwene

  • @IshimweNdikumana-td9es
    @IshimweNdikumana-td9es Рік тому +7

    Mlio mawindoni Mungu atafanyiwa wepesi
    munaowindwa Mungu awaonyeshe wawindaji wawaone❤❤❤

  • @DonathaMgimwa-xg1ih
    @DonathaMgimwa-xg1ih Рік тому +6

    mungu anisaidie niendeelee kuambatana na mme wangu hadi mwisho wa maisha ya hapa duniani

  • @halibesthb
    @halibesthb Рік тому +6

    Kwenye harusi yangu lazma niuilbe uwimbo pamoja na mke wangu mtarajiwa,,, naupenda sana , Mungu awa bariki

  • @agnesmhindi3520
    @agnesmhindi3520 Рік тому +17

    Woow wimbo mzuri, Mungu anijalie mwenzi mwema wa kuambatana nae. Amen

  • @dorahyohana7238
    @dorahyohana7238 Рік тому +7

    Namwamini mungu nami nitafunga ndoa nasubiri wakati wake

  • @stephenshapa3441
    @stephenshapa3441 Рік тому +7

    Anayependa kusoma Bible college kwa njia ya online class, weka namba yako nikuunge, kwa ni BURE kabisa, kwa Mwaka mmoja

  • @sashalemmoh3264
    @sashalemmoh3264 9 місяців тому +4

    Mumgu awalinde ❤❤.japo asanteni maana sitopatatabu yakutafuta nyimbo sikuyahalusi yetu mimi nayule ambae mungu atanibalikia ❤

  • @maxmilliangabriel5244
    @maxmilliangabriel5244 Рік тому +1

    Kati ya watu ninaowajua wamebahatika kuwa na wake warembo ni ambwene, pastor Nick shaboka, masanja...na mimi

  • @merceyallen24
    @merceyallen24 Рік тому +8

    Mungu wako atakuwa wangu,Na watu wako watakuwa wangu..Mungu atoe adhabu kali Kama nitatenganishwa na Wewe,chukuliana na lugha yangu,Chukuliana na historia yangu,Chukuliana na udhaifu wangu.... Hallelujah hallelujah!!! This song🔥,Ndagha Mwee...🌟

  • @SamsonEzekiel-or9xc
    @SamsonEzekiel-or9xc 3 місяці тому +2

    Nakula mziki mnene wa ambwene unadunda balaaa navyopokea masikioni mwangu unachuja balaa safiii ambwene nabarikiwaaaaaaa

  • @waringawajomo26
    @waringawajomo26 11 місяців тому +9

    Wimbo ya harusi nimepata,Bado mchumba sasa

  • @josephfungwa5719
    @josephfungwa5719 Рік тому +22

    ❤️❤️ Watu wako watakuwa watu wangu!! Mungu wako atakuwa wangu 🔥🔥

  • @KideNetworks
    @KideNetworks Рік тому +4

    Baada ya kuachilia, Mungu anatutumia ambao wataambatana nasi ...Thanks Ambwene.Mungu astawishe huduma yako..

  • @assuntamtewele8757
    @assuntamtewele8757 Рік тому +2

    Hakika nilikua nawaza wimbo wa harusi yangu kwakwel nimeupata weeee barikiwa sana mtumish

  • @jewelltruphena5478
    @jewelltruphena5478 Рік тому +11

    ❤❤woow. Finally a love song which is purely scriptural. Must use in my wedding God willing

  • @CalstarHuligha
    @CalstarHuligha 17 днів тому

    Eeeh Baba uliye juu mbinguni naomba nioatie wa kufananaa na mimi❤❤🙏

  • @faithmsungu3272
    @faithmsungu3272 Рік тому +5

    Amina namim naamin nitampata wa kuambatana nae had mwisho wa Maisha.

  • @HancePeterson-f1n
    @HancePeterson-f1n 4 місяці тому +2

    Safi sana shemeji yetu, dada yetu Jackline safiii...

  • @neemaothiniel4906
    @neemaothiniel4906 Рік тому +3

    2 weeks ago mume wangu aliniambia kila neno lille kwenye wimbo huu. Kusikia wimbo huu nimejikuta natambua ukubwa wa maneno yale na nimejikuta namshukuru sana Mungu. Once again Barikiwa sana Mtumishi naendelea kubarikiwa na utumishi huu na nakuombea Mungu aendelee kukutumia.

  • @floraomary7335
    @floraomary7335 Рік тому +1

    Playlist imeongezeka nasubiri Mungu afanye wepesi neno lake litimie

  • @hildamaziku4385
    @hildamaziku4385 Рік тому +3

    Kama Kuna mwimbaji Bora Tanzania Ni wewe Ambwene..nyimbo zako.huwa Zina ujumbe mzito siku zote.Mungu awe nawe siku zote

  • @sophiekivuyo6028
    @sophiekivuyo6028 Рік тому +1

    woooooooooooooooooooo❤❤❤❤❤❤❤❤ nyingine ikijaa wifii aimbeeee kabisaaa😂😂😂

  • @lucyringo4487
    @lucyringo4487 Рік тому +4

    Hatimae tumepata Wimbo wa kuingilia kwa harusi yangu🙏🙏🙏🙏hongr sana kaka Ambwene

  • @jacksonmenas6026
    @jacksonmenas6026 Рік тому +4

    Asante YESU niombi langu unipe mke mwema na mzuri ili niimbenae huu wimbo😍

  • @jangel203
    @jangel203 Рік тому +6

    Nina hakika nitapata wa kufanana nae atakaejua maana na thamani ya mke na ndoa naamini wakati wa Mungu ndio wakati sahihi.🙏

  • @mosesmkemwa1270
    @mosesmkemwa1270 Рік тому +7

    Hongera sana Ambwene. Wewe ni zawadi na hazina kubwa kwa jamii yetu!

  • @user-sg4kd2xc1d
    @user-sg4kd2xc1d 10 місяців тому +4

    🎉🎉🎉mungu kanipe ushuhud kupitia wimbo huu kabla ya mwaka kuisha

  • @markroy9170
    @markroy9170 Рік тому +4

    Kenya tumekubali kabisa Ambwene,,,huwa napendezwa Sana kuona vile Mungu ukutumia kuhubiri ujumbe wa upendo...ndoa nyingi zimepona kupitia huu wimbo kwa jina la Yesu.lets believe together 🙏❣️🥰

  • @rachelnicholaus
    @rachelnicholaus Рік тому +3

    Kaka abwene ubarikiwe mnooo,kaeimbo kazuri jmn,mungu nibariki namm hako kaeimbo nikaimbwe ukumbini nikiwa na mume wngu ,Ila namuamini MUNGU wngu kwa Hilo iko day

  • @dianamsuya4854
    @dianamsuya4854 Рік тому +4

    Kupitia huu wimbo mungu atafanya jambo maishan mwangu nitapata wa kuambatana namim

  • @salmamacha9434
    @salmamacha9434 Рік тому +5

    Yani Mimi nyimbo za Ambwene huwa zinanibariki sanaaaaaa,big up for a good song!

  • @FausterNgusi
    @FausterNgusi Рік тому +1

    ❤❤❤❤Mungu awabariki😭😭 Hapo kwenye kuchukuliana huwa na pagum kwa wengine utakuta mtu unamvumilia lkn yy anakutangaza mabaya kwa ndg wa pande zote mbili inauma sana

  • @marycharlesnyilu8251
    @marycharlesnyilu8251 Рік тому +4

    Wimbo mzuri saana kwa wanandoa ,Mungu AWABARIKI na nawatakia anniversary nyingi pamoja zijazo.Ninawapenda

  • @janethjackson9774
    @janethjackson9774 Рік тому +7

    Mungu nijalie nipemume kama mandiko yasemavyo

  • @vickynduku4753
    @vickynduku4753 Рік тому +5

    This will be my wedding song very soon

  • @shadukalangali6003
    @shadukalangali6003 Рік тому +1

    Yaan Nikirudi likizo huu ndio wimbo wangu pendwa takuwa mda wote nasikiliza nikiwa na mke Wangu Barikiwa Sana kaka

  • @purityndungwa788
    @purityndungwa788 Рік тому +9

    God. This is the song I would like to play as I walk down the aisle.

  • @petrojoel7644
    @petrojoel7644 Рік тому +5

    Hakika Mtumishi AMbwene Mungu akupe maisha marefu

  • @SuzanaJohn-pm6bj
    @SuzanaJohn-pm6bj Рік тому +3

    Kwakweli wimbo huu ukawe mwangaza katika maisha yangu ninapigwa vita sana juu ya swala langu la kuolewa

  • @habilimhapa
    @habilimhapa Рік тому +2

    Mungu akubariki Minister, Mungu akubariki familia hadi kizazi cha nne #Ambweneobadiamwasongwe

    • @elizasamaytu1065
      @elizasamaytu1065 Рік тому

      Ubarikiwe mtumishi wa Mungu,wimbo wenye funzo Kwa vijana na wanandoa. 🙏🙏

  • @florencemakaranga4787
    @florencemakaranga4787 Рік тому +6

    I receive this Blessings in Jesus Name🤲 Amen. It's a complete vow of Forever. Be blessed Sana Mtumishi wa Mungu.

  • @rachealjackson1312
    @rachealjackson1312 Рік тому +4

    Mungu napokea kwa Imani mabinti zako weng wanahitaji uwafanyie kupitia huu wimbo n kama nmegive up 😢

  • @patriciawanjiru3154
    @patriciawanjiru3154 Рік тому +3

    Hope one day God will bless me and this will the song of the when we are taking our vows 😭😭😭 wherever my husband is please locate me 😭😭...nimejiuza kimili Uli kuliea watoto wangu pekee yangu hope Mungu atafungua njia Na kunipumzia Haya yote 😭😭

  • @TungibwaghaKibasi
    @TungibwaghaKibasi 3 місяці тому +3

    Barikiwa mtumishi wa bwana unanibariki

  • @bethtobbyangelic.1622
    @bethtobbyangelic.1622 Рік тому +4

    Woooooow...... And it shall come to pass in my life. God's time Is the best.

  • @franciscamtolihela6277
    @franciscamtolihela6277 Рік тому +1

    Ambaye amejisikia kutafakari na kutoa machozi ya moyoni weka like yako hapa tuungane

  • @fridasosovele7481
    @fridasosovele7481 Рік тому +3

    New arrival....God bless you,ndoa nyinginzikainuliwe kupitia ujumbe wa wimbo huu🙏

  • @AgnesHillary-js4hd
    @AgnesHillary-js4hd Рік тому

    Yani ambwene anasauti ya kupenya uvunguni mwa mioyo ya watu na nyimbo zake zinabalikii na kutufundisha kumwabudu mungu tyuu

  • @user-ik6en7nc6m
    @user-ik6en7nc6m Рік тому +4

    Wimbo wenye nguvu na ahadi nzur kwa wanandoa ubarikiwe kaka Ambwene

  • @jessemushashu2507
    @jessemushashu2507 Рік тому

    Pongezi kwako Kaka Ambwene
    Utukufu nikwake Mungu alieruhusu yafanyike haya

  • @AnaEliasi-vl8ni
    @AnaEliasi-vl8ni Рік тому +7

    Wengi huanza katika roho walakini humaliza katika mwili

  • @upendomassawe2386
    @upendomassawe2386 Рік тому +3

    Waoo wimbo mzur Sana jamn ubarikiwe sana kwa wimbo huu na ubarikiwe sana kwa kumthamini mkeo
    Mungu akawape mwanzo mzuri na mwisho mwema mbebe maono yenu kwa pamoja .

  • @JKINGS123
    @JKINGS123 Рік тому +6

    Hizo trumpet 🎺🔥🔥 such an awesome song GOD bless your work

  • @nghindimakoye4139
    @nghindimakoye4139 Рік тому +4

    Nabarikiwa sana na huyu mtumishi wa mungu
    Hakika mungu aliishusha karama pahali sahihi

  • @lovenesskalenge2683
    @lovenesskalenge2683 Рік тому +3

    Kwa wanavyonisema vibaya hata sijuhi basi Mungu nasubili wakat wako.

  • @danielnjella4760
    @danielnjella4760 Рік тому

    Mungu awe nawe,,,,ilA visuluali kwa mabintk au waimbaji wako,huwa vinapelekea kuharibu namna ya utazamavyo .wambie watches kabisa.

  • @annwanjiku622
    @annwanjiku622 Рік тому +4

    Wimbo wa harusi tayari..Mchumba njoo niko tayari.🎉🎉🎉🎉

  • @AmaniPFungo
    @AmaniPFungo Рік тому +11

    beautiful love song , inspired by the holy scripture. Safi sana Mtumishi

  • @sitikatembo5835
    @sitikatembo5835 Рік тому +9

    Watu wako watakuwa wangu, Mungu wako atakuwa Mungu wangu🎉❤❤❤❤

    • @mshindindidi2240
      @mshindindidi2240 Рік тому +3

      Amina blessed song Mtumishi wa bwana itaokoa ndoa nyingi zinazotaka na zilizovunjika ktk Damu ya Yesu kristo wa Nazareth

    • @rosemwaijande3391
      @rosemwaijande3391 Рік тому +2

      Wimbo unasisimua saana kweli Mungu atusaidie kuambatana na weza wetuzhadi mauti

  • @atuganilekalinjila8385
    @atuganilekalinjila8385 Рік тому +2

    Wimbo wa maharusi 2023❤ tayari tutafute sasa mashela

    • @ezyjob5083
      @ezyjob5083 Рік тому +1

      😂kwakweli, pia tupate mabwana harusi 😅

  • @christinekioko3948
    @christinekioko3948 Рік тому +3

    Been praying for a soul mate,God I need to be loved,I need a man who loves you, he'll love me back🤲🤲😭

    • @Gr9814
      @Gr9814 11 місяців тому

      Aaww Christine your words got me emotional. I speak the Grace of God upon your life in Jesus name Receive a husband after God’s own heart. Amen

  • @glorysangei5387
    @glorysangei5387 Рік тому +3

    Blessed song ever.yaan sichoki kusikiliza...."watu wako watakua wangu,Mungu wako atakua Mungu wangu" hakika Namshukuru Mungu ndoa ni baraka ya ajabu ambayo inatakiwa iatamiwe na Mungu sio motivation speaker,wadhamini au makungwi....Barikiweni sana watumishi wa Mungu .

  • @naominyanzilamachongo9642
    @naominyanzilamachongo9642 Рік тому +7

    "MUNGU ATOE ADHABU KALI KAMA NITATENGANISHWA NA WEWE"
    Ubarikiwe mno mtumishi wa Mungu

  • @joshuamariki1734
    @joshuamariki1734 Рік тому

    Mm napenda tu Namna Ya Mkewako. Hakika kunawatu tukiwaona inabidi tumtukuze Mungu tu. Ni mtaratibu, Mpole na mengine Mengine

  • @Pastor.Joseph_Mwakatobe
    @Pastor.Joseph_Mwakatobe Рік тому +3

    Wimbo mzuri sana Tena Kwa mifano kutoka katika Biblia mbarikiwe sana umenigusa sana

  • @estomngwema6705
    @estomngwema6705 Рік тому +2

    Hatimaye nimepata wimbo wa siku yangu ya harusi😊

  • @aidancharlz3724
    @aidancharlz3724 Рік тому +20

    Meanwhile on this weekend with a gospel healing song❤️

    • @saikonelson9110
      @saikonelson9110 Рік тому

      Ubarikiwe saaana kaka hakika ninahuishwa saana na huduma yako

  • @Destin-b.12
    @Destin-b.12 Рік тому +1

    Napenda kazi zake

  • @zakayozacharia8202
    @zakayozacharia8202 10 місяців тому +4

    Heee mungu niguse na Mimi

  • @ScolaMichael-to4ev
    @ScolaMichael-to4ev 8 місяців тому +2

    Barikiwa sana mtumishi utoe video nyingi zaidi ya hii MUNGU akutangulie

  • @tumainkaduma6057
    @tumainkaduma6057 Рік тому +3

    Waaoooo maneno mazuri ya Ruth kwa Naomi ndio maana napenda nyimbo zako

  • @janethjkavishe589
    @janethjkavishe589 Рік тому +2

    Nice Song. 99% ya nyimbo zako ninazipenda na kuzisiliza. Umebarikiwa.
    Kwa yeyote mwenye kitaka kumfahamu Mungu zaidi asikilize nyimbo za Ambwene Zina jumbe nzito sana.

  • @jeps.e4305
    @jeps.e4305 Рік тому +7

    Congratulations for this beautiful song Ambwene.
    Watching from Europe

  • @NashipaiLaiser-it1ob
    @NashipaiLaiser-it1ob Рік тому

    Kuna watu walikuwa wanafikiria entrance song ya wedo Yao. Couple wauchangamkie Kwa kweli. Mzr for entrance