"Mwana FA Alinipigia Simu, Ikabidi Nitorokee Hostel Kuja Dar" | SALAMA NA MAUA SAMA PART 1

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 5 вер 2024
  • #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
    ARCTOTIS
    Imagine siku moja usharekodi video yako kama msanii anaye chipukia alafu unaenda kumuonyesha ‘Boss’ kwa mbwembwe zako zote, pale mezani mwake unamkuta anaangalia video ya msanii mwengine na kuisifia sana, huku akikuambia wewe kwamba ile sasa ndo yenyewe, ndo njia sahihi huku akiwa hata bado hajaiangalia video yako. Utajiskiaje? Utaondoka au utabaki? Utanuna au utaskiliza kwa roho safi na kwenda kuhakikisha unayafanyia kazi yote aloambiwa? Kumbuka pia huyo ambaye umeonyeshwa video yake yeye ana support kibao, support ambayo wewe unaitamani hata robo yake na ki ukweli kwa juhudi zako ukipata basi ilikua kutoboa ni LAZIMA.
    Hii ni story ya Mauwa Sama ambayo ukimpa sikio au macho na ukamskiliza vizuri basi niamini mimi utakua umefanya jambo la maana sana na nakuahidi utajifunza mengi sana. Mauwa alitokea kupendwa tu na Mwana FA ambaye yeye anamuita ‘God Father’ wake kwa jinsi ambayo alifanya na anaendelea kufanya mengi ambayo yamemueka hapa alipo sana, hapa ambapo mimi na wewe ndo tumepata kumfahamu vizuri na kuwa shabiki yake. Ingawa mimi nakumbuka siku ya kwanza ambayo Mwana FA alinisikilizisha wimbo wa Mauwa ya kwanza ambayo ilibamba huko mkoani Moshi, jinsi Hamis alivyokua anaongea kwa excitement, pale tu niliamini alikua kwenye mikono salama. Baada ya hapo alipovutwa kuja Dar napo pia nlikua na pata kipaumbele cha kuskiliza ngoma zake kabla hazijatoka.
    Kufanya kazi kwa nguvu, kujitolea, kujitoa na kuchukua risk ni moja ya mashimo ambayo Mauwa aliweza kuyafunika vizuri, humu anatuhadhithia jinsi ambavyo Mama yake alimsaidia kupata ruhusa ya kuja Dar kwa mara ya kwanza kuonana na Mwana FA ambaye alimuambia aje, ila alipofika sio Mwana FA ambaye alimfuata badala yake alikutana na mtu mmoja mrefu mwenye mabega yanayoanzia mlango huu mpaka mlango ule, anasema alishtuka maana hilo halikua tegemeo lake, yeye alijua akifika basi atakutana na Mwana FA na mambo mengine yaendelee kutokea hapo.
    Purukushani, maneno, scandal, kupanda, kushuka na kupanda tena na tena kwa Mauwa Sama ni khadithi ya kusisimua, na yeye si muongeaji saaana ila kwa kiasi flani tuliweza kupata chochote kitu. Story ya familia yake na masomo ambayo wazazi wake walimkazania ayamalize ndo moja ya silaha zake kubwa kwa sasa, anaamini kwa jinsi ambavyo wazazi walimlazimisha kumaliza masomo hiyo ndo kitu ambacho kinamtofautosha yeye na wasanii wengine kwa umbali mkubwa hasa.
    Rafiki yangu matumaini uta enjoy na kama ilivyo kawaida yetu pia imani ni kwamba utajifunza kadhaa ambayo yatakusaidia huko mbeleni.
    Nikutakia Kheri ya Mwaka Mpya, Rafiki.
    Amani,
    Salama.
    Support us through anchor.fm/yahs...
    SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
    Listen our Podcast on
    Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
    GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
    Audiomack Link bit.ly/YahSton...
    ‪UA-cam Link bit.ly/UA-camS...
    Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown
    Channel Administered by Slide Digital
    Instagram: slidedigitaltz

КОМЕНТАРІ • 47

  • @abubakarsuleman1983
    @abubakarsuleman1983 Рік тому +1

    Mungu amlinde mtu wangu mwana fa , ndio maana mungu anambaruki af kwa wema wake.

  • @rommelmauma8081
    @rommelmauma8081 2 роки тому +3

    Mahojiano hujenga mazingira ya aina fulani. Na mazingira hayo yana vigezo vyake: washiriki, kusudi / lengo, mipaka, lugha ikiwa ni pamoja na mengineyo ya mbwembwe za mwili, nk.
    Runinga haiitaji mbwembwe nyingi za mwili; la sivyo, mzungumzaji ataonekana kama dude tu. Hakuna kinachochafua mazingira ya mazungumzo kuliko kuchanganya lugha, yaani, mseto wa lugha.
    Ushauri: Endapo kweli Tanzania yetu inataka kutoa mchango wake kwa Afrika na nje, yafaa sana lugha hii itumike ipasavyo bila kuichanganya na Kiingereza.
    Mwisho, Kiingereza neno *ask* au *asked* si *aks* au *aksed*, kama 'linavyovurundwa' na baadhi ya Wamarekani wengi.

  • @fatmasalim8293
    @fatmasalim8293 2 роки тому +4

    Nakupenda sana sister salama mashallah ❤❤❤❤🥰🇴🇲🌹

  • @Tino_Official_tz
    @Tino_Official_tz 2 роки тому +1

    Waow!! what a story!! Nafikiri inabidi uandae movie kabisa

  • @SaidSaid-ef8md
    @SaidSaid-ef8md 2 роки тому +1

    Salama unaheshimika sana kwa ajili umejiheshim kwenye safari yako big up sana. Pamoja na kua ulinizingua sku moja na kofia yangu pale maeneo flani ila nakukubali sana kenge ww. Fanya tu kama nimejilipa kukwita kenge ila sio kwa ubaya ✌

    • @ucjvvjcjjvih9934
      @ucjvvjcjjvih9934 Рік тому

      Kenge mwenyewe🤐 tuwachie Salama wet alikulazimusha umsifie mbona umechellewa kulipiza kisasi sio kwa ubaya AMKA 🤛

  • @vevo3130
    @vevo3130 2 роки тому +1

    best interview....yaani Maua anajua kufunguka hana wasiwasi amerelaaaaaaaax....

  • @hussennshimirimana5736
    @hussennshimirimana5736 2 роки тому

    Mauwa sana msani wangu mpendwa..... Good interview watching from Burundi 🇧🇮

  • @floramlowe7078
    @floramlowe7078 2 роки тому +1

    Maisha sio raisi kweli watu wanatoka mbali sana hongera hiyo ni fundisho kwa wasichana wengine.

  • @asiaashraph4227
    @asiaashraph4227 2 роки тому +1

    The best interview

  • @ujenziwanyumbakisasatanzan6343
    @ujenziwanyumbakisasatanzan6343 2 роки тому +1

    Very talented Maua..

  • @ucjvvjcjjvih9934
    @ucjvvjcjjvih9934 Рік тому

    ❤Salama jabir akimaliza mauwa tuletee mwasiti tume miss❤

  • @ramashemngindo5719
    @ramashemngindo5719 2 роки тому +2

    Interview nzuri sana

  • @namelockmaasailady8002
    @namelockmaasailady8002 2 роки тому +1

    Dada salama umenenepa sana dear

  • @agricolamirinde6111
    @agricolamirinde6111 2 роки тому

    best interview ever

  • @ramadhanasadu1305
    @ramadhanasadu1305 2 роки тому

    Umetisha Sana sister mauwa sama

  • @nicolenabintu2509
    @nicolenabintu2509 2 роки тому +2

    Mauwa kigugumizi 🤣💕

  • @user-wk1ix1gm1p
    @user-wk1ix1gm1p 2 роки тому

    Maua wewe ni msanii usoshuka , upo unapanda na huna mambo mengi , napenda kazi zako

  • @dastonamichaels1854
    @dastonamichaels1854 10 місяців тому +1

    Iyo intro ndefu sana boring

  • @saumusalimuhassan2499
    @saumusalimuhassan2499 2 роки тому

    Duh! Maisha sio rahisi sahisi kwakweli

  • @nasramasimba3532
    @nasramasimba3532 2 роки тому

    First 1 to comment...

  • @barakakusa7606
    @barakakusa7606 2 роки тому +1

    Salama wambie wasanii/wageni wako waongee kiswahili zaidi.

    • @deboraezekiel784
      @deboraezekiel784 2 роки тому +1

      Ndugu usilazimishe mambo yaende hivo nchi ina lugha mbili anglo na kiswa

    • @trueexplorer894
      @trueexplorer894 2 роки тому +1

      Kwani unateseka?

  • @gbwile1257
    @gbwile1257 2 роки тому

    Kwa namna mama alipambana naww ndy mana watt wa kike wakiharibika lawama zote Kwa mama

  • @devothamkemangwa5720
    @devothamkemangwa5720 2 роки тому

    Uko vzr sana Maua

  • @mubarakhassan2618
    @mubarakhassan2618 2 роки тому

    Ao nawew uritoa kitu mbona hukusimama

  • @julianamushi3392
    @julianamushi3392 2 роки тому +1

    Kwani salama ni lzm uvae nguo nyeusi tuu

  • @user-po8hz7xw9j
    @user-po8hz7xw9j 2 роки тому

    Jamani salama uwe ndugu yangu wahiyari. Ila nipo MISRI nikija TZ nitafika kwako nawewe uje kwangu kwetu

  • @jmjthinker6363
    @jmjthinker6363 2 роки тому

    salama shikamoo?

  • @zumbeshauri8114
    @zumbeshauri8114 2 роки тому

    Maua leo kawa mtu wa moshi sio wa mazinde tena??

  • @owlbig
    @owlbig 2 роки тому

    ☄️❤️

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 2 роки тому

    Kumbe tuna unzaa 🙄😱

  • @asmassan
    @asmassan 2 роки тому

    Naomba mulete Diamond platnumz

  • @barakakusa7606
    @barakakusa7606 2 роки тому

    Maua anajua sanaaaa💯

  • @thabitdaudi9815
    @thabitdaudi9815 2 роки тому +1

    Maua apunguze kingerez kingi wakat wa kuongea kinampoteza na hakimpendez na honestly hakijui vizur. ila ni msanii mzur sana.

  • @hussennshimirimana5736
    @hussennshimirimana5736 2 роки тому

    Mauwa sana msani wangu mpendwa..... Good interview watching from Burundi 🇧🇮