"Matatizo yavavokaba shingo skimbii ....Napambana mpaka mwisho like realMen" ka imekutia hamasa basi like hapa twende sawa na Dizasta Vina as real Men.
Lipia copy yako ya album ya #AFF sasa. Album itatumwa kwa EMAIL, WHATSAPP au TELEGRAM. Tuma 10,000tzs /700ksh kwenda MPESA 0762 158 871 au TIGO PESA 0655 696 811 (jina EDGER MWAIPETA) kisha tuma sms ya muamala wako kwa namba uliyolipia. Usisahau kutuma Email au namba yako ya WhatsApp kwa ajili ya kupokea album. Let's go #DZSTVN
Uumbaji ni mara moja tu. Muumbaji huwa hageuki nyuma. Akishaumba mara moja anaweka vimelea vya usahihi katika mahesabu yake na kuacha utashi na chembe ya usahihi katika viumbe na miimili ya uumbaji na kila kiumbe kujiendesha chenyewe. Muumbaji ndio uumbaji wenyewe, Muumbaji sio mtu, sio baba, sio mama, wala sio mtoto. Muumbaji ni nishati huru, nguvu kubwa uliyopo katika kila kitu. Muumbaji hahusiki na dini wala siasa, hahusiki na mifumo yoyote dhalimu ya kibinadamu. Muumbaji anaona na haoni, Muumbaji yupo na hayupo. Muumbaji ni kila tunachokiona na tusichokiona. uumbaji ni fumbo. Muumbaji hahukumiwi wala hahukumu. So Hakuna hukumu bali kujihukumu wenyewe. Ila kuna hatia. HATIA IS REAL. and the writer is confronting his own consciousness, na mwandishi pia hana hatia. OVER!!
Nimesikiliza mara kadhaa nimejifunza mambo mawili, mara ya kwanza nilijua baba anayeongelewa ni baba mzazi ambaye alitelekeza familia yake akiwemo mtoto wake huyu ambaye ameamua kumuweka wazi kuwa hamtaki tena, Baadae nimegundua aliyezungumziwa ni Mungu baba ambaye ameumba dunia na akawatelekeza watoto wake wanashambuliwa na matatizo kama umasikini na njaa vinavyopelekeq chuki na maovu, anasema UNAJUA NI NGUMU SANA KUWA MWEMA UKIWA NA NJAA. Mungu ameacha wosia ambao haujulikani ni wa Mungu kweli au ni wa kufoji ? hapo anamanisha BIBLIA
@@Njokaa anamwongelea mungu ndomaana kuna verse kasema umejenge nyumba kwa siku 6 Biblia inaamini mungubaliumba dunia na kila kilichomo kwa siku 6 yasaba akapumzika
Enyi watoto wa 2070, nawakumbusha kwamba huu wimbo umetoka leo 05/01/2024. Na huyu ndiye msanii wetu pendwa wa hip hop. Toleo la mwisho la viumbe wa aina yake
2 Tim 2:13 SUV Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe. Mungu aturehemu sisi viumbe wake tusio stahili hata kulitaja jina lake. Utukufu wako Uishi Milele na Milele Amina
Kumamake hadi nimeogopa ila sio kwa ubaya bali kwa fact ulizoongea asee ziko on point daah yani kifupi am speechless mwamba sina la kukulaumu pia sina la kumlaumu mungu Dizasta wewe ni zaid ya fire ama moto wa jahannamu 🔥🔥🔥
Tunapaswa kutambua kua msanii ni kioo cha jamii dizasta alichokifanya humu ni kizuri kabisa maana kunawatu wanawaza hivi....yeye kazungumzia mawazo ya mtu au watu waliokata tamaa na wamejaribu kumkaribia Mungu lkn wanahis bado hawajapata majibu Tunapaswa kujua msanii ni mtu huru na ni muwakilishi wa watu,wanayowaza na wanayoyapitia so the guy is presenting peoples feelings Imani inachangamoto nyingi sana Mm ni mkatoliki na naipenda imani yangu...wakati fulani nilipokua katika huduma moja namuubiria mtu aliniuliza je utajuaje kama Mungu amekusamehe na humuoni!? So dizasta ametisha sana humu..MUNGU akubariki edger kwa watu wa imani ya kweli hii ni challenge wala sio kufuru🔥🔥
Good artistic work. Ni ishu ya kugusa existence (uwepo) and inexistence (kutokuwepo) kwa Mungu yaani, imani ya kuamini yupo na yanayofanyika yote ni kwamba kwanini hatuoni reaction yake physically, halafu imani ya kuamini hayupo na yanayofanyika yote ujinga tu wa hii dunia. Ukiwa una akili nzuri utaelewa hapo kwenye uwepo wake amegusa imani hasa ya Kiislamu(wenye majoho meupe na tafsiri za kiarabu) na hapo anapozungumzia inexistence (kutokuwepo kwa Mungu) anazungumzia imani ya wale "Wasioamini Mungu"(ATHEISTS), hapa kawagusa sana Jamaa zetu ambao wengi ndio Matajiri wa dunia(Mabilionea na watu maarufu) walipoegemea na ndipo wimbo ulipobeba maudhui yake makubwa na hoja nyingi alizozizungumza humu ni za hawa ATHEISTS. Skiza vzuri wimbo then, ukielewa ninachokwwmbia like hapa.
@@Macaveli_tz Bado hujataka kuelewa Bro, ngoja nikupe mwanga kidogo labda utafungua bongo yako, ni hivi; "HATIA" ni hali ya kushuku au kubaini uwepo wa makosa/ dhambi yaliyotendeka au kutokuwepo, yeye Msanii ame-act kama ni mtoto anayejaribu kuteta au kulalama uwepo wa Baba yake au kutokuwepo kwake wakati yeye (Msanii) yupo physically kwa maana anaonekana na mhitaji wa mambo lakini mahitaji hayo huyapata kwa shida bila uwepo wa kuonekana kwa Baba yake kwa lengo la msaada wa wazi so, ww unadhani ni Baba gani anayezungumzwa!!!??? Hilo moja, lakini pia unapaswa kutambua kuwa, yeye hana uhakika na mafundisho juu ya maisha yake na imani yatokanayo na watoto wenzake(Mitume, Maaskofu, Mapadri, Makasisi, Walimu, Masheikh, watu wa kawaida kwa ujumla waliopita zamanj na wa sasa) hapo alimgusa Yesu kama ni mtoto kwa maana alikimbia baada ya dhiki kwa maana hajarudi hadi sasa na hajui kama amekwenda mazina bila kurudi tena ulimwenguni, tatu ni kwamba yeye Msanii anajaribu kutaja Imani 3 ambazo ni Uislamu kwa maana pale alipotaja waliojivisha majoho meupe na wenye kumtafsiri Mungu kwa lugha ya kiarabu, imani ya pili ya kikrosto pale aliposema Wakivutana kwenye majadiliano na wakati mwengine humuomba hela(sadaka na zaka makanisani) kwa maana kuna usanii, lakini pia imani ya 3 ni hiyo aliyoibeba yeye zaidi kwenye wimbo na kuwekeza mawazo yake mbayo ni imani isiyoamini Mungu (ATHEISM). Bro nadhani kichwa chako bado kina akili changa, pull up your socks utaelewa ukiwa muda umeshakupita kitambo.
Umeenda mle mle ninamofikilia mfano hii verse "sio kosa langu kutokuwa na uhakika upo , sikujui sura maana hauna picha google, nipe ishara kuwa unaishi hata nikituma bakishishi niwe najua kuwa zinafika huko" kwa nilivyoelewa anaongelea swala la kutoa sadaki
Hii ngomaaa nimeisikiliza zaidi ya mara 24 ndio nimeielewaà..tena nimetafuta eneo ambalo hakuna sauti nitakayosikia zaidi ya sauti ya hii nyimbooo.. Ukiwa na imani ndogo hii nyimbo inakupoteza Na ukijifanya unaiman sana utashindwa kujibu hoja hata moja... ....he think more and more "Utanihukumu vp na una hubiri masamaha""
The black Maradona,hakika hiki ni kiumbe kipo katika dimension ya pekee, Mungu akuweke tuendelee kupata madini kwani kwa sasa tumetumia robo ya akili yako hata nusu hatujafika hii ndo maana ya MSANII NA MWANAFALSAFA. Be blessed Dizasta
Napiga magoti chini na kushukuru uwepo wa @dizasta ,sanaa na ujuzi alonao ni safi ni kama nanasi kwa maana ni tamu sana, HESHIMA KWAKO BROTHER kwa maana unatupa tunavyovihitaji na sio tunavyovitaka , Nakiri Kwa kusema Elimu yako ni kubwa zaidi ya masterz levels. I love u so much bro, Napenda sanaa yako ,napenda uwasilishaji wako , napenda ideas zako❤❤❤
Fikra zilizoandikwa hapa hazipaswi kuhukumiwa kama utashi wako haujauacha iwe huru. Kwanza ruhusu utashi wako upokee hizi frikra huru alaf usione hvyo vitu unavyoviona vya thaman kila mmoja anaona hivyo. Hii ni kubwa sana inahitaji mtu mwenye moyo huru na akili huru
Kwanza nimechukua maji ya uhai makubwa kabla sijamsikiliza T'TCHA DIZ kisha napitia comments za wanna kisha kila mmmoja unapiga like kwangu kisha tunamsikiliza GENIUS himself✔️
Mungu yupo ila shida nikujua jinsi anavyofanya kazi, Mungu ayupo kwajiri ya kumsaidia mtu au kumpendelea mtu, Mungu yupo kwajiri ya kuwatendea haki binadam wote duniani. So ukitaka jambo lolote inatakiwa ulipambanie mwenyewe then ukistahiri ndio unapewa, alafu Shetani sio mtu mbaya kama tunavyoaminishwa kwenye dini, Shetani na Mungu uwa wanapiga story na nimarafiki wazuri tu.
Dizasta vina a living genius. Kumbukumbu zinaonyesha watu kama hawa hawakufikia idadi ya 100 miongoni mwao ni Dizasta vina, leonardo da vinci, michalangelo, socrates na wachache wengine kadhaa… kama sisi ni wanae BABA kwann hajengi daraja tumfikie, alipopata changamoto ya dhambi zetu hima alitoeka asirudi kwann kajificha na anajua mm ni kiumbe dhaifu yeye ndiye alinizaa… hakika nimemtafuta sana lkn kajificha hatak nimuone hivyo nimechoka nae ni dhamu yake kunitafuta maana anajua pakunikuta dear. Wachungaji na masheikh wananiomba pesa ya kuwa wanamtumia lkn sina hakika kama hizo bakshishi zinafika huko.. vina GENIUS 😂😂😂
Kweli Unapika Mawe Yanaiva Maverse... Salamu Baba Mi Mwanao Naandika Waraka Kwa Maana Hutaki Vikao Nahitaji Majibu Nikihisi Ni Haki Yangu Najihisi Vibaya Nikusikia Unahishi Na Sina Nguo... VINA 💪
I wish dear father angejibu hii diss track kwake ili Dizasta aendelee kusema maana anaonekana bado ana meng ya kumuuliza Baba hasa juu ya Bakshishi anazotuma
Mungu kashamjibu kabla ya yy kuzaliwa... kamjibu kwa kumpa pumzi aliyotumia kuandika na kuingiza vocal kwenye hii Beat. Binafsi kanichanganya, wengi hawaelewi aliyeongelewa humo "Baba"
kuna mengi sana mekubaliana nayo kuhusu huu wimbo ila kumbuka kuna upande wa pili wa shilingi na hivyo kuna mengi sijakubali kutokana na kua njia yangu au viatu yangu sio viatu vya muandishi na tunatakiwa tujue hajakosea kwasababu hata wewe ungekua kwenye viatu vyake maybe ungewaza na kujiuliza maswali anayoyauliza yeye.. Dizasta ni Giant kwenye hii game ❤
Dizasta ni msanii bora kwa story telling Hatia ii, iv na v zitabakia alama kubwa kwake wengi tunamfuatilia kwa uandishi wa namna ile sababu unaakisi uhalisia wa maisha unasisimua na unaburudisha pia
Mwanzo nilidhani unazungumza na Mungu ila mwishoni nimegundua ni dear father, nafikiri umemkumbusha kila dingi wajibu wake kusimama kama Baba. Akili za ndani sana hizi, kipaji sana D.Vina
Hatia namba 6 ni wimbo ambao nimeuelewa vizuri na mkasa ote unamuhusu mungu lakini pia unaweza usimuelewe vizuri kama utatumia vitabu vya kidini kumuelewa sababu dini hujazaliwanayo ni (program) ambayo baada ya kuzaliwa ndio ukaanza kuwekewa taratibu ili ubongo wako uzowee. Lakini pia dini zinaweza zikawa hazijakosea kufundisha ila uelewa wa watu wenyewe ndio tatizo linapoanzia mfano: nikisema "mungu yupo" simaanishi ni (object) au ni kiumbe bali ninguvu ambayo ipo kila sehemu, kwakila mtu na kila kiumbe lakini wapumbavu ndio wanamuumba mungu nakusema yupo sehemu anaangalia wanadamu tunavyo teseka😢
Mm nilikosea badala ya kusikiliza wimbo kwanza nikatizama comments na comments ya kwanza kuiona ilisema jamaa anaongea na Mungu na ndo maana nilienda kuiskiza ngoma nilipata taabu sana kuielewa mpaka kichwa kikaanza kuniuma an
Hiki kisa ni cha kweli na kuna watu wameishi maiaha ambayo mnyama DIZASTA VINA kayoongelea kabisa. Daima utabaki kuwa mwana hip hop bora na storyteller wa muda wote🎉🎉❤❤
Ushauri wenye upendo kabisa..naamini vina ni muelewa na hii ni challenge kwetu tunaompenda ila yuko imani tofauti na sisi...tutafte namna ya kujibu hoja zake za msingi...yeye anadai Mungu amejificha, anakwepa majukumu nk.. Shida ni kwamba elimu kuhusu Mungu aliyonayo inafikia hapo... Shida nyingine anaamini sana ktk yeye mwenyewe(selfbelief) ambavyo ni vzr kujiamini kuliko kiumbe kingne chochote isipokua Muumbaji, ..natamani nipate mda nae tuelekezane unabii, kama ni mwana wa Mungu ataelewa, kama ni mwana wa Lucifer ataendelea na msimamo na inabaki kuombeana tu mwisho mwema.....kwa kifupi uyo anaetamani kuonana nae siku si nyingi kila jicho litamuona, na maswali hayo kama hataruhusu au kutafta majibu yake kwetu tunaojua atajibiwa na yeye mwenyewe..Baba hajajificha wala hajakimbia wala hajatuacha wapweke..Baba ni roho(anaishi ndani ya mioyo ya watoto wake_we feel his presence through holly spirit)).Anachodai D kua yuko mpweke ni sawa maana atheist hawaamini uwepo wake hivyo hayuko nao na amewaacha wafuate akili zao za upotovu...yaani wanafanya karma/jin(mf aladin lamp)-nguvu ya asili kua ndo mungu kumbe hiyo nguvu ya asili nayo imewekwa na Muumbaji(Mungu)....uzuri tupo ndani ya saa moja wa shetani na mawakala zake kutawala kisha Masihi arudi na kuondoa matrix iliyopo na kusimika falme mpya ambamo ndani yake Baba tutamuona kama alivyo katika utukufu wake...Tumepewa ishara za mwisho kabisa kabla ya masihi na Baba kushuka na mji wa yerusalemu hapa duniani....moja ni yule mwana wa kuasi kujidhihirisha na kujiinua ndani ya hekalu la Mungu na pili ni ni watu wote kutiishwa chini ya utawala wa mwana huyo wa kuasi...uzuri sasa ata wenye nuru kiasi wameanza muona na mifumo inazidi imarika adi mataifa ya uku kwetu ambako teknolojia ndo kikwazo kikubwa cha kuyatimiza haya..Nimekuombea rafiki yang D, hunijui ila mi ni mmoja wa fun wako wakubwa mno...imagine kwenye simu yangu sina nyimbo za secular zozote ila zako tu...napenda namna unavyotazama mambo kwa namna tofauti na huo ndo ubunifu unaonivuta kila ukitoa ngoma lazima niitafute, Umekua ukimsema sana Mungu nae ni mwingi wa rehema anakujua vzr kuliko sisi tunavyokujua ndo maana maana bado anakuvumilia kama anavyotuvumilia sote...nakuombea uo utaji uliofunga sub conscious yako utoke ndo conscious mind yako itaweza ngamua ukweli kuhusu Baba...kama kweli unataka majibu toka kwa Baba-sikiliza majibu toka kwa ndugu zako-kua na moyo wa kisomi uliotayari kujifunza maarifa mapya na kukubali ulipopungua ila wajuzi wakujazilizie....
@@reaganmakallo6824ametoa mda mrefu wa waovu kutubu na kusamehewa makosa yao kabisa--alivumilia maovu yetu ata baada ya kuteswa aliwaombea msamaha, bado anawaita watu watubu ili anapoenda kuishiliza dhambi wasipotee pamoja na waasi..Mungu hafurahii kuangamiza alichoumba
@@mhogomchungu7882consciousness(utashi) ni sehemu ya ubongo inayotusaidia kuamua kutenda jema au baya...Mungu katupa hii ili tumpende kwa utashi pasipo kumonitiwa kama robot....ni kwel Mungu ni omnipresent ila haimaaniishi yeye ni sehemu ya uumbaji-yey ndiye aliyeumba na yupo kila sehemu kupitia nguvu ya roho mtakatifu-ulimwengu wote unathibitika kwa nguvu yake
Ambaye ameeleza kuusu baba embu tumpongeze dizasta vina yaan dizasta anajua sana Tena sana yaan hii imekuwa kelo Sasa man anajua sana mungu sijui kama umemsikia dizasta akukumbusha kwamba sisi wa Hali ya chini imefika muda tunakosa imani
Yaani hii ngoma usiposikiliza zaiidi ya mara 2 sidhani kama utailewa haraka hajamuongelea Mungu sikilizeni vizuri tena .ukienda kichwa kichwa utatoka kapa au kuelewa tofauti
Never disappoint kabisa vina// kila ngoma ukiitoa inakuwa noma// magonjwa mengi verses zina tibu homa// kwa upande wangu hakuna wakukushusha vina// umeshika industry hip pap ume gusa mioyo bab// ume fanya music wako anaskiza babu// kila rika gusa kila chocho mitaa baa wote twapata vibe// Vina noma 👁👁👁👁👁👁
the talent immense
"Matatizo yavavokaba shingo skimbii
....Napambana mpaka mwisho like realMen" ka imekutia hamasa basi like hapa twende sawa na Dizasta Vina as real Men.
Lipia copy yako ya album ya #AFF sasa. Album itatumwa kwa EMAIL, WHATSAPP au TELEGRAM. Tuma 10,000tzs /700ksh kwenda MPESA 0762 158 871 au TIGO PESA 0655 696 811 (jina EDGER MWAIPETA) kisha tuma sms ya muamala wako kwa namba uliyolipia. Usisahau kutuma Email au namba yako ya WhatsApp kwa ajili ya kupokea album. Let's go
#DZSTVN
Kutoka Panorama🎉🎉
Pamoja sana
Yeeesiir ❤
Deal done, gv us music bro
Wazi
Uumbaji ni mara moja tu. Muumbaji huwa hageuki nyuma. Akishaumba mara moja anaweka vimelea vya usahihi katika mahesabu yake na kuacha utashi na chembe ya usahihi katika viumbe na miimili ya uumbaji na kila kiumbe kujiendesha chenyewe. Muumbaji ndio uumbaji wenyewe, Muumbaji sio mtu, sio baba, sio mama, wala sio mtoto. Muumbaji ni nishati huru, nguvu kubwa uliyopo katika kila kitu. Muumbaji hahusiki na dini wala siasa, hahusiki na mifumo yoyote dhalimu ya kibinadamu. Muumbaji anaona na haoni, Muumbaji yupo na hayupo. Muumbaji ni kila tunachokiona na tusichokiona. uumbaji ni fumbo. Muumbaji hahukumiwi wala hahukumu. So Hakuna hukumu bali kujihukumu wenyewe. Ila kuna hatia. HATIA IS REAL. and the writer is confronting his own consciousness, na mwandishi pia hana hatia. OVER!!
Hii hatia no ngap
Mim nmekuelewa thanks...
@@AhmedNadhiru-qe5pl 6
👏👏👏👏
Noma jamaa kaandika haswa
Kabla sijaskiza nacomment kwanza coz najua Vina anajua sana
Nimesikiliza mara kadhaa nimejifunza mambo mawili, mara ya kwanza nilijua baba anayeongelewa ni baba mzazi ambaye alitelekeza familia yake akiwemo mtoto wake huyu ambaye ameamua kumuweka wazi kuwa hamtaki tena,
Baadae nimegundua aliyezungumziwa ni Mungu baba ambaye ameumba dunia na akawatelekeza watoto wake wanashambuliwa na matatizo kama umasikini na njaa vinavyopelekeq chuki na maovu, anasema UNAJUA NI NGUMU SANA KUWA MWEMA UKIWA NA NJAA.
Mungu ameacha wosia ambao haujulikani ni wa Mungu kweli au ni wa kufoji ? hapo anamanisha BIBLIA
Rudia tena kusikiliza broo hajamaanisha Mungu
@@Njokaawe ndo umepotea kabisa rud ukasikilize vzuri,,huyo mwamba kaongea sahihi
@@Njokaa anamwongelea mungu ndomaana kuna verse kasema umejenge nyumba kwa siku 6
Biblia inaamini mungubaliumba dunia na kila kilichomo kwa siku 6 yasaba akapumzika
Enyi watoto wa 2070, nawakumbusha kwamba huu wimbo umetoka leo 05/01/2024. Na huyu ndiye msanii wetu pendwa wa hip hop. Toleo la mwisho la viumbe wa aina yake
😂😂😂😂😂umeiweka kitaalamu kaka utakumbukwa
2 Tim 2:13 SUV
Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.
Mungu aturehemu sisi viumbe wake tusio stahili hata kulitaja jina lake. Utukufu wako Uishi Milele na Milele Amina
Meen shut up
Dizasta vina ni next level bongo nzima hakuna huyu jamaa n hatar ni umeme mkubwa
Kumamake hadi nimeogopa ila sio kwa ubaya bali kwa fact ulizoongea asee ziko on point daah yani kifupi am speechless mwamba sina la kukulaumu pia sina la kumlaumu mungu Dizasta wewe ni zaid ya fire ama moto wa jahannamu 🔥🔥🔥
be careful what you saying next broo 😅😅😅
Tunapaswa kutambua kua msanii ni kioo cha jamii dizasta alichokifanya humu ni kizuri kabisa maana kunawatu wanawaza hivi....yeye kazungumzia mawazo ya mtu au watu waliokata tamaa na wamejaribu kumkaribia Mungu lkn wanahis bado hawajapata majibu
Tunapaswa kujua msanii ni mtu huru na ni muwakilishi wa watu,wanayowaza na wanayoyapitia so the guy is presenting peoples feelings
Imani inachangamoto nyingi sana
Mm ni mkatoliki na naipenda imani yangu...wakati fulani nilipokua katika huduma moja namuubiria mtu aliniuliza je utajuaje kama Mungu amekusamehe na humuoni!?
So dizasta ametisha sana humu..MUNGU akubariki edger kwa watu wa imani ya kweli hii ni challenge wala sio kufuru🔥🔥
Good artistic work. Ni ishu ya kugusa existence (uwepo) and inexistence (kutokuwepo) kwa Mungu yaani, imani ya kuamini yupo na yanayofanyika yote ni kwamba kwanini hatuoni reaction yake physically, halafu imani ya kuamini hayupo na yanayofanyika yote ujinga tu wa hii dunia. Ukiwa una akili nzuri utaelewa hapo kwenye uwepo wake amegusa imani hasa ya Kiislamu(wenye majoho meupe na tafsiri za kiarabu) na hapo anapozungumzia inexistence (kutokuwepo kwa Mungu) anazungumzia imani ya wale "Wasioamini Mungu"(ATHEISTS), hapa kawagusa sana Jamaa zetu ambao wengi ndio Matajiri wa dunia(Mabilionea na watu maarufu) walipoegemea na ndipo wimbo ulipobeba maudhui yake makubwa na hoja nyingi alizozizungumza humu ni za hawa ATHEISTS. Skiza vzuri wimbo then, ukielewa ninachokwwmbia like hapa.
Sikiliza tena huu wimbo kwa umakini,,, upo nje ya theme Kuna code bado hujazipata vzr ili kuelewa DZST anaongea na nani hasa kwenye huu wimbo
@@Macaveli_tz Bado hujataka kuelewa Bro, ngoja nikupe mwanga kidogo labda utafungua bongo yako, ni hivi; "HATIA" ni hali ya kushuku au kubaini uwepo wa makosa/ dhambi yaliyotendeka au kutokuwepo, yeye Msanii ame-act kama ni mtoto anayejaribu kuteta au kulalama uwepo wa Baba yake au kutokuwepo kwake wakati yeye (Msanii) yupo physically kwa maana anaonekana na mhitaji wa mambo lakini mahitaji hayo huyapata kwa shida bila uwepo wa kuonekana kwa Baba yake kwa lengo la msaada wa wazi so, ww unadhani ni Baba gani anayezungumzwa!!!??? Hilo moja, lakini pia unapaswa kutambua kuwa, yeye hana uhakika na mafundisho juu ya maisha yake na imani yatokanayo na watoto wenzake(Mitume, Maaskofu, Mapadri, Makasisi, Walimu, Masheikh, watu wa kawaida kwa ujumla waliopita zamanj na wa sasa) hapo alimgusa Yesu kama ni mtoto kwa maana alikimbia baada ya dhiki kwa maana hajarudi hadi sasa na hajui kama amekwenda mazina bila kurudi tena ulimwenguni, tatu ni kwamba yeye Msanii anajaribu kutaja Imani 3 ambazo ni Uislamu kwa maana pale alipotaja waliojivisha majoho meupe na wenye kumtafsiri Mungu kwa lugha ya kiarabu, imani ya pili ya kikrosto pale aliposema Wakivutana kwenye majadiliano na wakati mwengine humuomba hela(sadaka na zaka makanisani) kwa maana kuna usanii, lakini pia imani ya 3 ni hiyo aliyoibeba yeye zaidi kwenye wimbo na kuwekeza mawazo yake mbayo ni imani isiyoamini Mungu (ATHEISM).
Bro nadhani kichwa chako bado kina akili changa, pull up your socks utaelewa ukiwa muda umeshakupita kitambo.
Fact
Umeenda mle mle ninamofikilia mfano hii verse "sio kosa langu kutokuwa na uhakika upo , sikujui sura maana hauna picha google, nipe ishara kuwa unaishi hata nikituma bakishishi niwe najua kuwa zinafika huko" kwa nilivyoelewa anaongelea swala la kutoa sadaki
majoho meupe ma dhahani Catholic..Tafsiri za kiarabu ni Quran
Dizasta ni msanii, ni kioo. Taswira yake ni reflection ya alichokiona au kusikia kwa watu.
Hana hatia kuwakilisha mawazo ya watu.
Hii ngomaaa nimeisikiliza zaidi ya mara 24 ndio nimeielewaà..tena nimetafuta eneo ambalo hakuna sauti nitakayosikia zaidi ya sauti ya hii nyimbooo..
Ukiwa na imani ndogo hii nyimbo inakupoteza
Na ukijifanya unaiman sana utashindwa kujibu hoja hata moja...
....he think more and more
"Utanihukumu vp na una hubiri masamaha""
The black Maradona,hakika hiki ni kiumbe kipo katika dimension ya pekee, Mungu akuweke tuendelee kupata madini kwani kwa sasa tumetumia robo ya akili yako hata nusu hatujafika hii ndo maana ya MSANII NA MWANAFALSAFA. Be blessed Dizasta
Napiga magoti chini na kushukuru uwepo wa @dizasta ,sanaa na ujuzi alonao ni safi ni kama nanasi kwa maana ni tamu sana, HESHIMA KWAKO BROTHER kwa maana unatupa tunavyovihitaji na sio tunavyovitaka , Nakiri Kwa kusema Elimu yako ni kubwa zaidi ya masterz levels. I love u so much bro, Napenda sanaa yako ,napenda uwasilishaji wako , napenda ideas zako❤❤❤
Fikra zilizoandikwa hapa hazipaswi kuhukumiwa kama utashi wako haujauacha iwe huru. Kwanza ruhusu utashi wako upokee hizi frikra huru alaf usione hvyo vitu unavyoviona vya thaman kila mmoja anaona hivyo. Hii ni kubwa sana inahitaji mtu mwenye moyo huru na akili huru
Haswaa
Welcome vina Company
Kama humpendi dizasta vina nenda Muhimbili kapimwe mkojo + akili nitalipia Gharama za matibabu🎉
🔥Hamuongelei baba uliemuacha nyumbani.... Mwana ana kikao na BABA WA MBINGUNI... UTUNZIIIIIII NI NEXT LEVEL. 🔥
I ngoma naisubiri sana mana kila ngoma ya vina lazima iwe kali
The writing is incredible and very relevant to the socio-economic setting of African communities.
Great love from Kenya.
Dizasta FANS ..we are in safe HANDS🙌🙌🔥…the kid delivers what we’ve been waitin for
Kaka umemgeukia na mshua kabisaa
Siku zote huwa nategea kupata muziki mpya kutoka kwa dizasta vina 🔥💯
Toleo la mwisho la viumbe wa aina yake na hawatokuwepo tena big up to Dizasta vina (KING VINA)
Huyu dizasta ni rafiki yangu sana japo hajui Hilo
Nakubali sana this story-teller
Kwanza nimechukua maji ya uhai makubwa kabla sijamsikiliza T'TCHA DIZ kisha napitia comments za wanna kisha kila mmmoja unapiga like kwangu kisha tunamsikiliza GENIUS himself✔️
Mungu yupo ila shida nikujua jinsi anavyofanya kazi, Mungu ayupo kwajiri ya kumsaidia mtu au kumpendelea mtu, Mungu yupo kwajiri ya kuwatendea haki binadam wote duniani. So ukitaka jambo lolote inatakiwa ulipambanie mwenyewe then ukistahiri ndio unapewa, alafu Shetani sio mtu mbaya kama tunavyoaminishwa kwenye dini, Shetani na Mungu uwa wanapiga story na nimarafiki wazuri tu.
Dizasta vina a living genius. Kumbukumbu zinaonyesha watu kama hawa hawakufikia idadi ya 100 miongoni mwao ni Dizasta vina, leonardo da vinci, michalangelo, socrates na wachache wengine kadhaa… kama sisi ni wanae BABA kwann hajengi daraja tumfikie, alipopata changamoto ya dhambi zetu hima alitoeka asirudi kwann kajificha na anajua mm ni kiumbe dhaifu yeye ndiye alinizaa… hakika nimemtafuta sana lkn kajificha hatak nimuone hivyo nimechoka nae ni dhamu yake kunitafuta maana anajua pakunikuta dear.
Wachungaji na masheikh wananiomba pesa ya kuwa wanamtumia lkn sina hakika kama hizo bakshishi zinafika huko.. vina GENIUS 😂😂😂
Mwaka haujaisha ila hii tayari ishakuwa my TOP SONG
Aiseh huyu mwamba noma
Uyo baba anakuja kama Mungu alafu anakata,yani kiufupi sielewi
Wakwanza kukoment daah the long wait is over
Nikiteta hadithi utahisi NGUGI 🔥🔥🔥
Kweli Unapika Mawe Yanaiva Maverse... Salamu Baba Mi Mwanao Naandika Waraka Kwa Maana Hutaki Vikao Nahitaji Majibu Nikihisi Ni Haki Yangu Najihisi Vibaya Nikusikia Unahishi Na Sina Nguo... VINA 💪
Vina anaongea na Mungu .
I wish dear father angejibu hii diss track kwake ili Dizasta aendelee kusema maana anaonekana bado ana meng ya kumuuliza Baba hasa juu ya Bakshishi anazotuma
Mungu kashamjibu kabla ya yy kuzaliwa... kamjibu kwa kumpa pumzi aliyotumia kuandika na kuingiza vocal kwenye hii Beat. Binafsi kanichanganya, wengi hawaelewi aliyeongelewa humo "Baba"
Vinaah mwanamuziki genious anaeishi.... Tz kwa sas hv
We jamaa una sayari yako 👊
Utakuwa muongo ukisema umeielewa hii ngoma kwa kuisikiliza mara moja tu. Its need 🔂🔂🔂
Yaani mara ya kwanza tu bila hata kurudia, nimejua anaongea na Mungu, maybe anatafsiri yake lakini kwangu hiyo ndio theme ya ngoma nilong'amua.
the hottest raper @dizasta Vina "nashangaa wenzangu wanakesha wakiimba utukufu Wa dhambi zako"
Co malaika we n Mungu w rap!yesu wa hi generation,🎉,
huna baya bkack maradona sijui huwa unawaza nini upatunga tungo tata much respect
We. Ni nyoko Ngoma Kali
Uyu ni baba mungu kama sikosei ila umemqambia ukweli yeye anajua pa kukutia
uweziii kua mwema ukiwa na njaaa
kuna mengi sana mekubaliana nayo kuhusu huu wimbo ila kumbuka kuna upande wa pili wa shilingi na hivyo kuna mengi sijakubali kutokana na kua njia yangu au viatu yangu sio viatu vya muandishi na tunatakiwa tujue hajakosea kwasababu hata wewe ungekua kwenye viatu vyake maybe ungewaza na kujiuliza maswali anayoyauliza yeye.. Dizasta ni Giant kwenye hii game ❤
Nakubaliana na wewe
Dini nayo ni matrix mbaya sanaa
Tiba ya ubongo skuzote💪
Dizasta ni msanii bora kwa story telling
Hatia ii, iv na v zitabakia alama kubwa kwake
wengi tunamfuatilia kwa uandishi wa namna ile
sababu unaakisi uhalisia wa maisha unasisimua na unaburudisha pia
Mwanzo nilidhani unazungumza na Mungu ila mwishoni nimegundua ni dear father, nafikiri umemkumbusha kila dingi wajibu wake kusimama kama Baba. Akili za ndani sana hizi, kipaji sana D.Vina
Uyu mwamba akitoaga ngoma sina muda wa ku loading chapo na download then naunganisha Bluetooth nasikia HIP HOP ASILI 😅😅. Ndomaana ni DIZASTA VINA
mmmmmh kumuelewa vina inabidi uwe umekula umeshiba na huna stress 🔥
Yaani mm mpaka kichwa kimeanza kuuma bado sielewi , kwani ka zungumzia nini broo!
@@Njokaamjomba nenda kamsikilize zuchu na mond wameachia ngoma mpya kwa huyu maradona utameza sana panado
Sikupingi genius , naenjoy coz kila nikisikiza ngoma zako huwa na madetate uwezo ulio nao wa uwandishi
Miaka 6 iliyopita kwenye kanisa nikasema this man is hopsin wa bongo and he prove again
NI NGUMU SANA KUWA MWEMA UKIWA NA NJAA👏👏👏👏🔥🔥🔥🔥🔥🔥🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🙋
Umeiweka hip hop lever za juuu sana
Fundi kama fundi hatia namba 5,, n shidaaaa,, hii ni hatia seriz
Hatia namba 6 ni wimbo ambao nimeuelewa vizuri na mkasa ote unamuhusu mungu lakini pia unaweza usimuelewe vizuri kama utatumia vitabu vya kidini kumuelewa sababu dini hujazaliwanayo ni (program) ambayo baada ya kuzaliwa ndio ukaanza kuwekewa taratibu ili ubongo wako uzowee. Lakini pia dini zinaweza zikawa hazijakosea kufundisha ila uelewa wa watu wenyewe ndio tatizo linapoanzia
mfano: nikisema "mungu yupo" simaanishi ni (object) au ni kiumbe bali ninguvu ambayo ipo kila sehemu, kwakila mtu na kila kiumbe lakini wapumbavu ndio wanamuumba mungu nakusema yupo sehemu anaangalia wanadamu tunavyo teseka😢
Bro..wwe ni black Maradona pia
Uwanja ni wako mwenyewe
Akili kubwa Sana 🔥🔥🔥
Nime like kabla sijaskiza maana najua hatia ni noma kila siku
Aujui ningumu sana kuwa mwema ukiwa na njaa 😂😂😂
Kumbe sijachelewa
Mwamba huyu hapaaaa🔥🔥👏👏
Kwanza beat kali na limekutana na fundi wakuchora
Mungu anakupenda atakupenda mpk uamue ww!!! Kama unavyo jiona kuwa Baba bora Mungu n Bora Zaid wala hakuchukiii
Mm nilikosea badala ya kusikiliza wimbo kwanza nikatizama comments na comments ya kwanza kuiona ilisema jamaa anaongea na Mungu na ndo maana nilienda kuiskiza ngoma nilipata taabu sana kuielewa mpaka kichwa kikaanza kuniuma an
Ngoma Kali blood uko vizuriii
Ringle beats aksante kwa mdundo.
Hiki kisa ni cha kweli na kuna watu wameishi maiaha ambayo mnyama DIZASTA VINA kayoongelea kabisa. Daima utabaki kuwa mwana hip hop bora na storyteller wa muda wote🎉🎉❤❤
❤❤❤
Siri ipi na Siri zetu hazilingani / G.O.A.T shukrani sana 🙌🔥🔥🔥
Vina ndo jina🙌
Kaka ulimaliza KANISA
Hatia V1 umegusa muhusika
Salute sana
Wenye akili kama za DIZASTA, mara nyingi hujenga hoja kwenye kila jambo na ni ngumu kuamini kuhusu MUNGU
Kaka unajua mpaka unatia huruma 😊
Brother brother brother.....unatumia kichwa gani kuandika brother mbona unatari sana 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥💯💯💯💯💯💯💯
Nani ameelewa baba anaye zungumziwa 🔥🔥 Dizasta vina tunzi zimetukuka...✊🏾✊🏾
kaka mm sijaelewa
Jamaa anateta na sir God
Hii ngoma ni ya kusikiliza hata porin pasipo na kelele la sivyo huwezi ambulia kitu hajamaanisha Mungu
Hikii kichwaaa🔥🔥🔥🔥
Nimechelewa ku coment wahuni wamewai hii 😂 kama una mkubali Dizasta weka moto 🔥
Ushauri wenye upendo kabisa..naamini vina ni muelewa na hii ni challenge kwetu tunaompenda ila yuko imani tofauti na sisi...tutafte namna ya kujibu hoja zake za msingi...yeye anadai Mungu amejificha, anakwepa majukumu nk..
Shida ni kwamba elimu kuhusu Mungu aliyonayo inafikia hapo... Shida nyingine anaamini sana ktk yeye mwenyewe(selfbelief) ambavyo ni vzr kujiamini kuliko kiumbe kingne chochote isipokua Muumbaji, ..natamani nipate mda nae tuelekezane unabii, kama ni mwana wa Mungu ataelewa, kama ni mwana wa Lucifer ataendelea na msimamo na inabaki kuombeana tu mwisho mwema.....kwa kifupi uyo anaetamani kuonana nae siku si nyingi kila jicho litamuona, na maswali hayo kama hataruhusu au kutafta majibu yake kwetu tunaojua atajibiwa na yeye mwenyewe..Baba hajajificha wala hajakimbia wala hajatuacha wapweke..Baba ni roho(anaishi ndani ya mioyo ya watoto wake_we feel his presence through holly spirit)).Anachodai D kua yuko mpweke ni sawa maana atheist hawaamini uwepo wake hivyo hayuko nao na amewaacha wafuate akili zao za upotovu...yaani wanafanya karma/jin(mf aladin lamp)-nguvu ya asili kua ndo mungu kumbe hiyo nguvu ya asili nayo imewekwa na Muumbaji(Mungu)....uzuri tupo ndani ya saa moja wa shetani na mawakala zake kutawala kisha Masihi arudi na kuondoa matrix iliyopo na kusimika falme mpya ambamo ndani yake Baba tutamuona kama alivyo katika utukufu wake...Tumepewa ishara za mwisho kabisa kabla ya masihi na Baba kushuka na mji wa yerusalemu hapa duniani....moja ni yule mwana wa kuasi kujidhihirisha na kujiinua ndani ya hekalu la Mungu na pili ni ni watu wote kutiishwa chini ya utawala wa mwana huyo wa kuasi...uzuri sasa ata wenye nuru kiasi wameanza muona na mifumo inazidi imarika adi mataifa ya uku kwetu ambako teknolojia ndo kikwazo kikubwa cha kuyatimiza haya..Nimekuombea rafiki yang D, hunijui ila mi ni mmoja wa fun wako wakubwa mno...imagine kwenye simu yangu sina nyimbo za secular zozote ila zako tu...napenda namna unavyotazama mambo kwa namna tofauti na huo ndo ubunifu unaonivuta kila ukitoa ngoma lazima niitafute,
Umekua ukimsema sana Mungu nae ni mwingi wa rehema anakujua vzr kuliko sisi tunavyokujua ndo maana maana bado anakuvumilia kama anavyotuvumilia sote...nakuombea uo utaji uliofunga sub conscious yako utoke ndo conscious mind yako itaweza ngamua ukweli kuhusu Baba...kama kweli unataka majibu toka kwa Baba-sikiliza majibu toka kwa ndugu zako-kua na moyo wa kisomi uliotayari kujifunza maarifa mapya na kukubali ulipopungua ila wajuzi wakujazilizie....
Ameuliza ni vipi utanihukumu na unahubiri msamahaa??
Mungu ni conscioussness yenyw it is here and now. Be at the present and sense your being (essence)
@@reaganmakallo6824ametoa mda mrefu wa waovu kutubu na kusamehewa makosa yao kabisa--alivumilia maovu yetu ata baada ya kuteswa aliwaombea msamaha, bado anawaita watu watubu ili anapoenda kuishiliza dhambi wasipotee pamoja na waasi..Mungu hafurahii kuangamiza alichoumba
@@mhogomchungu7882consciousness(utashi) ni sehemu ya ubongo inayotusaidia kuamua kutenda jema au baya...Mungu katupa hii ili tumpende kwa utashi pasipo kumonitiwa kama robot....ni kwel Mungu ni omnipresent ila haimaaniishi yeye ni sehemu ya uumbaji-yey ndiye aliyeumba na yupo kila sehemu kupitia nguvu ya roho mtakatifu-ulimwengu wote unathibitika kwa nguvu yake
Ulipo andika neno lucifer nimejua kitu kuhusu wewe 😂😂 am so sorry
Wa pili
Huyu jamaa n hatar sana
Sio rahisi kuwa dizasta vina sio rahisi kama huamini jaribu kutafuta
After hardwork na mapambano ya January then napata nafasi ya kuskiliza hii Masterpiece🔥.... "Utahisi mkono wa mungu" umeandika hii asee🙌🏾
Hakuna rapper kama Dizasta apa Bongo case closed 🔥👨⚖️🙌
Uyu mwamba anajua Sana nikisikiliza izi Sina hatia 🎉Nampa maua yake
Here we go
Kichwa cha uyu jamaa ni hatari aiseee,anawaza mbali sana uyu jamaa ni 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
Your The speaking book 📖 🙏 thank you for the free class fam 🙏🙏
Ambaye ameeleza kuusu baba embu tumpongeze dizasta vina yaan dizasta anajua sana Tena sana yaan hii imekuwa kelo Sasa man anajua sana mungu sijui kama umemsikia dizasta akukumbusha kwamba sisi wa Hali ya chini imefika muda tunakosa imani
Mh vina umesoma shule Gani
Achia majala kwenye nambar ya dizasta vina maka sapot 🔥🔥🔥 kupata album
Dude was born in wrong era.. much love and blessings from Kenya.
the verteller mwenyewe dvina never fail❤💪💪💪
NI NGUMU SANA KUWA MWEMA UKIWA NA NJAA🔥🔥✊🏾
Bana hii ni uzito
Nimeikubali kabla sijasikiliza 😁.
Nikisikiliza ngoma mpya ya Vina lazima niisikilize zaidi ya mara tatu ❤
Yaani hii ngoma usiposikiliza zaiidi ya mara 2 sidhani kama utailewa haraka hajamuongelea Mungu sikilizeni vizuri tena .ukienda kichwa kichwa utatoka kapa au kuelewa tofauti
Kamwongelea nani sasa na wewe em tuambie au we ndo umetoka kapa man
Magufi Njo anamuogelea duh 🙄
@@BenMamadou-w9esyo Magu
Nakubali sana dizasta vina sijwahi kupinga ngoma zako❤❤❤❤
Hakuna Rapper kama Disaster Vina DUNIA nzima 💪💪💪💪💪💪
Una wazimu
Mufti mLamba haraM🔞
Never disappoint kabisa vina//
kila ngoma ukiitoa inakuwa noma//
magonjwa mengi verses zina tibu homa//
kwa upande wangu hakuna wakukushusha vina//
umeshika industry hip pap ume gusa mioyo bab//
ume fanya music wako anaskiza babu//
kila rika gusa kila chocho mitaa baa wote twapata vibe//
Vina noma 👁👁👁👁👁👁