Dizasta Vina - Hatia IV

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 1 лют 2025

КОМЕНТАРІ • 666

  • @dizastavina
    @dizastavina  4 роки тому +103

    “JASIRI JOHN….. ALIYAANGALIA MAISHA YAKE
    HAKUONA JINSI ANGEWEZA KUISHI BILA JANE
    MSICHANA ANAYEMPENDA
    LICHA YA KUZONGWA NA UMASIKINI
    ALIJITAHIDI KUMPA JANE MAHITAJI MADOGOMADOGO KADRI ALIVYOWEZA
    LAKINI ALIFAHAMU SHUBIRI YA KUSUBIRI KUPENDWA HUKU ANAFAHAMU KUSUBIRI KUPENDWA NI
    MATUMAINI YANAYOUMIZA. KAMA WANAVYOSEMA, MTAFUTAJI HACHOKI AKICHOKA KASHAPATA…
    .ALIENDELEA KUNGOJA”
    Ah! Sikuwa na zali sikuziamini ndumba
    Sikuwa na mali za kufuja
    Nilijitahidi kuuza mitumba kufuga mipunga
    Ili siku nimpe gari nimpe nyumba. Nilishindwa…
    Niliishia kumpa chai, ‘chipsi’ mayai na ‘vocha’
    Nywele za kimasai na mkoba
    Pesa za magauni, majuba na viatu vya kuzuga
    Nilimpa muda ila bado haikutosha, kwani…
    Nilipomwambia nampenda hakujibu
    Akaweka moyo wangu maumivu
    Na mtima wangu akauweka ‘solemba’
    Nikaapia kuwa sitakuja kupenda ‘forever’
    Ah! Nilimpa upendo nilimpa sifa
    Niliweka mitego ya faida, haikuwa shwari
    Nikabadili mwenendo wa maisha
    Niliweka malengo sikutimiza, hakunikubali
    Alikuwa na ndoto kubwa kushinda mimi
    Alikuwa na misimamo kuipita dini
    Aliniambia ameomba nije kuokota utajiri
    Amengoja sana na sasa amechoka kusubiri
    “JOHN ALIFAHAMU HALI YA JANE, KUWA JANE ALIZALIWA KWENYE
    FAMILIA MASIKINI, NA ALIUCHUKIA MNO UMASIKINI.
    ALIFAHAMU UMASIKINI ULIVYOCHUKUA UHAI WA MAMA YAKE KIPENZI,
    ALIYEFARIKI KWA KUKOSA MATIBABU. ALIIFAHAMAU NADHIRI ALIYOIWEKA JANE YA KWAMBA
    HATOKUBALI TENA KUISHI KWENYE MAISHA YA KIMASIKINI, NADHIRI ILIYO MWEKA JOHN NJIAPANDA”
    Ah! Sikuwa na hali ya kuikosha roho yake
    Nilimwacha aende aufate moyo wake
    Alipata bwana wa kizungu magharibi
    Alimwahidi kuishi maisha ya ndoto zake
    Nilipata uchungu niliishia kuhamaki nilitaka nijiue
    Nilitaka nimzuie abaki nikakumbuka
    Ukipenda ua haulikati unaliacha likue
    Duka langu nilifunga biashara niliacha zote
    Uchumi uliyumba kwa maana nilianza pombe
    Niliumwa bado kidogo moyo uzime
    Nilimfanya ndoto kumbe naye ana ndoto nyingine
    Alisema anakwenda jiji la Miami
    Hakuna alichowaza zaidi ya kuishi kifahari
    Kamtumia picha na ‘mchizi’ kazikubali
    Na yupo tayari kumlipia gharama za safari
    Aliondoka na kipande kimoja cha mwili
    Nilikonda nilipata ugonjwa wa akili
    Haikuwahi kupita hata sekunde nisilie
    Nilitamani mpaka ardhi ipasuke niingie
    “JANE ALIPOONDOKA ALIMWACHIA JOHN KIDONDA KILICHOCHELEWA SANA KUPONA
    NA YEYE AKAWEKA NADHIRI YA KUTOJIHUSISHA NA MAPENZI TENA MAISHANI MWAKE.
    ALIKAA KWA MUDA MREFU BILA MAHUSIANO. LAKINI…
    HAKUNA DAKTARI MZURI KAMA MUDA, JOHN ALIPONA MAUMIVU NA ALIIRUDIA HALI YAKE YA KAWAIDA”
    Ah! Muda ukaenda nitapata ‘Mwanamwali’
    Nikamwomba awe mwenza wa maisha akakubali
    Nikamvisha pete nikalipia mahari
    Sikumpenda lakini nilijifunza kumjali
    Aliuliza kama nampenda, nilimjibu
    Sikutaka kuweka moyo wake maumivu
    Sikutaka kuuweka Mtima wake solemba
    Kiasi aseme hatakuja kupenda ‘‘forever’’
    Ah alinikumbatia nikamfunga kwa ishara
    Akanikabidhi tunda nikala
    Akaniamini tukajuana nikapanga kumwoa
    Akaidhisha na tukaanza na mipango ya ndoa
    “WAKATI KARNE YA 21 INAINGIA, JOHN ALIKUWA NI MIONGONI MWA
    VIJANA WALIOKUWA ‘FASCINATED’ NA UKUAJI WA TEKNOLOJIA YA MITANDAO YA KIJAMII.
    ALIJIUNGA NA DUNIA HII MPYA, MARA KADHAA ALIKAA KWENYE UBARAZA, AKIANGAZA SIMU YAKE.
    AKIPAPASA KILA KITUFE, NDIPO SIKU MOJA AKAPATA UJUMBE KUTOKA KWA JANE”
    “Habari naamini u bukheri wa afya
    Unaendeleaje maisha na huyo mpenzi wa sasa
    .nashukuru nahema ughaibuni si kwema
    Nakiona cha mtema mpaka naona ni heri nikafa…
    Ah! Maisha niliyowaza yote ni uongo
    Nauzishwa madawa nalazimishwa ngono
    Nafungiwa ndani kama mtumwa ufungwani
    Roho yangu rehani kiasi sasa naitamani Bongo
    Ukubwa umekuja kunisafisha jicho
    Ndoto imeisha na taswira imenionyesha sivyo, ah
    Naomba unifate uniondoshe kwenye hichi kifo
    Na hii namba ya msamaria atakueleza nilipo”
    Sherehe ilikuwa na mipango madhubuti
    Kabla mimi kuichukua michango ya Harusi
    Nikatoroka ughaibuni kufuata hisia zangu
    Kwenda kumfata njiwa wangu mahususi
    Nilivuka majangwa na majabali
    Sehemu ya safari anga sehemu nyingine bahari
    Niliacha kila kitu nyuma upendo na huruma vilinijaa
    Penzi likanipeleka mbali
    “JOHN ALIFIKA UGHAIBUNI, AKAMTAFUTA MSAMARIA ALIYETAMBULISHWA NA UJUMBE,
    MSAMARIA AKAMWELEKEZA NJIWA WAKE ALIPO, NA NIKWELI… HAPAKUWA PEMA”
    Nikakutana na bopa la kizungu
    Lenye sura ya kuichachisha mboga kwenye chungu
    Kiko kwenye mdomo,Tatuu kila kona na wapambe
    Pamoja na vishoka wenye mtutu
    Sio siri alizungukwa na wasichana wengi
    Sikujua umri walikuwa wadogo ka’ “madent”
    Baadhi walikuwa uchi wanahesabia “chenchi”
    Wengine masaji huku wengine wanamchezea nyeti
    “MASIKINI JOHN, ALIDANGANYA KWA KUJITAMBULISHA KAMA KAKA KWA JANE,
    AKIMSIHI YULE MAFIA AMRUHUSU AONDOKE NA JANE WAKAANZE MAISHA MAPYA,
    LAKINI… PALIPOSHINDWA SHOKA WEMBE HAUWEZI TAMBA. KWA KUZIDIWA NA UOGA WA KUUAWA…
    JANE ALIMKANA JOHN KWA KUSEMA HAMJUI…”
    Hata nilipomuuliza kama ananipenda hakujibu
    Akaweka moyo wangu maumivu
    Nilijua hawezi kufa kwa sababu hakunipenda
    Na ni rasmi nikapoteza shilingi kwenye msitu
    Nilikiambia kifo kama unakuja njoo
    Maana sikuwa mtu ilishakufa roho
    Sikuumia kama alivyoniumiza yeye
    Kwahiyo sikujali jinsi nilivyoteswa na wale mbwa no
    Aliambiwa ambusu bosi hakubisha
    Alipewa bunduki hakusita
    Aliishika risasi akaiingiza
    Akaambiwa anipige kwenye kichwa
    JOHN ALIKUWA NI JINA JIPYA LA WAHANGA WA UPENDO WA DHATI, VIPOFU WA MAPENZI, WAJINGA WA MAHABA...
    JOHN ALIKUWA ROMEO KWENYE ROMEO AND JULIETH, ALIKUWA SAMSON KWA DELILAH KWENYE WAHUKUMU WA AGANO LA KALE, ALIKUWA JACK KWENYE TITANIC, FRED WEASLEY KWENYE HARRY POTTER..
    JOHN ALITUKUMBUSHA KUWA UPENDO NI SADAKA, SADAKA YA MUDA NA PESA, ALITUKUMBUSHA UPENDO NI SADAKA YA DAMU
    JOHN, ALIPOTEZA UHAI AKIWA KWENYE SAFARI YA KUTAFUTA UPENDO WA MTU ALIYEMHUSUDU NA
    JANE ALIPOTEZA AMANI NA THAMANI YAKE KAMA MTU AKIWA KWENYE SAFARI YA KUTAFUTA UTAJIRI ALIOUHUSUDU
    Hatia iko wapi?

    • @challymchaff374
      @challymchaff374 4 роки тому +1

      Daaah dizasta wewe ni vina hivi naanzaje kuchoka kusikiliza nyimbo zako

    • @wilsontonga3728
      @wilsontonga3728 4 роки тому +1

      🤝🏾

    • @dullywamashairi121
      @dullywamashairi121 4 роки тому +4

      Naskiza ngoma mpaka moyo unataka kupasuka. Dizasta vina, MC Mahiri, Mc Katiri. Yaan hauishi kbs katika dunia tunayoishi sisi!
      Huku kwetu kitaa kizima wanajua n kiasi gani Mwamba unawika, wameacha kuniita jina langu, sikuhizi wananiita Dizasta Vina.
      Ngoma zako ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri na hana hatia. Ngoma zako zinaweza kumfanya mtu akatishe ktk msitu mnene wenye kutisha na asiogope. Ngoma zako zinamfanya mtu ajifunze kuwa mwenye maamuzi magumu bila kuhofia lawama la mwenye kulaumu!
      Dizasta vina, katika ulimwengu wa Hip Hop zaidi yako wewe bado sijamuona mwingine. Hata Fareed Qubanda umemtupa kule, kabakia jina tu!
      Hebu pitia hii ili uone uzao wa tungo zako broo
      ua-cam.com/video/_vGu4l1MoMw/v-deo.html

    • @castorymwaipopo290
      @castorymwaipopo290 4 роки тому

      Nakukubali sana bro 💪

    • @sautidawa2222
      @sautidawa2222 4 роки тому

      Real talent

  • @gerrymainmunisi6677
    @gerrymainmunisi6677 5 місяців тому +11

    Nani anasikiliza hiki chuma August 12, 2024... Dizasta mtu mbaya sana

  • @emilysaimon481
    @emilysaimon481 4 роки тому +11

    Dizasta vina bro we ni mkaliii
    Sikumpenda lakini nilijifunza kumjali Kama tupo pamoja tia like 25-12-2020

    • @dizastavina
      @dizastavina  4 роки тому

      Thanks.. Please share. Usisahau kuorder my new album

    • @emilysaimon481
      @emilysaimon481 4 роки тому

      @@dizastavina pamoja bro nigei no yako

    • @dizastavina
      @dizastavina  4 роки тому +2

      @@emilysaimon481 pre order kupitia tigo pesa 0655696811 au Mpesa 0762158871

  • @joshmangi
    @joshmangi 4 роки тому +16

    "Nilimfanya ndoto, kumbe naye ana ndoto nyingine"

  • @mdouharoon66
    @mdouharoon66 Місяць тому +3

    16/12/2024 Hili dude bado liko 🔥🔥🔥🔥🔥

  • @wawesttv
    @wawesttv Рік тому +2

    ... nilipo mwambia nampenda hakujibu... 2024

  • @maishacenter-eastafricatv3976
    @maishacenter-eastafricatv3976 4 роки тому +10

    Duuhh nlichelewa😪😪😪
    Dizzasta's fan number one from +257🇧🇮🇧🇮🇧🇮

  • @ashuramuhammed3257
    @ashuramuhammed3257 Рік тому +1

    Dizasta hii nyimbo ni funzo tosha yani ww ndo mwalimu wangu najifunza vitu vingi nkasikiliza nyimbo zako$

  • @abdfattah883
    @abdfattah883 Рік тому +2

    Kitu kinachoniuma ni kuona jamii inasikiliza miziki isiyo ya mafunzo yoyote na kuacha mziki wenye mafunzo Kama huu

  • @winfredykahwili1513
    @winfredykahwili1513 4 роки тому +5

    Huu mziki wako ni dawa ya ubongo asee Viva dizasta vina 💪💪💪👊👊💥💥💥

  • @shabannyamsalika
    @shabannyamsalika 4 роки тому +25

    Hii ngoma ni zaidi ya albamu nzima ya Weusi, Prof Tungo we ni 🔥🔥🔥🔥🔥

    • @dullywamashairi121
      @dullywamashairi121 4 роки тому +1

      Ngoma zake ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri asiye na hatia. Hebu pitia na hii link ili uone video, ni kitu kilekile ila mapishi tofauti. Haya ni mambo ya kutisha
      ua-cam.com/video/_vGu4l1MoMw/v-deo.html

    • @shabannyamsalika
      @shabannyamsalika 4 роки тому

      @@dullywamashairi121 Hip hop inahitaj wenye uwezo mkubwa wa kufkr, pole sana kwako mwny uwezo mdogo nkushauri kasikilize waaah!!!

    • @dullywamashairi121
      @dullywamashairi121 4 роки тому +1

      @@shabannyamsalika inaelekea wewe ndo hujanielewa Mimi. Wewe bado mbana pua. Wagumu wakipita wataelewa nimemaanisha nini.
      Umekurupuka mzee, maana kitaani wamenibatiza jina wananiita Dizasta vina!!💪💪💪

    • @shabannyamsalika
      @shabannyamsalika 4 роки тому

      @@dullywamashairi121 We ndo umekurupuka kusema huu wimbo ni wawagumu, hii ngoma anasikiliza mtu yeyote na anaelewa. Tuondoe mawazo finyu ya kudhania kuwa hip hop inasikilizwa na watu wagumu, cjui makatiri km wewe ulivyosema mwanzo...

    • @obeidjoseph3610
      @obeidjoseph3610 4 роки тому

      @@dullywamashairi121 mwanangu ww bado Sana na hilo jina la dizasta mwalichafua kitaan kwenu

  • @louiskhan7372
    @louiskhan7372 4 роки тому +6

    Hii True story nimesikiza ×10....song imenipeleka mpaka gaibuni ....utahisi mkono wa mungu umeandika Hii✔✔#KingOfRap

  • @kelvinshayo608
    @kelvinshayo608 4 роки тому +8

    Nilikwambia unajua na ctoacha kukwambia unajua💪💪

  • @rachelgmartin6850
    @rachelgmartin6850 4 роки тому +1

    Sauti yako tu mi hoiiiii🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🌹🥰❤️

  • @novatusanthony8563
    @novatusanthony8563 4 роки тому +2

    Hii goma inatakiwa wasambaziwe wanafunzi Tanzania mzima maana hili ni somo linajitegemea.

  • @fadhilimponzi2242
    @fadhilimponzi2242 Місяць тому

    ni nyimbo niliyosikiliza mara nyingi kuliko nyimbo yoyote dizasta vina

  • @jamesngadaya2791
    @jamesngadaya2791 4 роки тому +3

    dizasta unao uwezo mkubwa sana wenye nguvu kama meli ya mizigo aiseee

  • @shedzooytv4099
    @shedzooytv4099 24 дні тому

    Dizastavina greater thinker my best hip hop artist in tz nyimbo kama fasihi only for greater mind

  • @kangeyg6879
    @kangeyg6879 4 роки тому +5

    Master vina fan toka 🇰🇪🔥✅ tumengoja sana umewakilisha kama kawaida

  • @mwajumakarim8520
    @mwajumakarim8520 4 роки тому +5

    Wewe wewe weeeeeewe🥺🥺🥺ulishushwa ututeke🇹🇿❤️

    • @dullywamashairi121
      @dullywamashairi121 4 роки тому +1

      Ngoma zake ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri asiye na hatia. Hebu pitia na hii link ili uone video, ni kitu kilekile ila mapishi tofauti. Haya ni mambo ya kutisha
      ua-cam.com/video/_vGu4l1MoMw/v-deo.html

  • @ramsmambea2318
    @ramsmambea2318 16 днів тому

    This is my number one hip hop artist in Tz

  • @johnkerrysibomana9062
    @johnkerrysibomana9062 2 роки тому +1

    Nimerudi hapa baada ya mistari mingi kunigusa na kuendana na ninachikipitia kwenye maisha ya mahusiano

  • @learntoearn9588
    @learntoearn9588 4 роки тому +1

    Muda utafika Inshaallah dizasta utakua jina kubwa na ramani ya maarifa kwa kizazi kijacho

  • @Tobey1988ful
    @Tobey1988ful 3 роки тому

    New fan from +254 hapa.... Huyu kaka balaa sanaa dah

  • @ARUSHA_NAILS
    @ARUSHA_NAILS 4 роки тому +18

    Dah dizasta umezigusa hisia umenifanya nijione mwenye hatia

    • @erastompongo8400
      @erastompongo8400 4 роки тому

      Dah Kama umeniimba mimi vile
      Haso za mapenzi duniani zinaumiza wengi

  • @michaelmasanja6343
    @michaelmasanja6343 4 роки тому +2

    Verteller ...Dah huwezi amini nimeiona movie yote kichwani mwangu the way Mwamba unavoflow... nilichofeli ni kuipata sura ya Jane.

  • @lonely8682
    @lonely8682 4 роки тому +1

    Najivunia kua shabiki ako bro...hujawahi kuniangusha🙏🙏🙏🙏🔥🔥🔥🔥

    • @dullywamashairi121
      @dullywamashairi121 4 роки тому +1

      Ngoma zake ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri asiye na hatia. Hebu pitia na hii link ili uone video, ni kitu kilekile ila mapishi tofauti. Haya ni mambo ya kutisha
      ua-cam.com/video/_vGu4l1MoMw/v-deo.html

  • @kelvinmzopola5186
    @kelvinmzopola5186 4 роки тому

    Daaaaah so sad 😌 ila we jamaa unajua kinoma

  • @msolidwagalilaya6094
    @msolidwagalilaya6094 10 місяців тому +3

    Brother ushaandika HATIA nyingi sana lakini hii hatia IV ni funga kazi brother

  • @mosesbond202
    @mosesbond202 4 роки тому +1

    Wewe mwamba ni mwehu sema tuu unafikiri sana
    Yaani movie moja classic

  • @KelvinEmersonSteven
    @KelvinEmersonSteven 4 роки тому +5

    Aisee hii ni ya moto kushinda jua🔥🔥🔥🔥

    • @dullywamashairi121
      @dullywamashairi121 4 роки тому

      Ngoma zake ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri asiye na hatia. Hebu pitia na hii link ili uone video, ni kitu kilekile ila mapishi tofauti. Haya ni mambo ya kutisha
      ua-cam.com/video/_vGu4l1MoMw/v-deo.html

  • @kennywizy1009
    @kennywizy1009 4 роки тому

    Dah stor Kama yangu vile

  • @clementactor5366
    @clementactor5366 19 днів тому

    USIJIITE MUHUNI KAMA HUMJUI DIZASTA VINA (THE VERTELLER) broo you always teach me many lessons kwa mistari yakoo daaaah

  • @rizikicharles5109
    @rizikicharles5109 4 роки тому +1

    Dizasta hv ww ni nan daah unapasua xn hisia zungu kaka unajua xn

  • @awetubello5399
    @awetubello5399 4 роки тому +2

    Brother unawezaaaaah na xo unaweza 2 we ni MWALIMU

  • @dullyhaleem6962
    @dullyhaleem6962 2 роки тому

    Hii nyimbo itungiwe movie kummmke duuh😓😓🔥🔥🔥

  • @edvanpeter7547
    @edvanpeter7547 4 роки тому +1

    Dizasta vina unastahili kuwa mtu Wang wa kalibu Ila sio mbaya hata hap nakupata

  • @aaronjohn9518
    @aaronjohn9518 4 роки тому +1

    Deep sana hii ni kama movie

  • @jeovangisc7957
    @jeovangisc7957 3 роки тому +1

    Daaaa bro unajua mpaka unaboa.. masikio yetu hayalali njaa kila unaposhika kipaza!!

  • @EmmanuelAsifiwe
    @EmmanuelAsifiwe 2 місяці тому

    Paliposhindwaaa shokaa wembee hauweziii tambaaaa🤔

  • @BabaNasritz
    @BabaNasritz Рік тому +2

    naikubali kinoma hingoma bigp bro

  • @nassoromnyengo2263
    @nassoromnyengo2263 2 роки тому +1

    Wewe ni mkari sana

  • @yusuphmyinga
    @yusuphmyinga 4 місяці тому

    2024 Tunard kula madin kwa mwamba Ngoma hazichoshi vina Zawad yetu wapenda hip hop🙏

  • @hassanihanzel
    @hassanihanzel 4 роки тому +5

    Wa KUMI kutazama 🙌

    • @dizastavina
      @dizastavina  4 роки тому

      👏🏾 👏🏾 👏🏾 👏🏾

  • @binyezanch8271
    @binyezanch8271 4 роки тому +5

    Wimbo wangu wa mwaka kbsa Asante dizasta 2020

    • @dizastavina
      @dizastavina  4 роки тому

      Apreciate, umeshaweka order ya album

  • @esromkalulu7705
    @esromkalulu7705 4 роки тому +1

    Dizastaaa vinaaa ww nouma MC mahiri unatoa madini ambyo lazima ukubali

  • @peterbenjaminpeterbenjamin9566
    @peterbenjaminpeterbenjamin9566 4 роки тому +1

    Aisee dizastar noma Sana mshkaji wangu darasa Hilo namimi napenda Nije nipate mautundu ya asali ya hip-hop

  • @brainfigure94
    @brainfigure94 4 роки тому +1

    Dizasta vina saiv umesha convert akili yangu kwenye hiphop naenjoy sana napo usikia mziki wako nakuwa makini ili nielew unachokimaanisha nanukuu kwenye hatia 2 ulisema wanaume wote mbwa ila cjui sasa wewe ni kubwa la ma mbwa mana sioni wa kucompare na mziki unaoimba

    • @dizastavina
      @dizastavina  4 роки тому +1

      Shukrani sana ndugu, please share na marafiki

  • @chibalevicent822
    @chibalevicent822 2 роки тому +1

    You are so Genius, asante kwa uwezo wako wa kunifanya niamini kuwa wewe ndie Rapper Bora

  • @bonnifacewilly3026
    @bonnifacewilly3026 3 роки тому +1

    Daaah huyu jamaa anafanya mziki kwa bongo hakuna tena kama dizasta amani kwako brother

  • @boygavana4674
    @boygavana4674 4 роки тому +1

    Dizasta ww sio binadamu wa kawaida aseee haijawahi tokea

  • @danielmalimi9890
    @danielmalimi9890 3 роки тому +1

    Duuuhhh.... hii inabeba sababu muhimu ya muziki kwenye maisha....

  • @flovamanmusic3663
    @flovamanmusic3663 4 роки тому +1

    jamaa unajua sana unaandika vizuri sana big up sana kwa kazi nzuri

    • @dizastavina
      @dizastavina  4 роки тому

      Appreciate, please share and order my album now
      Tigo pesa 0655696811, mpesa 0762158871

    • @dizastavina
      @dizastavina  4 роки тому

      Appreciate, please share and order my album now
      Tigo pesa 0655696811, mpesa 0762158871

  • @ombenedwin136
    @ombenedwin136 4 роки тому +1

    Mungu ametupaga disaster vina

  • @muddyjumaa604
    @muddyjumaa604 4 роки тому +1

    Umetisha sana mzee baba bonge moja la ngoma

    • @dullywamashairi121
      @dullywamashairi121 4 роки тому +1

      Ngoma zake ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri asiye na hatia. Hebu pitia na hii link ili uone video, ni kitu kilekile ila mapishi tofauti. Haya ni mambo ya kutisha
      ua-cam.com/video/_vGu4l1MoMw/v-deo.html

  • @nashonshimba7997
    @nashonshimba7997 4 роки тому +1

    Imenitoa machoz hii ngoma mapenz yanauma sana

    • @dullywamashairi121
      @dullywamashairi121 4 роки тому

      Ngoma zake ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri asiye na hatia. Hebu pitia na hii link ili uone video, ni kitu kilekile ila mapishi tofauti. Haya ni mambo ya kutisha
      ua-cam.com/video/_vGu4l1MoMw/v-deo.html

    • @ramadhanally138
      @ramadhanally138 4 роки тому

      My broo really umenitoa mazur kweli VINA NI HAFAHI KABISA

  • @tiktoktv8678
    @tiktoktv8678 4 роки тому +4

    Wasanii kama hawa Bongo ni wachache Sana... Big up bro....

  • @erickpaschaljr8667
    @erickpaschaljr8667 4 роки тому +1

    Ahsante sana Dizasta Vina Kwa Muziki Mzuri unaoacha/utakaoacha Alama ya Milele

  • @revocatuscharles1512
    @revocatuscharles1512 Рік тому +1

    Jamaa unaimba sana aiseh🔥🔥🔥🔥

  • @oscarsospeter8034
    @oscarsospeter8034 2 роки тому

    Wewe ni mtunzi Huru Dizasta vina God Abless njia zako

  • @woltabenad8311
    @woltabenad8311 4 роки тому

    Kaka unajuw sana nakufatilia sana Kama ile sikumbaya

  • @sylvestermtweve2895
    @sylvestermtweve2895 4 роки тому +4

    Dizasta..... you're very UNIQUE broo...Mungu akuzidishe maarifa na afya tele just because unajua kutupa Raha mashabiki zako..GOD BLESS TOUR TALENT

  • @obeidjoseph3610
    @obeidjoseph3610 4 роки тому +1

    Unatishaaa yaaaani hiii ngoma mengne live

  • @tebeswiper2307
    @tebeswiper2307 2 роки тому

    My best movie ever @dizasta🙌🧠🧠🧠

  • @raymondtsumah6410
    @raymondtsumah6410 11 місяців тому +1

    Ogopa mwanamke💔

  • @ommygraphics4355
    @ommygraphics4355 4 роки тому

    Wewe jamaa ni fundi miaka yote nimeangaika kumeza nobody is safe 3 mwishoe umetoa dude lingine

  • @vandiddyy5733
    @vandiddyy5733 3 роки тому +1

    Duuh..! sijui nikupe jina gani broh... una hatari kubwa sana. 🙌🙌🙌

  • @sayeedally8152
    @sayeedally8152 4 роки тому +1

    kazi nzuri bro,,,, nakubali kazi zakoo

  • @fanikishashoppingmall
    @fanikishashoppingmall 4 роки тому +1

    Hujawahi niangusha brother,,,,,,🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

  • @raphaelhudson9699
    @raphaelhudson9699 4 роки тому +1

    Bonge la talent big up ..unazungumza na mimi kama

    • @dizastavina
      @dizastavina  4 роки тому

      Thanks, my album is out. Nunua kwa whatsApp au Email kwa namba hizi 0762158871 MPESA au 0655696811 TIGO PESA.

  • @valentinesyekeye6846
    @valentinesyekeye6846 Рік тому +1

    Upewe maua yako mzee. Hizi ni zaidi ya tungo

  • @franciscojonja1164
    @franciscojonja1164 4 роки тому +1

    Asie elewa kazi ya hiki kichwa aisee hatokuja kuelewa milele @dizasta vina ndio nembo ya hip hop isio vunja nguzo ata moja ya hip hop brother umetisha sana

  • @joshuacharles4313
    @joshuacharles4313 4 роки тому

    hujawahi kufeli broo hii ngoma hatari

  • @johnbahuta169
    @johnbahuta169 4 роки тому

    dizasta vina ni kina joh 70 // sio wakazi kadhaa wa kitongoji mkija njoo makini

    • @dullywamashairi121
      @dullywamashairi121 4 роки тому

      Ngoma zake ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri asiye na hatia. Hebu pitia na hii link ili uone video, ni kitu kilekile ila mapishi tofauti. Haya ni mambo ya kutisha 💪💪
      ua-cam.com/video/_vGu4l1MoMw/v-deo.html

  • @jofreymfugale4752
    @jofreymfugale4752 4 роки тому

    Aliondoka na kiungo cha mwili 😃🔥🔥

  • @harrismalone2316
    @harrismalone2316 4 роки тому +1

    Disasta bro 💪 hiphop ngumu ya kiakil na yenye uelewa wa kwel💥💥

  • @Joshi-LastKing
    @Joshi-LastKing 4 роки тому

    Nimesuburi kinoma hii ngoma

  • @furahinandrew9704
    @furahinandrew9704 4 роки тому +1

    We jamaa nomaa

  • @aloycemaembe8116
    @aloycemaembe8116 4 роки тому +1

    Nmekubar bro salut kwa hii kaz

  • @balikiabdala823
    @balikiabdala823 Рік тому

    🤔🤔🤔🤔 Noma sana ngoma kali sana

  • @meshack2559
    @meshack2559 4 роки тому +1

    Mistar unachora Broo!!! Ni nomah ,we mkali aise,big up

  • @alextanzania
    @alextanzania 4 роки тому +5

    Dizasta vina ni akina Joh 70.
    Mtiririko mzuri ,kazi nzuri. Big up brother.

  • @mullanochamp3860
    @mullanochamp3860 Рік тому

    ‘’Nilimfanya ndoto kumbe nae ana ndoto nyingine🙌🏽’’

  • @_Jayreally1
    @_Jayreally1 Рік тому +1

    Ebana kalii sana hii 🤔😥😥

  • @mwajumakarim8520
    @mwajumakarim8520 4 роки тому +1

    Nakuona mbali

  • @ommymsomi4362
    @ommymsomi4362 4 роки тому

    Ningekua baraza la sanaa ngomaa zako kaka zingetumika kujibia mitihan kaka...yan wanafunz ningewataka waskize kisha wachambue kila kipengele cha fasihiiiiiii

  • @salehekasangas3291
    @salehekasangas3291 Рік тому +1

    Umeshushwa.brooo...yan.unajuaa.brooo

  • @emmabelljohn4086
    @emmabelljohn4086 4 роки тому +3

    Nomaa sanaa

  • @directorluganongonya7212
    @directorluganongonya7212 3 роки тому +1

    Daaah ! Shikamoo tena

  • @brainfigure94
    @brainfigure94 4 роки тому +1

    Kuna haja ya dizasta kufungua chuo cha mziki wa hiphop ili vizazi vinavyokuja vielewe maana ya muziki wa hiphop

    • @dizastavina
      @dizastavina  4 роки тому

      👏🏾 👏🏾 👏🏾 👏🏾

  • @pst.AngeMwande
    @pst.AngeMwande 4 роки тому

    Aseee wewe ni mtu hatari kwelikweli big up kka

    • @dizastavina
      @dizastavina  4 роки тому

      Shukrani sana ndugu, please share

  • @octavianmushi928
    @octavianmushi928 4 роки тому

    Brazaaa umegusa maisha ye2 kwa hii ngoma

  • @benyvoice9415
    @benyvoice9415 3 роки тому +1

    Kaka hii ngoma naomba niifanyie cover yn nmeikubal Kias kwmb mpk nawaboa watu Everyday nackiliza

  • @Mchora_tz
    @Mchora_tz 4 роки тому

    Dizasta we jamaa ni hatarii no kiki no kelele ila mtaani unaleta kile tunachohitaji yaan hip hop ingekuwa hv labda tungeongea mengine mtaani #sioni km una ngoma mbovu

  • @kibafteshadau222
    @kibafteshadau222 2 роки тому

    Yule dogo raptcha akae mbali....ajifunze kuchana, sio fujo nyingi ....dizasta ni disaster balaa🔥

  • @nelsonkedmon8534
    @nelsonkedmon8534 4 роки тому

    Nakubali sana hujawahi kosea the vertller

    • @dullywamashairi121
      @dullywamashairi121 4 роки тому

      Ngoma zake ni ngumu, mtu akiziskiliza sana lazima awe Jasiri, awe katiri asiye na hatia. Hebu pitia na hii link ili uone video, ni kitu kilekile ila mapishi tofauti. Haya ni mambo ya kutisha💪💪
      ua-cam.com/video/_vGu4l1MoMw/v-deo.html

  • @geofreymboyelwa614
    @geofreymboyelwa614 2 роки тому

    Nyimbo nzur sana

  • @richardtitus8539
    @richardtitus8539 4 роки тому

    Daaah black maradona.. home boy unajua

  • @richardlugano8709
    @richardlugano8709 4 роки тому

    Dah Dizasta, uko hatua ambayo mimi naiota kufikia.

  • @BrightoneAyubu
    @BrightoneAyubu 2 місяці тому

    Appeiciet mzee baba🔥🔥🔥