TANGA UWASA RASMI KUHUDUMIA KILAPULA, MUHEZA

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 23 чер 2024
  • Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Andrew Mathew (Mb) ameilekeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (TangaUWASA) kuanza rasmi kutoa huduma katika eneo la Kilapula wilaya ya Muheza kuanzia Julai, 2024 ambapo awali eneo hilo lilikuwa likipatiwa huduma na Wakala wa Usambazaji maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kanda ya Muheza, Tanga.
    Maelekezo hayo ameyatoa katika Mkutano wa hadhara na wananchi wa eneo la kilapula Wilaya ya Muheza pamoja na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji ikiwemo mradi wa vizimba ya kutolea maji eneo la Kilapula wenye thamani ya Shilingi Milioni 156 ambapo Tanga UWASA imefanya ukarabati wa mradi huo kwa kulaza mabomba yenye urefu wa 2.5 km pamoja na mradi wa maji wa Miji 28.

КОМЕНТАРІ •