KVZ WAPANIA KUWAVAA M/MAKUMBI
Вставка
- Опубліковано 31 січ 2025
- Msemaji wa KVZ umesema kuwa kesho wataonyesha namna ya ubora wa kikosi chao kilivyo kwa kikosi cha wafuga punda kutoka Mwembe Makumbi utakaochezwa Uwanja wa Mao Zedong.
KVZ kesho wataikaribisha Mwembe Makumbi kwenye mchezo wa ligi kuu ikiwa ni mzunguko wa kumi nne.
Ofisa Habari wa KVZ, Abduljalil Muhammed amesema wanatambua ushindani uliopo kwenye ligi na namna kila timu inavyotafuta matokeo ila wao wataonyesha utofauti.
"Kikosi kipo sawa na tupo tayari kwa mapambano, tutaingia uwanjani tukiamini kwamba tunacheza na timu ngumu, ila kikubwa tutakachofanya ni kutumia vema Uwanja wa nyumbani," amesema Abduljalil.
#pbzpremiareleague #kvz #zanzibar