RC MAKONDA ASISITIZA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI MKOANI ARUSHA.
Вставка
- Опубліковано 25 лис 2024
- RC MAKONDA ASISITIZA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI MKOANI ARUSHA.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda Leo Jumatano Oktoba 23, 2024 amesisitiza umuhimu wa utunzaji wa mazingira ili kuhakikisha Mkoa wa Arusha unakuwa na uhakika wa maji safi na salama yasiyotibiwa na Kemikali.
Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020/25 katika sekta ya Maji Kwenye Kata ya Terrati Jijini Arusha, katika kuhakikisha kuwa huduma ya maji inapatikana kwa wananchi wote na kwa gharama nafuu.