DC FRANK MWAISUMBE AMEFUNGA MAFUNZO JESHI LA AKIBA WILAYA YA MONDULI KUNDI LA 40 LA MWAKA 2022

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 2 жов 2024
  • MKUU WA WILAYA YA MONDULI MH.FRANK MWAISUMBE AMEFUNGA MAFUNZO JESHI LA AKIBA WILAYA YA MONDULI KUNDI LA 40 LA MWAKA 2022.
    Katika hafla ya ufungaji wa mafunzo hayo yaliyo fanyika katika uwanja wa barafu Kata ya mto wa mbu iliyohudhuriwa viongozi wa Serikali na Wananchi waliweza kudhuria ufungaji wa Mafunzo hayo.
    Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alikagua gwaride lililo andaliwa kwajili kumaliza Mafunzo, pamoja ameweza kupokea gwaride lililopita Mbele yake wakitembea Kwa mwendo wa pole pamoja na mwendo haraka.
    Katika kuwapongea Askari waliomaliza mafunzo kundi la 40 la mwaka 2022 Dc Frank Mwaisumbe amekabidhi zawadi ya Cheti Kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika uwanja wa medani katika kulenga shabaha,Usafi Pamoja na Masomo ya darasani.
    Katika hatua nyingine Askari Jeshi la Akiba wapatao idadi 111 ikiwa Wanaume 89 na Wanawake 22 waliweza kula kiapo Cha utii mbele ya Mkuu wa wilaya Monduli Mhe Frank Mwaisumbe.
    Nae Mgm.Greta Robert Gombe akisoma risala kwa niaba ya Askari kundi la 40 la Mwaka 2022 amesema wao Kama askari mafunzo waliyopata yatawasaidia kuwaimarisha na kuweza kutekeleza majukumu yao ikiwemo kupambana vitani.
    Vijana hao Askari wa Jeshi la Akiba waliweza kuonyesha umahili wao Kwa kuonyesha michezo mbali mbali ikiwemo kuchoma singe, kuchekesha,Kombat kareti na Mbinu za Kusaidia majeruhi wakati wa vita.
    Nae Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Monduli Meja Emmanuel Shayo amesema Mafunzo waliyoyatoa Kwa vijana hao ni ya muhimu Kwa kuwaandaa Vijana katika Ulinzi wa Taifa hasa Kwa Wilaya ya Monduli Pamoja kusaidi shughuli mbalimbali watakazo pangiwa.
    Mkuu wa wilaya Monduli amewapongeza vijana hao kuhudhuria Mafunzo hayo ya Jeshi la akiba kwani kufanya hivyo ni kitendo Cha kizalendo.
    Hivyo mkuu wa Wilaya ya Monduli amepongeza Suma Jkt pamoja Hifadhi ya Manyara Kwa kuwachukuwa vijana hao wapatao 110 na kuwataka vijana hao kuwa mabalozi Wazuri huko wanapokewenda ili waweze kuleta sifa ndani ya wilaya ya Monduli na Sio kuwaharibia wengine wanaofuata.
    Nae Mwenyekiti Umoja wa vijana wilaya ya Monduli Ndg.Paniel Tutunyo amepongeza kutolewa Kwa mafunzo hayo Kwa vijana ambayo yataweza kusaidi vijana katika kutekeleza majukumu yao mbalimbali.

КОМЕНТАРІ • 12

  • @AdamuAndendekisye
    @AdamuAndendekisye 17 днів тому

    Hongereni japo mananga ni wengi 😊

  • @GehaziMetelii-p4m
    @GehaziMetelii-p4m Місяць тому

    Mbn wamemalizia magongo tena

  • @emanuelmalale7853
    @emanuelmalale7853 Рік тому

    Hongera sana kwa vijana was monduli kwa kuonyesha uzalendo pia jkt suma kwa kuwapokea kwa ajili ya kuwawezesha

  • @habibumohamed1543
    @habibumohamed1543 Рік тому

    Natoa pongezi Sana Sana
    Mafunzo ya jeshi la akiba ni zuri Sana hii inajenga uzalendo na utayari muda wowote katika kulinda na kulijenga Taifa
    Ukakamavu unatakikana Sana Kwa vijana wengi wa kitanzania

  • @annakwathema8555
    @annakwathema8555 Рік тому

    Makamanda hi ni nzuri kwa kweli nawa pongeza Sana akina KP, Mbagwa ,Mwaisa ,Devi,na Haniu😁😁

  • @ndimimaskati3641
    @ndimimaskati3641 Рік тому

    Hawa jeshi la akiba ndio watakao tumika kutesa watu watakuwa watu wasiojulikana.

  • @KilusuMigaro
    @KilusuMigaro Рік тому

    Mungu akuongozee miaka mingi za kuishi Makanda wetu

  • @salummzee9739
    @salummzee9739 Рік тому

    munanikumbusha mbali daaah ww acha tu,naumia moyo leo hii na randa na mtaaa

  • @StellaAndrea-d7k
    @StellaAndrea-d7k Рік тому

    Mungu awabariki sana makamanda wetu

  • @nikolaussanga5602
    @nikolaussanga5602 Рік тому

    Makamandaa monduli wako njemaa

  • @StellaAndrea-d7k
    @StellaAndrea-d7k Рік тому

    Mungu ibariki tanzania

  • @livingkiwali3572
    @livingkiwali3572 Рік тому

    Mungu atubariki makamanda