Dizasta Vina - Shahidi
Вставка
- Опубліковано 5 січ 2025
- audio
Boomplay - www.boomplay.c...
Audiomack - audiomack.com/...
Lyrics - genius.com/Diz...
Mdundo - mdundo.com/son...
Lyrics
Nilipanda kwenye jukwaa, watu walinishangaa,
Unadhifu wa meli haukufanana na nilivyovaa
Kabla sijatoa salamu, walipoteza hamu
ya kuburudika wengine wakaanza kusambaa
Nilikuwa na nywele nyingi zilionyesha pia siku ni nyingi tangu mara ya mwisho ziwekwe maji,
Wale Matajiri waliosheheni kwenye viti walicheka wakihisi mi’ chizi au mchekeshaji
Walio karibu pia wakaanza kun’tunza pesa
Na walio mbali walijaribu kurusha fedha,
Kwa yote niliyowaeleza hakuna alieyaweka kichwani
Wote walihisi kuwa nataka kuchekesha
Walinitemea shombo kwa kejeli
Wengine walihisi nalianzisha zogo kwenye meli
Mwonekano haukuyabeba maneno yangu
Hawakuamini niliposema kuwa chombo kina mushkeli
Niliwaeleza kuwa kule ndani kuna tundu dogo
Linapitisha maji linazamisha chombo
Waliendelea kujadili siasa na vibonzo
Hakuna aliyejadili kuhusu roho
Za wasakatonge wanyonge wasafiri daraja la tatu
Hawakulipa pesa nyingi ila walikuwa ni watu
Maji yalianza kuingia vyumbani mwao
iliwekwa mipaka hivyo taarifa hazikufika katu
Nilienda mpaka chumba cha sauti
Nitoe tangazo kabla hatujakumbwa na mauti
Mtoa sauti aliwataja matajiri
akiwapa sifa majina makubwa na saluti
Niliwaambia wekeni glasi chini mtege masikio
Hizo kelele mnazosikia si sherehe ni vilio
Wakasema nimedata nataka kuanzisha vagi
Ilionyesha wazi hawakuona mbeleni tishio
Hata kwenye vyumba vya wasomi maarufu
Vyeti walihodhi maradufu
Niliwahoji kuhusu ubovu wa meli wengi
waliujua ubovu lakini walisema haiwahusu
Naapa haki nilienda kote..
Nilihamaki kuona wote wamepewa cocktail
Nilimwona nahodha nikahisi nimeipata nafuu
Alikua kando ya mrembo fulani hivi daraja la juu
Gauni refu mwili mzima amepakaza tatuu
Aliponiona aliendelea kuikata tamboo
Kweli starehe inaweza kukufanya hauoni
Kukufanya hauoni
Kwani licha ya kujua nipo hapo kutoa
taarifa nahonda na mrembo waliendelea kushikana maungoni
Nahodha akaipaza miguno, akinipuuza
Mrembo naye akafata mkumbo,
Nahodha akachukua chupa akakata mafundo
Wakaendelea kupapasana mifumo
Ya viungo vyao vya uzazi walikuwa radhi kuzika shift
Hawakusikia chochote nilichosema
Nakumbuka mrembo alidiriki kuniita mwizi
Nikafatwa nikaja kupigwa na walinzi
Wenzangu waliogundua ubovu wa chombo walihofu
Wakaamka wakawahi kubeba vyombo vya wokovu
Walikaa kimya kwa sababu tu ya ubinafsi
Mi’ nikabaki ili niziokoe roho za wachovu
Ilikuwa bahati mbaya hakuna aliyesadiki,
Mshereheshaji akaongeza sauti kubwa ya mziki
Kiasi sauti yangu ikaanza kuwa haisikiki
Walinzi walitumwa wanidhibiti
Nilifungwa kwenye chumba chenye giza chini nisihame
Nikachapwa mijeledi thelathini na minane
Nikapambana nikatoroka na mtumbwi kwenda kando
Usalama wangu ulianza hapo
Nilishuhudia kila inchi ya ile meli ikizama
Roho za kila mkwezi zikihama
kutoka uhai kwenda kifo, sikufurahi kuona hivyo
Ila sikuwa na jambo ningeweza ‘fanya
Wakati walokole wakiombea kupona
Tajiri na maskini waligombea maboya
Wanazi walionicheka wakasema mi’ ni zuzu
walikufa wote hata walionisema kinoma
Ahadi ya maisha mapya ilisemwa ila hakuna aliyekumbuka,
Pesa zilizagaa na hazikuguswa,
Hata wale waumini walioitamani mbingu
Na kuisifu, kumbe wote waliogopa kufa
Waliokuwa wanajikweza na ukubwa na ubosi mwingi
Yaliwaishia majivuni
Njia walizibuni, waliua mpaka wenza ili ‘kufosi kingi’
Kifo kiliwatia mbavuni
Walikufa wengi kama kuku kote walizagaa
Hata wanajeshi waliozijua ‘kareti’
‘Walidedi’ maana ujuzi wa mitutu haukufaa
Mbele ya kufa hakuna mwenye nguvu au shujaa
Nilishuhudia makafiri wakiungama
Masikini na Matajiri waligusana
Utu uliwatoka uasi ulisogea
Tofauti za kabila na rangi zilipotea
Watu wenye bendi na ‘tisheti’ zao za kijani
Walisahau kuwa nao pia wapo ndani
milango ilokuwa wazi yote ilijifunga
Walipiga kelele na mwisho walikufa maji
Washairi waswahili na tashtiti zao
Matajiri na masikini wote chini yao
Kwaya hazikutoa sauti ndimi zao
Walikufa wote mpaka mahujaji na dini zao
Wakati wa kufa hakuna dawa
Hakuna kiongozi hakuna chawa
Hakuna tofauti ya mali na milki zetu
Kwenye kufa hata wenye nacho na wasio nacho wanakuwa sawa
Hazikusaidia diplomasia za digitali
Asili ilihakikisha walosalia hawafiki mbali
Waliendelea kungoja msaada kwa tumaini
Mwisho wote walikufa sababu ya baridi kali
Walikufa makini sababu ya wapuuzi wachache
Walofanyia uzembe tangazo langu
Wamiliki walikula bima wakasingizia ajali
Ilihali meli ilizama mbele ya macho yangu… ah!
Viongozi hawakubebwa na vyeo vyao
maana wote walikuwa mbali na ridhaa
Niliona kofia za ufalme zikielea kando yao
Ila hakuna aliyekuwa hai kuzivaa
Niliwapa taarifa lakini wakanitwika maudhi
Waliishia kulia na hazikusikika sauti
Walipambana Mwisho yaliwafika mauti
Nilibaki hai kuziandika sarufi
No major record label
No media tour
No management
No kick or scandals
Just a poet with poetry
Just pure artistry
Greatest of all time
Appreciate
✍🏿✍🏿✍🏿
We appriciate u bro maana unatema content tupu bila blaablaa na wadau wanelewa na kununua kazi zako.Tena mbali zaidi inatia moyo kuona msanii mwenzio anaalbum yako na anasema hadharani kuwa unajua
this man knows asee✊🏿👏
Fffa
Meli ,,,ni TZ,,na shaidi no 2ndulisu,,,,Ajari ni yale mamikataba ya ovyo ,,,,Yaliyosababisha kimbunga Cha CORONA baadaee vifo vya kutisha vya viongoz TZ,,,,🎉🎉🎉🎉🎉🎉🎉 noma sanaaa HICHI kiumbe so mchezo
Thank you for the love family. Peace ✌🏼
We love you broo 🦾💥
dizasta shikamoo 🙌
😂 et nilikulea kaa babaako sio mim ni mapenz juu yako 😂
Mwafrika
Kanisa
Lost one
Kijogoo
Hatia 1 to 4
Musculer
No body safe 1 to 4
Ndoano
Naacha game
Connection (mad man,mad teacher,mad son,mad profeser)
Kibabu
Almasi
Siez maliza nkianza mention but Kila kitu Na mda wamebana sana but its ur tym now
We love you dizasta
Taratibu tunaeleweka sasa
Lyrics
Ah
Nilipanda kwenye jukwaa, watu walinishangaa,
Unadhifu wa meli haukufanana na nilivyovaa
Kabla sijatoa salamu, walipoteza hamu
ya kuburudika wengine wakaanza kusambaa
Nilikuwa na nywele nyingi zilionyesha pia siku ni nyingi tangu mara ya mwisho ziwekwe maji,
Wale Matajiri waliosheheni kwenye viti walicheka wakihisi mi’ chizi au mchekeshaji
Walio karibu pia wakaanza kun’tunza pesa
Na walio mbali walijaribu kurusha fedha,
Kwa yote niliyowaeleza hakuna alieyaweka kichwani
Wote walihisi kuwa nataka kuchekesha
Walinitemea shombo kwa kejeli
Wengine walihisi nalianzisha zogo kwenye meli
Mwonekano haukuyabeba maneno yangu
Hawakuamini niliposema kuwa chombo kina mushkeli
Niliwaeleza kuwa kule ndani kuna tundu dogo
Linapitisha maji linazamisha chombo
Waliendelea kujadili siasa na vibonzo
Hakuna aliyejadili kuhusu roho
Za wasakatonge wanyonge wasafiri daraja la tatu
Hawakulipa pesa nyingi ila walikuwa ni watu
Maji yalianza kuingia vyumbani mwao
iliwekwa mipaka hivyo taarifa hazikufika katu
Nilienda mpaka chumba cha sauti
Nitoe tangazo kabla hatujakumbwa na mauti
Mtoa sauti aliwataja matajiri
akiwapa sifa majina makubwa na saluti
Niliwaambia wekeni glasi chini mtege masikio
Hizo kelele mnazosikia si sherehe ni vilio
Wakasema nimedata nataka kuanzisha vagi
Ilionyesha wazi hawakuona mbeleni tishio
Hata kwenye vyumba vya wasomi maarufu
Vyeti walihodhi maradufu
Niliwahoji kuhusu ubovu wa meli wengi
waliujua ubovu lakini walisema haiwahusu
Naapa haki nilienda kote..
Nilihamaki kuona wote wamepewa cocktail
walikunywa na kula bata, walikunywa hata
mziki waliruka mpaka mafundi walilewa pombe
Wakasema huyu ni mjinga hajielewi
Kisha wakanituhumu mi’ ni mlevi wakati
Wamelewa wao, wakanipa matusi ya kienyeji
Hawakutaka kusikiliza hata semi
Nilimwona nahodha nikahisi nimeipata nafuu
Alikua kando ya mrembo fulani hivi daraja la juu
Gauni refu mwili mzima amepakaza tatuu
Aliponiona aliendelea kuikata tamboo
Kweli starehe inaweza kukufanya hauoni
Kukufanya hauoni
Kwani licha ya kujua nipo hapo kutoa
taarifa nahonda na mrembo waliendelea kushikana maungoni
Nahodha akaipaza miguno, akinipuuza
Mrembo naye akafata mkumbo,
Nahodha akachukua chupa akakata mafundo
Wakaendelea kupapasana mifumo
Ya viungo vyao vya uzazi walikuwa radhi kuzika shift
Hawakusikia chochote nilichosema
Nakumbuka mrembo alidiriki kuniita mwizi
Nikafatwa nikaja kupigwa na walinzi
Wenzangu waliogundua ubovu wa chombo walihofu
Wakaamka wakawahi kubeba vyombo vya wokovu
Walikaa kimya kwa sababu tu ya ubinafsi
Mi’ nikabaki ili niziokoe roho za wachovu
Ilikuwa bahati mbaya hakuna aliyesadiki,
Mshereheshaji akaongeza sauti kubwa ya mziki
Kiasi sauti yangu ikaanza kuwa haisikiki
Walinzi walitumwa wanidhibiti
Nilifungwa kwenye chumba chenye giza chini nisihame
Nikachapwa mijeledi thelathini na minane
Nikapambana nikatoroka na mtumbwi kwenda kando
Usalama wangu ulianza hapo
Nilishuhudia kila inchi ya ile meli ikizama
Roho za kila mkwezi zikihama
kutoka uhai kwenda kifo, sikufurahi kuona hivyo
Ila sikuwa na jambo ningeweza ‘fanya
Wakati walokole wakiombea kupona
Tajiri na maskini waligombea maboya
Wanazi walionicheka wakasema mi’ ni zuzu
walikufa wote hata walionisema kinoma
Ahadi ya maisha mapya ilisemwa ila hakuna aliyekumbuka,
Pesa zilizagaa na hazikuguswa,
Hata wale waumini walioitamani mbingu
Na kuisifu, kumbe wote waliogopa kufa
Waliokuwa wanajikweza na ukubwa na ubosi mwingi
Yaliwaishia majivuni
Njia walizibuni, waliua mpaka wenza ili ‘kufosi kingi’
Kifo kiliwatia mbavuni
Walikufa wengi kama kuku kote walizagaa
Hata wanajeshi waliozijua ‘kareti’
‘Walidedi’ maana ujuzi wa mitutu haukufaa
Mbele ya kufa hakuna mwenye nguvu au shujaa
Nilishuhudia makafiri wakiungama
Masikini na Matajiri waligusana
Utu uliwatoka uasi ulisogea
Tofauti za kabila na rangi zilipotea
Watu wenye bendi na ‘tisheti’ zao za kijani
Walisahau kuwa nao pia wapo ndani
milango ilokuwa wazi yote ilijifunga
Walipiga kelele na mwisho walikufa maji
Washairi waswahili na tashtiti zao
Matajiri na masikini wote chini yao
Kwaya hazikutoa sauti ndimi zao
Walikufa wote mpaka mahujaji na dini zao
Wakati wa kufa hakuna dawa
Hakuna kiongozi hakuna chawa
Hakuna tofauti ya mali na milki zetu
Kwenye kufa hata wenye nacho na wasio nacho wanakuwa sawa
Hazikusaidia diplomasia za digitali
Asili ilihakikisha walosalia hawafiki mbali
Waliendelea kungoja msaada kwa tumaini
Mwisho wote walikufa sababu ya baridi kali
Walikufa makini sababu ya wapuuzi wachache
Walofanyia uzembe tangazo langu
Wamiliki walikula bima wakasingizia ajali
Ilihali meli ilizama mbele ya macho yangu… ah!
Viongozi hawakubebwa na vyeo vyao
maana wote walikuwa mbali na ridhaa
Niliona kofia za ufalme zikielea kando yao
Ila hakuna aliyekuwa hai kuzivaa
Niliwapa taarifa lakini wakanitwika maudhi
Waliishia kulia na hazikusikika sauti
Walipambana Mwisho yaliwafika mauti
Nilibaki hai kuziandika sarufi
yo
Kaka ww ni noma,
Hatari sana
HIPHOP SANAA
Brother izi idea zako ni nomaa mzee👊🏽👊🏽
Msanii wang wa Hip Hop ninayemsikiliza sanaaa...em mwageni miLIKES wale mnaomkubali huyu kijana
💪🏽💪🏽💪🏽
bro kuna manabii wa hiki kizazi cha karne zetu na hapa Tanzania katika huu umri na ufahamu wangu mdogo nimebahatika kuwatambua watatu 1:MWALIMU JK WA KWANZA
2:JPM KAZI
3:DIZASTA VINA
may Jah be with you
unaongea vitu visivyohitaji tafsiri kutoka google zaidi ya ubongo usio na msongo za teknolojia ya kisasa isipokua ngano za wahenga na mababu wa kibantu kwa lugha rahisi fasihi ulonayo sio ile inayoitwa literature kwa lugha ya wafanyabiashara wa magharibi hii ni ya jando na unyago kaka yapo mengi ya kuandika kuhusu sanaa yako ila sanamu yako itajengwa mioyoni mwa mamilioni ya watanzania siku moja maana majuto hurejesha mafunzo yaliyopuuzwa baada ya matokeo haribifu asante
Wayaaaa🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
Kuna sehemu unatakiwa uwe asee! Kikubwa kuliko vyote ni Unajua kuchezea lugha
Hawakulipa pesa nyingi Ila walikua ni watu🙌🙌🙌🙌
Huwa natanguliza like kabla , nauhakika na Dizasta
Uwo ndiyo uwarisilia watu watu wa nyanda juu kusini na kasizini
4:58 ndio nimepata picha Sasa unaongelea Nini 😂😂🙌🙌🔥, akili nyingi Sana imetumika
DIZASTA YOU ARE THE BEST LYRICIST AND BEST STORY TELLER EVER,You are just not famous coz JAMII IMEJAA UJINGA as U said..but be proud u got us your disciples Not Only FANS
Well said brother
Very true huyu jamaa na Nacha ni hatari sana
Word up✊
@@yassinuddi yeah huyu jamaa na Nacha wanafanana kufikiri..wote wapi smart sana
He's not a storyteller he is The Verteller
Dah broo sijui nkuite nan dah hiki chakula kbsa kaka n nmekuelewa umezungumzia nn simamia misingi hvyo hvyo kaka
Wakwanza kabisa kwenye kichwa changu nikitajiwa hipapu apa bongo na east Africa toleo la mwisho la kizazi Cha Aina yangu🚭🚭🚭🚭
Nyimbo zako hazifai kusikilizwa kwa masikio pekee , lazima utumie na akili kuzielewa ... wenye akili pekee ndo watu wanaozielewa kama hii nyimbo ni ujumbe ambao nahisi ni current situation .... Mungu ibariki Tanzania🇹🇿
Kaka wewe yaani wewe Dizasta Vina hakuna kama wewe najivunia kuwa shabiki wako, ntakuwa SHAHIDI kwa vizazi vijavyo.. Ahsante sana kaka kwa chakula cha ubongo 🙏🏿
🙏🏼🙏🏼🙏🏼
asante kwa ujumbe mzuri,,tuache kupuuzia mambo tunayoambiwa
Mungu endelea kuifadhi hii talanta, kuna vizazi vya miongo mitatu vitajifunza somo lake. Dizasta vina🙌🙌
Amen
Now days tuna trend tu soon tutakua kwenye kioo Cha jamii
Ahsante kwa kumbukumbu hii, tutamkumbuka sana JPM.
🎉🎉
Hujawa koseaaa Naninachoo fulaii hadi sasa hujafikilia kuachaa Muziki mzuliii kamaaa huuuuu ##
Watu wenye bendi na tshart za kijana🙌
aiseee kumbe iliyozama sio meli bali na mv Tanzania nchi yetu kabisa nimekuelewa bro bado naendelea kuisikiliza nanaweza kugundua mengine
Jee ni story ya kweli
Africa ni mda wetu sasa wa kujikomboa na kujitambua hizi dini ni biashara za watu kama dini Africa tulikuwa na dini zetu... Wake up Africa 🧠🧠🙌
Shahidi upande wa mahakama nitakuwa wa kwanza
🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Kwa kweli disasta ni zaidi ya mwandishi,zaidi ya. Mtunzi au tumwite vpi.mwageni makopa yake💖💖
Hii Meri ni nchi yetu Tanzania, asante sana Shahidi wetu, asante Dizasta, asante ewe Mc Katili
Na ndiomaana tunaokuelewa tunasema kuwa hauishi kabisa dunia tunayoishi sisi, upo mbali umesafir kwa mtumbwi, unatuona tunavyozama na meli kwa ujinga wa viongozi wa meli
Tanzania😭
naisikiliza 2024,huyu mwamba anakituuu asikilizwe
Ningekua natoa tuzo mim
1;best rapper ni dizasta
2;best album the verteller
3;best song wimbo usio bora
Ila nashangaa wanaopewa tuzo hata awa stahilii kabsaa wana acha kichwa cha hip hop kama hikii bro endelea kutuma madimi maana wajinga hawajui unafanyaa nn me nishabiki yakoo nambaa 1 ngoma zakoo zote ninazo ❤❤❤❤❤
Tatizo tunzo zamchongo awasikilizi mashaili wanaangariya nani mwekiki ndiyo anapew 2nzo sisi 2nao juwa 2nasikiza mzk mzr ngoma kali kamaizi na mafundisho 🙏God bless dizasta🙏✍
Dizasta vina wewe ndo mfalme wa hip hop tz hiz ndo fasihi ya ukwel basata watahifadhi makumbusho ngoma zako
If you are listening this song in 2050, the singer called Dizasta Vinna. He was the most genius talented guys in Tanzania. He had no label or any kick but he did the best all the time. We enjoyed true poet music from him at that time,
Ningekua na hela ningefungua media ambayo ingepiga hip hop,, na wewe ningekupa kipindi cha uchambuzi wa mashairi ya ngoma kama hizi, nakukubali sana sana
🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Been a while since i last witnessed the masterpiece, best storyteller by far most , true definition of hip hop, true hip hop never die, Elementary hip hop💪🏾🤝
Dizasta vina nipo zangu Malawi napenda sana Ngoma zako Yani zote ni kali sana ya wewe ni zaidi hata ya NACHA
Moja ya verses zako nakumbuka ulisema "nipo underground na huku ndo mitutu inapofichwa" nakubar sana majina madogo Yana contents nyingi sana za kujifunza i wish ningekuanazo fedha ili hizi jumbe zifike kwa urahisi Zaid kwenye jamii zetu... Ila mungu mwema blood one-day Yes
Thank you so much
HARDCORE
Damn!!
Damn
Damn
Damn!!!!!!!
Dizasta umeua kinoooomaa.....
Ngoma kaliii sana.........
Daaa Flow kalii sana
Sidhan kama itakuwa rahic mbele yko nkamuweka mcee ambye atakuw the best kupta ww Kijana wa kaz, isipokuwa tu tunaokuckilza weng wetu hatuna namna ya kku-push far. 👑👑👑 One of the better than better best STORY TELLERS MASTER MIND EVER
🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Watanzania hatuna Cha kuklipa kaka dizasta ila tutaksapot kwa tlch nach Mungu akubarik bro unajua
Its almost 6x nasikiliza hii ngoma ....ebana umetisha sana kwenye upangiliaji na uandishi wako kwenye hii ngoma...iko na ujumbe.mkubwa sana ....hii ndo maana ya usanii...fanani na hadhira iko hapa
🤏
Ahsante
THE FACT THAT HE IS DOING IT WITHOUT MAJOR RECORD LABEL IS AMAZING
👊🏽👊🏽👊🏽
Non sense like wasafi will just fuck on his style
Kioo cha jamii,fan since day 1 🇰🇪🇰🇪
U'r impeccable, u'r on unique class ...best story teller WORLD wide
Thank you
Toka day one nlikuamin we genious.kaka ulipo sipo ulipokua kumaanisha tunasogea ...mda utatafsiri ukubwa wako.
👊🏽🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Wakati wakufa hakuna dawa, hakuna kiongozi wala chawa.💪🏿
👊🏽👊🏽👊🏽👊🏽
Daaah nahisi Mungu haje mwenyewe akutoe ili ujulikane EastAfrica yote sema ndo ivooo! Uko hai bd siku yko inakuja Mungu wa rap.
🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Dizasta Vina is a master Swahili story teller of our time!
Aaah kaka we una kipaji cha pekee sana..
Uandishi wako unafata kanuni zote za fasihi.. Mashairi yako yanafaa kutumika kufunzia watu kwa kweli..yeyote atakayeskiliza wimbo wako wowote bhasi ni lazima atamani kusikiliza na zingine pia
Kichwaa kimetapakaa books kama ribrarry 🔥🔥🔥🔥 genius and talented
🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Hata comment nayo iandika haitoshi kuelezea your GREATEST MY BROH GOD BLESS YOU☠️☠️
💪🏽💪🏽💪🏽👊🏽👊🏽
Huyu mwamba anajua sana pia nyimbo inafikirisha tafsida zakutosha tulizeni vichwa mtamuelewa tu huyu jamaa yupo deep sana kwa kuzazi chetu rudieni ata mara 10 mtaelewa👏👏
🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Huyu Dizasta Vina Ni Rapa Nouma Anaehitajika Kupewa Sikio, Sababu Anaandika Vitu Vya Maana....
🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Mungu akulinde sana
UkifuMbua FUMBO, Wewe ni HADHIRA MAHSUSI... ✊🏿
😄kwel
Not just a fan , I'm a disciple here.
Mad Love from Kenya My G.🇰🇪🔥
🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Huy jamaa ni mshairi... Sana'a..
ambao hawasikilizi mzik wa dizasta wanapoteza madini
my best storyteller all the time. let narrate this king
te t
🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Uyu mwamba kwenye hip pop anatisha ni zaid y msimuliaj
You are not just a rapper you're talented genius.
Indeed
We mkali sana mfundishe rapcha.... Dogo hakuez
Wow 😲 very long verse and fantastic as well, no. 1 story teller in our country
Thank you
Watu wenye bend na tishet zao za kijani, walisahau kuwa nao wapo ndani
The best hip hop artist in Tanzania right now
midia na tanzania na mashabiki wa all musin in tanzanian iv tunamuelewa dizasta vizuri kwangu mm naona haina aja ajielezee kama Nacha tuelewe anacho kifanya watanzania wete na vyombo vya habar sisi upendo niasili yetu tumpe nafas uyu kijana abebe hii 🇹🇿🇹🇿🙏🙏🙏
🙏🏼
🔥🔥💫🔥BRO HAKUNA KAMA WEWE KWENYE ULIMWENGU WA HIP HOP 👏👏👏👏
🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼
dizasta vina mwenyezi mungu akubariki nafurahia sana mziki wako
Thanks my fav MC for having made my day! Veener!
huyu ndo @Dizasta na sanaa yake yake kwenye sayari yake. Good Job brother
Ukimsikiliza sana brother Dizasta utagundua kwenye hii Ngoma anaongelea mambo tofauti aliyowahi kuifundisha jamii kupitia Mangoma yake afu wajuba wakapuuzia ,sasa yeye akatumia maarifa yake akakaa pembeni anachek dunia inavyoangamia huku yeye akiwa ameshafanya kazi yake yakuelimisha
Shahidi ametisha saana ,hii Ngoma Dizasta alitakiwa kuiachia siku ambayo angekua anastaafu game ili iwe kama summary ya safari yake yote ya muzii, ASANTE
Daaah mdau wee noma...
Message ya ukwelii kabisa
utasema mkono wa mungu umeandika... mungu wa rapp 'kazi imekazika kizazi sana.
"Kweli starehe inaweza kukufanya hauoni"
🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Uandishi una make sense chuma za kuteka hisia, well done master
one of the best story tellers ...presenting dizasta vina
Thank you
Nakubali my brother
Tanzania mzima hakuna msanii Anaeandika kama Dizasta Vina ukitaka chakula cha ubongo msikilize huyu msanii utapata Exposure ✊✊✊
🙏🏼🙏🏼🙏🏼
This is a masterpiece for real. This guy should consider writing a book about this. This is historical. The rate at which I'm putting this song on replay is unhealthy🤭
Aisee hii ngoma, video unakuwa nayo mwenyewe kichwani😁😁
I like the way u relate with ur fans, Reading and replying to their comments shows ur good personality unlike other artists,GOD bless you bother, SHAHIDI is a Hit🔥🔥🔥
All love brother 👊🏽👊🏽
na-refer hii meli na kizazi ambacho kila siku Dizasta amekuwa akipiganacho kelele kuhusu mambo mbalimbali (mfano hatia 3) lakini kimekuwa kinampuuza, hayo ndio kilichowakuta japo kuna wachache sana tuliomuelewa tutapona
🙏🏼🙏🏼🙏🏼
You're gifted, , Best story telling..GOAT
Oya weeee mkubwa vinna we nishida sijawahi kupangana nawewe
Genius,Rapper,Unique Storyteller bro naappreciate kazi zako kaka
Thank you so much
Mhhhhh
Dizasta ur a lyrical genius
Scripts writter Hollywood levels
🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Daaah mwana unajua Sana sichoki kukusikiliza Na kukufuatilia mungu akuweke sana ka mkubwaa
LYRICAL STORY TELLING DEMON. The Best i Ever Know. Salute pia kwa huyu Kiumbe Ringle Beats. Bonge la Mdundo. 🔥🔥🔥🔥🔥🔥
Sure.
Thank you
Naweza sema Ni mpango
Maana hata rubani wa meli mpya
Unadi yake na kuicheka T912🦾🦾
🙏🏼🙏🏼🙏🏼
The most lyrical gifted Rapper...Game is in the safe 🧤..🎶🔥
Mnyama wangu vina
The real meaning of Dizasta
Yes ur
Big up sana brodah 💪
Best story teller
Thank you
All da best
🙏
Dua nying 🙏
Kweny cm nna ngoma zako kama 31
Kati ya nyimbo pendwa moja NI hi sijawahi choka kuiskiliza big up kaka
Dizastar you are the real meaning of true poet
Thank you so much
Huu ushairi wa huku ni wenye akili tu ndo watauelewa Naipenda sana FASIHI kwa sababu inakuachia room ya kufikiria vile ambavyo wewe unahitaji😁
🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Dizasta Murder Dis Bro Hii Ni Shule Sio Burudani ✊
🙏🏼🙏🏼🙏🏼
We jamaa unatisha Kama nini/kwenye story unawaacha unawaacha wengi wamesimama ka Sanam bismini/💪💪
The king of story teller
Thank you
De real dizasta unajuaa brother chakulaa bora cha ubongo kimebeba shibee zotee bigthinker dizastaa
BEST STORYTELLER OF ALL TIME 🙌🙌🙌
Thank you
Kioo cha Jamii unafaa kuigwa dizasta nouma sanaa💫💫
Meeen 🙌🙌🙌🙌🙌🙌
Lyrical scientist Himself Dizasta Vina, Keep it Bro Yo the Inspiration to us.
We are following up the foot steps.
Thank you 🙏🏼
Vina mwanzo kati na mwisho