MAAJABU!!! WAFARIKI ZIWA VIKTORIA WAKITOKEA KWA MGANGA, KAMANDA ASEMA BAADA YA MTUMBWI KUZAMA....

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 30 вер 2024
  • Watu wawili wamefariki dunia baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama ndani ya Ziwa Victoria katika Kijiji cha Burere wilayani Rorya mkoani Mara huku wengine wawili wakiokolewa.
    Tukio hilo limetokea juzi Jumapili Septemba 29, 2024 saa 11 jioni wakati watu hao wakiwa wanatoka Kijiji cha Busanga walikokuwa wamekwenda kutibiwa kwa mganga wa kienyeji wakiwa wanaelekea Kijiji cha Busimbiti wilayani Rorya.
    Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku 14 tangu kuzama kwa mtumbwi katika Kijiji cha Igundu wilayani Bunda na kusababisha vifo vya watu sita huku 14 wakiokolewa.
    Akizungumzia tukio hilo jana Jumatatu Septemba 30,2024 mjini Musoma , Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Agostino Magere amesema baada ya mtumbwi huo kuzama watu wawili waliokolewa wakiwa hai muda mfupi baada ya tukio hilo, huku miili ya watu wawili ikiopolewa jana.
    Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi
    (IMEANDALIWA NA ELIZABETH JOACHIM )

КОМЕНТАРІ • 2