WAZIRI AWESO ACHARUKA "NI MARUFUKU kumkatia Maji MWANANCHI siku za WIKIENDI"

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 8 вер 2024
  • WAZIRI AWESO ACHARUKA "NI MARUFUKU kumkatia Maji MWANANCHI siku za WIKIENDI"
    Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso ameshuhudia Wizara ya Maji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Gairo Mjini ikisaini mkataba na Mkandarasi FABEC Investment Ltd utekelezaji wa Mradi wa Majisafi kutoka Mto Chagongwe hadi Gairo Mjini kwa gharama ya Shilingi Bilioni 21,140,615,426.00.
    Unatarajia kuhudumia wananchi wapatao 156,000 wa Kata 11 za Chagongwe, Rubeho, Msingisi, Gairo, Magoweko, Ukwamani, Mkalama, Chigela, Kibedya, Chakwale na Madege.
    Akizungumza na wananchi waliojitokeza kwa wingi Mhe. Jumaa Aweso ameongea na wasoma mita kuacha mara moja kuwakatia maji wananchi siku ya sikukuu ama jumamosi na jumapili kwakuwa ni haki yao lakini pia amesisitiza wananchi waombapo kuunganishiwa maji kutokuzidisha siku saba wawe wameshaunganishiwa maji kwa kuwa sio ombi bali ni haki yake kama mwananchi

КОМЕНТАРІ •