Fahamu kuhusu Teknolojia ya kupanda Mbegu na kuweka Mbolea shambani

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 10 лют 2025
  • Na: Tatyana Celestine, Dar es Salaam
    Wakulima wameaswa kujitahidi kutumia zana za Kilimo ambazo zitawarahisishia kuongeza tija na matumizi madogo ya nguvu wakati wa kupanda mbegu pia kupalilia shambani.
    Hayo yamesemwa na Afisa Kilimo Yassin Msuya katika Kijiji cha Mikindani wilayani Kisarawe alipokuwa akiwaelekeza wakulima namna Bora ya Uchaguzi na Matumizi sahihi ya zana za Kilimo ili waweze kuzingatia na kuacha kulalamika kuwa Kilimo hakina tija nchini.
    Afisa Kilimo huyo amesema kuwa katika kipindi hiki cha Sayansi na Teknolojia wakulima nao wanatakiwa kutoka katika Kilimo cha mazoea kwani kinawazuia kufikia malengo yao kwakuwa hakizingatii taratibu Bora za upandaji, uandaaji shamba, muda na hakina tabia ya Kiuchumi.
    Amesifia kampuni za Tanzania ambazo zina zalisha, kuagiza na kusambaza zana zote za Kilimo, madawa, na kutoa ushauri kwa wakulima ikiwemo Farmbase Limited ambayo ina matawi kote nchini Tanzania lakini pia vifaa vyake vinapatikana katika maduka yote ya pembejeo na kumpa unafuu mkulima.
    Amesema Kampuni hiyo kwasasa imeleta Teknolojia ya kupandia mbegu yenye uwezo wa kupanda na kuweka Mbolea Kwa wakati mmoja pia ni rahisi kwa mkulima wa jinsi yeyote kuweza kuitumia.
    Bidhaa nyingine ni mashine ya kufanya palizi inayotumia petrol kidogo na kupalilia katika eneo kubwa kwa muda mfupi ambayo imelenga kumrahisia mkulima kutopoteza muda shambani bali kufanya kazi yake kwa uhakika na ubora maradufu.
    Aidha amewakumbusha wakulima wote kuendelea kufuatia na kujifunza mara zote zinapotokea fursa kama Semina, Shamba darasa na pia kuwatumia ma bwana shamba katika maeneo yao ili kusaidia Kilimo kiendelee kunifaisha kila mkulima nchini.

КОМЕНТАРІ • 13