Salama Na SAMATTA SE6 EP49 | HEADMASTER PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460
Вставка
- Опубліковано 9 лют 2025
- #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Kila kijana wa ki Tanzania ambae anaupenda na kuuthamini mpira wa miguu na ambaye angependa ndo iwe kazi ya maisha yake basi Mbwana Ally Samatta ndiye role model wake, hakuna doubt kwamba watakua na mapenzi na Cristiano Ronaldo au Leo Messi au Kylian Mbappe au Marcus Rashford ila yule ambaye amewaaminisha kwamba INAWEZEKANA ukacheza POPOTE hapa duniani na hasa kwenye ligi yetu pendwa ya Uingereza ni Samatta. Rafiki tu kutoka Mbagala rangi tatu ambaye kashacheza saaana ndondo na makombe ya mbuzi wakati anakua na mwisho wa siku akaenda kucheza kwa wazungu na bado anaendelea kutafuta rizki yake huko, hata kama sio ligi ile ambayo hata yeye mwenyewe angependa awepo ila BADO ni MWAMBA wetu. Samatta huyu huyu ndo ambaye alijitwika mpira kichwani na kuitika nyavuni mbele ya beki ambae anaaminika kuwa BORA kwa misimu hii miwili mitatu ndani ya Virgil van Dijk. Hata wakati naandika hii bado mwili unanisisimka kwa wazo tu kwamba nililishuhudia lile, pata picha kwa mtoto ambaye ana ndoto hizo. Lile goli lilimfanyia NINI kwenye ndoto zake. KRC Genk walipoteza mchezo ule wa ugenini wa kombe la mabingwa wa Ulaya kwa magoli 2-1 ila kwenye mitaa yote ya mikoa ya Tanzania ile mechi ilikua ya USHINDI.
Mbwana ametokea kwenye familia ya kawaida sana sana, wazazi wake wote kama kumbukumbu yangu itakua 100 basi walikua polisi, najua kwa hakika Baba yake alikua Polisi kwa asilimia 100. Kwa marehemu Bi Mkubwa wake ndo sina hakika sana ila kwa hakika jibu limo kwenye haya maongezi yetu. Anakumbuka jinsi ambavyo Mzee wake alikua anasisitiza kwenye suala la elimu na heshima, kama mtoto wa mwisho kwenye familia hiyo, Mbwana aliupenda sana mpira, zile za kujiiba na kwenda kucheza mechi za mbali alishafanya sana na matunda ndo haya ya leo. Nadhani ilifika kipindi Mzee mwenyewe aliona basi sawa, twende huko utakako. Familia yao yote ni wapenzi wa mpira na Kaka yake Mouhamed bado anacheza hapa hapa Tanzania. Sasa akiwa kama kioo kikubwa sana kwenye jamii hii Samatta anazungumzia presha ambayo hupewa hasa pale anapoitwa kwenye timu ya Taifa, jinsi maneno mengi ya kashfa yanaporushwa kwake kutoka kwa wananchi na anakumbuka pia wakati bado anacheza T.P Mazembe kuna kipindi kocha aliacha kumuita yeye na Rafiki yake Thomas Ulimwenguna ilisemekana kama pengine hakuna na interest na team au hakua anatoa 100. Pengine kipindi hicho aliumia zaidi maana hiyo haikua jambo zuri kwake.
Mbwana anazungumza na mimi kuhusu urafiki wake na Ulimwengu na maisha ambayo walikua wanaishi pamoja wakati wako DRC, anakumbuka jinsi walivyokua wanapanga kufanikiwa pamoja na mipango yao endelevu kwenye career yao. Ulimwengu nae ana siku yake kwenye kiti chetu In Shaa Allah maana nae ana mengi ya kutuelezea. Majeraha ya mara kwa mara bila ya shaka yalisababisha kwa kiasi kikubwa ndoto zake za kucheza Ulaya kutochukua hatua ya juu kama ambavyo angependa, ila mimi naamini hayo yote maisha tu, kila kitu kilikua tayari kimesha andikwa.
Samatta ni Baba ambaye watoto wake wanasoma hapa hapa nyumbani, nilimuuliza kama watoto wake wanajua yeye ni nani na akanipa story ndogo ya yeye kung’amua kama wanafahamu fika Baba yao ni nani.
Mwenzangu humu kuna mengi sana ambayo yatakufaa na kwa nafasi ya kipekee ningependa kumshukuru Captain wa Taifa kwa kuchukua time kwenye ratiba yake ambayo ilikua imebana kweli kweli ili tu aje kutubarikia meza yetu kwa uwepo wake.
Yangu matumaini uta enjoy sana.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahs...
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm
ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru
GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
Audiomack Link bit.ly/YahSton...
UA-cam Link bit.ly/UA-camS...
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz
Santa very humble and peaceful guy naona ananyayo kama za Ali hana mbwembwe and that's why he's unique ❤hii sampuli ndio kio cha jamii
The first ever sensible young Tanzanian born and raised in Tanzania. Proud of who you have become.
Labda wewe kingereza hakipo kabisa! 98% kaongea kiswahili..
Baada ile ya Jakaya....Hii tena umefanya kubwa Salama🙌⚽️💪
Big up kwa Salama kuweza kutuletea Samatta. Anaongea mambo mengi mazuri ya mfano kwa vijana wetu kwa soka letu.
Ila suala la maadili sikubaliani naye aliposema ni yeye mwenyewe. Bila shaka maadili yake mazuri yamejengwa ktk familia yao (baba na mama) na hususan kwakuwa ni familia ya kipolisi, timu alizopitia hapa bongo na tamaduni zetu za kitanzania. Sisi watanzania tupo vizuri kimaadili kuliko baadhi ya watu wa mataifa mengi.
Kila la heri kwake na Salama.
Mungu amempa uwezo ila hapendi show off anaishi kama Ali kiba good bless you
You are ths two people wamebarikiwa but wako humble na down to earth
Nature ya kazi yake pia
Ukiwa msanii makelele hayakwepeki
Sasa Alikiba ametokea wapi. Acha makasiliko 😀
Hes very humble like Ali Kiba...much love from🇶🇦🇶🇦
Yeah
Much appreciation for your popa🔥🔥🔥
Huyu mwanamme mbona best baba! Ni kioo cha jamii..... Vijana wajifunze kupitia tabia yake.... Ahsante Salama kumtafuta...
Kama bado unamkubali huyu jamaa gonga like twenzetu
Salama Hongera Sana. Nafatilia Sana Vipindi Vyako. Navipenda. 👍
Ulivofanya interview na Idris, nilitamani ufanye na Samatta as well. Nilivyoona hii leo, ilinikosha sana kwani Samatta ni nguli na role model to a lot of us young footballers. I am currently playing my football in The Thailand 3rd division and I dream one day not only to replicate the legend’s work but also I dream of being part of this show. Thank you Salama and Samatta for this wonderful interview
Keep it up Hanssen Benson.......your name sound Danish.......
@Hanssen God bless you ❤️🙏❤️
SAMATA NA KING KIBA
ALLAH BLESS YOU OTHER CELEBRITIES THEY HAVE TO COPE FROM YOU
Kama umegundua lafudhi ya samatta ishabadilika automatically kuwa ya kiingereza gonga like hapa😝
Wewe acha zako babu, Asa si lazima hiyo hata wwe ukitoka kwenu huko dongo kusimamia ukija mjini lazima kiswahili chako kibadilike, so sielewi unataka kumaanisha nn
The best interview
Hey kenyans give likes for it
Samanta MUNGU akubariki sana una busara sana
Nimechelewa sn kumjua samatta❤
Fantastic interview big up sister Salama 2023
This Guy is very humble and smart, he knows how to communicate
Exactly… he is truly a professional footballer, may Almighty Allah bless him abundantly 🙏🏿
Mbwana unayo hekima na busara sana.safi sana.
Nina mwanangu anakupenda na anacheza mpila hatari Huwa anajiita samata, sapoti wanetu vijijin kaka nao watimize ndoto zao Allah akufanyie wepesi uzidi kung'ara
Your the best not just of luck but you deserve it keep up samatta
kama baadhi ya majibu yanatakiwa Sana ili kutimiza mahojiano ni sawa ila kama sivyo, naomba salama punguza kujenga MASWALI yanayo mlazimu mtu ajibu katika mtazamo fulani.....awe huru tusitarajie atajibu nini I LOVE YOU SALAMA
I keep saying salama you got best questions for your guests.....you keep asking my questions every time i get time to see your sessions.....be blessed girl
Samatta anasound humble sana🔥🔥🔥
Aiseh! Jamaa Mbona Haongei Kingereza Kama Mimi Wakati Mimi Nimekaa Week Tu Nime Sahau Kiswahili 😁😁
🤣🤣🤣🤣 mie nimesoma tu English medium primary Ila mpka Sasa ninachanganya ngeli Kama nimeish mambele
Capten Diego
Uyu yomuli Dar Es Salaam Tz 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
Best player ever ♥️🇹🇿
Mimi mkenya Ila Huyu Jamaa namkubali🙌🏾⚽♥️⚽
Hakun ulazim wa kusema ww n mkenya
Mwamba huyu ni hatari sana
Nilisubili Sanaa asante sanaa
Noma sana
mbagala boy
Hyo ni nature ya intruvant peoples Huwa wanakuwa na rafiki wachche lkn wanapendwa na wengi na Huwa wanajifanyia maamuzi wenyewe na pia wapo focused na hutoboaa sanaaa.
leo salama na samata
Kauli nyepesi ni kwamba Mungu alimpa neema ya unyenyelevu huyu dogo
Mbwana you are what your father and mother groomed you to be what you are. Be appreciative of your parents
True
Was looking for this. Kajikuza mwenyewe? Heshima kwa wazazi
Mwamba kabsa
He's well programmed aisee
Waaaaoooh Asante kwa hii Salama
Nakkubali sana
Woyoooo mbwana samatta😜😜😜
Dah Salama kwa kumleta salama umenitouch saaaana yan. Hebu pokea 10k la soda hapooo.
Waoooooo fantastic mr Samatta
Tz oneeee🔥🔥🔥🔥
Huyu ni mimi kabisa hua naamua mwenyewe mambo yangu.
Usifanye hivyo mara zote jtahd baadhi ya mambo kuomba ushaur
Samagoal Mbagala Boy
Bless captain Diego
Salama jabir Ur on 🔥🔥
Kipendacho moyo dawa
Aliifunga Liverpool 😁😁
🔥🔥🔥🔥
Sam ✊🔨 keep it up bro unjua
Huna Baya bro
Naskia sauti ya ommy dimpoz zinafanana
Samatta mkali sana namkubali
Humble man...
Salama tunaomba ufanye interview na nadir haruob canavaro
MWAKINYO ANGEPATA NIDHAMU NA HESHIMA KAMA YA NDUGU NYETU SAMATTA ANGEFIKA ZAIDI YA ALIPO LEO.
Mbona na mwakinyo yupo fresh tu!
@@tztanzania2262 dharau nyingi
Mwakinyo mtu poa saaana kama utam chukulia poa ila kama ukiwa mduanzi utam hulia mbona ila ni mshikaji saaana tena zaid ya saaana
Legend Bro
Sama goal Sama Sama goal....
Samatta Goal 🇹🇿🇹🇿🇹🇿
Home boi
Sama goal Sama goal. You de best bro
Champion Boy 🇹🇿
Popa
SAMATTA 🔥🔥🔥 gonga like kwa mwamba
WA kwanza leoooooo
Champs Boy
Wanasema pesa ni sabuni ya roho
Mlete mandonga salama
😁🤣🤣🤣🤣😁😁😁😁 hatavuruga interview aiseee!!!🤣🤣
#SalamaNaDrLeaky
Laana ya wazazi ndio hiyo mitihani.
Samagoal #hainakufel
Kaka yangu
Tuletee na pastor Tony kapola,
SAMATTA anatabia kama zangu😁😁
Yan pia salama leo ujui umulize nn..
Kizaz san
Nafurahia wewe kujenga msikiti
Apo salama umenichanganya kabla amjaaanza nyuma muanze mbele mimi cjakuelewa kabisa
😂😂😂😂
Salama mbona watukatisha?
Kwan jaman ilo neno shock mbona watu ulitumia vibaya
SEMA hata wazungu hutumia Hilo neno mara nyingi Sana so Wala sio ajabu SEMA labda kwakuwa umeona wabongo pekee😅
Linatakiwa litumikaje?
Wewe ndo hulielewi
Wape points zao wazazi maana wao ndio source ya tabia yako
Masikito kua cjasikia hili kutoka kwake
@@mashamassingisa8738 eti ni yeye tu amejikuta yupo ivo yani kama vile alijikuza mwenyewe, naona kama vile kwa mbali ana katabia cha kujimwambafai flani hivi
Masikitiko makubwa kk
angevuta bangi na kuwa teja mngewapa point wazaz wake? Acheni kushinikiza ujinga
@izzi haya kk uko vyema sana
Apo mnatuchanganya Birmingham ipi sasa ya gwajima au?
birmingham ni mjini ndani ndio kuna club ya aston villa
Nakojoa. ..... Kwa kucheka
Tatzo utembei nawala ulizi pia mitandao uoni
Hahahahahahahahahahahahahahaha
ωχχ ο σαματαςς χαχα
ua-cam.com/video/bOC1NRBzhQA/v-deo.html
Ujumbe wa wafanyakazi Kwa Mama samia
Bro umetupa funzo kubwa cc vijana, wewe nd mchezaji usie kuwa na wajivuno na nadir haruob Kwa maono yangu
Kwani wewe Salam,Nani huaga anakushauri kuwakandia vijana wenye talent za mziki?
mbona sama goal anajifanya kama hajui kiswahil vzr, yan kama ameish eurupe since he was childhood
Kizungu gan kazumgumza apo izo actualy nyingi..
Sasa he was childhood ndo nini ..!? , Jifunze grammar mbwa wewe
@@bryanlimbi326 ilikua na ulazima wa kumtukana????
@@Nimebarikiwa wivuuu tu unawasumbua
@@bryanlimbi326 na aanze kubweka saivi
@samagoal77 #diego
Noma sana