SOMO:TAFSIRI YA KUOTA UNAFANYA MTIHANI NA NAMNA YA KUOMBEA (Johanitha Jeremiah)
Вставка
- Опубліковано 7 лют 2025
- ✓Lengo la mtihani huwa ni kupima uwelewa WA mtu
✓Kumvusha kumtoa hatua Moja kumpeleka hatua nyingine
✓Kumtoa hatua ya chini kumpeleka hatua ya juu
Na aina za mitihani unazofanya huwa zimegawanyika Kwa makundi mawili
a)kundi la kwanza ni kundi ambalo Ni mitihani inayopima welewa ili ikuvushe hatua Moja kwenda nyingine
Mfano mtihani WA darasa la Saba unamvuaha mwanafunzi kumpeleka kidato Cha kwanza
b) Mitihani mingine ni ili kupima maarifa ,katika usaili ili uweze kupata nafasi Fulani/kazi Fulani...
Ndio maana mtu anaweza kuwa amesona vizuri na ana VYETI lakini asiwe na maarifa ,Wala nguvu ya kutosha kuhusu hiyo kazi anayoomba .....ukifika muda huo WA kumpima ikaonekana Hana maarifa ya kutosha mbali na kuwa na VYETI huyu mtu hawezi kuipata ile nafasi aliyoomba ,itabidi arudi darasani ajifunze zaidi au akajifunze Kwa wengine /njia nyingine ili aongeze ujuzi
Daniel 1:3-
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³ Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana;
⁴ vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe
TAFSIRI YA NDOTO ZA MTIHANI
3)Ukiota hukai darasani wakati wengine wako darasani; au hukai kwenye mtihani wakati wengine wanafanya mitihani - ina maana huna utulivu unaotakiwa uwe nao ili uweze kujiandaa vyema kwa hatua iliyo mbele yako
2)Ukiota unafanya mtihani - ujue: au unapita mahali kimaisha ambapo unapimwa kiwango chako ulichofikia kimaandalizi; au mbele yako kuna kuja kipimo kwa ajili ya kujua ikiwa umefikia kiwango kinachotakiwa kwa wewe kuingizwa hatua nyingine ya maisha
1) Ukiota unaota unasoma, na ukaona na somo unalosoma, au ukaota unafanya mtihani na ukaona somo la mtihani huo - ina maana unaonyeshwa aina ya, au eneo la - maandalizi unalotakiwa kulifuatilia kimaandalizi
UNAPOOTA NDOTO YA MTIHANI ZINGATIA MAMBO HAYA ILI UWEZE KUTAFSIRI HIYO NDOTO.
1)Ulikuwa unafanya mtihani WA ninini,
Sasa hapa unaweza kutambua hili ijapo sio mara zote kuwa mtihani utakaokumbuka kuwa ndio huo kabisa Kumbuka hata kwenye maisha Kuna mitihani pia....Wakati mwingine unajulishwa juu ya jambo ambalo litakuja kama jaribu kukupima nguvu yako
2)Ulikuwa na Hali Gani Wakati WA mtihani ,Je ulikuwa unauelewa au ulikuwa haielewi mambo.
-Hali unayokuwa unaona kwenye ndoto ndiyo Hali ya mtu wako WA ndani
Ukiona ulikuwa mwenye kujiamini,umejiandaa ,huogopi basi jua ndani Yako una nguvu kuelekea mtihani huo na hata kama ni jaribu Bado utashinda
Lakini ukijiona kwenye mtihani ni mwenye mashaka ,mara unasahau daftari,mara umechelewa kwenye mtihani ujue wewe hauna MAANDALIZI ya kutosha katika jambo unaloliendea
3)Ulikuwa wapi Wakati unafanya mtihani,
-Mazingira unayokuwepo yatakusaidia kujua kuwa aina Yako ya mtihani ni ipi ??? Mfano unaona upo kanisani unaletwa mtihani...? Au upo nyumbani kwenu ulikozaliwa unaletwa mtihani..hii inaonyesha kuwa wewe mtihani unayotakiwa kufanya umeahikamana na masuala ya utumishi,au ya kifamilia pengine wewe ndiwe lango la familia na Kuna mambo unatakiwa kufanya na haujafanya Bado.nk
4)Mwisho wake ilikuwaje matokeo yake yalikuwaje ??
-Ukiona kuwa ulikuwa unafanya mtihani na mwisho wake umeweza ,umefauru,umeujibunvizuri bila shida ,au ulkuwa na shida lakini mwisho ukaujibu vizuri uwe na uhakika kwamba eneo ambalo unapimwa kiwango basi kiwango chako kinajitosheleza umefauru,kama ni utumishi ,wito ,nk basi ni ishara nzuri
-Ukiona mwisho umefeli,umepata vikwazo ,daftari mara limepotea ,mara unaingia kwenye mtihani unasahau...Basi ni dhahiri Mungu anakweleza katika jambo Hilo unalotakiwa kuliendea Bado hauna unuzi WA kutosha Bado haujasimama imara,Bado unahitaji maarifa zaidi ,Bado Kuna upinzani unatakiwa ushughulike nao ili uweze kufaulu.
MAANA NYINGINE
✓UKIOTA UNAFELI MTIHANI NA MAJIBU yake ulikuwa unayajua ila umechelewa
Ujue kabisa eneo lililokuwamisha ni Muda ,Adui ameshikilia majira Yako,MUDA ..Omba maombi kwaajili ya kukomboa Wakati
Majira /nyakati ni kati ya SIRAHA Ambazo shetani amezitumia kukwamisha maisha ya Watu,na kuyashikilia
✓UKIOTA UMRINGIA KWENYE MTIHANI NA BADO ULIKUWA UNAFANYA ILA MUDA WA KUKUSANYA..UMEFIKA
Ujue maarifa unayo ila imefungwa katika majira laizma ushughulike kukomboa majira ili uweze kufanya sawa sawa na kile unachotakiwa.
(Mhubiri 3:1)
✓UKIOTA UKO KWENYE MTIHANI NA HUNA UTULIVU UNAANGALIZIA ..
Ujue kuwa unachotaka kufanya hutaki kufanya ulichopewa wewe kilicho kwenye Kusudi la Mungu Bali unapiga ,hivyo basi unatakiwa ujitathmini ujue ni eneo lipi ambalo unaiga na sio ulichopewa wewe ..na Baada ya hapo umuombe Mungu MAARIFA YA KUSIMAMA NA KILE CHA KWAKO.
✓UKIOTA UKO UNAFANYA MTIHANI WA KIWANGO AMBACHO UMEVUKA TAYARI MFANO MTIHANI WA DARASA LA SABA WAKATI UKO CHUO.
Ujue hatua ,kiwango ulichonachobsasa sicho unachotakiwa kuwa nacho,Kwa kawaida unatakiwa uwe chuo ila rohoni Bado upo nyuma sawa na darasa uliloona
karibu jiunge darasani
0746003974
Asantee madam najifunza🙏🙏