YALIYOFANYWA NA TBA KATIKA IKULU YA CHAMWINO - DODOMA

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 27 сер 2024
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi jengo la Ofisi ya Rais, Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma ambayo imefanyiwa ubunifu na ujenzi wake kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
    Akizungumza katika Hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu hiyo, Dkt. Samia amesema, utekelezaji wa mradi huo ni matokeo ya dhamira kuu ya Serikali ya kuhamia Dodoma.
    Rais Dkt. Samia amebainisha kuwa uamuzi wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi ulifikiwa katika Mkutano Mkuu wa 16 wa TANU uliofanyika mwaka 1973 ambapo utekelezaji wake ulianza kufanyika kwa hatua na mwaka 2016 ulianza mpango wa uendelezaji na upanuzi wa Ikulu ya Chamwino kwa kuongeza eneo kutoka ekari 66 hadi 8473.
    Aidha, Mhe. Dkt. Samia amepongezaWakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa Ubunifu na Usimamizi mzuri wa ujenzi wa jengo hilo mpaka kukamilika.
    "Nawapongeza Wakala wa Majengo TBA, kwa ubunifu na usimamizi mzuri wa ujenzi huu" amesisitiza Rais Samia.
    Kwa upande wake Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kutenga eneo la ujenzi wa Ofisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) hapa Dodoma pamoja na kutoa ofisi kwa ajili ya Rais wa Zanzibar ndani ya Ikulu mpya ya Chamwino.
    Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi,Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daudi Kondoro amesema, usanifu wa jengo la Ikulu ya Chamwino unatokana na jengo la Ikulu ya Magogoni lililopo mkoani Dar es Salaam.

КОМЕНТАРІ • 1

  • @sdtz344
    @sdtz344 Рік тому

    Mnajitahidi ila muongeze matawi na bei ziwe ndogo kiasi cha kuwafikia watu wengii