MAUAJI YA KUTISHA DSM! MUME AMUUA MKEWE KWA KISU/PESA NDIYO CHANZO

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 6 чер 2022
  • MAUAJI YA KUTISHA DSM! MUME AMUUA MKEWE KWA KISU/PESA NDIYO CHANZO
    WATCH WASAFI TV📺
    AZAM - 411 | DSTV - 296 | ZUKU - 028 | STAR TIMES - 444 & 333 | COCONUT TV - 20 | DODOMA CABLE - 113
    LISTEN WASAFI FM 📻
    88.9 DAR/ZNZ/PWANI 📻 | 104.1 DODOMA 📻 | 94.5 ARUSHA 📻 | 97.3 MBEYA 📻 | 94.9 MWANZA 📻 | SHINYANGA 106.3 📻 | KIGOMA 101.7 📻
    Follow Us On:
    INSTAGRAM: / wasafitv || / wasafifm
    TWITTER: / wasafitv || / wasafifm
    FACEBOOK: / wasafitv
    𝑪𝒐𝒑𝒚𝒓𝒊𝒈𝒉𝒕 ©2021 𝑾𝒂𝒔𝒂𝒇𝒊 𝑴𝒆𝒅𝒊𝒂. 𝑨𝒍𝒍 𝒓𝒊𝒈𝒉𝒕𝒔 𝒓𝒆𝒔𝒆𝒓𝒗𝒆𝒅.
    #wasafi #wasafitv #wasafifm
  • Розваги

КОМЕНТАРІ • 288

  • @peteryukunda9239
    @peteryukunda9239 2 роки тому +7

    Mama ulokuwa unatetea hao watoto,Mungu akuweke sana,una busara,Embu Mungu akakupe kacheo cha utetezi.

  • @happynelson1136
    @happynelson1136 2 роки тому +7

    Yaani mume kaua mke kachukua pesa yake halafu ndugu wa mume wanawahi kuchukua vyombo halafu watoto wabakie bila kitu chochote yaani bongo ubinamu umekwisha yaani mtu kaua kwa laki sita tu na watoto wamebaki yatima nawaonea huruma hao watoto maana wataanza maisha mapya bila wazazi

  • @gililwise
    @gililwise 2 роки тому +12

    Mwenyekiti hongera sana.washindwe hao ndugu na walegee kwa jina la Yesu.mnakimbilia mali ni yenu?

  • @batashqiraa9936
    @batashqiraa9936 2 роки тому +9

    Huyo sio mwanaume ila khanithi barazuli mjinga mshenzi hajitambui yaani mwanamme mzima anamuua mke wake kwa pesa tena pesa katafuta mke!!!

  • @nadrahassan5241
    @nadrahassan5241 2 роки тому +10

    Mmmh jamani wanaume tuwaogope haki

  • @Mamatonny2065
    @Mamatonny2065 2 роки тому +7

    Poleni sana.
    Mheshimiwa waziri anayeshughulikia matatizo ya wanawake na jamii ,nakuomba utafute ufumbuzi wa tatizo la mauaji ya wanawake kila siku nchini Tanzania.

  • @hisanmwakijungu10
    @hisanmwakijungu10 2 роки тому +6

    Pole sana mdogo wangu baraka wazazi wasio jielewa ni tatizo kubwa

    • @sazanahussen6715
      @sazanahussen6715 2 роки тому

      Kbsaaa yanii wanaleta uchungu kwa watoto sijui itakuwaje jmn 💔

  • @janemhangomhango5841
    @janemhangomhango5841 2 роки тому +5

    Mwenyekiti Yuko sahihi kwanini wanawahi kuchukua mizigo

  • @jayjay4313
    @jayjay4313 2 роки тому +9

    Mngenyonga wachache wa mfano na watu wakaona, basi hayo manunda yangejifikiria kabla ya kuua binaadamu mwenzao.

  • @dianarobert3989
    @dianarobert3989 2 роки тому +21

    Hii hali inayo endlea kwa sasa siyo ya kawaida shetani amesha mwaga miroho michafu watu wanauana ovyo tuombe sana🙏

  • @faithjonathan3845
    @faithjonathan3845 2 роки тому +4

    Hujazikwa watu washakuja kubeba kila kitu chako😭😭

  • @omaryally1532
    @omaryally1532 2 роки тому +8

    Bunge linacha kuongelea mambo kama haya ya kikatili wanamaliza ya kupiga sarakasi bungeni na kuimba nyimbo ya mama amina

    • @clementiddi5708
      @clementiddi5708 2 роки тому +1

      Kweli. Ni uozo toka juu mpaka chini. Serikali hovyo sana hii

    • @annakadamanja2196
      @annakadamanja2196 2 роки тому

      😔😔😔😔

    • @khadijakdj8640
      @khadijakdj8640 2 роки тому

      Yaani naona Serekali ndo inasababisha haya matukio kwanini wasichukue uwamuzi wa nae uwa auwawe

  • @asnathmasegenya9890
    @asnathmasegenya9890 2 роки тому +1

    Asante mwk wa mtaa hao ndugu mazuzu sana bila kuwaza msiba wanawaza vitu wanataka hao watoto wataishije

  • @ruqaiamohammed345
    @ruqaiamohammed345 2 роки тому +9

    😭😭😭kila ck Joyce kiria anayasema jmn kwenye mahusiano ukiona unapigwa ujue hpo sipo kuna baadhi ya watu wanampiga hy sasa mauwaji kila kukicha mume kuuwa mke mke kuuwa mume 😭😭😭mungu atufanyie wepesi inshallah

  • @sambulugu9988
    @sambulugu9988 2 роки тому +4

    Mtakuja kuelewa tu kuwa nchi hii saizi iko chini ya shetani! Ila kwa vile hatuna macho ya kiroho tuendelee! Viongozi waliopo hawana baraka za Mungu!

  • @Mazoea
    @Mazoea 2 роки тому +4

    Unamtoa mtu roho kisa laki sita kweli jamani

  • @aminakunja277
    @aminakunja277 2 роки тому +13

    Dua zinaitajika kwa sana Tanzania yetu viongozi wa dini wakae wapitishe dua Maana hali inatisha

    • @birayan6823
      @birayan6823 2 роки тому

      ]

    • @ynyynyyny
      @ynyynyyny 2 роки тому

      DDC Mlimani park, mnanionyesha njia yakwetu

    • @rechokb1972
      @rechokb1972 2 роки тому

      Jmn mauwaji ni meng sana ckuhz

    • @gulfomanbb2119
      @gulfomanbb2119 2 роки тому

      Sana m mmoja naogopa ata kuolewa au kuwa na mausiano kwa ss ngj nisubili kdg

  • @rhobywerema6996
    @rhobywerema6996 2 роки тому +5

    Tumuombe sana mungu shetani yupo kazini

  • @neemamasimba2981
    @neemamasimba2981 2 роки тому +1

    Biiiiiig up mwenyekiti.hao ndg wana tamaa ya mali tu. Hata hawaoni uchungu na uhai wa mtu aliyepotea kikatili. Tena na wao mngewakamata wawekwe ndani. Nimeipenda sana mama aliyekuwa anawatetea watoto. Hii dunia kweli inahitaji maombi.

  • @Chapesatv
    @Chapesatv 2 роки тому +4

    Ambona tangu magufuli atangulie mauwaji mengi sana raisi na vyombo salama inabidi wawe makini sana nchi inachafuka msifurahie mabarabara na mijengo mkajuwa ndio maendeleo

  • @danielmanase7735
    @danielmanase7735 2 роки тому +17

    Maandiko Matakatifu yanasema siku za Mwisho mtu ataomba akutane na Simba lakini sio Binadamu, maana watakuwa wabaya zaidi kuliko wanyama. Ndicho tunachoshudia leo. Taifa liingie kwenye Toba, Mungu atuondolee laana hii inayoendelea. Mungu atusamehe.

  • @fatmaabdallah7709
    @fatmaabdallah7709 2 роки тому +3

    Hongera mwenyekiti kwa kuwasaidia hao watoto wapate haki Yao vikienda kwa hao ndugu wenye tamaa watoto hawatapata

  • @magrethmbangama1199
    @magrethmbangama1199 2 роки тому +4

    Jamn na cc wanawake hebu tujiongezage jaman yaan unapigwaa maalama,upo tuu ona Sasa unakufa unaacha watoto wako,Kama angejiongeza mapema mwanamke mwenzetu si ajabu yasingemkuta hayaa,ewe mwanamke ukiona jitu halisomeki sepaaa mapemaaaaa

  • @sumayafissoo2192
    @sumayafissoo2192 2 роки тому +2

    Inalillah wainnaillah rajion maskini watt watateseka baba atafungwa maisha mama yao hayupo Tena duniani

  • @thadeiandrea877
    @thadeiandrea877 Рік тому

    Ewe mwenyezi ilaze roho ya malehemu amina

  • @zawadihassan2324
    @zawadihassan2324 2 роки тому +3

    Hao ndugu wa mume waliokuwa wanaamisha vyombo nao wangekamatwa watoe ushirikiano itakuwa ndugu yao alipo wanapajua na ndio maana kuwatuma waamishe vyombo

  • @hanifatanzania7258
    @hanifatanzania7258 2 роки тому +4

    Inalillahi wainailahi rajuun poleni watoto Allah atawakuza lnshaallah 😭😭inauma lakini hakuna jinsi.

  • @nyamwinukankwera3749
    @nyamwinukankwera3749 2 роки тому +7

    Polenì sana 😭

  • @arafakiloli749
    @arafakiloli749 2 роки тому +14

    Innahlillah wainnah illah rajiun Allah amrehemu poleni sana ndugu na jamaa Allah awape subira katika kipindi hiki kigumu

  • @aishaamwalimu2887
    @aishaamwalimu2887 2 роки тому +12

    Pesa yake imemtoa uhai, Hilo janaume si lingeenda kuuza vidole vyake apate pesa, poleni watoto na ndugu za marehemu.

    • @salomewandya7257
      @salomewandya7257 2 роки тому

      😭😭😭😭

    • @hamisimohamedhamisi3241
      @hamisimohamedhamisi3241 2 роки тому

      Wez hao waupande wa mwanaume

    • @prosmacharius7074
      @prosmacharius7074 2 роки тому

      Wanaume jamani.yaan wake tutafte ela mzitake.tukae tu eti tunajza choo.sa tuwafanyeje nyie viumbe

    • @neemamaiko1342
      @neemamaiko1342 Рік тому

      Umeonaaa wenzie wanauzaa hata vodoree wapate pesaa Sasa yeye anamuua mkeee kisaa raki sitaaa mjinga kabisaaa huyoooo

  • @bujimuluhanga1804
    @bujimuluhanga1804 2 роки тому +6

    Ndugu wanafikria mali tu badala ya kufikria watoto ambao hawajui hatima yao Mungu wape nguvu ktk kipindi hichi kijana komaa na mdogo wako usiruhusu ndugu wamchukue kama una mashaka nao

    • @lucymwalisu5160
      @lucymwalisu5160 2 роки тому

      Poleni sana watoto wa marehemu Mungu akawakumbuke wanangu

    • @nguyatito8121
      @nguyatito8121 Рік тому

      Pole xana na mungu awaxaidie

  • @sebonikegobi6244
    @sebonikegobi6244 Рік тому +1

    Nimeumia sana 600000 inaoia roho ya mama ambaye watoto wake bado wanamuhitaji kwa malezi eee Mungu tusaidie sijui tunakwenda wapi

  • @kisalaTV
    @kisalaTV 2 роки тому +4

    Hawa ndugu wa mume hawana hata haya. Rohooo

  • @ashurayasini7085
    @ashurayasini7085 2 роки тому +4

    Wakinamama oyeeee ,,,,majirani oyeeeee

  • @jacklinejacklinejonh6530
    @jacklinejacklinejonh6530 2 роки тому +3

    Mama asante sana unaongea ukweli wengine wanaona mteremko

    • @heyumi2340
      @heyumi2340 2 роки тому

      ndugu wa mme wanataka vyombo 🙄🙄🙄🙄

  • @lucyjeremia1381
    @lucyjeremia1381 2 роки тому +1

    😭😭😭😭😭Ee Mungu tuonekanie taifa la Tanzania Baba

  • @halimarahma7450
    @halimarahma7450 2 роки тому +2

    Na hiyofamilia ni waroho wa Mali wanajuaje kama Mali za ndugu yao

  • @liciouscharles3370
    @liciouscharles3370 2 роки тому +3

    I still don't understand why women entertain their abusive relationships

  • @aminaabdalla9949
    @aminaabdalla9949 Рік тому

    Yaani nikiskia hizi habari zawanaume kuuwa wakezao hapa bongo nachoka kwanini mutudhulumu sisi wanawake ambao sisi pia ndio mamawawatotowenu 😭😭😭naumia kilakukicha lkn kaa ukijua mbiza sakafuni uishia ukingoni labda wende marekani lkn hapa bongo utapatikanatu tena wanafaa wapewe kifungo chakazi ngumu maisha jela maanakunyongwa itakuwa ajapitia maumivu mamamzazi wamke anapitia

  • @linamacha7686
    @linamacha7686 2 роки тому

    Jamani watoto wasaidiwe na ustawi wa jamii kwa sababu naona hali siyo nzuri ndugu mara hii wanataka vyombo hata uchungu kwa watoto hakuna hii ni hatar sana kwa kweli

  • @joycewanjiru4160
    @joycewanjiru4160 2 роки тому

    Mungu abariki hawa wamama ..hizo vitu singeenda hivo..Mungu uwalinde watoto wa marehemu🙏

  • @vanessalaizer4363
    @vanessalaizer4363 2 роки тому +5

    Duuh hawa wanaume imekuwa too much sasa!! Shuwain wahed

  • @mwanahamisi-yu6dv
    @mwanahamisi-yu6dv 2 місяці тому

    Inalilah waina Lilah la juun mungu amlaze Mahalia pena Pepon Amin

  • @halimachambuso9985
    @halimachambuso9985 Рік тому

    Mwenyekiti hngera sana

  • @salehrashidshekidele1039
    @salehrashidshekidele1039 2 роки тому +3

    Naliomba jeshi la polisi Tanzania liangalie hii hali iliopo Kwa ss mauaji ya mezid na piah Bunge liongelee haya mambo bungen sio mnaongelea kuhusu kosata tu

  • @vanessalaizer4363
    @vanessalaizer4363 2 роки тому +15

    Hao ndugu wa mume hawana hata haya lo!! Hawana uchungu kabisa na watoto utazani wanafurahia ndugu yao kutoa roho ya mama wa watu! Mijitu sijui ikoje sikuizi daah

  • @neemamaiko1342
    @neemamaiko1342 Рік тому

    Daaa poren sanaa watoto kuondokewa na mamaaa

  • @tunsumemwajumba7149
    @tunsumemwajumba7149 Рік тому

    Mwenyekiti yupo sawa

  • @zikenims6167
    @zikenims6167 2 роки тому +2

    Mmm hatar kila kikicha mauaji

  • @joyce55727
    @joyce55727 2 роки тому +1

    Kipind nimeolewa nilipingwa kofi moja nilitoka adi leo ni miaka 8 niliona nisije kuumia

  • @user-yj5zw8yi5i
    @user-yj5zw8yi5i 3 місяці тому

    Wanwake tunakutana na mengi sana na mbaya baazi ya jamiii azituamini wanaamini wanawake waongea sana awana eshima bila kujua mungu atusiaide wanawake sana jamani tunapitia mengi sana mungu wangu mungu atusaidie sana jamani uwiiii

  • @simbarajabu4157
    @simbarajabu4157 2 роки тому +2

    Mbona wanaume tunakuwa makatili namna hii , ehee mungu atuepushie haya maahsira sisi wanaume

  • @rajabumasanja5049
    @rajabumasanja5049 Рік тому

    Mwenyeki safi sana 👍

  • @salmaabdulabdul777
    @salmaabdulabdul777 2 роки тому +1

    Wanawake sisi wenyewe tunapenda kupigwa hivi unapigwa maharama kibao Bado upo tyu kisa umezaa inasikitisha kwakweli hata Kama unaofia kurudi kwenu kisa Kuna maisha magumu kwani huyo bwana si alikukuta umekuzwa kwenu manyanyaso yakizidi ondoka maisha yamebadilika mtu aofii kuuwa

  • @nadrahassan5241
    @nadrahassan5241 2 роки тому +4

    Nikweliii wasivipeleke nihaki ya watoto

    • @jovanafidelis2802
      @jovanafidelis2802 2 роки тому +1

      Watu Wana roho ngumu khaa,mtu hata hajazikwa wameanza kuhamisha vitu? Mmhh

  • @khayratmhina3735
    @khayratmhina3735 2 роки тому

    Mwenyekiti safi sana

  • @sarahkapange252
    @sarahkapange252 2 роки тому

    poleni sana yaani watoto wapelekwe upande wa mama yake marehemu

  • @saleemass9690
    @saleemass9690 2 роки тому

    Mwenyekiti uko vizuri ao wanataka kumficha ndugu yao

  • @zamzamhassan8643
    @zamzamhassan8643 2 роки тому

    Loooh
    Pesa zake zimemua😭😭😭mume Mario huyo atafutwe afungwe
    Mtoto nae anaonekana mkavuu sijui ndio hana uchungu

  • @irenewile
    @irenewile 2 роки тому

    Hiyo Familia ya Mme wanaroho mbaya Sana,,,yaani waue alafu wachukue vitu

  • @priscaphedrick5970
    @priscaphedrick5970 Рік тому

    Mwanamke mwenzangu ukiisha ona mmepishana kauli halafu tabia ya mumeo unaijua anza kuondoka

  • @zainabissa7986
    @zainabissa7986 2 роки тому

    Safi kabisa mwenyekiti

  • @paulinacherement2534
    @paulinacherement2534 2 роки тому

    Uko sahihi mama na wewe kaka uko sahihi viandikwe..my poleni sana wafiwa..innalillah wainna ilaih rajiun

  • @pendolazaro4686
    @pendolazaro4686 2 роки тому

    Eeh Mungu

  • @aishaomarry6996
    @aishaomarry6996 2 роки тому +1

    Pesa yenyewe laki 6 mtihani kwakweli

  • @mohamedfaris3000
    @mohamedfaris3000 2 роки тому +2

    Jeshi la Polisi Tanzania lilishatoa maelekezo kua ukiona sintofaham ktk mazingira yoyote yale toa taarifa Kituo chochote cha Polisi kilicho karibu yako ili kuepusha haya yanayotokea

  • @kimcash3079
    @kimcash3079 2 роки тому

    Inalilah. 😭mtangazaji sauti kma ya zamaradi mketema❤

  • @josephinenyakato8372
    @josephinenyakato8372 2 роки тому

    Ninaomba mawasiliyano ya hao
    Watoto ili niweze kutoa pole
    Nichangie kidogo Poleni sana
    Watoto

  • @angeljoakim6583
    @angeljoakim6583 Рік тому

    Mungu atusaidie sana laki sita inaua mtu!

  • @sabinaonline6575
    @sabinaonline6575 2 роки тому

    Sasa Kwanini hamjawapigia simu polisi

  • @rewardnjau7220
    @rewardnjau7220 2 роки тому +5

    wamama nimewaelewa sana, hakika mukiamua mnaweza, hawa jamaa wanaohamisha vitu waisaidie polisi kumpata mtuhumiwa

  • @helgahussein1413
    @helgahussein1413 2 роки тому +2

    Alikuwa anafanya kazi gani

  • @mentionedU
    @mentionedU 2 роки тому

    Watu wazima akili ndogo Kama ya mtoto 😓😢,watoto wameathirika vibaya sana ,wanahitaji watu kuwaliwaza,sio kuanza huo UPUZI WA kuhamisha vyombo🤔😓😢, Doo,wanadamu kweli hamna roho za huruma,WATANZANIA mlio mahali hapo pa mkasa,mmenishangaza SANA,kwa roho zisizo na huruma,kwa akili zisizofikiria, wallahi MWENYEZI MUNGU hajafurahishwa na mnayoyafanya,maamuzi yenu yamenisikitisha sana😢😢😢(WATCHING FROM KENYA)

  • @mamaahmad8615
    @mamaahmad8615 2 роки тому

    daaah😭😭😭😭poleni wanangu hili liuwaji lilishindwa kutafuta hela zake kwa jasho lake ona sasa umeuwa mkeo umekimbia utaishi maisha mabaya sana bora na ww ujinyonge mkono wa sheria utakupata tu mshenzi mkubwa unaroho ngumu ww muuwaji poleni

  • @halimarahma7450
    @halimarahma7450 2 роки тому +1

    Pesa utafute kwa jasho limtu lije lichukue kiurahs tu ukute mizigo wa kulea familia kakuachia

  • @zuenajohn8325
    @zuenajohn8325 2 роки тому

    Wanaume wanaume Mungu anawaona. Mtapata laana kwakutowa roho za watoto wawatu.

  • @zubedalema6634
    @zubedalema6634 2 роки тому +1

    Wakamatwe wamtaje ndugu yao alipo sio wanachukua vitu

  • @achouraachoura5763
    @achouraachoura5763 2 роки тому

    Kaka zangu mlio oa kwani mnaferi wapi kuua wake zenu bila huruma inaniumiza mno hasa nikifikilia awo watoto 😭😭

    • @hamzamahanyu5794
      @hamzamahanyu5794 2 роки тому

      Ndugu wa mume wanajua nini kuhusu mauaji hayo mbona wanawahiya vyombo vya marehemu? Waisaidie polisi kupatikana muuwaji ambae ni ndugu yao sivinginevo

  • @Mazoea
    @Mazoea 2 роки тому

    Daah Naona pesa kweli imekua ngumu sana

  • @michaelsamson9663
    @michaelsamson9663 2 роки тому +3

    Uundio ugaidi wa Tz tunako elekea nikubaya zaidi

  • @christsndushondi51
    @christsndushondi51 2 роки тому

    Joyce kiria kila siku anasema

  • @vanessadahnilly8551
    @vanessadahnilly8551 2 роки тому

    Sasa we muandishi unauliza swali gani lakiseng eti kwabini mnataka vitu viandikwe ?? 🙄

  • @cachec7930
    @cachec7930 2 роки тому

    Duuh😓

  • @selemanimasatu2421
    @selemanimasatu2421 2 роки тому

    Tatizo wanawake wakipeleka kesi kama hizi polisi unakuta hawasikilizwi kwa umakini na wengine hufukuzwa wakamalizane ndani kifamilia but inapotokea watu wameuana ndo wanakuja na mabunduki yao sasa.

  • @gbhxghxhhv7890
    @gbhxghxhhv7890 2 роки тому

    Yaani mwenzao Amekufa wao wanakimbilia kuchukua vitu hawana ata huruma dunia imekwisha

  • @farhannahomary5505
    @farhannahomary5505 2 роки тому

    Mmmmh jmn mbona wametoa vituu fasta jmn

  • @joachimompesh7387
    @joachimompesh7387 2 роки тому +1

    Hili jamaa ni senge si akauze vidole Zimbabwe.

  • @wardw3022
    @wardw3022 2 роки тому +3

    Duniani inaenda kasi sana duh pesa ni shetani kweli

    • @lucymwalisu5160
      @lucymwalisu5160 2 роки тому +1

      Mwenyekit hongera sana kwa msimamo uliouchukua baba yaan wangeondoka na vyombo watt wasingepata hata kijiko na ukizingatia asilimia kubwa vyombo hununuliwa na wanawake Mungu akurinde mwenyeti bigup sana kwako

    • @shillahsamwel7727
      @shillahsamwel7727 2 роки тому +1

      Mungu wasaidie watot o katika Uwezavyo Maana wewe NI Mungu wa Pekee

  • @najmaaa6548
    @najmaaa6548 2 роки тому

    Mbona watanzania mwauwana ivo astaghafiruuu hivi samia yuko wp jmani ama muute mashekhe mfanye baraza la kiislam 🤔🤔🤔

  • @rosemaryjanuary7146
    @rosemaryjanuary7146 2 роки тому

    Kweli nimetokwa na machozi maana mtu anadiriki kumuua mwenzie..

  • @hisanmwakijungu10
    @hisanmwakijungu10 2 роки тому

    Daaaah yaani kweli laki 6 unaua mtu duuuuu!!!....

  • @josephlorri431
    @josephlorri431 2 роки тому +2

    Wanaume tufanye kazi, tusipende kitonga.. wanaume wengi siku hz wanahudumiwa badala ya kuhudumia familia.

    • @gulfomanbb2119
      @gulfomanbb2119 2 роки тому

      Kumbe munalijua ilo ndio maana muna2uwa

    • @josephlorri431
      @josephlorri431 2 роки тому

      @@gulfomanbb2119 pesa na mali zote za mwanaume...piga kazi,lete hesabu yote mezani, matumizi napanga mimi,pamoja na kuhudumia mchepuko

    • @gulfomanbb2119
      @gulfomanbb2119 2 роки тому

      @@josephlorri431 subu2

    • @josephlorri431
      @josephlorri431 2 роки тому

      @@gulfomanbb2119 hahaa huogopi gunia la moto

  • @peterjames4669
    @peterjames4669 2 роки тому

    Duh ninja imeisha poleni sana

  • @khubeybjandal7435
    @khubeybjandal7435 2 роки тому

    Watanganyika, hatar kwa pesa, sioi bongo noma laki sita ameua mkewe noma

  • @mamakidunda4511
    @mamakidunda4511 2 роки тому

    Jamani tuthamini uhai WA MTU

  • @joycenuhu1566
    @joycenuhu1566 2 роки тому

    Yani nashindwa cha kuongea, Mungu nisaidie nikae kimnya tuu mana dunia inatisha jamani

  • @omnsultan383
    @omnsultan383 2 роки тому +1

    Mwenyekiti apewe ulinzi

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 2 роки тому

    😢😢

  • @atukuzwelameck4869
    @atukuzwelameck4869 2 роки тому +1

    😅😅Tumechoka sasa

  • @daisythetech
    @daisythetech 2 роки тому

    Kama ilivyo kwenye kila nyumba kumi kuna mjumbe...bas serikali inabidi kwenye kila nyumba kumi vile vile serikali iweke watu wa saikologia waweze kuzungumza na watu wenye uhitaji ....watu wanaumemwa siyo malaria bali kiakili afya haziko vizur ... people wanahitaji matibabu ya afya ya akili