VURUGU MARA !!! KONDAKTA , ABIRIRIA 16 WAMPIGA ASKARI WAKAMATWA

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 19 вер 2024
  • Dereva, kondakta na abiria 16 wakamatwa Mara kwa kumpiga Askari
    Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu 18, wakiwemo dereva, kondakta na abiria 16, kwa tuhuma za kumpiga askari wa usalama barabarani aliyekuwa akikagua gari walilokuwa wamepanda. Tukio hilo lilitokea Septemba 18, 2024, saa 12 jioni katika mkoa wa Mara.
    Akizungumza kuhusu tukio hilo, Ofisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Trafiki Kuu, Butusyo Mwambelo, amesema kuwa askari huyo alikumbwa na kipigo wakati akijaribu kushusha abiria waliokuwa wamesimama kwenye gari. Hata hivyo, kondakta wa gari hilo alifunga mlango na wote waliokuwa ndani ya gari, akiwemo dereva, kondakta, na abiria, walianza kumshambulia askari huyo.
    “Askari wetu alikuwa akitekeleza wajibu wake wa kuwataka abiria waliokuwa wamesimama kwenye gari washuke. Lakini ghafla walimzonga kwa maneno ya kebehi, na kondakta kufunga mlango wa gari. Ndipo dereva, kondakta na abiria wao wakaanza kumpiga askari akiwa ndani ya gari. Je, kweli tumefika hatua hiyo kama Watanzania?” alisema Mwambelo.
    Mwambelo alitoa maelezo hayo wakati wa operesheni ya ukaguzi wa magari iliyofanyika Septemba 19, 2024, katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Geita, ambapo alisisitiza kuwa tukio hilo ni la kusikitisha na halitavumiliwa. Jeshi la Polisi limechukua hatua za haraka kuhakikisha wote waliohusika katika tukio hilo wanawajibishwa kisheria.

КОМЕНТАРІ • 34

  • @Yassinseleman
    @Yassinseleman 7 годин тому +2

    Poleni askari wetu

  • @Hamy1109
    @Hamy1109 6 годин тому +3

    Mwenye magari anafungiwa magari yake kwa kosa lipi!? Acheni kunyanyasa wafanyabiashara😒

  • @ceciliaathanas3135
    @ceciliaathanas3135 6 годин тому +3

    Unatoa hukumu,wewe ni hakimu??!!kila mtu akae katika kitengo chake

  • @MBK92
    @MBK92 7 годин тому +2

    mbona km anatoa hukumu yeye

  • @CharlesMlaponi-h6z
    @CharlesMlaponi-h6z 6 годин тому +2

    Watu wanapaswa kufahamu "Watu wafikiri zaidi"

  • @FazilahFazilah2022
    @FazilahFazilah2022 7 годин тому +2

    Wananchi waache ushabiki kufuata mkumbo

  • @EliasMwita-q3x
    @EliasMwita-q3x 2 години тому

    Sasa unaingia MARA😅😅😅😅😅

  • @ramadhanishabani807
    @ramadhanishabani807 5 годин тому

    Asikari wapigwe tuu, kwanza kweny matukio hao ndio wezi,

  • @azariamarembo3653
    @azariamarembo3653 5 годин тому

    Hatari na nusu

  • @marcynhumbi3534
    @marcynhumbi3534 4 години тому

    Mmmmh ila watu wamevurugwa kabisa khaa

  • @gracemima5234
    @gracemima5234 6 годин тому

    Sasa wewe mama ndiyo hakimu na ndiyo asikali. Tayali umeshatowa hukumu. Unatakiwa kuwakamata na uwapeleke mahakamani na hakimu aamue. Asikali kaisha wa hukumu.. Hii ndiyo Tanzania yetu mob justice

  • @stevensoso7506
    @stevensoso7506 30 хвилин тому

    Kawa hakimu mwenyewe

  • @IssaTayari
    @IssaTayari 13 хвилин тому

    Kwan mwenyewe anasemaje

  • @johnmhina2351
    @johnmhina2351 4 години тому

    Nyie mbona mnauwa watu kila siku

  • @chrisedward3797
    @chrisedward3797 5 годин тому

    Mbna askari ndiyo watekaji ndiyo wauwaji wa raia

  • @aediayumgo8546
    @aediayumgo8546 7 годин тому +3

    Chadema watawaponza wengi watu wanashindwa kutumia akili😅

    • @MaryMwamwezi-xm3iz
      @MaryMwamwezi-xm3iz 7 годин тому +1

      Ni kweli chadema itawaponza watu.nao watu tutumie akili. .unaanzaje kumpiga askari kweliii. Haya gereza linawasubiri

    • @JoyceLuhasha
      @JoyceLuhasha 5 годин тому

      Kweli kabisa Alafu hao chadema wako zao nyumbani wametulia.

  • @denisipaulo7785
    @denisipaulo7785 7 годин тому

    Kwani asikali apigi raia

  • @dwasinjebele5361
    @dwasinjebele5361 2 години тому

    Na ss wananchi tuheshimu jeshi letu

  • @Afsa-z2v
    @Afsa-z2v 29 хвилин тому

    Mhuuuuu

  • @gililwise
    @gililwise 5 годин тому

    Piga hao watesaji na watekaji yaani siwataki hata kuwasikia hao wanaojiita walinda usalama natamani wafe wote na vizazi vyao maana wanawatesa watu wasio na hatia.ndio ombi langu kwa Mungu.

    • @marcynhumbi3534
      @marcynhumbi3534 4 години тому

      Mbona wew haujawahi kuwapiga kazi kuhamasisha wenzio tu

  • @selemankishema5780
    @selemankishema5780 7 годин тому

    Wananchi wanabeba slogani ya chadema wamekuwa hawana heshima na wanachukua sheria mikononi nyie mnachekanao

  • @user-yw3qh6qj8g
    @user-yw3qh6qj8g 5 годин тому

    ACHA USENGE WEWE NINANI UNASEMA WATAENDA MAGEREZA? PUMBAVU,WEWE SIOMAHAKAMA,PIA MNATEKA WATU ALAFU MNAKATAA NDIOMAANA RAIA HAWANAIMANI NANYIE

  • @denisipaulo7785
    @denisipaulo7785 7 годин тому

    Wewe ni akimu

    • @Hamy1109
      @Hamy1109 6 годин тому

      Ameshindwa kuzuia hisia zake huyu maza. Kiongozi unapaswa kuongea kwa kiasi na sio kwa hisia kama anavyofanya hapo mbele ya hadhara.

  • @ramadhanishabani807
    @ramadhanishabani807 5 годин тому

    Gereza lakwao wee ni hakim?

  • @YunisJerald
    @YunisJerald 4 години тому

    😂😂😂😂😂

  • @gerevasliyunga9831
    @gerevasliyunga9831 7 годин тому

    😂😂😂😂😂

  • @khadijahamisi5561
    @khadijahamisi5561 7 годин тому

    😂😂😂😂😂