Jaji Warioba anavyoitazama miaka 60, Muundo wa Muungano
Вставка
- Опубліковано 16 лис 2024
- Safari ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar imebakiza siku chache kufikisha miongo sita, ingawa muundo wake linabaki kuwa jambo linaloendelea kujadiliwa mara kwa mara.
Aprili 26, miaka 60 iliyopita ndipo mataifa hayo yalipoungana na kuunda Tanzania na hadi sasa zimesalia siku chache kwa Watanzania kuadhimisha miaka 60 ya Muungano.
Pamoja na ukongwe wa Muungano huo ulioasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume Rais wa kwanza wa Zanzibar, mijadala kuhusu muundo wake inabaki kuwa kitendawili kisichoteguka.
Mijadala hiyo kuhusu muundo huo wa Muungano imefikisha wananchi katika hatua ya kutaka ipewe uzito katika rasimu ya mabadiliko ya Katiba na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba analithibitisha hilo.
Jaji Warioba aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, anataja muundo wa Muungano kuwa moja kati ya mambo manne yaliyozungumzwa zaidi wakati wa ukusanyaji maoni ya rasimu ya Katiba mpya.
Soma zaidi kupitia www.mwananchi.co.tz
Jamani wee mzee sisi hatutaki huu muungano wenu kisanii tumechoka miaka 60 inatosha tena mjadala wa nini tena
Wee mzee sisi wazanzibar hatutaki huu muungano wenu wa kisanii mjadala wa nini tena miaka 60 inatosha sasa basi jamani
Hatutaki mungano wizii nyie na mwisho wenu umeshafika matapeli nyie
Huna sifa ya lugha fasaha na pia Huna sifa ya uzalendo ila ukimbizi.
Hivyo kimbilia ulaya au arabuni kama kawaiida