SABRA MACHANO (CHIPS CHAFU) AFUTIWA SHUTUMA, AREJESHWA KAZINI

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 22 жов 2024
  • TAKRIBANI miaka Mitatu baada ya kusimamishwa kazi kwa tuhuma za Ubadhirifu wa mali ya umma, aliekuwa Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi za Jamii Zanzibar Sabra Issa Machano hatimae amefutiwa tuhuma zinazomkabili pamoja na kutakiwa kurejea kazini.
    Sabra Issa Machano alishtumiwa na kusimamishwa kazi kwa kile kinachaodaiwa Ubadhirifu wa Mali za Umma katika utekelezaji wa baadhi ya Miradi mbalimbali ya Serikai pamoja na upotevu wa Fedha kiasi cha Shilingi Bilion Tatu.
    Akizungumza kwa Mara ya Kwanza leo na CLOUDS TV amesema kuwa, amefurahishwa baada ya kupokea taarifa za kukamilika kwa Uchunguzi na kutoonekana na shutma ambazo zilikuwa zinamkabili na kupelekea kusimamishwa kazi kwa takribani miaka Mitatu.
    Amesema kuwa, tayari amepokea barua kutoka taasisi mbalimbali za serikali ambazo zinaonyesha kutokuhusika na shutuma hizo za upotevu wa fedha za Bilioni tatu katika mradi wa ukarabati wa Jumba maarufu visiwnai Zanzibar linajulikana kwa jina la Jumba la Treni (Chawl Building) ambalo liligahrimu Bilioni kumi na tatu
    "Nimepokea Barua kutoka Ofisi ya Rais Ikulu ambayo inathibitisha kuwa sina Hatia kwa tuhuma ambazo zilikuwa zinanikabili hapo awali," amesema.
    "Nmefurahi na hapa nimpongeze Mhe Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa sasa Shutma ambazo zilikuwa zinanikabili zimefutwa na sina hatia," ameongeza.
    Sabra amesema kupitia sakata hilo amejifunza mambo mbalimbali lakini pia imekua sehemu ya fursa kwake baada ya kusimamisha kazi kwa kuanzisha Taasisi yake inayotetea na kusimamia masuala ya wanawake pamoja na kufungua biashara zake
    Akizungumzia kuhusu msimamo wake wa kurudi katika utumishi wa umma amesema licha ya barua hiyo kutoelekeza kituo cha kazi anachotakiwa kurudi lakini yeye atakua tayari kuendelea kutumikia serikali katika kazi yoyote atakayopangiwa na mamlaka za utumishi

КОМЕНТАРІ •