Mwanzo-Mwisho Profesa Issa Shivji Akieleza Dira ya Taifa ni Nini: Wasilisho Zito la Kifalsafa

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 7 чер 2024
  • Akizungumza leo Juni 08,2024, katika kongamano la kwanza la kitaifa la maandalizi ya dira ya taifa ya maendeleo lililofanyika katika ukumbi wa Nkurumah, Profesa Issa Shivji ameeleza kuwa dira ya taifa ni tofauti na mipango ya maendeleo yenye muda maalum.
    "Dira haina maana ya mpango wa maendeleo, mpango wa maendeleo unakuwa wa muda maalum. Kwa maoni yangu dira haina muda maalum," ameeleza Profesa Shivji.
    Profesa Shivji alifafanua Zaidi kuwa moja ya mfano wa dira ya taifa ni Azimio la Arusha. Akijibu hoja hii Waziri wa OR Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo alieleza kuwa wameyapokea maoni hayo.
    Katika wasilisho lake hilo Shivji ameasa juu ya taifa kuepuka kufanyiwa majaribio katika utengenezaji wa dira yake.
    "Tusikubali kufanyiwa majaribio, majaribio yaliyofanyika miaka ya 1960 yanatosha. Tuwashirikishe wananchi kikamilifu popote pale walipo tupate maoni yao kuhusu nchi wanayotaka, Tanzania wanayoitamani, matamanio yao yapewe kipaumbele.Hii haiwezekani bila kuwa na mjadala wa kitaifa," alieleza Profesa Shivji.
    Alifafanua Zaidi: "Tusifanye ile tuliyozoea wananchi wanatoa maoni, halafu wataalamu ndio wanachambua maoni haya. Popote pale walipo wananchi; vijijini, viwandani, mashuleni na kadhalika ili kujenga muafaka wa nchi tunayoitaka. Na mengine ya kupanga mpango wa muda mrefu wa muda mfupi itafuata."

КОМЕНТАРІ • 30

  • @richardmwandanji65
    @richardmwandanji65 29 днів тому +5

    Yes viongozi wanadanganya sana safisana Mzee ndio naamini hivyo dira ni baba wa ilani mwongozo au matarajio ya nchi hawa wanatupeleka nagali hawajui kitu mfano wadira ni tunatamani kufika 2050 mwalimu wa elimu msingi awedalaja la ufaulu waju alau chuo na form six saizi tuna feris na form for na diploma tunataka mishahara iongezwe wasomi watamani KWENDA kufundisha elim msingi

  • @user-ut4vt1kn7w
    @user-ut4vt1kn7w 26 днів тому +1

    Mungu Akuepushie Madhara Ya Asadi Profesa Issa Sivuji

  • @ceciliamagalabajimmy4391
    @ceciliamagalabajimmy4391 27 днів тому +1

    ❤ Yaani Professor Shivj nilikufuatilia tangu mwanzo kabisa, unatoa elimu tulivu na ya kueleweka. Wewe ndiye uliyetufumbua macho na kuzibua masikio kuwa:
    Walala hai
    Walala heri na
    Walala hoi. Rasimu yenu ni yetu sisi kwa maoni yetu .
    Ingefaa uwe miongoni w
    Mwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba. Tupate katiba mpya kwa maslahi ya taifa.

  • @RichardOjendo
    @RichardOjendo 28 днів тому +2

    Prof Shivji I salute you

    • @selemapingon9286
      @selemapingon9286 28 днів тому

      Huyu ni zaidi ya Profesa. Sijui hata tumuitaje

  • @festokemibala5832
    @festokemibala5832 27 днів тому +1

    Mimi kwa maoni yangu napendekeza Dira yetu 2050 ilenge kuwa Nchi ya Uchumi wa Juu (Higher Income Country - HIC). Marengo yetu ya namna ya kufikia hiyo dira yaendelee kuwa yale yake ya Utawala bora na Utawala wa Sheria, na mengine yaliyomo ktk Dira tunayoikamilisha Juni 2025.

  • @selemapingon9286
    @selemapingon9286 28 днів тому +1

    Issa Shivji, una akili nyingi sana mtanzania mwenzetu

  • @florencejohn6427
    @florencejohn6427 28 днів тому +1

    Hata Jenerali Ulimwengu naye yuko vzr kwenye kufikisha ujumbe kiurahisi kwa mbwembwe na bashasha. Shivj anatakiwa kuwasilisha peke yake tu, na kama kwenye makongano yenye waongeaji wengi kama hili basi awe wa kwanza kuwasilisha. Ukimweka mwishoni huko watu watasinzia

  • @eliaskangabo779
    @eliaskangabo779 26 днів тому +1

    Kweli tuna hazina kubwa ya ushauri tuutumie

  • @drkalokola5861
    @drkalokola5861 27 днів тому +1

    Hana alijualo.
    Mzishi TU.

    • @festokemibala5832
      @festokemibala5832 27 днів тому

      Wewe ndiye hujui linalozungumzwa. Dira tunayoikamilisha sasa ni "Tanzania yenye Uchumi wa Kati (MIC). Masuala ya elimu, afya, utawala bora na utawala wa sheria nk hizo ni objectives za na namna ya kufikia hiyo dira. Tujielimishe ipasavyo

  • @festokemibala5832
    @festokemibala5832 27 днів тому

    Kitilya na waliomtuma hawataki Muafaka wa Kitaifa bali upande mmoja ndo utuelekeze nanamna ya kuenenda!!

  • @augustinemachumu6978
    @augustinemachumu6978 27 днів тому

    Nimemsikiliza vizuri sana Shivji lakini Dira ya nchi msingi wake ni Katiba. Katiba si kitabu tuu ni mwongozo kama ilivyo sylubus kwa shule. Katiba ya sasa haiwezi kutupa dira ya Tanzania inayokidhi serikali au nchi zote 2. Zanzibar na serikali ya muungano zina katiba tofauti sasa tutapataje dira ya pamoja . Bila katiba mpya huwezi kupata dira Tz ila tratará dira ya Tanganyika kisiri siri maana ndiyo imevaa koti la muungano. Katiba ya Tanganyika ni lazima irudi mezani ipange dira yake nje ya muungano. Then nchi hizi sasa zinaweza kukaa na kupanga kwa pamoja dira ya Tanzania ikiwa ni pamoja na dira muungano miaka 25 zijazo. Hata tukiweka maprofesa wa dira hawawezi maana Tanzania sio nchi moja as one unit. Ni muungano wa nchi 2 zenye muelekeo tofauti. Kwahio in total Tanzania sio nchi, nchi ni Tanganyika na Zanzibar katika muktadha wa maandalizi ya dira ya 2050

  • @borntochange5333
    @borntochange5333 26 днів тому

    Prof ni Mwalimu mkuu wa taifa. Muwe na adabu mwachani amalize paper yake sisi wajukuu zake tunasikiliza maana nyie wazazi hamkuitumia vizuri nafasi ya kumsikiliza

  • @festokemibala5832
    @festokemibala5832 27 днів тому

    Namuona chawa mmoja hapo yeye kachanganyikiwa

  • @drkalokola5861
    @drkalokola5861 27 днів тому

    Upuuzi mtupu.
    Sakatonge wanamdanganya Samia.
    Hivi Sasa hatuna furaha zaidi ya wakatii wa enzi ya Baba wa Taifa na Mwinyi.
    Mafisadi wamewaweka watanzania katika maisha ya huzuni na unafiki.
    Wapumbavu wameharibu kiwango cha elimu tuliyokuwa tunaipata. Hivi Sasa vijana wanaenda shule lakini hawaelimiki ipasabyo kwa manufaa ya Taifa.
    Mkumbo mwenyewe majanga.

  • @nestor384
    @nestor384 28 днів тому +2

    Mawazo mazuri changamoto yanapotolewa kwa nchi na viongozi wanaozunguka na kudalalia ardhi na maliasili ya nchi kwa Waarabu, Wachina na wakorea!😌

  • @ebenezernnko8251
    @ebenezernnko8251 27 днів тому

    Shivj ungetakiwa uwe Rais miaka10 Jaji Joseph sinde Oriyoba miaka10 lkn ndio hivyo sasa

  • @florencejohn6427
    @florencejohn6427 28 днів тому

    Mzee Shivj ana madini sana. Lkn madini haya watu wanaweza wasiyafaidi sana kwa sababu zifuatazo: Sanaa ya kuongea. Hana sanaa ya kuongea. Kuanzia kwenye lafudhi au fani ya kumfanya afikishe ujumbe kiulaini. Anaongea maudhui/mafundisho/madini tu. Hana ile ya kuweka asali au sukari kwenye mafundisho yake ili watu wawe attention kupata huo ujumbe wake. Watu wanaweza wakasinzia au kuhama kimawazo. Hadithi, mifano, cases, utani, tabasamu nk ni vitu muhimu sana kufikisha ujumbe.
    Mfano Tundu Lissu angepewa nafasi hii watu wangemsikiliza kwa makini bila kuchoka wala kusinzia kwa sababu anajua kufikisha ujumbe kwa lugha rahisi sana.
    Hata kwenye uandishi wa vitabu au magazeti waandishi huweka fani ili ujumbe ufike kwa hadhira kiurahi bila kuchosha.

    • @josephmkami
      @josephmkami 28 днів тому

      Kumbuka huyu ni Prof anaongea facts
      Hapo anaongea na wasomi. Unaweza kuongea kwa mifano na vichekesho kwa watu wa kawaida.
      Hivyo Prof yupo sahihi. Mwenye upeo unamwelewa.

    • @drkalokola5861
      @drkalokola5861 27 днів тому

      Hana alijualo.
      As nawadanganya wapumbavu wenzake.

    • @drkalokola5861
      @drkalokola5861 27 днів тому

      Uprifesa ni wadhifa wa kuwa mkuu wa kitengo chuo kikuu. Inatolana na kufanya tafiti.
      Mwelekeo wa Taifa unategemea ujuzi wa uchumi na hulka ya uzalendo.
      Hayo mawili shivji hana.
      Anatafuta kiki TU za kusaka matonge.
      Mpotoshaji huyo. Muogope kama ukoma.

    • @festokemibala5832
      @festokemibala5832 27 днів тому

      Madini konki hata Mkataba wa Waarabu alitoa nondo lkn wajamaa wakatemper nayo na kufuata ya kwao kumfurahisha aliyewatuma na matumbo yao.

    • @ceciliamagalabajimmy4391
      @ceciliamagalabajimmy4391 27 днів тому

      Porojo na propaganda zinawafaa mapropangandist. Wasomi wanataka facts, lakini maneno ya kutia chumvi na sukari ndio yaliyotufikisha hapa tulipo.
      Mf: Mkinichagua mimi mabomba yote nitahakikisha yanatoa maziwa!! Watu wanaangua vicheko na kweli wanampa kura! Haya sasa hata maji ya kawaida tu hayatoki bombani! Hata hivyo jina linakuambia kuwa mtanzania huyu sio msukuma wala mhehe wala mzaramo. Anajitahidi sana ktk lafudhi wengine kama akina Chavda, Davda , Remtulla nk, ukisikia wanavyoongea hawawezi kulingana na Prof. Mungu ambariki ana uchungu sana na nchi yake, anatuambia ukweli lakini tuliozowea kudanganywa hatumwelewi, ni shida sana.

  • @drkalokola5861
    @drkalokola5861 27 днів тому

    Hamna kitu hapo.
    Dira alitengeneza Baba wa Taifa. Sakatonge mafisadi wanaibomoabkuhalalisha ufisadi wao.
    Wanamuonea Samia.
    Watawadanganya wapumbavu wenzao TU.

    • @festokemibala5832
      @festokemibala5832 27 днів тому

      Dira ya JKN ilikuwa ni Kujenga Nchi ya Ujamaa na Kujitegemea. Dira tunayoitimisha ni Tanzania yenye Uchumi wa Kati. Sasa tutoke uchumi wa Kati (MIC) twende Tanzania kuwa nchi Uchumi wa Juu (HIC). Ndani yake tuchukue vile vipaumbele vyetu ikiwemo Utawala bora na Utawala wa Sheria nk nk kama vilivyo sasa.

  • @GodfreyOsward
    @GodfreyOsward 29 днів тому

    Ndiyo wana wa Israel walitembea jangwani miaka 40 wakiendea nchi ya asali na maziwa.

    • @festokemibala5832
      @festokemibala5832 27 днів тому

      Umechemka

    • @GodfreyOsward
      @GodfreyOsward 27 днів тому

      @@festokemibala5832 kuna shughuli binafsi au kazi tunazifanya zinafanana na ujenzi wa taifa. Ukiwa unataka kujenga nyumba. Lazima uwe na kiwanja, kisha ramani, kisha vigezo vya fundi, vifaa vya ujenzi au budget, kuamua nyumba mbele na nyuma ya nyumba wapi. Kiwanja ni Tanzania, Ramani ni katiba, fundi na vigezo ni watanzania wawe na uelewa upi kutenda waliojipangia ndani ya katiba. Uelekeo wa nyumba ni dira. Na huo ni mchakato hatakiwi kuruka chochote. Kama kubadili mitaala bila kuanza na katiba. Unajenga nyumba bila ramani usilaum fundi wako. Hivi sasa tunakumbiza upepo wa tz. Ndiyo maana unaona kila kona kunapya.