Rais Samia Awashukia Wazee wa Vikokotoo: 'Tunafanya Uzembe, Mzigo Tunaushusha Kwa Wafanyakazi'
Вставка
- Опубліковано 29 вер 2024
- Akizungumza leo Juni 11,2024, kwenye shughuli ya kupokea gawio kutoka kwenye taasisi na makampuni, Rais Samia ameutaka mfuko wa PSSSF kujitathmini hasa kutokana na kuwa na hali mbaya katika vitabu vyake.
Ahsante Sana Mh.Raisi Kwa kuwajali wafanyakazi na kutambua madhaifu ya mifuko hii ya jamii
Mifuko inasimamiwa na nani? Serikali na huo uwekezaji nani aliubariki? Seeikali!! Sasa hapa mfanyakazi amejaliwaje?
Wajinga amuishi 😢😅😅😅
Kikokotoo hicho ni dhuluma, Mh Rais tunaomba kifutwe haraka
Tunashukuru Mh. Rais hao lazima waelezwe ukweli ili mambo yaende.
Umewasema vizuri watu wa vikokotoo 5:52
Hongera sana mh Rais kwa kuitambua shida ya wastaafu
kutolipwa jasho lao,simamia walipwe mafao yao yote . hongera kwa kina Kasalali, Msukuma na Bulaya kwa kuwatetea wastaafu .mama kura ni zako tu nawabunge wote wanaowatetea watanzania wenye tabu Mungu akubariki
Napita tu mimi 🎉
Mama yetu rais tusaidie tunanyanyaswa kwenye mikopo ya mitandaoni hasa kampuni ya kisasi pamoja na mkopo faster ni zaidi ya kausha damu twafa
The most incremental successful people in the world is the one which is driven by a sense of puepose
Today is monday change
Mheshimiwa rais sisi watu wa chini tunaokopa kwenye kwenye app mitandaoni tunalipishwa mara saba zaidi hasa kampuni ya kisasi na mkopo faster tusaidie
safi sana mama
Mama Samia nakupenda kabisa! Umesema vema mno. Ujue NSSSF wamuturudisha nyuma sana kimapato tukistaafu. Hatukufanya kosa lolote la kustahili kupunguziwa mafao ya kustaafu kijanjajanja: kikokotoo kimetutafunia pato, pato la mkupuo wametufyeka, umriwa kuishi baada ya kustaafu umepungua ili kupunguza tena pato, halafu wanatuambia eti wamejumuisha wasiochangia walipwe pensheni - ili tu tulioonewa tusiungwe mkono kudai haki ya pato kulingana na patano tulipoajiriwa! Mama, tutetee!
Kuhusu mifuko ya jamii pssf sio uongee tu kama ungekutana na wahusika uwasikie vile wanamatatizo utashangaa kuongea tu haitoshi!
MAMA UMEONGEA LWA HUSARA SANA
Mama FUTA kabisa kikokotoo
Sawasawa watendaji wetu jitafakalini jamani mnachelewesha maendeleo
Mama samia umechoka sana inabidii uwachiee lisu inchi yetu maana uwezani na kazi zetu kazi yako kama rais una usa inchi yetu kwa ndugu zako warabu
Lisu ni mwanaharakati kazi yake ni KUBWEKA hana leadership skills yeye na mbowe wale RUZUKU 😢😢😢😢😢😢😢
Nani wa kubebeshwa lawama? Aliyefilisi mfuko? (ujue hapo sio uongozi wa mfuko) si siri kali? Hayo maagizo ya mhe rais yanamlenga nani?
Serikali unajua vizuri na imehusika asilimia 100. Mama kakake huko nje ili watu wakwe haki zao.
AKINA PATROBASI KATAMBI WANATETEA KANUNI KANDAMIZI WAJITATHIMINI
Sheria zinasema kwamba wewe Samia ndiye ulisaini kikokotoo
Sasa Luka mkojo
Alisaini baba yenu aliyeenda kuongoza malaika.Acha upumbavu.Ndio maana alikufa.Mnafiki mkubwa
Mungu akubariki mama kwa kuliona tatizo la kikokotoo!!
Tafadhali Mh Rais hiki kikokotoo ni kidogo sna, naomba angalau msitaafu alipwe kwa mkupuo 75% kwani hilo ni jasho lake Halali. Natanguliza shukurani
Tulione kama zamani. Tunaomba kitu ambacho ni haki yetu! Serikali nikakope watu walipe haki zao. Kila mwezi unakatwa mshahara.
Mama UPO VIZURI KWELI WEWE NI MSEMA KWELI,MITANO TENA
Namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kutoa kauli hiyo ya ukweli. Chukua hatua zaidi usiishie kuongea
Mazingaumbwe hao anajuwa kila kitu
Hajasema kitu wafanyakazi wanataka kifutwe kiondoshwe
Acidophilus hatua, ungekuwa sana na bore.
Kwanini akiba ya wafanyakazi ya mifuko ya n s s f. Na ps s f isitumike kwa wafanyakazi kuwa dhamana kwa kukopa benki
Kikokotoo Cha Sasa ni dhuluma tupu. Ni vema na Haki Kulipa asilimia 50 Kwa Kikokotoo Cha awali 1 Kwa 540 siyo ya Sasa 1 Kwa 580 mtatuua mapema.
Mama amejaribu, japo suala la kikokotoo kwa wafanyakazi bado ni kandamizi, asulimia Saba iliyoongezwa ni sawa na ongezeko la milioni Saba.
Bora mngetoa mikopo kwa wafanyakai kwa asalimia ndogo.
Kikokotoo Ni dhuluma kubwa Sana kwa wazee wetu. Huwezi kuwadhulumu wazee ukabaki salama. Wote waliobuni kikokotoo Cha 33% Machozi ya wazee hayatawaacha salama. Hongera Sana mhe Rais kwa kuliona Hilo,lifanyie kazi MAPEMA iwezekanavyo!
Mungu akutunze na kukulinda Mama kipenzi. Futa Kikokotoo kabisa
Kuhusu hili la mifuko kuwa hali mbaya nakuunga mkono
Mama mimi hapa nilipo naumwa nimelala kitandani sina hata mia ya kujitibia nimewaandikia nssf barua wanilipe hela yangu nikaambatanisha na barua ya matibabu natakiwa nifanyiwe nilijibiwa una degree huwezi lipwa mafao .Nimechoka nimechoka
Nssf .Mama tusaidie Sheria zilizopo zinzumiza. Mfano mtu ame achishwa KAZI TOKA 2000 na kuambiwa umesoma tafta KAZI . Ni HAKI kweli. Nisipopata KAZI je?Hela ambayo ingetumika kama mtaji inakuwa maumivu
Mama unarikiwe sana kwa ishu ya kikokotoo, bt kipekee nampongeza sana Mh Ester Bulaya maana amelipigia kelele mno hili jambo
Mama asante kutuonea imani tunaumizwa saaana wasitaafu
Unachota Pesa unalipia madeni na posho za safar😂😂nani hajui
Tumechoka maneno Kila siku,Nchi hii Ina maneno mengi.wafanyakazi wanaongelewa leo.muongo anajua
MAGU ALIMIAMBIA VYUMA VIMEKAZA 😢😢😢😢😢
Tusubiri mpaka 25. Usiwe maneño bila kitendo. Utaumizwa sana
@@monicamwita7865 SIASA HAINA ADUI WALA RAFIKI MY DEAR 🤩🤩🤩🤩🤩🤩
Usiishie kuongea tu wawajibishe.Wamezoea vibaya.
Rudisha mafao kama yalivyojuwa awali kabla ya kuanzisha Kikokotoo dhalimu.Serikali iweke fedha kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii haraka kuziba udhaifu wa mifumo mliyoiunda wenyewe.
Hilo neno. Achukue hatua Swahili.
Tunakishukuru mheshimiwa Rahisi .BADO Nssf.,dhuruma ipo pia. Mifuko hii inatengeneza taratibu ngumu kuumiza wafanyakazi
Kweli wanalala na kusubiri kula pesa za watumishi na kukopeshana wakati huku chini tumeshikiwa chini tumefungwa mikono ndiyo maana wafanyakazi tunakufa haraka tumekuwa watumwa tu
Mh rais maanisha unachowaambia maana watendaji Huwa wanatuangusha nk nk
Mh tifutie hii dhulma adhwiiim
Mama Asante sana kwa kuzungumzia mifuko ya jamii.Mungu akulinde mama yetu.Mitano tena bila ubishi.Barikiwa sana
Mi 5 ya nini? Kama 4 tu tumeumizwa.
mdaumekaribia kauri za uchaguzi wa tz amkeni, uo usingozi mpaka lini?
GENGE la WEZI
Ukisimamia utekelezaji wa hili.Mitano mingine kwa watumishi unastahili ✅✅✅✅
Kwa kweli kiasi cha 33 1/3% tunacholipwa wastaafu ni kidogo kwa kipimo chochote kile. Kiwango cha theluthi moja kimekadiriwa na watu ambao wao wanapokea mishahara mikubwa kuliko tuliyokuwa tunalipwa sisi bila kujali sasa sisi tuliokuwa tunapata mishahara midogo sasa hatuna hata huo mshahara mdogo. Jamani Mwenyezi Mungu anawaona.
Hapa mimi mama Asante ❤
Tunatakiwa tufikirie njia za kuwasaidie watanzania kama samia
Mama ubarikuwe Sana kiondoe kikokotoo,umesema kweli!
Aaahhh magufuli lala salama uliko Leo wanabembelezwa hivi
Ni kweli kabisa Rais wetu mpendwa unachokisema ila kuna baadhi ya wasaidizi wako hasa huko mikoani wapo busy na maslai binafsi na siyo kuwasaidia wananchi kama ulivyowatuma.
Mawaziri wake, hasa fedha.
Mh rais Kwa heshima naomba toa kauli thabiti kikokotoo kifutwe wewe ndio ulie bariki na wabunge wako acheni kutesa waastafu jamani mnaenda makanisani misikitini kusali kweli?
Kililetwa na kilibarikiwa na magufuli.Acha kumsingizia huyu mama.
Wanafiki wakubwa
PIGA KAZI MAMA HII NDIO REALITY CHECK HAKUNA MIUJIZA
Mama hapo nimekupenda naomba vikokotoo hivyo vifutwe kabisa wafanya kazi wakistaafu wapewe pesa zao zote
Aondoke ndipo kumpenda.
KAMA UNAMUUNGA MKONO MAMA KUWA ADHABU WANAPEWA WATU WA CHINI YAANI WASTAAFU SEMA HAPO CHINI MAMA 2025 MITANO TENA
Ya nini. Kama 4 th watu tumechoka. CCM kama so goli la mkono wamegoma ñamba
Nakupenda sana mama. Umeeongea kweli tupu❤
Uko vizuri Rais wangu wenye kusikia watekeleza na kuyaishi maelekezo yako
Yaani Uishi miaka mingi sana.Umemwaga ukweli
Mh Rais kuongelea tu kikokotoo kisiasa half sera bado ileile sioni kama tunabadilisha kitu ............... Kusema ukweli kikokotoo ni janga la aibu sanaaaa ni Bora kifutwe half kodi iongezwe kidgo Kwa wafanyakaz ... Bora mara sabini
Wastaafu wanaumizwa na mbogamboga
Yaani Mheshimiwa Rais pokea maua yako.Mstaafu anaumizwa sana akistaafu
Maura ya nini? Mpe najua akishaondoa2 KIKOKOTOO.
Wewe uwe raise wa maisha
10 mingine na mama.
Tupo na Samia❤❤
Tupate matokeo siyo kusema tu,pesa za wastaafu wslipwe bila masharti yote. Waliozikopa eazirudishe.
Kila siku anaongea vitendo hakuna.
KWAKWELI NINGEKUWA NA UWEZA AU KATIBA INGEKUWA NA UWEZO,,. NINGEAMURU RAIS WETU, MAMA YETU DR SAMIA ASISUMBUKE KUZUNGUKA MWAKANI KUOMBA KURA,, APITE BILA KUPINGWA,, MI 5 MINGINE
TUFANYE TU KWA WABUNGE NA MADIWANI ILI WAZEMBE WAPUMZISHWE KAZI.
Pumbavu. Chawa mkubwa na mnafiki usiyeyejitambua
Kikokotoo wakokotoe wabunge wenye mishahara kidunchu walalahoi achana nao
Magari ya mawaziri
Mama mamaa Mungu akubariki sana❤ umesema ukweli
Sasa unajua pesa zinafichwa we unachukua hatua gani?ukiishia kusema tu na wao wanachukulia poa na wanazipiga kwelikweli
Shida iko hapo. Yeye pia phenylalamika. No vizuri wote wanaosababisha tatizo hilo wachukuliwe hatua.
Yeye amekuta tatizo, kama unakumbuka na mwenda zake aliwaambia waziwazi, mama nae ameendelea kupigilia msumari, mbona LAPF hakukuwa na tatizo hili? Wanaanzishaje miradi mingine wakati iliyopo haijaleta tija?Mimi nashauri kuwe na bodi ya wawakilishi wa mfuko itakayojumuisha wastaafu na wastaafu watarajiwa ili kiwe chombo Cha kufuatilia mwendo wa mfuko huu, na kuwe na uwazi wa mapato na matumizi kama ambavyo tumeona katika mashirika mbalimbali yakifedha yanavyofanya.Asante sana mama kwa kutetea wastaafu na kukemea ubadhilifu huu.h
Wisdom
Mbona Hawa wanaopitisha. Dhuluma hizi wao Kila miaka mitano wanajilipa zakwao. Tena. Nyimgi ajabu huu ni unyama. Waliochezea. Mifuko. Wapi walipe. Kwani pesa wamechukuwa halafu wanaleta stori. Warudishe. Wale zakwao ha Mheshimiwa .Raisi itakuwa umewafundisha kitu..kwani hawajui hasara Wala faida.
Umeongea madini sana mama inakuwaje uwezo mdogo wa kuendesha mifuko igeuke adhabu kwa wachangiaji?.warudishe fedha za watu kama wameshindwa au wawape bank wazizalishe wasianzishe miradi isiyo na tija au wakajenge nyumba za kupangisha wanafunzi
Mh. Rais. ni. kweli. kabisa. wanaoingusha. mifuko. ni. watumishi. wa. mifuko. na. wakuu. wao. wanajinufaisha. wenyewe. dawa. nikuwatimua. na. warudishe. fedha. zetu. walizoziiba. wachukuliwe. hatua. wanahusika
"....ni menejiment na pengine serikali..."!! Anajua anachokisema kwamba serikali ilikuwa ikidaiwa michango yake almost matrilion na hiyo nyingine...!
Ungekuwa unakubali ushauli ungemwindoa mwigulu wizara ya fedha ukamweka Hata Jerry Skaaa maana amesababisha uchumi kufa na pesa yetu kushuka Kila siku, nimetafuta Dollar 5,000. niende Rwanda nimetembea bank kama saba zote hakuna labda tukuelemeze Kwa bei ya 3000. Kwa Dollar wakati mabango yameandikwa 2630.kwa dollar, hii bei hupati Hata ukilia.majanga ya mwigulu.
Hivi mnajua kikokotoo kimebuniwa na nani? Kwa sababu gani?
Serikali kujitoa kwenye maamuzi haya ya dhuluma si sahibi.
Madeni ya fedha zilizokopwa na serikali yote yalirejeshwa kwenye mfuko?
Nani amewaruhusu watumishi kutumia michango ya watumishi kuwekeza ktk miradi?
Tozo ni nyingi mno
Mikataba iliyosainiwa ya Korea iwekwe adharani.
Tunataka mgombea huru tangu ngazi ya kitongozi asiyetegemea chama chochote cha siasa
Diaspora waruhusiwe kupiga kura
Mama Samia tizama na kodi kubwa tunayotozwa kama PAYE kwenye mishahara, hii inafanya mtumishi kuona tu namba kubwa ya pato lakini akishakatwa hadi 35% kiuhalisia anabaki tu masikini! Nyerere alikusudia kutuwezesha kupambana na umasikini. Bora wenye kipato wote tutozwe kwa asilimia ile ile! Mfano kama 9% kwa mwenye pato zaidi atatoa kingi kulingana na pato lake kubwa. Tusikomoane kwa kuweka kwamba eti anayezidi pato fulani kinachozidi kinakamuliwa karibia chote! Hii nchi kila mtu afaidi uwezo wake au cheo kinachomhalalishia pato! Asante mummy!
Mheshimiwa Rais utaratibu wa kikokotoo kwa wastaafu nikibaya na ni dhuluma. Mtu ametumikia taifa anastaafu badala ya kumpa stahiki yake eti mnamwekea, kwanini wabunge wao hamuwawekei mnawapa stahiki zao zote? Hii siyo sawa. Mmeua mifuko halafu solution nikuwadhulumu watumishi. Hii siyo sawa hata kidogo
Mheshmiwa Rais ungesema tu tulipwe hela zetu 100%. Na hao wasiokua na vision weka pembeni.
Miradi isiyokuwa na tija IUZWE, na Fao la kujitoa LIRUDISWE pesa ni za mfanyakazi, makosa ni yenu serikali.
Hawana hata aibu
Mama tunasubiri hekima yako maana Kuna idara zingine zinahumia kupita kiasi hatuna pa kusemea tu hivi milioni 17 na umefanya kazi miaka 34 na una mkopo wa nyumba na ulitegemea ulipe kwa kiinua mgongo au hujajenga unategemea kujenga kwa hicho kiinua mgongo tutafika kweli au ndiyo unasogezwa karibu na kaburi tutakufa na kuacha familia zetu zikiteseka, tuondolewe hicho kikokotoo
Sisi Wananchi tunataka
1 Katiba mpya
2 Tume huru ya uchsguzi
3 Wakurugenzi wasisimamie uchaguzi
4. Tunataka Tanganyika yetu.
5 .Tunataka tumiliki ardhi Zanzibar
6. Gharama za maisha ziko juu
Jamani, kazi kweli. Sheria hupindishwa na watu sio katiba wala tume. Kikokotoo si kina sheria na mikataba ya kudumu? Mbona kimebadilishwa. Na katiba ipo. Sheria nzuri ipo. Inaongea nini wewe.
Hongera
Mpe mstaafu pesa yake yote. Mnapata dhambi wote. Unampa kidogo kidogo mungu yupo tuu.
Mama fuatilia pia mapoto yanayotokana na miradi ya hii mifuko wastaafu wanafaidikaje maana ni hela za wastaafu ziliwekezwa😱
Mama selikar yako inafer Kila sehem wakurugenz wanasumbua kuripa pesa zawazabun ukiuliaza wanasema serikar Haina hela
HII .MIFUKO WASISIMAMIEVIJANA WAMAUMIZA WAZEEHAWA AKINA PATROBASI KATAMBI UMRI HUU NI TATIZO
Mh. Rais. basi. madeni. ya. WASTAAFU. wayalipe
Ww mama huna sifa ya uongoz hufatilii unasemaj tu mambo hayaendi Kwan mtanguliz wako hukujifunza kwake unakaz ya kubembeleza wez mm staki hata kukusikia kwaza jiuzul kbsa
Mama umeongea vyema sana, inatukera na inauma sana. ananipangiaje na hela yangu? kufika kustaafu ni neema tu. Bado unipe stress na changu?
Halafu kazi ipo pale palè.
Mzembe Wa kwanza ni yy coz ameshindwa kusimamia nchi kama mkuu wa nchi
Tanzania inahitaji rais kma magufuli mwenye maamuzi magumu.
Msajili akalifanyie kazi wapi? Ilitakiwa utoe tamko la kufuta kikokotoo sio maneno tu.
SUBIRA HUVUTA HERI,KAMA HUJAELEWA HIYO HOTUBA NENO KWA NENO HUTAELEWA
WATANGANYIKA WANAIBIANA WENYEWE KWA WENYEWE🤣🤣🤣👁️👁️
Tumechoka maneno kila cku tunataka vitendo.
Wabunge wanajionaje?!!
Wapiga kura hivi mnajua wajibu wenu?!!
Bunge la CCM hivyo sana. Hawawajali watu wao. Wanajua wao ni wa kupita kwani goli la MKONO ndilo nguzo yao.
kama utafuta Sheria ya kikokotoo we Hadi 2030
Akifute sasa. Hatua 40 bado no dhuluma kubwa
Mama watendaji wako wanakuangusha. Hiki kikokotoo ni hatari😢
Mazingaumbwe
Tatizo wananitoa sana badala ya kueleza ukweli
Nchi hii kila mtu analalamika hakuna mwenye majibu
Mpaka mama naye phenylalamika!
ASANTE LISSU MAMA KASIKIA
Hili jembe. Nawashangaa wanaomkejeli.