Rais Samia ataja uzembe, matumizi mabaya ya fedha PSSSF

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 3 жов 2024
  • Rais Samia Suluhu Hassan amesema ripoti inaonyesha Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) haupo vizuri huku akiuliza ni nani aliyefanya ufikie ulipo.
    Pia, ametaja uzembe na matumizi mabaya ya fedha kumesababisha hali hiyo katika mfuko.
    Haya yamebainishwa kwenye hafla ya kukabidhi gawio kwa Serikali kutoka kwenye mashirika ya umma na binafsi ambayo Serikali ina hisa zake, Ikulu ya Dar es Salaam leo Juni 11, 2024.
    Hivi karibuni, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson akiwa bungeni aliielekeza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi wa Jamii kuwaita na kuwahoji wakurugenzi wa mifuko ya hifadhi za jamii nchini kuhusu madai ya wanufaika kutakiwa kulipa fedha za michango ambazo waajiri wao hawakuilipa mifuko hiyo, ili wapatiwe mafao yao.

КОМЕНТАРІ • 1