Safisha Njia || Dodoma Adventist Chorus

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 6 лип 2023
  • SAFISHA NJIA

    Verse 1
    Mimi ni mdhaifu
    Siwezi kutembea,
    Nimebeba mzigo mzito,
    Sijui ni nani atanitua,
    Nimesikia leo,
    yupo mtu anaeweza
    kunitua mzigo wangu,
    Yesu naomba nionane naye.
    Verse 2
    Nguo zangu Ni chafu
    Siwezi jisafisha
    Hata mwili huu wa udongo
    Naona hauna thamani tena
    Kweli ninayo haja
    Kuonana naye sasa
    tabibu na mwokozi wangu
    Yesu naomba anitakase.
    Chorus
    Safisha njia ili nipite
    Nataka kumwona mwokozi kwanza
    Nizunguze naye kwa kina,
    Nimweleze ya moyoni mwangu,
    Suluhisho pekee lililobaki
    Ni NENO lake na Upendo wake
    Neema yake Rehema zake
    Msamaha vitaniokoa
    Verse 3
    Macho yangu dhaifu
    Siwezi ona mbele
    Hata Baraka nil'opewa
    Sioni ni Kama zimejificha
    Tazama Leo nimekuja
    Kufunguliwa macho yangu yaone
    Nataka kumwona Bwana
    Leo haja yangu isikiwe
    Chorus
    Safisha njia ili nipite
    Nataka kumwona mwokozi kwanza
    Nizunguze naye kwa kina
    Nimweleze ya moyoni mwangu,
    Suluhisho pekee lililobaki
    Ni NENO lake na Upendo wake
    Neema yake Rehema zake
    Msamaha vitaniokoa
    Chorus (unison)
    Safisha njia ili nipite
    Nataka kumwona mwokozi kwanza
    Nizunguze naye kwa kina,
    Nimweleze ya moyoni mwangu,
    Suluhisho pekee lililobaki
    Ni NENO lake na Upendo wake
    Neema yake Rehema zake
    Msamaha vitaniokoa
    ......
    Hali ya mwanadamu Ni dhaifu kiasi kwamba hawezi kutembea peke yake,
    Nguo zake ni chafu, hawezi kujisafisha mwenyewe na isitoshe,
    Katika hali ya kiroho mwanadamu Ni kipofu, hawezi kuona hata mibaraka mingi aliyopewa na Bwana.
    Suluhisho pekee lililobaki Ni kwenda Bwana na Mwokozi aliyemuumba ili akapate NEEMA, REHEMA na MSAMAHA ambavyo hupatikana kwa Bwana pekee.
    Bwana akubariki unapotazama na kusikiliza wimbo huu.
    Artist: Dodoma Adventist Chorus
    Song Title: Safisha Njia
    Audio Mixing and mastering: BJ Brand
    Email: dodomaadventistchorus21@gmail.com
    CONTACTS
    +255 712 227 383
    +255 784 291 945
    You can also find us on:
    Audiomack: audiomack.com/dodomaadventist...
    Boomplay:
    www.boomplay.com/share/music/...
    Instagram
    / dodomaadventistchorus

КОМЕНТАРІ • 164