KWANINI HAVITOKEI KWA WAKATI (I) - PASTOR SUNBELLA KYANDO

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 12 жов 2024
  • Mathayo 25:1-12
    Kuna aina mbili za wanawali katika hii mistari.
    (a)Wanawali wapumbavu
    (a)Wanawali werevu
    Wanawali wapumbavu ni wale ambao hawakubeba mafuta ya ziada,na wale werevu ni ambao waliobeba mafuta ya ziada.
    Wanawali wapumbavu hawakubeba mafuta ya ziada kwa sababu walipiga hesabu ya muda ambao bwana arusi atafika na muda harusi itatumia yale mafuta waliyobeba yangewatosha.Kwahiyo hawa wanawali hawakuwa na kosa.
    Wanawali werevu hata kama walijua muda ambao bwana arusi atakuja na harusi itatumia,walijiandaa kwa lolote na ndio maana wakabeba mafuta ya ziada.
    Kitu cha kwanza kutokea ni bwana arusi kukawia,hii inamaanisha kuna kitu kilitokea kikamchelewesha kufika.Na ukimuuliza atakupa sababu ya kimwili kabisa.Bwana arusi anaingia kwenye matatizo kwa sababu kuna watu ambao amewaalika ambao shetani hataki wafanikiwe.Kuna vita ambazo tunapigana sio kwa sababu shetani ana shida na sisi bali watu ambao tumewaingiza kwenye maisha yetu.Unapigwa wewe kwa sababu msaada ambao unataka kuwapelekea shetani hataki msaada uwafikie.
    Kitu cha pili wanawali wakalala usingizi.Neno linasema wakasinzia wote.
    Ukisinzia unaanza kutokufahamu kile kinachoendelea katika eneo ambalo una changamoto(unazubaishwa).Unaweza kujua kabisa hilo eneo una shida lakini hufanyi chochote kutoka kwenye hiyo shida.
    Ukishatoka kwenye kusinzia unafuata hatua ya kulala.Ukifikia hatua hii unaweza kuwa kanisani na somo linalofundishwa linakuhusu kabisa,lakini kila ukisikiliza unamuona mtu mwingine unayemjua kuwa hilo somo linamhusu na hujioni wewe.
    Ukifika hatua hii jua umelala kabisa.
    UNAWEZA WASILIANA NASI AU KUTUMA SADAKA YAKO KWA NAMBA HII : 0657 173 322
    Unaweza kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii
    Like our Facebook: / therealityof. .
    Follow our Instagram: / realityofch. .
    Subscribe our UA-cam: www.youtube.co....
    Also Subscribe Roc worshippers youtube channel: / @rocworshipperz

КОМЕНТАРІ • 30