KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA EVENING GLORY: THE SCHOOL OF HEALING 04/ 07/ 2024

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 2 жов 2024
  • KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA EVENING GLORY: THE SCHOOL OF HEALING 04/ 07/ 2024
    UJUMBE WA LEO: VITA YA KESHO YAKO
    [SEHEMU YA PILI]
    Hagai 2 : 9
    Ayubu 13 : 27, 33 : 11
    Habakuki 2 : 2
    2 Wafalme 4 : 3 - 4
    Yoshua 1 : 3
    Waefeso 6 : 15
    Amosi 3 : 12
    Hagai 2 : 9
    9 Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema Bwana wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema Bwana wa majeshi.
    Ayubu 13 : 27, 33 : 11
    27 Waitia miguu yangu katika mkatale, na kuyaaua mapito yangu yote; Wajiandikia alama kuzizunguka nyayo za miguu yangu;
    11 Hunitia miguu yangu katika mkatale, Na mapito yangu yote huyapeleleza.
    Habakuki 2 : 2
    2 Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.
    2 Wafalme 4 : 3 - 4
    3 Akasema, Nenda, ukatake vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usitake vichache.
    4 Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge.
    Yoshua 1 : 3
    3 Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.
    Waefeso 6 : 15
    15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
    Amosi 3 : 12
    12 Haya ndiyo asemayo Bwana; Kama vile mchungaji apokonyavyo kinywani mwa simba miguu miwili, au kipande cha sikio; ndivyo watakavyopokonywa wana wa Israeli, wakaao Samaria katika pembe ya semadari, na juu ya mito ya hariri ya kitanda.

    AGENDA ZA MAOMBI
    1. TOBA.
    2. Shukrani kwa Miezi sita 2024.
    3. Omba Neema ya Mungu.
    4. Omba uwepo wa Bwana uende pamoja nawe.
    5. Omba Mungu akuepushe na Majaribu yasiyobeba kitu kwa ajili yako.
    6. Ombea AKILI yako na Kushughulikia Hilo Zuio la NDANI
    Mhubiri: Mwl. Eng. Googluck Mushi.
    Kwa maombi na ushauri :
    Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
    Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
    Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
    Simu: +255 713 553 443
    UA-cam: Kijitonyama Lutheran church
    Barua Pepe: Kijitonyamalutheran@gmail.com

КОМЕНТАРІ • 10