TABIA 5 SUMU UNAZOHITAJI KUACHA

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 16 вер 2024
  • Katika mnnendo wako wa kila siku kuna baadhi ya Tabia 5 sumu unazohitaji kuacha kabisaa ili ukuwe vyema:
    1. MAZUNGUMZO HASI MOYONI:
    Kujiweka chini kila wakati na kuwa na kujistahi kwa chini.
    Jinsi ya kurekebisha:
    • Akili Chanya = Matokeo Chanya
    • Daima uwe na mtazamo mzuri
    “Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”
    ‭‭Wafilipi‬ ‭4‬:‭6‬-‭7‬ ‭NEN‬‬
    2. USIMAMIZI MBAYA WA WAKATI:
    Kutumia muda kwa ufanisi kunaweza kusababisha kuongezeka kwa msongo na kuzuia malengo ya mafanikio.
    Jinsi ya kurekebisha:
    • Panga siku zako
    • Kuwa na utaratibu
    “Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri, ili tujipatie moyo wa hekima.”
    ‭‭Zaburi‬ ‭90‬:‭12‬ ‭NEN‬‬
    “Kila kitu kina majira yake, kila jambo duniani lina wakati wake:”
    ‭‭Mhubiri‬ ‭3‬:‭1‬ ‭BHN
    3. MSONGO WA MAWAZO:
    Kuwaza sana matukio ya zamani na kuyaruhusu kuishi kichwani mwako. Hii inaweza kuathiri maamuzi ya sasa na yajayo.
    Jinsi ya kurekebisha:
    • Yaliyopita ni yaliyopita; Jifunze kutoka kwake, endelea.
    “‘Msiyang’ang’anie mambo yaliyopita, wala msifikirie vitu vya zamani.”
    ‭‭Isaya‬ ‭43‬:‭18‬ ‭BHN‬‬
    4. KUJILINGANISHA NA WENGINE:
    Hii inaweza kusababisha hisia za kutostahili na kuzuia ukuaji wako binafsi na kuondoa furaha.
    Jinsi ya kurekebisha:
    • Siku zote ni Wewe dhidi yako.
    “Usiitamani nyumba ya jirani yako, wala mke wake, wala mtumwa wake wa kiume au wa kike, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala chochote kilicho mali ya jirani yako.”
    ‭‭Kutoka‬ ‭20‬:‭17‬ ‭BHN‬‬
    5. KUTOJITUNZA:
    Kupuuza ustawi wako wa kimwili na kiakili kunaweza kusababisha uchovu, na kuathiri vibaya afya yako na furaha yako kwa ujumla.
    Jinsi ya kurekebisha:
    • Daima jali afya yako ya kimwili na kiakili. Mawazo chanya ndio nyenzo yako kuu.
    “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.”
    ‭‭3 Yoh‬ana 1‬:‭2‬ ‭SUV‬‬
    Naamini kwa uwezo wa Roho mtakatifu kuna mambo mbalimbali utainuliwa kwayo kupitia ufafanuzi huu. Hivyo, Mwenyezi Mungu akuwezeshe kuyaishi vyema katika vitendo na utufuku wa Mungu uwe nawe siku zote.
    Unaweza kushiriki kuwezesha huduma hii kwa fedha yako kupitia njia zifuatazo:-
    M-Pesa Ac No: +255 763 221 424
    NMB Back Ac No: 33410008547
    CRDB Bank Ac No: 0152895272000
    Jina: Endson Fanuel Mabamba
    Mungu akubariki sana.

КОМЕНТАРІ • 23