Simulizi ya mwanafunzi wa darasa la Sita anayelea wadogo zake watano kwa kuomba omba mtaani

Поділитися
Вставка
  • Опубліковано 10 вер 2024
  • Rombo.Mtoto James Efram(14), mkazi wa kijiji cha Kwalakamu, wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, amejikuta akibeba majukumu ya familia kwa kuwalea wadogo zake watano baada ya familia yake kukumbwa na hali ngumu ya maisha baada ya baba yao kufariki dunia mwaka 2011.
    Mtoto huyo ambaye anaishi na mama yake mwenye matatizo ya afya ya akili pamoja na ndugu zake hao wamekuwa wakiishi kwenye pagale la udongo(jumba bovu la udongo) lenye matobo na hata wakati wa mvua maji huingia ndani na kulowanisha matandiko yao ambayo hutandika chini kutokana na kwamba hawana kitanda.
    James, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la Sita katika shule ya msingi Mamonjo, iliyopo wilayani humo, amejikuta katika wakati huo mgumu wa kuilea familia yake na wakati mwingine akilazimika kukosa vipindi darasani na kwenda kuomba msaada mtaani ili wadogo zake waweze kupata angalau chochote kitu.
    Mwanafunzi huyo, ambaye huitwa majina ya kila namna kwenye kijiji anachoishi kutokana na kuomba omba kwake, amesema hawezi kukata tamaa ya kutafuta ili aweze kuwasidia wadogo zake kwani akikata tamaa wadogo zake hawataweza kusaidika na yeye ndiye msaada katika familia yao.
    Hata hivyo, Mwananchi digital ilifika nyumbani kwa mtoto huyo na kuona hali halisi ya maisha wanayoishi ambapo katika nyumba hiyo ya udongo wanayoishi yenye matobo kila kona imeanza kubomoka hali ambayo inahatarisha usalama wao, hasa nyakati za usiku ama mvua kubwa itakaponyesha.

КОМЕНТАРІ • 51

  • @andrewmaiga4331
    @andrewmaiga4331 24 дні тому +3

    Hongera sana Walimu, huu ndiyo ulezi.

  • @f.a6043
    @f.a6043 25 днів тому +3

    Tunaomba namna ya kuwachangia hawa watoto wanaoishi ktk mazingira magumu
    maisha ndio haya haya hamna mengine tujitahidi kutenda wema kabla MWENYEWE MUNGU hajatuita kuondoka ktk Dunia hii
    tukipata Chance ya kutendwa wema tuwe wepesi kutenda mema itatusaidia baada ya maisha haya hapa Duniani🥹🥹

  • @HanifaOman-oo4pl
    @HanifaOman-oo4pl 25 днів тому +2

    Subuhanallah. Mtihani mungu awape.kilalaheri awaondoshee.mitihani mtotomdogo anamoyo sana nimtoto mwema

  • @mwanamosishah4104
    @mwanamosishah4104 9 днів тому +1

    Dah! Ukisikia ualimu ni wito ndio hiyo.
    Mungu azidi kukuzidishia Imaan, kama ulivyomtete uyo mtoto na wewe Mungu atawatetea kizazo chako bila hesabu.
    Hakika nimelia kwa furaha 😢😢😢

  • @AngelMazola
    @AngelMazola 9 днів тому

    Mungu awbariki sana

  • @epimackjohn461
    @epimackjohn461 25 днів тому +4

    MWALIMU MKUU ANATAMBUA WAJIBU WAKE WA UONGOZI NA PIA UUMINI WA UBINADAMU , PONGEZI SANA MWL MKUU WEWE NA STAFF YAKO . MUNGU AWABARIKI NINGEKUWA MWAJIRI WENU NINGEWAPA PROMOTION HARAKA SANA .

  • @robsonlotyloy5678
    @robsonlotyloy5678 24 дні тому +1

    Mungu hawa bariki sana.

  • @estermathias8354
    @estermathias8354 9 днів тому +1

    Pole mtoto mzuri lkn mwalimu apewe maua yake ni mfatiliaji mzuri😢😢😢😢

  • @azizamvungi1871
    @azizamvungi1871 24 дні тому +2

    Wewe unayesema kazaa watoto wengi watoto ni baraka sana Mungu atatenda atainuka tu

  • @dignachami7382
    @dignachami7382 25 днів тому +3

    Daaa dogo atakuwa mtu mkubwa sana

  • @user-sx3id3rv8l
    @user-sx3id3rv8l 2 дні тому

    😭😭😭😭

  • @NeemaNabintu
    @NeemaNabintu 9 днів тому

    Mwalimu, ubarikiwe sana dada.nakuombee MUNGU akutetee sana .❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤

  • @MillenMlay
    @MillenMlay 25 днів тому +3

    Warombo hapa tume feli hili linatakiwa likaliwe kikao cha dharura....

  • @user-rf9vn7lz1n
    @user-rf9vn7lz1n 13 днів тому +2

    Ila serekal wanachangia magol na wadog zet wanaish kwa tabu 😢

    • @MsNajma-j7e
      @MsNajma-j7e 10 днів тому

      Kabsaa wanawasaponti wacheza mpila na wasani tu

  • @user-wl4yo4zp9t
    @user-wl4yo4zp9t 9 днів тому

    Pole sana mwanangu mungu ni mwema

  • @NeemaNabintu
    @NeemaNabintu 9 днів тому

    Mwanangu ,moyo wako ni ya pelée sana.MUNGU aendelee kukutetea, ubarikiwe sana kijana mzuri.

  • @jacobramale9685
    @jacobramale9685 24 дні тому

    Pole sana ndogo ang,mungu yupamoja na ww na sisi pia tupamoja na wewe.

  • @japhetmombia
    @japhetmombia 24 дні тому

    Mungu akulinde my Son

  • @reganuisso1256
    @reganuisso1256 24 дні тому

    Inaumiza sana kwakwel..

  • @user-db4cg5mh5b
    @user-db4cg5mh5b 25 днів тому +1

    Daa 😭😭😭😭😭😭😭😭😭

  • @johnjescajohnjesca
    @johnjescajohnjesca 25 днів тому +2

    Tujifunze wema ni akiba

  • @verdianabanabi2205
    @verdianabanabi2205 24 дні тому +1

    Hela ya watanzania huwaga ni ya kununua majiya kuwasha na risasi za kuwapiga wapinzani ila za kusaidia mambo kama hayo haipo.

  • @abdul-rahmanfakijuma1879
    @abdul-rahmanfakijuma1879 25 днів тому

    😰😥😭😭😭

  • @emmanuelsaria7975
    @emmanuelsaria7975 25 днів тому +2

    Mzee wangu mkenda fanya kitu kwa hiyo familia saidia uwezo unao

    • @GraceMarine-vo9hu
      @GraceMarine-vo9hu 25 днів тому

      Hata awajengee basi nyumba ya vyumba viwili tu 😢

  • @sadamissa5687
    @sadamissa5687 24 дні тому +2

    Goli moja million 5 ,yanga wamefunga manne wamepata million 20! Kwa mbili mbili Kwa mbili mbili imeisha hyo

  • @abdul-rahmanfakijuma1879
    @abdul-rahmanfakijuma1879 25 днів тому

    😢😢😢😢😢

  • @audaxbizimana8084
    @audaxbizimana8084 25 днів тому

    😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢

  • @emmanuelsaria7975
    @emmanuelsaria7975 25 днів тому +1

    Atakuja kuwa mtu mkubwa sanna

  • @japhetmombia
    @japhetmombia 24 дні тому +1

    Tunachangishwa Michango ya Harusi kila siku, badala ya kuchangishwa michango ya vitu kama hivi.

    • @israelkisaila8401
      @israelkisaila8401 24 дні тому

      Nilienda mahali Moshi,nilikuta mtaa Fulani aise,kila familia inatoa MICHANGO ya kuwapeleka watoto shule,tena mpaka nje ya Nchi,walishaachana na mambo ya kuchangiana kwenye harusi,wapo mbali zaidi aise

    • @hubakombe586
      @hubakombe586 23 дні тому +1

      Me nshaachaga kuchangia maharusi.. Nikipata nanunua chakula au dawa za muhitaji ninayemfahamu

    • @israelkisaila8401
      @israelkisaila8401 23 дні тому

      @@hubakombe586 Kwa kweli,MUNGU akubariki sana Kwa hilo

  • @DosianaLulakuze-bv7fg
    @DosianaLulakuze-bv7fg 25 днів тому

    Haya Maisha ni hatari kabisa Mungu wetu atusaidie

  • @Veronicahquithern
    @Veronicahquithern 10 днів тому

    ❤❤❤

  • @iwishtv7907
    @iwishtv7907 24 дні тому

    Tunaomba mawasiliano ya mtoto

  • @aediayumgo8546
    @aediayumgo8546 24 дні тому

    Wachaga pesa tunazo mpaka tunashindwa kuzihesabu tunashindwa kweli suala dogo hili oh!!; meku😂😂

    • @RehemaJustine-co2kp
      @RehemaJustine-co2kp 4 дні тому

      Ila kweli ebu wachaga tuungane ktk hili! Mchanga mwenzetu yuko shidani .

  • @ilynpayne7491
    @ilynpayne7491 24 дні тому

    Kuzaa watoto wengi ni 😮tatizo

    • @FIFO28
      @FIFO28 24 дні тому

      Mpuuzi ww nenda kafe sasa utoe na kizazi....

    • @epimackjohn461
      @epimackjohn461 24 дні тому +3

      Huwezi kumpinga MUNGU na mipango yake kwa wanadamu , mbona wewe husemi kuwa kuzaliwa kwako ni kosa ?

    • @mrambabashim3571
      @mrambabashim3571 24 дні тому +1

      Wee kwenu upo peke yako

    • @RehemaMtono
      @RehemaMtono 24 дні тому

      ​@@epimackjohn461kabisa ndugu yangu mbona hasemi kuzaliwa kwake nikosa

  • @edsonnelson4464
    @edsonnelson4464 25 днів тому

    Ndugu wa wazazi wake wako wapi?

    • @audaxbizimana8084
      @audaxbizimana8084 25 днів тому

      Ndg tena😢😢😢😢

    • @edsonnelson4464
      @edsonnelson4464 25 днів тому

      @@audaxbizimana8084 baba wakubwa/wadogo, shsngazi/mjomba, mama wakubwa/wadogo

    • @FIFO28
      @FIFO28 24 дні тому

      Siku ukipata shida, tafuta hao ndugu uone kama utapata...

  • @user-xp8fu5tu2k
    @user-xp8fu5tu2k 21 день тому

    😭😭😭😭😭