RAIS SAMIA AUFUFUA MRADI WA MWAKA 1930 ULIOPO CHUO CHA UFUNDI ARUSHA
Вставка
- Опубліковано 23 лис 2024
- Serikali ya Tanzania kupitia Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) inatekeleza mradi wa ujenzi wa Kampasi yake ya Kikuletwa ambayo hapo mwanzo ilikua kituo cha kuzalisha umeme kilichoanzishwa na serikali ya ujerumani mwaka 1930.
Mradi huo wa ujenzi uliopo wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro unatekelezwa kupitia mradi wa Afrika Mashariki wa kujenga ujuzi kwa mlingano na uingiliano wa kikanda (EASTRIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia unalenga kuboresha kampasi hiyo kuwa kituo cha umahiri kwenye nishati jadidifu.
Akizungumza baada ya kufanya ziara kwenye Kampasi hiyo na kukagua ujenzi unaoendelea, Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Amiri Mohamed Mkalipa amesema mradi huo umeibuliwa na Rais Samia kutokana na tija itakayokuja kupatikana hapo.
“Tunamshukuru Mhe. Rais kwa sababu mradi huu ni wa tangu 1930, sasa Mhe Rais ameliibua wazo hili na kulitekeleza leo, wazo la 1930, mradi ni mzuri sana tunawapongeza wenzetu wa Arusha Technical chini ya Mkuu wa Chuo wanasimamia vizuri, majengo yamekwenda vizuri na viwango vimezingatiwa” alisema Mhe. Mkalipa.
Aidha ameongeza kuwa “ sisi kama serikali tunaangalia tija itakayokuja kupatikana hapa, kwa mkupuo mmoja hapa watasoma wanafunzi karibu 600, na hao ni wanafunzi wadogo, Chuo hiki dhamira yake ni kutengeneza vijana wa kitanzania waende kwenye mradi mkubwa wa Bwawa la Mwalimu Nyerere na bahati nzuri imeangukia kwenye Wilaya yetu ya Hai” aliongeza Mhe. Mkalipa.
Naye Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha Dkt. Musa Chacha amesema Kampasi hiyo baada ya kukamilika itaweza kuzalisha wataalamu watakaoweza kukidhi vigezo kufanya kazi katika nchi za Afrika Mashariki.
“Mradi huu ni wa Afrika Mashariki, vituo hivi vya umahiri vipo Tanzania, Kenya na Ethiopia, jukumu tulilopewa Chuo cha Ufundi Arusha ni kuandaa vijana watakaofanya kazi Afrika Mashariki na duniani kote” alisema Dkt. Chacha.
Chuo cha Ufundi Arusha kilipokea jumla ya shilingi Bilioni 37 za Tanzania kupitia Mradi wa EASTRIP ulioko chini ya Benki ya Dunia ili kuboresha Kampasi yake ya Kikuletwa kuwa kituo cha Umahiri kwenye sekta ya nishati jadidifu
#Kikuletwa
#wilayayaHai
#mradi
#arusha_technical_college
#Chuo_cha_Ufundi_Arusha